Kiwanja Kinauzwa kwa Tshs Milion 30.
Kipo Mbweni maeneo ya karibu na shule na Bakili Muluzi na nyumba za NHC Mbweni. Ukubwa wake ni Square Meter 668.
Muuzaji ndiye mmiliki mwenyewe na hakuna mtu wa kati (Dalali).
Kina hati miliki ya miaka 33 na kimelipiwa ada zote mpaka 2008/2009.
Kwa yeyote anaekihitaji tafadhali wasiliana kwa namba
+255-763-475977
Asanteni
Mdau hapo unauza nini maana kwa sheria za TZ ardhi ni mali ya serikali wewe umekodishwa tu kwa miaka hiyo 33!!!!
ReplyDelete21m x 31.8m ni Tsh. 3m au 30m?
ReplyDeleteViliuzwa bei ya kutupa Juzi tukadengua. sasa Angalia bei juu kabisa
ReplyDeletenauliza hicho kiwanja kina huduma zote kama vile maji , umeme nk. pia punguza hiyo bei kwanza ni mbali na mjini pili ni kidogo sana hata mahali pa kuweka kuku wa sikukuu hanna nadhani hiyo ni HIGH DENSITY, nitatoa 15M. UPO HAPO?
ReplyDeleteHii ni HIGH DENSITY subiri miaka mingine 10 ili upate bei hyo.Ukipata zaidi ya 10 million utakuwa na bahati.Mimi ninacho Tegeta Barabarani natafuta 30 leo mwaka unakatika!!!
ReplyDeleteHata kingekuwa na maji na umeme, je kuna barabara ya kwenda huko kwenye kiwanja? Ukiumwa usiku si mpaka ambulance itoje kule mjini kariakoo? Na je, uchafu wa maji ya choo ya jirani utakuwa ukipitia kwenye hicho kiwanja? Njoo Tokyo, Boston, NYC, nk ukitoa pesa hizo kama downpayment utapata nyumba ya kuishi kwa miaka 30 yenye thamani isiyopungua 300,000,000!!! Na kuna vianasa (infrastrature) zote/vyote hapo juu na kadhalika.
ReplyDeleteUmemsikia JK kasemaje, wenye kufikiria kwamba pesa na starehe zinapatikana kwa hivi siku zenu zinakaribia mwisho (au mtazikuta hizo kule mbinguni, alisema heaven)
Ndugu yangu Michu (moderator/six), naomba kutoa hoja!
huko Tokyo Boston, NY ni kwenu????? hebu acheni jamani kutukana nchi yenu, huko mnapopasifia mnanyanyasika kama nini, you will always be second class citizens hata mkioa au kuolewa na hao mnaowasujudia. EAST OR WEST, OUR HOME IS BEST!!!!
ReplyDeleteBongo sasa hivi kuna Real Estate bubble, tunangojea tu ipasuke. Watu wanakaa na kubuni tu bei za viwanja hoping that watapata mtu na kumlalia kwa bei za ajabu ajabu. A high density plot in the outskirts of DSM for 30K USD???? Si ajabu hakuna access ya maji, umeme au hata barabara kwa urahisi, ukinunua kiwanja hicho, inabidi bado ugharamie hayo mazagazaga mengine mwenyewe.
ReplyDeleteThey had a similar unrelialistic Real Estate market in the USA...now the bubble has burst nyumba zinanunuliwa mpaka nusu ya bei zilizokuwa zinauzwa mwaka jana. Wajanja tunasubiri tu hiyo bubble ipasuke ndio tushuke kama tai kununua viwanja bongo.
Mbweni kiwanja kwa sasa ni Tsh.15m kwa ukubwa wa kuanzia 1000sq. mts sasa huyo anaetaka Tsh30m kwa udogo huo anatakiwa akamatwe kwa uhujumu uchumi.
ReplyDeleteHuyo anaesifia NYC, Boston n.k. nadhani amelowea huko siku nyingi. Unafikiri Mbweni hakuna barabara za kufika kwenye nyumba za kuishi? Barabara hadi kwenye viwanja ambavyo havijajengwa zipo kama ulikuwa hufahamu sasa fahamu hivyo. Huwezi kulinganisha maisha ya Mbweni na ya ughaibuni ndugu. Wangapi wameondoka huko? Hizo ambulance zitakuwepo tu kizazi chochote kijacho nakuhakikishia kwa imani. Ukipata watu wenye mawazo kama yako unadhani nchi yao itaendelea kweli? Utabaki kusifia tu nchi za wenzako na kutukana kwenu. Mjenga nchi ni mwananchi.
