. Mdau Aron Msigwa (wa pili kulia, ambaye ndiye anayetuletea taswira hizi) akiwa na vijana wengine kutoka Tanzania ndani ya Beijing Language and Culture University, China.
Khalfa Abdalla Ali ambaye ni Katibu mkuu Vijana CUF katika Chuo Kikuu cha Zanzibar akiwa miongoni wa vijana walioko ziarani China kutoka TZ alipata bahati ya kuiadhimisha siku yake ya kuzaliwa “ Birthday” kwa mara ya kwanza nje ya nchi ndani ya Beijing Language and Culture University.
Hili ni eneo la Ukuta mkuu “The Great Wall” ambalo ni miongoni mwa maajabu saba ya dunia eneo ambalo huvutia watalii wengi kutoka pande zote za dunia ambao huja kushushudia ustadi mkubwa uliotumika katika kujenga eneo hilo na pia mandhari nzuri.
Vijana katika picha ya pamoja nje ya uwanja wa Olimpiki ya mwaka 2008 Beijing
kutoka nchini Tanzania walio katika ziara ya mafunzo ya siku 10 nchini China wakiwa na wenyeji wao wakiendelea kupata utangulizi kuhusu historian na kazi zinazofanywa na chuo hicho ndani ya chumba cha mikutano katika Chuo Kikuu cha Lugha na Utamaduni cha mjini Beijing. Chuo hicho kinaongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi kutoka mataifa mbalimbali.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2009

    Nauliza tena maana sikujibiwa hapo awali. hawa vijana walichaguliwa chaguliwaje? ni vigezo gani vilitumika kuchagua vijana hawa? au ilikuwa ni kujuana tu? jee ni kutoka katika kundi fulani tu? jee wanatoka katika mikoa tafauti ya tanzania? jee kama wamechaguliwa kisiasa jee wametoka katika vyama mbali mbali vilivyo halali tanzania? na mwisho kabisa jee watoto wa walala hoi wamo katika msafara huo? asanteni.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2009

    wanaweza wakawa wote ni ndugu, cousins, and friends si unajua tena TZ undugu kwanza! halafu wanawake wa bongo kwa kanga hawaziachi nyuma! hata china?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2009

    annon #1

    najiuliza pia...

    sielewi hii blogu mbona huwa haijibu maswali ya msingi kama haya,ilhali ndio imeleta hii newz sijui wanafikiri ni cartoon tunavotaka maelezo km hayo?

    michuzi vipi?sema ata km umefatilia au unafatilia au hawajakupa majibu kwa sababu zao.

    uhuru wa habari mfinyu sana bongo

    lol

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2009

    maskini hawa vijana wa kitanzania wanaonekana kabisa wametoka kwenye umaskini hawana hata camera,nimeona vijana kutoka uk au us ambao nao wamekuja huko,yaani karibu kila mtu ana nondos kama zako bwana michuzi za kuchukua kumbukumbu,all in all i thing they both enjoyed the tour

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2009

    ingekuwa hiyo ni bongo basi ingefungiwa kuingia,walipa kodi wangeingalia kwa nje kama mnazimmoja

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2009

    JIBU kwako anoni uliyeuliza swali katika first comment hapo juu.
    JIBU SAHIHI
    Hapana, walalahoi si sehemu ya vijana hawa. wote ni watoto watokao kwenye familia zenye mtandao mzuri na mpana mawizarani. uchaguzi wa vijana uliegemea zaidi kwenye vimemo vilivyotokana na vijana wengi watoto wa wajulikanao kuomba kuwemo kwenye msafara.
    pia katika kundi hilo wamo vijana wafanyakazi katika idara mbalimbali wizarani.
    ni aina fulani ya bahati ya kiutalii ambayo raisi wa china aliitoa kwa vijana hawa. haikuhitaji mchakato kuwapata!!
    ahsante

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2009

    Nakumbuka wimbo wa Mr NICE - kila mtu na demu waaaaake!! picha namba 1. waosha vinywa munasemaje?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2009

    wanaoitwa Vijana kula China ukiwaona kwenye picha ukawalinganisha na vija wetu wa kutoka bongo wa huko china wanafaa kuitwa watoto, lakini wasikilize akili kunkichwa

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2009

    Wewe Anonymous wa Kwanza..hapo hakuna watoto wa walala hoi. Ngoma kama hizi lazima uwe na connection au God father akupigie pande.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 24, 2009

    harufu ya upendeleo...

    mweeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...