KWA MBELE
KWA NDANI
KWA NYUMA mdau mwenye kulitaka aje alinunue. Limetoka japan. lina mwezi mmoja Bongo. ni aina ya Hino. Halina tatizo lolote. Limetembea 245,000km tu. Lina engine nyuma, 9880CC. Ni cylinder 6 straight. Lina kiyoyozi, mikanda na milango miwili ya umeme. linauwezo wa kubeba abiria 95. ni maalum kwa usafiri wa mijini (City Bus).
mwenye kuweza kulisimamia kama daladala litamlipa vizuri sana. liko katika hali nzuri sana. Limeshasajiliwa na kodi zote zimelipwa T 451 BAR.
Linauzwa 53M/- Tsh.
maelewano kidogo yapo.
mwenye kulitaka anipigie
0713 60 28 00
au
0784 60 28 00.
Asante
JB


Hicho kitu kinapanda mlima ile mbaya ila Mil. 53 kweli mimi sijui.
ReplyDeletekaka mwambie mwenye hilo basi akaliuze ulaya! hayo mahela mengi sansana! labda kama ataliuza sh. mil kumi hivi! si mtumba? au? alafu tena litakuwa la kichina! alama yake kubwa kelele kama simu zao
ReplyDeletewe acha kutuingiza mjini kaka, hii dunia ndogo sana siku hizi. nipe dola 25,000 nikuletee gari kama hilo. acha wizzi
ReplyDeleteDola elf 25 ni sawa na Tsh ngapi?
ReplyDeleteBro Michu, tangazo kama hilo ni kiasi gani kwenye blog ya jamii? Maana na mimi nina uza Bajaj, Vipanya na gari ndogo nyingiiiiiiiiii
Milango wa umeme ni hatari sana hiyo.
ReplyDeletehilo bac na baraX2 za hapa bongo,foleni plus hiyo bei naona kama unaumiza saana.
ReplyDeletekuwa city bus ni hasara kwani itakuchukua hadi miaka 30 kuweza kukaribia kurejesha hiyo 53M.
ila Mola akujaalie upate mteja na ikishindikana bac fanyia kazi wewe mwenyewe.teh teh
Abiria 95? mbona kazi? straphangers rider kufa hatufi cha moto tunakiona
ReplyDeleteAbiria 95? Embu anaglia seat arrangement yake then utakubali 95, yaani 20 wa kukaa afu 75 wakusimama, si bisbis hzo na pick poket
ReplyDeletemichu umebana comment yangu, dongo nini? powa kuhusu milango ya umeme sio tatizo ila sisi wabongo ndio washamba....
ReplyDeletekwa siku hesabu alfu 40 hadi 60..!!? hapo halijaharibika kwa bei ya milioni 53 ni sawa na kupaka rangi upepo!!!
ReplyDeleteMmmh, Shughuli! Haya yetu macho!
ReplyDeleteTutaendelea kufa tu kwa ajali zisizokuwa na sababu. Hii basi in uwezo wa kubeba abiria 20 hivi. Ndo sababu ina seats kumi upande mmoja na kumi au nane au tisa upande mwingine. Sasa hao wengine wanakaa wapi? au kuna seat zingine kwenye keria, na keria yenyewe siioni. Kudadeki Bongo. Yaani jamaa anataka kututapeli na picha ipo, jee kama angelikuwa anauza mbuzi kwenye gunia ingelikuwaje?
ReplyDeleteExagerated price, exagerated features, si ajabu ukaenda kuliona ukaambiwa gesi imeisha hivyo AC haifanyi kazi kwa sasa tumemtuma mtu afuate gesi town.
Hapo nimekoma. Wananchi kuweni makini na hizi biashara za bongo, duuuh.
Waugwana, hilo basi lina sifa zote zilizotajwa na nyingine hazijatajwa, hakuna exaggeration hata kidogo. Hino ni kampuni kubwa sana ya magari Japan hususan magari makubwa. kwa bei ya $25,000 uweke na kodi ya TRA (takribani 40% ya hizo $25,000) weka na port charges, gharama za clearing agent, shipping line then utajua kama bei iliyotajwa ni ya kawaida au iko exaggerated! hili ni basi la kusafiri mijini hivyo nafasi kubwa ni ya kusimama sio kukaa. idadi ya abiria (95) ni kwa mujibu wa Japan Export Certificate. manake ni kuwa likiwa japan basi hili linaweza kubeba mpaka abiria 95. nasikia kwa wenye kuyasimamia vizuri hesabu ya kutwa ni kati ya 120,000-160,000 kutegemea na bei za mafuta na shurba nyingine za barabrani...JB
ReplyDeleteAcha kudanganya wananchi ww Anon wa01:30 nipo Japan kwa muda sasa sijaona msongamano wa abiria kwenye mabasi wa kufikia angalau watu 50. Sasa hili basi la kubeba watu 95 sijui lipo wapi katika Japan pengine kwenye makumbusho!
ReplyDelete