ReplyDeleteWewe anon - Tarehe Tue Aug 04, 06:07:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
ReplyDeleteHatukatai nyumbani ni nyumbani, lakini ngoja nikufahamishe kidogo kwa mfano hai (miaka ya 70-80 hivi).
Zamani niliandika ombi la kufanya mradi mmoja "proposal" Tanzania. Katika maombi kama hayo, mwombaji anatkiwa achangunue kwa undani anahitaji hela kwa ajili ya nini na nani hadi mradi utakapoisha. Mchangunuo wa vifaa ulikuwa bomba sana, mchanganuo wa fedha zangu za matumizi ndio ilikuwa kiboko "moto wa kuotea karibu". Ilikuwa hivi: Niliomba kupewa malipo ya kutafiti "consultancy/research fee" ya kiasi cha hela za kitanzania, sawa na dola za marekani 980 kwa siku ($980/day). Utafiti wangu nilikuwa ninaufanyia sehemu zinafanana na Babati, Handeni, Manyoni, Gezaulole, nk.
Unajua nini? Nilikosa hiyo grant. Sababu kubwa niliyoambiwa ni kwamba "Mbona nimeomba fedha za malipo ya watu wa Amerika ya Kaskazini, Ulaya au Japani".
Kwa misingi au msingi hiyo/huo ndugu anon uliyeuliza iwapo NYC au Boston ni nyumbani - la hasha - ule mfano wa kununua nyumba sehemu hizo kwa bei ndogo kuliko bei mdau wetu anayotaka kwa kiwanja na si shamba na zaidi sehemu hiyo ni ambapo hakuna maji wala...wala...wala...), ni kitendo cha kushangaza na ninakifananisha na maombi ya ule mradi wangu wa 77 (sio 47). Mfano ule uliotolewa, mimi kwa binafsi nasema uliwekwa katika ufahamisho/maana/misingi (context) hiyo iliyoelezwa hapo.
Mwisho, naomba niseme, hatuwezi kabisa kuendelea iwapo watu wengine wanakaa/watakaa tu wakitegemea wataamka asubuhi na kusema, (alhamdulalahi - waende long room, warudi nyumbani na millio mia moja, million mia mbili))) au nyumba yangu pale mabibo ninaiuza kwa billioni moja ya kimarekani. Watu hao watakuwa wendawazimu, hata kama nyumba hiyo ni hekalu linalofanana na n/land ya MJ/Jacko. Hayo ndio JK ameyakaa amesema watu hao inabidi wajiandae kwenda kula hizo starehe huko "heaven"
Michu baba naomba kutoa hoja
nawaung amkono wote hao wnaosema hicho kiwanja ni overpriced. East west home is best lakini ukweli usemwe. Nchi yetu ni 3rd world country lakini bado kuna vitu watu wala hawajiulizi hii bei ni nani atanunua kweli?
ReplyDeleteUnrealistic minds...ndio huyo aliyenacho anauza sasa hivi kwa mwaka hapati mtu can you figure why?
Hiyo bei nenda Honduras (underdevelopment county) utapata nyumba nzuri tu pembeni ya bahari. {Angalia House hunter international.....}sasa kwanini siye tuwe na bei za ajabu ajabu? Unawauzia watu wanaopata mshahara wa laki 4 kwa mwezi au milioni 7 kwa mwezi hivyo viwanja?
$30,000 unapata kiwanja kizuri sana USA ( sio kwangu) but the truth must be known and told....na kama aliyesema huyo hapo...kama una million 30 ya kiwanja basi you can have a very good house for a down payment of million 30...na the rest can be paid in 30 years....and guess what you pay that much at the same time you live in da house.....sasa hiyo unayoask kwa kiwanja kama sio fisadi ukishatoa saving yote ya million 30 utajennga na nini tena?????......tuache kudanganyana watu ohhhh hizo ndio bei za viwanja sasa hivi Dar...wewe hujafika bongo siku nyingi nini????...kumbe wayu wanaenda na upepo tu ....wao hawavinunui hivyo viwanja kila kukicha kutusakazia tu siye mkizania huku tunaokota hela....tutaishia kununua nyumba hukuhuku na kuishi hukuhuku kama wahindi..... bongo mnalangua langua tu........aghhhhrrrrrrr...acha niwe second class citizen forever huko nje lakini nikija jioni nina kwangu ninakoafford no pressure......manake hiyo kazi ya bongo yakulipa mtu anaunue kiwanja hicho kihalali ni ipi? Na tukishia huku tukikataa kurudi mtatulaumu kweli?
