Wanamuziki na wanenguaji wa bendi mpya ya Extra Bongo wakiwa kwenye mazoezi makali ya pamoja kambini kwao kujiandaa na onyesho lao la kwanza tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo, linalofanyika kwenye Ukumbi wa New Msasani jijini Dar leo chini ya Kamarade Ali Choki ambaye baada ya kumaliza mkataba wake na TOT Band sasa ameifufua tena bendi yake na kwa kweli huyu mdau ana kipaji cha aina yake maana extra bongo hii inatisha si kawaida. hakuna mchezo extra bongo, ni kazi tu
vipaji vipya vya extra bongo
nyuzi bin nyuzi za extra bongo mpya




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Tatizo la choki ni tamaa iliyomzidi hapa anaanza vizuri sana baada ya onesho lake la kwanza, na kuonekana na watu atawatelekeza wenzake na yeye kuanza na bendi itakayomlipa dau kubwa. hao wana muziki wake wajiandae kuwa peke yao wasijefikili kuwa wana kamanda!! kamanda wao mwepesi kuongeka!!.

    ReplyDelete
  2. Namuona rafiki yangu Greygory hapo na solo guitar...Greygory tulikuwa pamoja Arusha ..mitaa ya kanisa rd.. enzi za Kurugenzi jazz...wewe na kaka Gerald Nangati ndio mlionipa mwanga wa kupiga guitar pale kanisani... nafurahi kukuona unaendeleza libeneke...wako wapi akina Charles, shabani dogodogo n.k.? nasikia kaka Gerald ametangulia mbele ya haki R.I.P.

    ReplyDelete
  3. mbona akina baba wameficha makwapa yao kulikoni? au akina mama ndio watu wa kuekwa utupu hadharani na kuchezeshwa viuno.
    hata kama ni kutafuta riziki basi kuwe na uwiano...najua wengi litawachoma hili lakini ni lazima tubadike na wanawake wasiwe chombo cha starehe.

    ReplyDelete
  4. Michuzi unapoongelea suala la muziki wa kibongo ndo huu. Ukisikia mtu ana kipaji ni kama hivi kina Choki, Muumin, Banza, Bitchuka, maalim Gurumo, n.k. Haya masuala ya kubatiza miziki ya watu kuwa yetu tuachaneni nayo, Bongo dansi ndo muziki wetu na si Flava.

    ReplyDelete
  5. la wanatia huruma jamani!

    ReplyDelete
  6. sawa choki tunakutakia kila heri ila tatizo wanamziki wa kizazi kipya mkitoa single moja mnanyanyua mabega,nasikia ndio maana komandoo hamza kalala aliimba ule wimbo kuwa eti toka lini ngoma za watoto zikakesha?na toka lini ngozi ya kitimoto ikawambwa ngoma?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...