Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. wabongo tupeni kisiwa chetu yakhee...

    ReplyDelete
  2. sawa ni katuni na wacha iwe na madhumuni ya kuchekesha tu, lakini haitoi ujumbe sahihi

    ReplyDelete
  3. Bwana Mpangala. ahsante kwa mchoro wako mzuri ambao umeukusudia kudipict hali ya muungano tuliyonayo.
    Lakini mchoro wako mzuri upo mbali sanaaa na ukweli wa muungano tuliokuwa nao hivi sasa.
    In short mchoro wako unaonesha kuwepo na usawa katika muungano na hiyo sio hali inayokubalika.mchoro wako unapotosha ukweli uliopo.
    Ukweli ni kwamba Muungano tulionao umejengeka katika misingi ya kuikandamiza pande moja ambayo ni Zanzibar,kisiasa,kiuchumi na kijamii.
    Tanganyika ni nchi iliyoneemeka kuwa na utajiri mkubwa sana wa madini.lakini madini hayo hayajawahi kuineemesha Zanzibar ,ikiwa kama ni pande moja ya huo muungano.Watanganyika wenyewe walio wengi wamekuwa hawanufaiki na neema hiyo seuze Zanzibar.Aidha haikuwahi kusemwa kuwa Neema hii ni ya muungano hivyo Zanzibar nao ni lazima wapewe fungu lao.hilo kwa ufupi halikuwahi kutokea.
    Sasa Iweje neema ya mafuta na gesi inayotegemewa kupatikana huko Zanzibar iwe ya muungano?kwa misingi ipi?
    Wanaosisitiza kuwa Mafuta ya Zanzibar ni ya muungano wanatakiwa waueleweshe umma ni vipi Zanzibar imekuwa ikineemeka na madini ya Tanganyika tokea huko nyuma ambapo wanasema suala hili limeingizwa katika mambo ya muungano.
    Kabla ya Watanganyika kupigia makelele suala la mafuta ya zanzibar kuwa ni ya muungano ,wanatakiwa wawaulize viongozi wao ni lini Mtanganyika ataanza kuona neema ya madini yaliojaa nchi nzima.
    Kwa uchambuzi mdogo tu mtu mwenye akili timamu anaoweza kuufanya ,atagundua kuwa Viongozi wa Tanganyika wamefeli vibaya sana kuwapatia raia zao haki na neema inayotokana na madini.Raia tumekuwa tukishuhudia viongozi kadhaa kuimiliki migodi kama mali yao binafsi.
    Raia tumekuwa tukiishuhudia serikali kuaandaa mikataba mibovu ambayo mbali na kutowa mwanya kwa mashirika ya nje kujineemesha kupitia madini yetu lakini pia huandaa mikataba amabayo humkandamiza raia wa chini.
    Hadi hii leo Raia tunashuhudia kuwepo na mambo mengi yanayohitaji kusawazishwa kuhusiana na mikataba ya madini.
    Madini kwa mtanganyika yamekuwa ni nakama badala ya kuwa neema kwake.
    sasa kwa kuyazingatia hayo machache tu ni vipi Wazanzibari wawe tayari kuchukuwa mafuta na gesi yao na kuwakabidhi hawa viongozi walafi na wizi wa mali ya umma?
    Kwa hali iliyofikiwa sasa huko visiwani,ibainike kuwa vijana wa kizanzibari wako hata kumwaga damu zao ili kuhakikisha neema hii ya mafuta na gesi haiendi mikononi mwa wizi na walafi ambao wamekuwa wakikuza matumbo yao kwa kutumia rasilimali ya nchi.
    Mafuta na gesi yataendelea kuwa ni masuala ya zanzibar na kuwanufaisha wazanzibari Daima.
    Watanzania tuamkeeeeeeee hii ni karne ya 21.

