FAMILIA YA DAVID SOWA MGWASSA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MPENDWA BABA YAO, MZEE DAVID ELIYA MGWASSA, KILICHOTOKEA LEO MCHANA KATIKA HOSPITALI YA TMJ JIJINI DAR.
MAREHEMU, AMBAYE NI BABA MZAZI WA DAVID SOWA MGWASA WA TANZANIA BREWERIES LIMITED, NI MKURUGENZI MSTAAFU WA JIJI LA DAR ES SALAAM NA PIA MKURUGENZI MSTAAFU WA MANISPAA YA DODOMA.
MSIBA UPO NYUMBANI KWAKE MAREHEMU KIJITONYAMA NYUMA YA SAMOYAZA CAR MART, AMA USONI PA KIJITONYAMA MAGHOROFANI JIJINI DAR ES SALAAM.
MWILI WA MAREHEMU UTAAGWA RASMI HAPO NYUMBANI KIJITONYAMA SIKU YA ALHAMISI AGOSTI 27, 2009 SAA SABA MCHANA.
SISI TULIMPENDA, BWANA ALIMPENDA ZAIDI NA KUMTWAA. MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
AMINA



Naomba nitumie fursa hii kumpa pole mdogo wangu David pamoja na wanafamiia wote kwa msiba wa mzee wetu -Mzee David Mgwasa. Mzee huyu alikuwa mwalimu wangu wa somo la Office Management miaka ya 1972 hadi 1975, Mzumbe IDM. Alikuwa mwalimu wetu ambaye sisi kwa kweli alitupatia misingi mizuri ya utawala wa umma. Walimu wengine wakati huo walikuwa ni mheshimiwa Jackson Makwetta Mbunge wa Njombe Kaskazini, akina marehemu Patrick Sostehenes Kalanje, Costantine Kazi, AJ Fernandes na kadhalika chini ya Mkuu wa Chuo Mwalimu CJ Omari.
ReplyDeleteMzee Mgwasa tulikuwa tunampenda sana sisi tuliokuwa wanafunzi wake wakati ule. Ninakumbuka miaka ile tukiwa wanafunzi wa Public Administration tulikuwa tunatayarishwa ili tuje kuwa Mabwana Shauri (District Officers) kwa mfumo wa wakati ule wa Serikali. Style yake ya kufundisha ilikuwa ambayo "was practically oriented". Yaani mafunzo yake yalijikita katika mazingira halisi ya kikazi ambayo tungeenda kukutana nayo. Kuna angalizo moja ambalo aliwahi kutufundisha mimi mpaka leo, miaka 37 baadaye bado ninakumbuka. Alituambia 'msije mkafanya makosa ya kuidhinisha malipo bila ya kuisoma payment voucher kwa makini kwa kuilinganisha na dokezo (minute) husika kama ipo. Hususan usikubali kuidhinisha na kuisaini pale ambapo karani au mhasibu anakufuata ukiwa uko nje ya ofisi unataka kuingia ndani ya gari ukiwa mkao wa haraka kuondoka. Mwambie akusubiri mpaka utakaporudi ofisini kwako ndipo akuletee. Ukifanya kosa na ukaisaini huwezi kujua kama ni malipo halali kwa hiyo watch out msije mkaingia mkenge'. Mzee alitufanya tulipende sana somo lake la Office Management. Kwa vile alikuwa analimudu kisawasawa.
Lazima niseme I have always been proud na Mwalimu Mgwasa. Siku zote ambapo nilipokutana baadaye sasa nikiwa mtu mzima I have always adressed him "Mwalimu". Kwa kweli Mzee Mgwasa was like a father to many of us tulipokuwa chuoni. When I recall IDM of Mzumbe and not the current university I can not help but become nostalgic about it. Kama wanavyosema "enzi hizo zilikuwa nzuri jamani". Mwalimu Mgwasa tutakukumbuka daima.
Namuomba Mungu Mwenyezi Ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi. Na wana familia wote nawaomba muwe na subira kipindi chote cha majonzi. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe. Amen and Amen.
Munga ailaze roho yake mahali pema peponi
ReplyDeleteMichuzi kuna makosa kwenye hili tangazo aliyekufa jina lake sio lilioandikwa kama hayati
ReplyDelete