Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya chama cha Kikomunisti cha China, Zhong Weiyun akimuonyesha Mkurugenzi wa shule za sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Leornad Musaroche kitabu kinachoitwa “ Selected Works of Deng Xiaoping Volume 3” kilichotungwa kuanzia mwaka 1982-1992. Kitabu hicho chenye kurasa 400 pamoja na mambo mengine kinazungumzia uhusiano wa Tanzania na China na pia kazi nzuri waalizozifanya waasisi wa mataifa haya.
Mkurugenzi wa shule za sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Leornad Musaroche akimkabidhi zawadi ya kinyago cha mnyama kifaru Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya chama cha Kikomunisti cha China, Zhong Weiyun ikiwa ni zawadi maalum kutoka kwa vijana wa Tanzania walio nchini China kwa ziara ya mafunzo ya siku 10.

Bw.Rogatius Shao ofisa anayeshughulikia masuala ya nchi za Asia/ China wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Tanzania akisalimiana na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya chama cha Kikomunisti cha China, Zhong Weiyun wakati vijana kutoka Tanzania walipotembelea ofisi za Idara ya Kimataifa na Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.
Balozi wa Tanzania nchini China Ramadhan Omari Mapuri akizungumza na vijana kutoka Tanzania wakati wa hafla maalum ya kuwakaribisha iliyoandaliwa na Makamu wa rais Umoja wa Vijana wa China Bw. Lu Yongzheng jijini Beijing.

Mfanyakazi wa kituo cha makumbusho cha Beijing (Beijing Planning Exhibition hall) Bi. Cindy Wang akitoa ufafanuzi kwa kundi la vijana kutoka Tanzania kuhusu historia ya kale ya mji wa Beijing.Takribani vijana wapatao 50 wako nchini China kwenye ziara ya mafunzo kufuatia mwaliko wa rais wa nchi hiyo Hu Ji ntao alioutoa kwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete Februari mwaka huu.
Hili ni eneo la mbele yalipokuwa makazi ya kifalme nchini China. Hapa wanaonekana wenyeji na wageni mbalimbali wakimiminika kwa wingi kutembelea eneo la makumbusho linalojulkana kama Forbidden City ambalo enzi za utawala wa kifalme haikuruhusiwa kwa mtu yeyote kuingia. picha na mdau aaron msigwa wa maelezo





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. New YorkerJuly 21, 2009

    Hala Hala Vijana, U-china siyo New York. Kazi za "BOX" huko hakuna.

    So that "mkijilipua tu" huko mjue ndo "mmelipuka kiukweli"

    Maana wao wenyewe wana njaa balaa.

    Hivyo malizeni ziara yenu muwahi kurudi nyumbani mkaijenge nchi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2009

    'Missing' footballers prompt new entry rules

    The disappearance of five Tanzanian youth footballers has prompted the Swedish Migration Board (Migrationsverket) to tighten entry requirements for non-European players in the Gothia Cup, the world's largest youth football tournament.
    Migration Board bans 'racist' lawyer (15 Jul 09)
    Sweden U-21 coach faces ban after halftime Balkan row (25 Jun 09)
    Swedish football: A beginner’s guide to the Allsvenskan (2 Apr 09)
    Online football betting by www.bwin.com
    The event is held every July in Heden, outside of Gothenburg in western Sweden, and features 1600 teams from 60 nations.

    Starting in 2011, players will be required to provide a fingerprint in order to receive an entry permit to Sweden, reported Göteborgs-Posten (GP) newspaper.

    The Migration Board wants to make it more difficult for players to drop out of the tournament and seek asylum under false pretenses.

    Fingerprints make it easier to recognize individuals who apply for asylum elsewhere in Sweden or in other Schengen countries.

    Five players from Tanzania disappeared after this year's tournament. As of Monday, none of them had file asylum claims.

    But Leif Andersson of Migrationsverket in Gothenburg says that most defectors wait awhile before applying for asylum. That makes it less likely that the Migration Board will be able to make a connection between the applicant and the Gothia Cup, reported GP.

    The five who disappeared are born between 1990 and 1993 and all played for the same team. According to Nils Lundqvist, police inspector at in Gothenburg, it's not uncommon for players to disappear in the wake of the tournament.

    “It's a common occurrence after Gothia. Every year, we have young people who disappear. There are always a handful, most often from African countries, who take off,” he told GP.

    Lundquist told GP that last year, an entire team from Libya disappeared. In another case, a number of Tanzanian girls left their team in 2002. Four years later, two of them were found working as prostitutes in Gothenburg.

    Source: http://www.thelocal.se/20810/20090721/

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2009

    Vijana hawa walipatikanaje patikanaje? wanatoka sehemu gani au katika jumuia gani? jee ni wamechaguliwa kwa kuzingatia nini hasa? je kuna watoto wa walala hoi katika msafara huo mzima?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2009

    Yani weee hapo juu unaakili sanaaaaaa mm mwenyewe najiuliza hawa vijana 50 ni wengi kweli walipatikanaje vigezo gani vilitumika maana tumeshangaa watu wapo china tupo Tz hatujasikia hii habari hata kutangazwa nafasi hizi
    Bongo tambarare kweli

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2009

    Hebu acheni kulalamika eti ni mchongo wa watoto wa matajiri kwenda China.

    Kwa kuwangalia tuu hao vijana unaona kuna shape za Masaki na Oysterbay hapo? angalia tuu walivyo ,utajua ni watoto wa walala hoi tuu hapo , hakuna wa geti .Tena inaonyeshe wengi ao ni wa vijijini , angalia mavazi yao.

    ReplyDelete
  6. wewe hapo juu hacha kujaji mtu kwa mavazi yalikuwa ya long time ago siku mtoto wa masaki wala pugu huwezi jua mpaka akwambie la sivyo utaumbuka kitu mandodo na ugali fish utamtaka mavazi ni pambo tu kama ilivyo pambo lingine na siku hizi simple pamba tu kwa kwenda mbele soma nyakati, jibu swali kama huwezi kaa kimya. uko china sasa hivi ni bonge la joto hakuna mfano.ni hayo tu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2009

    sioni vijana wa visiwani hapo, selection inanipa mashaka na kama wapo basi tuupongeze muungano.

    ndugu yangu usihoji kwa nini huoni watoto wa walalahoi katika ziara, si unaelewa kua mwenye kisu kikali ndie anekula nyama.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...