Habari za kazi kaka,
Sasa nimeona bandiko hili
http://issamichuzi.blogspot.com/2009
/07/libeneke-la-bei-za-vocha-za-simu.html
Ambapo watu wanalalamika kuhusu kupanda kwa bei za Vocha.
Ushauri wa bure ni kwamba wanaweza kununua Vocha kwa bei halisi kupitia M-Pesa.
-> Kufungua akaunti - Bure
-> Kudeposit pesa kwenye akaunti - Bure
-> Kununua airtime kupitia M-Pesa - Bei halali (yaani Tshs. 1,000/-kwa muda wa maongezi wa Tshs. 1,000/-) ...
Pia mambo ya kuscratch nakujaza namba hakuna.
Au unaonaje? Si ni solution bomba hii?
Siku njema
Mdau Fred

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2009

    Hiyo imekaa kwa wale wanaoishi mjini, na ujue M-pesa ni saa za kazi tu. Nafikiri kuna haja ya kutafuta muafaka,kwani hadi hii leovocha bai ni juu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2009

    Nafikiri hiyo M-Pesa pia inagharama za uendeshaji, unapotuma pesa unachajiwa kwa asilimia fulani, je huoni kwamba bado hakuna unafuu wowote??????? pia uwezo wa kuendesha na kufungua account kutokana na hali ngumu ya maisha kwa anaeye fanya kazi yenye kipato kidogo (kuuza karanga, maji, nk) unamfikiriaje na anataka VOCHA ya sh 500 baada hata ya wiki mbili??

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2009

    KWA MIMI MTU WA TIGO NIFANYAJE? AU NDO UNAFANYA ADVERTISEMENT TUINGIE HUKO. HONGERA MICHUZI KWA KUIFANYA BLOG YETU ITOE MATANGAZO YA BIASHARA BURE

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2009

    Mimi nafikiri mdau hajaeleweka,kuweka pesa kwa M-pesa ni bure kabisa,hata kufungua account ni bure kabisa,sasa ukiweka 2000 yako kwa m-pesa na ukanunua salio la 1000 hautalipia kitu na muda wako wa maongezi utaongezwa kwa 1000 na m-pesa yako itabaki 1000,gharama iko wapi?pia sio kweli mpesa ipo mijini,kibororoni ni mjini?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2009

    Bongo tambarare!!!!!!

    mambo haya yakija wale wanaokula nchi kwa mrija wala hawafungui mdomo. Walala hoi ndio wanazungumza ukweli

    Mwaona sasa....mwasema rudi home rudi home. Vocha ya sh 500 mtu hawezi? Ukweli ndio huo bongo wachache tu ndio wanaishi wengine wote wanasindikiza tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...