    ReplyDelete
  4. HONGERA PINDA WAPE UKWELI,MUUNGANO HUU HAUTUFAI KILA MOJA ACHUKUE CHAKE IKUMBUKWE WENGINE HAWAJUI SERIKALI YA MUUNGANO INAGHARAMIA NINI??? KWA ZANZIBAR MAFUTA YENYEWE HAYAJAPATIKANA TUNAANZA KUTISHANA JE YAKIPATIKANA???MIMI SIKUZOTE NASEMA KUWA IKIPIGWA KULA ZA WATANZANIA BARA NA ZANZIBAR ASILIMIA 95% HAWAUTAKI MUUNGANO HATA MIMI KWA KWELI KAMA RAIA WA BARA SIUTAKI KABISA HAUNA MANUFAA ZAIDI YA MANENO TU MENGI LEO HIKI KESHO HILI NA CHUKI TU INAENDELEA KUPANDWA,ZANZIBAR NI NDOGO KULIKO HATA WILAYA YA BAGAMOYO KWA UKUBWA LAKINI NAFASI YAKE KATIKA MATUMIZI YA MUUNGANO NAFIKIRI INAZIDI HATA MKOA WA MWANZA WENYE WATU WENGI KULIKO ZANZIBAR.NINAWAOMBA HAO VIONGOZI WA SERIKALI YA TANZANIA KUITISHA KULA YA MAONI NA KUACHANA NA HUU MUUNGANO,HAUNA MAANA KABISA KABISA.NA HAUTUSAIDII MBONA WALE WALIOJIONDOA KWENYE MUUNGANO WA SJIRIKISHO LA SOVIET UNION WANAENDELEA KUSIHI TU,SEMBUSE ZANZIBAR????? INA NINI CHA AJABUWAACHENI WAJIENDESHEE MAISHA YAO NA BARA WAJIENDESHEE MAISHA YAO VILE VILE

    ReplyDelete
  5. Kwa taarifa ya wengi humu, wazanzibari tukiitana yakhe tunakusudia kumaainisha ya-akhii ikiwa na maana ya ewe ndugu yangu. hata hivyo tukimuita mbongo au mtanzania bara yakhe huwa tunamaanisha maana nyengine ambayo siwezi kuisema hapa kwa kuhofia brother michuzi kutoitowa post hii. kwa hiyo mchoraji kicheko ni cha kwako kwani wazanzibari tunacheka kwa kuweka katuni ya mzanzibari akimwita mbongo yakhe. ha ha ha ha ha toba mbavu zangu!!!!

    ReplyDelete
  6. mzanzibar makiniAugust 01, 2009

    aaaaah mchoraji mbona kakosea mbara kamwita mzenji na mzenji kamwita mbara ?

    kawaida wabara huwa na vichwa vya sampuli fulani na pia nywele haieleweki kichwani . ni hapo tu kakosea mchoraji .

    mimi kwa maoni yangu finyu wazanzibari wanaogopa yasije yakatokea yale ya kiwira na masakata mengi yanayoendelea kule tanganyika.

    halafu muheshimiwa pinda inaonekana anajua madhara yapo upande gani ingawa ni nchi mbili ndizo zilizo ungana .

    ukweli usiofichika tanzania inajiendesha kwa kuomba omba kama nchi zote za africa sasa hata zanzibar haitoyumba ukizingatia population yake hata milioni inafika kwa tabu.

    kuna washeli sheli , wa comoro ,mauritius na wenginewo mbona wanajiendesha ? lakini hapa kuna kitu haiwezekani watu milion karibu 40 wasumbuliwe vichwa na watu wasifika hata milion 2.

    kaka michuzi ukiona mawazo yangu yanaharibu hali ya hewa unaweza ku edit kwani yametawaliwa na utani. kazi yako ni nzuri katika jamii.

    ReplyDelete
  7. Lakini huu Muungano huwa haku make sense kabisa. Bara inabidi tuwaachie Wazenji kisiwa chao. Nina uhakika Wazenji ambao wako less than a million watapiga hatua kubwa kivyao vyao kama wakitoka kwenye huu Muungano.

