HABARI ZINASEMA WATU TAKRIBAN 10 WALIOKUWA WAKISAFIRI KATIKA BASI LIITWALO 'JORDAN' AKIWEMO RAIA MMOJA WA KOREA WAMEFARIKI KATIKA AJALI YA BASI KATIKA BARABARA YA ARUSHA-SINGIDA MCHANA HUU.
GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA AJALI HIYO NA ITATOA TAARIFA KAMILI KWA KWADI ZITAVYOPATIKANA
Jamani ufisadi utatumaliza, haya ni matokeo ya utoaji leseni kwa rushwa. Madereva karibu wote wa dala dala za DSM ni vijana wadogo ambao sielewi wamewezaje kupewa leseni Class C na kila mtu anajua wanavyoendesha magari ya abilia kama vile hawakubeba binadamu. Sidhani kama walipata leseni ki halali halafu wakabadilika!! Any way poleni wafiwa na tuunganishe nguvu kupinga ufisadi wa aina zote siku moja tutafanikiwa.
ReplyDeleteHawa watu watatumaliza jamani duh hii mambo ya ajali kila siku sisi tu jamani?ah
ReplyDeleteYale yaleeeee, tuliyosema juzi na jana na kusema barabara zitajengwa zipendeze lakini hawa madereva (nawaita V====I====C===H====A===A) kwa msingi kwamba wanaendelea kuuwa watu wetu. Mungu ibariki Tanzania, tupate idara ya KUTOA LESENI INAYOFUATA TARATIBU ZILIZOPO. Mimi nasema, ipo siku, na hiyo siku, Kambarage ataamka aseme, msitumie tena jina langu kwa kejeli. Kwa nini tupate ajali nyingi Tanzania kwa muda mfupi tuu - tena ajali zenyewe za UZEMBE HIVI? Mimi nalia ninavyoandika ujumbe huu. Sina ndugu katika waliopata ajali, lakini wote ni binadamu na zaidi ya yote ni watanzania wenzangu!! Eee Mungu baba zilaze roho za marehemu pahala pema, na wape nguvu waliopata majeraha. Na haraka, kama Mungu unanisikia wapeleke madereva wote VICHAA kule kuzimu kwenye MOTO wa milele.!!
ReplyDeleteWabunge wetu mpo? Mko wapi? Kemeeni hili kama vile RICHMOND, EPA nk....
Michu mdogo wangu, naomba nitoe hoja yangu yenye chozi zito!!
Kwa mtazamo wangu, nadhani ni bora USALAMA BARABARANI iwe na wizara yake kamili. Kwa sababu, this is too much, and it make me sick! Mimi sielewi mkuu wa hii idara ya usalama barabarani anapata vipi usingizi, huku akijuwa fika kwamba ni wafanyakazi wake ndio wanasababisha hizi ajali kwa kupenda kuneemesha matumbo yao.
ReplyDeleteNa ABIRIA nao wanastahili lawama. Dereva anaendesha kama kichaa, abiria wamekaa kimya huku wakijua kwamba, dereva akibabatizwa kidogo tu au tairi likipasuka dereva hatoweza kucontrol gari na ndio mwisho wao. Cha ajabu ni kwamba wote wamekaa kama WANYAMA wanaopelekwa machinjoni. This is CRAZY, HII HAIHITAJI DARASA. KWA NINI MNAWAACHIA HAWA VICHAA WAENDEELEE NA HUU MCHEZO WA KUPOTEZA MAISHA YA WATU? EBU FIKIRIA, UNAAGA KWAMBA UNASAAFIRI; NDUGU NA JAMAA HAWANA UHAKIKA KAMA UTAFIKA UENDAKO.
SIAMINI KABISA KWAMBA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, NA MKUU WA HIKI KITENGO CHA USALAMA BARABARANI BADO WANAFANYA KAZI SERIKALINI. KWA SABABU HII NI AIBU, HAWATHAMINI MAISHA YA BINADAMU HATA KIDOGO.
