Mwanaume mmoja wa nchini Singapore anaipenda zaidi Liverpool kuliko hata mke wake, harusi yake ilifanyika katika mazingira ya ki-liverpool, pete yake ya dhahabu ya harusi ina nembo ya liverpool na hata watoto wake anategemea kuwapa majina ya wachezaji wa Liverpool.

Vikinisvaran Suppiah mwenye umri wa miaka 31, anaipenda zaidi Liverpool kuliko anavyompenda mke wake. Mke wake Bawani Arumoh,29, analijua jambo hilo na ameridhia kuwa kama mke wa pili baada ya Liverpool.
Habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2009

    Huyo ana maisha mafupi mnooo atakufa tuu kwa pressuer kwa sababu liverpool hawajawahi kulibeba kombe barclays tangu lipewe hilo jina toka coca-cola premier cup..

    Mshaurini aachane na bwawa la maini kuna timu za maana duniani..

    mdau dublin, rep. of ireland.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2009

    Duh! iko kazi hapo kwa bibie...
    Hao ndio wale wanaume wanaukua kwenye TV 24/7.

    Bahati yake ni mhindi kwani bibie wa kibongo angeibua mwingine wa pembeni....

    J.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2009

    masikini liverpool, inaolewa na kuachika kila siku, mi nilifiri sie man ndio waume halali wa bwawa la maini sasa inakuwaje tena wanaolewa singapore,au mnataka hela za kununulia vifaa? maana mnatia aibu kwenye usajili, hata yanga wanawashinda

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2009

    mnatakiwa tu mfahamu kwamba kuna watu wengi tu wana matatizo ya ubongo, ila huwa sio rahisi kuwatambua ukiwaona barabarani hadi pale labda wakilazimika kupimwa ndipo watafahamika. kwa msingi huo basi wengi matatizo yao ya kiakili hujificha ktk ushabiki wa vitu fulani,dini,n.k na kwa wachache yanapovuka mipaka ndipo hujidhihirisha wazi na kujulikana kuwa kumbe ni kichaa na sio mzima.
    binadamu wa kawaida hufikiri na kutenda rationally.ukiona mtu anatenda jambo fulani ktk mahali pasipo sahihi lazima ana walakini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2009

    wewe anony wa jul 22 07:11:00 pm una akili unayoitumia vizuri kwa hiyo nasema una akili sana. mimi ni mshabiki wa man u lkn hata ningemuona mtu kaweka nembo za man u kwenye harusi namna hiyo ningefikiria ana matatizo. hao ndio liver siku ikifungwa anaweza fufungia familia yake na kuwatwanga risasi wote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...