    ReplyDelete
  8. Unajua nikicheki jinsi biashara ya madini inavyowaumiza wananchi wa Tarime, mara wapigwe risasi na polisi, mara vyanzo vyao vya maji 'viwekezwe' tindikali basi naona kabisa kwa nini ndugu zangu wa Zenji hawataki mikono ya wabara kwenye sekta hiyo. Ni dalili ya kutafuta kutengana lakini imesababishwa na mafisadi wa bara.
    Pamoja na hayo ni vema zaidi kutafuta namna za kuendeleza muungano badala ya kuusambaratisha. Sasa hivi ndugu zetu wengi wa kutoka visiwani wanaishi vizuri tu na ndugu zao wa bara, wakifanya biashara zao kwa amani na upendo. Nadhani kila mwanaglobu hapa ameshapata kununua bidhaa "kwa Mpemba". Tunalotakiwa kufanya ni kutumia bunge kuwasilisha hoja za nguvu kupambana na mambo ya ovyoovyo. Tusipige kura kwa aliyetupa kapelo au fulana, tupige kura kwa atakayeweza kutuwakilisha bungeni kwa hoja. Tupige kura kwa atakayeifanya serikali itambue kwamba inawajibika kwetu wapiga kura na sio wawekezaji. Vinginevyo tutaendelea kufarakana kwa sababu ya kuwekezwa.

    ReplyDelete
  9. Kwako Anonymous (08.43.00 am)
    Hatua yako ya kumpa hongera PENDO inaonyesha ufinyu wa mawazo uliokutawala.
    Pendo ni kensa ndani ya muungano.ni mtu aliyetawaliwa na chuki,uhasidi,udini na ufisadi.si mtu anayeitakia mema Taifa la ZANZIBAR hata kidogo.

    Rafiki yangu ulipohoji juu ya wananchi walio wengi wa nchi hii kutokujuwa gharama zinazotumika kuendeshea maendeleo ya ZANZIBAR kupitia serikali ya muungano, ni kweli wananchi wa pande zote mbili hawajui maana HAKUNA CHOCHOTE ZANZIBAR INACHONUFAIKA NACHO KUTOKA KATIKA MUUNGANO.la kama kungekuwepo na chochote basi raia wangefahamu.muungano huu umekuwa ukiinufaisha Tanganyika tu na ndio maana ZANZIBAR imekuwa hauutaki
    huu muungano.

    Suala lako kuwa ZANZIBAR imekuwa ikinufaika kuliko bagamoyo au mkoa wa mwanza.pengine ni kweli hoja yako hiyo lakini kumbuka kuwa Tanganyika ilipoamua kuunda muungano ilikubaliana kuungana na nchi ya ZANZIBAR.hivyo ni lazima ZANZIBAR iwapo kutakuwepo na usawa ndani ya muungano basi itakuwa inanufaika kuliko mikowa mingi tu ya hapa Tanzania bara.
    Iwapo hilo lakunufaika ZANZIBAR zaidi kuliko mwanza au dodoma linakukera basi mshauri Pinda avunje huu muungano kwa kulinda maslahi ya mtanganyika

    Kuna sababu nyingi zinazowafanya watanganyika wasiutake muungano. wazanzibari wanazisapoti sababu za watanganyika hao kwa asilimia mia moja na wanaungano mkono nao katika kuutaka huu muungano uvunjike.

    Lakini kwa upande wa ZANZIBAR wao wamekuwa na sababu pengine tofauti za kutoutaka muungano.
    wazanzibari wanaamini iwapo watakuwa huru kutokana na pingu za huu muungano mbovu basi wataweza kuliendeleza Taifa lao la ZANZIBAR kwa ufanisi zaidi hivyo kuweza kuinuwa maisha ya raia wake.
    Kuwemo ndani ya muungano kumeipelekea ZANZIBAR kurudi nyuma kisiasa,kiuchuni na kijami.
    ZANZIBAR inawaambia maandui wote wa zanzibar kuwa baada ya miaka mingi zanzibar kunyanyaswa,kudhulumiwa na kuonewa chini ya kivuli cha muungano,sasa muda umefika kwa wazanzibari kuikombowa ZANZIBAR yao.


    Wazanzibari wanataka wawe huru ili waweze kuungana na wenziwao kama vile SEYCHELLES,MAURITIUS NA COMORO.
    ikumbukwe kuwa hivi ni visiwa jirani ya ZANZIBAR.licha ya udogo uliokuwa nao visiwa hivi vimekuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi,kisiasa na kijamii kuliko hata nchi kubwa kama Tanzania ambayo imekuwaikijiendesha kwa kupita dunia nzima kuomba misaada.

    IDUMU JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.