mimi ninachosema ni kwamba hiyo bei ni kubwa sana kwasababu mbweni ni mbali sana na jiji. anyway mtu anaweza kuuliza bei yeyote lakini ni vigumu sana kumpata mtu wa kununua unless huyo mtu ni mjinga sana. hivi ni kwanini real estate companies zetu hazi advertise kwenya magazeti kama wenzetu wa kenya. companies za kenya zimekua zikitoa list ndefu za viwanja au nyumba kila wiki. wamekua wakifanya hivyo toka 2960s it is high time companies zetu zifanye kama za kenya.
ReplyDeletejamani watu mtasema weee lakini labda ni sababu hamjakaa TZ kwa muda mrefu. Hapo utakuta selling price ni 20m au hata 15m lakini kama kawaida lazima mtu aanzie huko juu ili muweze kunegotiate. kwahiyo mwenye nia ya kiwanja na ajitose tu. Ongea na mwenye nacho na nina uhakika bei itashuka tuu. Hii ndio Bongo bwana....
ReplyDeleteWEWE MUUZAJI VIPI! MBONA KIWANJA KINADAIWA ADA YA 2009/10 KWANI HUJUI ADA HUISHIA MWEZI WA SITA? KUWA MKWELI UNAPOUZA KITU.
ReplyDelete30m ni nyingi sana kwa kiwanja hicho maana ni high density kingekuwa na sqm 1500 kuendelea at least. Ila mshkaji hapo anatafuta super profit maana serekali hivyo waliviuza 600,000 mwaka 2003. Halafu badili tangazo lako maana hizo sq meter ulizoziainisha hapo haziendani na tangazo maana hicho ni kiwanja tena cha kawaida sana ambacho serekali ililenga wale low income earners nao waweze kupata, hivyo sii bonge la kiwanja ni kijiwanja.
ReplyDeletemwenye kiwanja hajui ukubwa wa eneo lake ameandika kwa kufuata hati aliyonayo.pia tafuta washauri.
ReplyDeleteHii bei ya ajabu kweli.au ndo kutafuta utajiri
ReplyDeleteMimi ningependa sana kujenga home tatizo ndo hilo hapo juu, who determines the market value of any property in Bongo? Yaani inasikitisha nchi sijui inakwenda wapi, mtu anaamka anauza $9,000corolla ya 1995 na hapo mjep kacheza na odometer kama hana akili nzuri vile,is this real?? Siamini market Value ya bongo iko determined na demand and supply but rather greedness na kutojuwa dunia iko wapi yaani ulimbukeni wa vitu nakutojua nchi nyingine zinafanya nini.... Acha tu niendelee kulipia condo yangu hata Virginia nisipomaliza deni binti yangu atauza itamsomesha shule na bongo nitaendelea kwenda kwa visa.
ReplyDeleteJAMANI MBONA MPAKA SASA NYUMBA NA VIWANJA BONGO VINAUZWA KISIRISIRI NA MADALALI. REAL ESTATE COMPANIES ZIKO WAPI. BADO MAMBO YANAFANYWA KAMA KARNE ZILEEEEE. WATU WAFUNGUE MACHO KUNA BIASHARA HAPO. HAKUNA UBAYA KUPATA USHAURI KUTOKA KWA MAJIRANI ZETU KAMA KENYA KWA VILE WAO NI WATAALAM WA HAYO MAMBO HAPA EAST AFRIKA. TUSIPO FANYA HIVYO MAMBO YATAKUA HAYO HAYO YA WATU KUULIZA BEI ZA AJABU. HIVI SERIKALI INAPATA KODI ZOZOTE KUTOKANA NA UUZAJI KAMA HUU.
ReplyDeleteMnashangaa viwanja vya milion 30 bongo wakati kuna viwanja mpaka vya billioni moja na nusu ufukweni!
ReplyDelete