msanii usher raymond akiimba katika hafla ya kumbukumbu ya michael jackson jijini los angeles ambapo mamilioni ya wadau dunia nzima walishuhudia shughuli hiyo ya majonzi.
Globu ya Jamii ambayo imefuatilia shughuli hiyo toka mwanzo hadi mwisho kupitia CNN na globu kibao zilizokuwa laivu, imeguswa sana na maneno ya wasemaji wote wakiwemo wacheza basketball kobe bryant na magic johnson, msanii stevie wonder, mcheza sinema brooke shields na gwiji la muziki smokey robinson pamoja na wengineo ambao wote wamekiri kwamba MJ alikuwa mfalme wa pop na pia msamaria mwema ambaye hatosahaulika.
Maneno ya Martin Luther King III alipomnukuu marehemu baba yake mpigania haki Martin Luther King jnr., kwamba ni vyema mtu kufanya kazi uliyonayo kwa ustadi wa hali ya juu ili usifike na kukumbukwa. Hata kama ni kazi ya kufagia barabarani, ifanye kwa moyo na ustadi ili kila mtu akukumbuke kwamba ulikuwa mfagiaji hodari sana.
Wote walipenda MJ akumbukwe hivyo. Kwamba ni mtu aliyeweza kuifanya kazi yake ya muziki kwa moyo na ustadi wa hali ya juu kiasi si rahisi kumsahau.
Mola aiweke mahala pema peponi roho ya Michael Jackon - Amin
-Michuzi
Rest in peace MJ,utakumbukwa siku zote na tuliokupenda na hata ambao hawakukupenda.Mengi yamesemwa na yataendelea kusemwa ila ukweli unabaki palepale kwamba "you were the king of pop"that will never change MAY BE in another generation.Watu wanasahau wewe pia ulikuwa mwanadamu na hivyo hukuwa mkamilifu kama ambavyo wao si wakamilifu. Inachekesha ambavyo walikuwa ni wepesi wa kuhukumu!
ReplyDeleteUmekwenda, nenda kapumzike sasa Michael.
We thank God almighty kwa kutupa wewe,we thank him more kwani kupitia kwako tumejifunza mengi pia, si burudani peke yake bali kupendana na kujali kwani to make a difference doesn't require one to have millions in the bank!
We thank God for your life.
MUNGU AKUSAMEHE NA AKUREHEMU.
MJ's Fan.
jamani kama kuna siku nimeumia roho nipamoja na ya jana siwezi kusahau hasa pale mwanae alivyomuelezea baba yake rest in peace michael
ReplyDeleteAh, wabongo kwa kudandiadandia,kifo cha MJ kikuumize una uhusiano nae gani, acheni hizo! he was no more than a normal person na anapata adhabu kali kwa kumkosoa mwenyezi Mungu.
ReplyDeleteWewe anon hapo juu, nani kakupa mamlaka ya kumjudge mtu?unajuaje kama alitubu kabla ya kukata roho,hayo ni maelewano yake na Mungu wake,you're just supposed kumuombea kheri afike peponi as we always do to everybody,suala la hukumu muachie Mungu mwenyewe....
ReplyDeleteme sio shabiki wala sikumfagilia kiivo MJ
ReplyDeleteila yule mtoto wake Paris dah yale maneno na chozi dah...nimeangusha chozi kamenigusa aswaa!!
afu watoto wake "halisi" Prince I na Paris mbona WAZUNGU PURE??jamen au ndo mambo ya mipesa kila kitu kinawezekana km MJ avotengenezwa kua mzungu??
ila kale prince II ndo mchina sijui
duh!!
mbona ina-sua sua???
ReplyDeleteinakohoa bwana hii video
jamani nimelia jamani nimelia saaaaaaaaaana yaani jana nilisikia uchungu sana, maneno fulani yalinitouch wakati jennifer hudson alipokuwa anaimba then yakatolewa yale maneno ya michael jackson( in our darkest hour, in my deepest despair, will u still care aahhh jamani i cried like ababy kwakweli i will never forget MJ....HE WAS THE BEST.......MY EVERYTHING.....
ReplyDeleteWAZUNGU KWA KUWA MAMA YAO NI MZUNGU, NENDA KAULIZE GENEOLOGISTS watakuhabarisha inawezekanaje?. INAWEZEKANA KABISA WAKAWA WAZUNGU PURE, BIOLOGY HATA O- LEVEL HAIPANDI KWANI KUNA X NA Y MCHANGANYIKO WAKE NDIO UNAO-DETERMINE MTOTO.
ReplyDeleteYaani binti yake Michael, Paris alipoongea kuhusu Baba yake, nimejikuta machozi yananidondoka kama mtoto mdogo! Really heartfelt message from an angel of 11 years old!
ReplyDeleteWewe Tarehe Wed Jul 08, 02:35:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
ReplyDeleteEti "MJ....HE WAS THE BEST.......MY EVERYTHING..." Alikuwa hata hakujui sasa itakuwaje alikuwa your "everything"? kama sio uzushi ni nini?
we anon wa 02:35 nini haswa kinakuuma kama mie mwenyewe nimesema he was my everything ama ulikuwa unataka niseme weye ndio ma everythin..hebu acha hiyo roho mbaya kama mkaanga sumu....kila mtu duniani anayemtu wake anayemuhusudu, anampenda, anamfeel, hata kama hajawahi kuonana naye kwahiyo niache nimpende MJ maana he was my Greatest Idol, my one n only musical genius n i feel him to the core of my heart.....if u know what i mean.....!!!!wewe kama huna umupendaye tuache sie tunaojua kupenda tupendee wewe endelea kuwa na roho ya kwanini....roho ya kutojua kupenda....
ReplyDeleteWewe Tarehe Thu Jul 09, 01:37:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
ReplyDeleteLabda tatizzo lugha. Unajua maana ya "my everything"?? Sio kudandia maneno tu. Hakuna hater hapa ni kuelimishana tu.
Wataimba sana tu harudi yupo chini anapata mkongoto vibaya sana.
ReplyDeletemdau 10:14pm
ReplyDeletesina mbavu,wewe uko salama??