    ReplyDelete
  10. shetwani yuleyule wa kujitenga akiingia jamii huwa haiachii, ataendelea kuigawa hadi ndugu wa tumbo moja pia hufikia huyu akasema hiki changu,kile chako. hiyo ndiyo kawaida ya laana hii.
    lakini pia kuna laana ya pili,ambayo inaitwa MAFUTA. hii ikiingia ktk nchi tu,basi ujue na damu huwa haichezi mbali,hasa kama MAFUTA hayo hayamilikiwi na mzungu ktk ardhi yake.
    kwa mwenye akili na aelewe,asomaye na afahamu!maana watu kusikia wanasikia lakini hawaelewi,na kuona wana ona lakini hawatambui!ukiwa nje ya uwanja wa michezo mchezo unauona rahisi sana na makosa unayaona mengi,ila ukiwa mshiriki ktk mchezo mchezo unausikilizia mwilini na hata makosa hayo utayaona ukisha maliza gemu ndipo hujiseme ningejua,lakini jua lenyewe haliwaki!hahaha

    ReplyDelete
  11. NI UKWELI USIOPINGIKA KUWA WAZENJI WAKIJITENGA NA MUUNGANO BASI WATANAGANYIKA TUTAUMBUKA , KWANI WAZENJI WATENEDELA KWA KASI YA AJABU KULIKO WABARA, HII ITACHANGIWA NA IDADI YA WAZENJI,UTAMADUNI.NCHI YA NORWAY INA IDADI NDOGO SANA YA WANANCHI UKILINGANISHA NA PATO.NCHI INAWEZA KUAMUA WATU WASIFANYE KAZI KWA MIEZI KADHAA.KAMA ZENJI BAJETI YAO NI 400 BILIONI, WATU WACHACHE NI DHAHIRI KUWA KAMA MISADA YA NJE IKIWAFIKIWA WAO MOJA KWA MOJA BASI WATAPIGA HATUA KUBWA SANA

    ReplyDelete
  12. Acheni jazba jamani, muungano ni muhimu kwetu sote na hakuna ubishi juu ya hilo, ingawaje kuna kasoro mbalimbali ni budi turekebishe kasoro hizi badala ya kuonyeshana kuwa nani bora. Muungano ukisambaratika yatakayotokea sote tutajuta.

    ReplyDelete
  13. Watanganyika ndio wameonewa hapa.
    Zanzibar kama nchi bado ipo, lakini Tanganyika hakuna tena. Cha tanganyika ni cha Tanzania, lakini cha Zanzibar ni cha Zanzibar. Mi naona ni bora lifanyike jambo moja kati ya haya mawili
    (1) Kuwe na serikali moja tu na serikali ya Zanzibar ivunjwe. Au
    (2) Muungano uvunjiliwe mbali. POTELEA MBALI!.

    ReplyDelete
  14. Kwako Anonymous (08:22:00 pm)
    Baadhi ya mawazo yako ni mazuri tu na ni mawazo yanayoungwa mkono na wananchi walio wengi wa pande zote mbili za muungano.hapa ninazungumzia mawazo yako yanayotaka kuuvunja huu muungano.
    Ukweli utaendelea kubaki kuwa wananchi wa Tanganyika na Zanzibar hawautaki muungano.
    Wachache ambao wanaupigia debe huu muungano ni hawa viongozi wachache walio walafi ambao wameweka maslahi yao binafsi mbele kuliko maslahi ya wananchi wanaowaoongoza.

    Kuhusu wazo lako la pili (kwanza) la kutaka kuivunja serikali ya ZANZIBAR,hili halikubaliki.
    Wazanzibari kamwe hawatakuwa tayari kuifunta nchi yao katika ramani ya dunia.period!!!
    Napenda kukufahamisha kuwa kutokuwepo Taifa la Tanganyika ni kosa na uzembe wao wenyewe watanganyika.
    WAZANZIBARI wamekuwa wakiamini kuwepo serikali tatu ndio suluhisho pekee lakuuokowa huu muungano.
    Hivyo Tunakuomba ufahamukwamba kutokuwepo na serikali ya tanganyika wakulaumiwa ni watanganyika wenyewe.


    IDUMU JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...