mabingwa wa soka nchini dar young africans maarufu kama yanga wakila tizi kwenye ufukwe wa coco beach katika kujiandaa na ligi kuu inayoanza kutimua vumbi mwezi ujao
Home
Unlabelled
yanga wakila tizi coco beach
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Keneth Mkapa ni beki ambayo sijawahi kuona hapo yanga katika kipindi changu cha kufuatilia soka ya bongo kwa karibu,kaka nashauri ungejaribu kutafuta shule za kueleweka za soka ukajiendeleza maana tunapenda kuona watu kama nyinyi mkiwa mnaiongoza soka yetu.
ReplyDeleteDuh Bongo wamebadili ratiba za Soka na kuiga ratiba za ulaya.Ujinga na ulimbukeni wetu wa afrika utaua.
ReplyDeleteHivi hawa FAT wanajua kwa nini ulaya ligi zao zinaanza August na Septemba?
Jamani wenzenu wanafanya vile sababu ya mazingira ya hewa(Climate) ya ulaya.
kweli Shule haiwezi badilisha mtu.hawa viongozi wa FAT na serikali kwa ujumla wameenda shule lakini hawawezi kutumia Elimu yao.
Ndiyo hivyo tulishachelewa kubadilika,wazungu watatupelekesha sana.Siku hizi ni TFF sio FAT!
ReplyDeleteMazoezi gani sasa hayo? Hakuna hata utaratibu unaofuatwa kah! Bongo Tambarare kweli kweli
ReplyDeleteww mbigiri huo ni mfumo ulio dunia nzima na unaendana na kalenda ya FIFA,CAF na hata kama ni kuiga kwani vibaya si tunaia kizuri na pia ww mbonaumeiga kuvaa nguo ww unajua kwanini wazungu wanavaa nguo?Halafu inaonekana kuhusu soka bado uko enzi za FAT inawezekana hadi sasa unajua rais wa TZ ni mzee Mwinyi,nikuhabarishe kuwa siku hizi rais wa TZ ni Kikwete na kwenye soka mambo ya FAT tulishayasahau kuna TFF na kiongozi wake ni Ndg Tenga.
ReplyDeleteUsikurupuke na kuropoka hovyo!!!
we mbigi tff haijaiga ulaya. kama unafuatilia moja ya sera za tenga alipokuwa amgombea urais aliahidi kufanya mabadiliko ili ligi iendane na ratiba za caf. sasa huni kama ilikuwa hailet maana kwa bingwa wa tz apatikane desemba alafu michuano ya afrika inaanza miezi (saba) baadaye?
ReplyDeleteushahidi umeutoa mwenyewe kwamba shule haiwezi badilisha mtu maana kama wewe umeends shule unashindwaje kuona jambo kama hili na lilisemwa sana. nwatu kama wewe ndio maskini wa mawazo kwani kila mkiona jambo mnalinganisha na ulaya
bora nisingesoma maoni yako nikaishia kuangalia rugby ya yanga tu
Mabingwa Yanga. Good Job vijana wa jangwani.
ReplyDeleteYanga wanakwenda na wakati. Hayo ndiyo mazoezi ya mabingwa ,Yanga, (Umoja wa Mataifa).
ReplyDeleteYanga siku hizi inacehza Rugby?/
ReplyDeleteHivi we Anon wa Thu Jul 30, 06:08:00 PM nakuuliza je uliwahi kucheza mpira maishani mwako ama hata cha ndimu tu? Yaani kenneth Mkapa ni mchezaji? Yule jamaa hakuwa mchezaji wala nini. Kwa kifupi Simba na Yanga wamekalia majungu na uchawi tu, na ndio hawa wanaoua mpira wa TZ. Sie Bongo (Taifa Stars) tunapigwa magoli ya kijinga jinga na timu finyu kutokana na hawa wachezaji wa Yanga na Simba wasio na ujizu (hawafundishiki).
