Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. michuzi zadisha sauti ya taarab bana

    ReplyDelete
  2. Mustakabali wa nchi hii Mungu anaufahamu maana kwa hali hii tutachinjwa wengi tangu lini dereva agome kisa traffic amemkamata akitokea fichoni? hivi hii inaingia kichwani kweli na hao waliokufa katika ajali ya Mohammed Trans mustakabali wa waliowaacha nyuma inakuwaje? nashauri leseni zianze kugawiwa upya maana hata hao madereva kwenye hiyo filamu sidhani kama wako fit to drive hasa huyo wa pili anaonekana anatumia mihadarati kabisa!

    ReplyDelete
  3. kama hawa ndio madreva bac tumekwisha yaani jambazi anampangia mlinzi namna ya kufanya kazi ili kwamba wakimwona trafiki wapunguze mwendo ambapo hamna trafiki wafanye wanavyotaka. Mimi niko uk huku wakati mwingine police wanajificha hivyohivyo. Kama dreva unatakiwa kufuata sheria za barabani wakati wote police ajifiche au la wewe fuata sheria. mimi mabasi ya bongo nimepanda sana naona dreva wetu hawajui sheria na alama za barabarani maana wakati mwingine unaona alama zinakataza kuovateki yeye anaovateki

    ReplyDelete
  4. Hapa pande zote zina walakini ila upande wa serikali umezidi. Ni kweli ajali nyingi zinsababishwa na uzembe, ila huwezi kulalamikia kuwa tunda ni chungu wakati shina ulihudumia kwa kulilisha shubili. Hapa serikali inatakiwa ishughulikia chanzo na si ugonjwa.

    1. Uzembe wa madereva: sababu kubwa ni utoaji wa leseni, nani anatoa leseni?, hao traffic kwa kupokea rushwa na ukifuata taratibu hasa utazunguushwa wewe hata kama umequalify. Hili ndiyo tatizo.

    2. Mahakama biased(zinanuka rushwa): Mfumo wetu wa sheria hautoa haki sawa, Chenge aligonga bajaj kaua wawili tokea mwezi wa tatu, kesi hata kusikilizwa haijaanza, dereva wa basi tairi limechomoka(siyo fault yake/ ni mechanical faulty) hata mwezi haujapita kesi imeisha kapata mvua 30 wapi haki?. Serikali na vyombo vyake wanatakiwa waonekane kuwa wapo kwa ajili wa watanzania wote na si kwa baadhi ya watanzania/ sheria ni msumeno isiangalie sura wala wadhifa. hapo tutajenga imani ya serikali kwa wananchi

    3. Traffic waache kucheza mchezo wa Tom & Jerry barabarani (Kuvizia magari yanayofanya kosa ili wapate rushwa). Traffic wanafanya mabasi kuwa miradi yao, kama suala ni kudhibiti ajali wawe peupe ili madereva wawaone na kujenga nidhamu barabarani, siyo kujificha na kuvizia makosa ili wapate rushwa. Je unapojificha dereva akifanya kosa kabla hujamkamata akasababisha vifo kwa ajali ni nani wa kulaumiwa?(ni wote).

    4. Tanzania overhaul ya utendaji, hatuwezi kuendelea kwa style ya sasa. Kama walivyopania kutoa onyo kwa kumfunga dereva aliyechomokewa tairi miaka 30 vivo hivyo wawachukulie hatua matraffic na watendaji wote wasiofanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi. Yaani rushwa na kujuana wanaweka mbele

    ReplyDelete
  5. Wote bangi hao watatuchinja sana hawaelewi hata tatizo nini,serikali ianzishe program nzuri ya madereva,(wapimwe,waelimishwe,hao bangi wafungiwe kuendesha.

    ReplyDelete
  6. Hadi sasa sijaelewa chnzo cha huo mgomo wao wanagoma kwa ajili ya matrafiki au mwenzao kafungwa miaka 30?Kama trafic kujificha mm naona sawa na asilimia kubwa ya matrafiki wa tochi wanakaa sehemu zenye vibao vya speed limit kwa hiyo kama kukamatwa ni haki yao kibao kinaelekeza mwisho speed 50 ww unakamua hadi jiti hapo hakuna msamaha.

    ReplyDelete
  7. TATIZO LA MADEREVA WENGI HAPO WANADHANI KUENDESHA GARI NI KUJUA KUWEKA GIA NA KUKANYAGA MOTO TU GARI LIENDE, MIMI NAONA LESENI ZAO ZIKAGULIWE UPYA NA WAFANYE MITIHANI UPYA HATA KWA FREE ILIMRADI TUPATE MADEREVA WANAOJUA NA KUIWEZA KAZI,, PIA HATA USAFI ONA HUYO HATA HIYO MIDEVU HANYOI!!