ReplyDeleteJamaa wanaiga kila kitu kinachoanzishwa na simba. Simba walianzia mazoezi coco beach na yebo wameiga, walianzisha friends of simba jamaa wakaiga na kuanzisha yanga family (sijui kama bado ipo) walianzisha Taifa kubwa jamaa wakaiga na kujiita umoja wa mataifa, wakisikia mchezaji fulani anataka kusajiliwa wanamkimbilia. Inaonesha pale hakuna wabunifu, wanangojea kijana wa kihindi atoe fedha ndipo mambo yaende asipotoa timu hakuna inachofanya!!!
ReplyDeletenakubaliana kabisa yaani moja kwa moja na mshiriki wa Fri Jul 31, 07:08:00 AM. Hizi Simba na yanga inabidi zife, hizi timu zimepitwa na wakati na hazina chochote cha maana wanachokifanya katika kukuza ama kuendeleza mpira wa TZ. Ebu angalia mpira unaochezwa na hawa jamaa, yaani ndo mpira kweli ule. Yaani kufuatilia mpira wa Yanga na Simba inabidi uwe zoba kweli tena lile zoba lisilokuwa na chembe hata moja ya akili kichwani. Uweni Simba na yanga mtaona mpira wa Bongo unakuwa.
ReplyDeleteYANGA Ni timu ya Mfano Iangalie sasa inaendeshwa ki Profeshino....uwanja unakuja,Hostel ipo,swimming pool ipo,wachezaji wanalipwa vizuri na pia nimesikia wanafatilia HAKI MILIKI YA LOGO yao,Lakini hawa watani wetu MMMMh TAMBARAREEZZ
ReplyDeleteMdau Davie, umeongelea mfano wa kuigwa na kutaja matumizi ni bora ungeongelea pia mapato ili pande zote mbili zikamilike na tujue fedha zinatoka wapi ili na wengine waige. Wataigaje matumizi peke yake?
ReplyDeleteWala mimi kwa hili naona tu TZ kwa nchi za Afrika tuwe wakupigwa tu.Si vilabu si timu ya taifa,,hamna mpila kabisa.Tuko wakufunga Burundi napenyewe kwakubahatisha,hakuna nchi ya ufisadi badae eti soka litaendelea! mpila ni hela sasa hata mishahala yenyewe yawachezaji hata starehe zao hazitoshi,..Ukiwa vijijini utasikia kwenye redio Simba na Yanga,utadhani ni vigoogo,kumbe bado wako kwenye pila wa uchawi tu.
ReplyDeletenakubaliana na baadhi ya wenzangu humu ndani. Ni kweli kabisa kufuatilia mpira wa Yanga na Simba yabidi uwe zoba kichizi. Ule si mpira, mpira gani usiokuwa na tacticts. Tujichezee tu netiboli. Kila mwaka wazee wa yanga wanasema hivi ama wazee wa Simba wanataka hili. Hivi hawa wazee zaidi ya kuleta uchawi vilabuni wanasaidiaje timu kukuza vipaji ama hata tacticts ili mpira uonekane ni mpira?
ReplyDeleteKuna wakati tanzania mpira ulikuwa wa kuvutia na upinzani ulikuwa mkubwa. Hata miaka ya 90 katikati kulikuwa na timu zilizokuwa zinatoa upinzani mkubwa kwa yanga na simba - timu kama sigara, ushirika, pamba - kiwango kilikuwa kikubwa. wachezaji kama hussein marsha, george masatu, athumani china, method mogella etc. walikuwa na kiwango cha kimataifa kama mchezaji yoyote leo ulaya.
ReplyDeleteWengi wenu ni mashabiki wa mpira wa uingereza. Ufundi wa wa Premier League hauna tofauti yoyote, if anything, na mpira wa yanga na simba mwaka 1993-1994 wakati yanga inachukua ubingwa wa EA kule kampala na simba kufikia fainali ya CAF.
Tatizo leo wachezaji hawana motivation ya kuwa masuperstars. Wanalipwa vizuri kuliko wachezaji wa miaka ile lakini hawana ushindani kati yao utakayowasaidia kufikia viwango vya juu. Itachukua muda mpaka kurudi enzi za golden age.