    ReplyDelete
  8. Michuzi na wewe nawe umejichokea yaani hapo ukiondoa huyo Mwenyekiti peke yake basi lakini wengine wote hamna kitu na kama madereva wenyewe wa mabasi tena ya safari ndefu ndio hawa basi Tanzania tumekwisha woooooote asubuhi yote hiyo watu wapo chicha mbaya (WAMELEWA) sasa unategemea kama ndio anapewa basi kwenda safari si ndio mwanzo wa kuwatumbukiza watu mto wami pale.

    Serikali sasa hivi inabidi iangalie na kutilia mkazo kilevi kwa waendesha magari wote kwa ujumla yaani kama mm ni independent inspector kwa haraka najua kabisa ajali aliyosababisha mwenzao inaweza kwa kiasi kikubwa ikawa ilisababishwa na ULEVI na ushahidi tumeuona kwa hao uliowahoji.

    Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake

    ReplyDelete
  9. Wanataka traffic waonekane ili wasifanye maovu yao?

    Its everywhere ktk hii dunia especially nchi zilizoendelea kama USA...Traffic hujificha na kupima kama mtu ana-speed au kufanya foul yeyote.

    Hao Madereva waache hujinga, ndio mana Ditopile aliwa-shoot. Mimi napata sana tabu kuendesha gari kwasababu za madereva wajinga kama hao.

    I thnk its a great idea for cops(police) to hide and monitor the rough drivers. we are tired of them. A government should have a stand, not to listen to everythng that a citizen wants...like this issue it doesnt make sense(they complain because cops are hiding??? thats stupid)...

    Police wajifiche ili wakamate madereva waovu...ajari zimezidi sana Tanzania.

    ReplyDelete
  10. Hao madereva mapumbavu kweli. Waambie waje huku Virginia halafu waspeed hivyo waone ilivyo rahisi kuingia jela marekani, mimi nilishalipa reckless driving by speeding $ 1500 na polisi alikuwa kajifisha kwenye shimo nilikuwa ninawahi airport.Madai yao ni baseless na ya kitoto yaliyojaa pombe na bangi yaani wewe unamwambia baba ako awe analala mapema ili utoke kwenda disko?? shame on you drivers

    ReplyDelete
  11. Kweli bado kuna kazi kubwa. SUMATRA MPO?

    ReplyDelete
  12. Michuzi hawa jamaani ni washenzi kweli, maana wanafanya trafic violation wakijua kwamba wakienda mahakamani is easy doze, they will just pledge guilt and pay 20,000 Tshs only? They must be serious with people's lives, killing 30 people is more than robbery acts. Hizi sheria lazima ziangaliwe upya. Vilevile trafic police must also be serious, haya mambo ya kupokea rushwa wakati watu waangamia kisa njaa jamani uzalendo hakuna kabisa.

    ReplyDelete
  13. kama kungekuwa na uwezekano wa kutembea kwa miguu mpaka mikoani ningefanya kuliko kuendeshwa na walevi
    Hii ni aibu kabisa hawa ndio madereva wetu.
    bora enzi zile za mabasi ya TRC, manake madereva wake walikuwa wazee na wanafuata speed limit kweli kweli

    ReplyDelete
  14. Jehova utusimamie lol

    ila sishangai ni upeo wa akili za watu

    ReplyDelete
  15. Hawa ndiyo watanzania. watanzania wa Nyerere, Karume, Mzee Ruksa, Nkapa, JK, Kingunge, Makamba, Inatisha kuona ufahamu wa watu wetu. Hiyo ndiyo kamati inayojadili na serikali yetu, Hawa ndiyo watu wanaojadili fate ya abiria wapato elfu kumi wanaosafirishwa kila siku, hii ndiyo kamati inayowaamulia nini cha kufanya wamiliki wa mabasi.
    Hivi ni nini hasa?? watanzania tumekumbwa na kitu gani kilichovisha uwezo wetu wa kufikiri. Natamani kurudisha viboko, natamani kumrudisha Sokoine aje atoe siku saba kwa madereva, wamiliki wa magari na matrafiki, natamani kurudisha mabasi ya Relwe, natamani kurudisha TANU youth league, natamani ku-overhaul system nzima. Tunasafari ndefu na ambayo inatisha kweli. I am sorry to say this.

    ReplyDelete
  16. Ndoto ya mchana SwedenAugust 15, 2009

    Mhh Tanzania imeingiliwa maana nikisoma katika ya misitari wanachongea inasikitisha sana.Hawa ndio wanaobeba roho za watu,Serikali ingeanza upya ugawaji wa leseni za kuendesha magari/mabasi.Watu waandike mitihani ya theory na wafanye test ya vitendo inayoeleweka na maafisa ambao sio wachukua rushwa.Labda wazungu wakitusimamia hilo zoezi litakwenda vizuri.Nchi za Ulaya/Scandinavia wako makini sana na kutoa leseni.Kweli masikini hajali maisha yake na ya watu wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...