ILI KUTATUA HILI TATIZO, INABIDI WATU SERIKALINI WAANZE KUWAJIBISHWA ILI KULETA NIDHAMU. WANANCHI WACHUKUE HATUA ZINAZOSTAHILI PINDI WANAPOONA DEREVA ANAHATARISHA MAISHA YAO. SERIKALI NA MAKAMPUNI YA BIMA WASHIRIKIANE ILI KUWABANA WENYE MAKAMPUNI YA USAFIRISHAJI NA MEDEREVA WABOBU NA WASIO THAMINI MAISHA YA WATU. WAONGEZE BEI YA BIMA ZA MAKAMPUNI YANAYOONGOZA KWA AJALI MARADUFU, AU KUYANYANG'ANYA LESENI ZAO ZA USAFIRISHAJI.
LABDA, NASEMA TENA LABDA HII HALI ITABADILIKA.TUANZE KUFIKIRIA HAWA WATOTO YATIMA NA WAJANE WA WANAOFANYIWA UKATILI NA HIZI AJALI
MIMI NAONA MADEREVA WA ABILIA WAPIMWE AKILI NA MATUMIZI YA MADWA YA KULEVYA NA POMBE KILA MWEZI, UKIKUTWA UNA MATATIZO KATI YA HAYA HIVYO VITU UNANYANYWA LESEN NA USIENDESHE MILELE ILA UKAFANYE KAZI NYINGINE, HAUNA FAINI WALA NINI SASA KAMA NDIO ILIKUWA AJIRA YAKO BASI BORA UWE HAUNA KAZI ILA WATU WAWE HAI, UTAFANYA HATA KAZI NYINGINE TU, KAZI SIO UDEREVA WA MABASI YA ABILIA TU
ReplyDeleteHILO LITAKUWA FUNDISHO KWA WATU WENGINE
ILIIR na RIP marehemu. Poleni saana wafiwa, M. Mungu atawapeni nguvu na subira, inshaallah !
ReplyDeleteMaafa yosoisha, kila kukicha !! : migodini/barabarani/majini.. halafu, sisi ati, ooooh, dereva vichaa/wanaenda kasi/turafiki/barabara mpya/magari mitumba/eneo la korogwe kuna ‘nyonya damu..nk nk..nk!...waaapiiiiiiiiiiiiiii……....mtaishia kulaumu kipanga, mwewe yuwesha kuku!..(ki-kristo : « you are barking up the wrong tree !)
munahangaika na mutahangaika kutafuta chanzo cha matatizo na pia kupendekeza suluhu mujarabu za chanzo..hongereni !!!! kwa lugha nyepesi saaana « haya ni matokeo ya UFISADI..Watu wengi hutumia neno hili kwa wepesi lakini unapolitafautisha na kitu 'RUSHWA' ni kwenye kina na kiini cha matatizo nchi yetu inakutana nayo hasa sasa hivi..huyu ndo mdudu "grand corruption"...maana asili/halisi ya neno ufisadi kiarabu ni 'UHARIBIFU'..nchi yetu siyo ile ile, masikini!..hatuna tulijualo kwenda mbele wala kurudi nyuma..yaani thamani ya maisha ya watu imekuwa ni shs. 1,020,000 (labda za leseni)..kila eneo matatizo…kwa ufupi tuu : serikali yasema mtu hana makosa, lakini eti wamemuonya- kwa lipi ?..maalbino..EWURA wanapiga kelele uongo/kweli na chakachua la mafuta moja kwa mia!..bulk procurement na strategic oil reserve ni story tuu- tumeikalia politiki/kiini macho, shirika la umeme wanakarabati nyumba kwa shs. milioni mia 6, ili wauziane kwa milioni 60! (bungeni leo)- wizi mtupu!...EPA/richmond, zebaki na sumu ziwa victoria tufe vizuri kuanzia wanywa maji na wala samaki (na samaki waliwa hadi Dar, patamu hapo!), nk..nk,,nk.....yameshatokea meeengi..huu ndo wakati wa kuchuma, wakati wa mavuno, tunavuna tulichopanda..tumuombe M. Mungu manusura yake lakini tukae tukijua bila miujiza yake, maafa mengi yapo njiani..lazima kumtazama shetani usoni wakati ma kumlaani- kumkoma nyani, gladi !!. ama sivyo, tumelikoroga..na tutalinywa !!!..kwa uchungu sana !...
RIP
ReplyDeleteMmeshaanza kuua na watalii? Kazi ipo. Watanzania wakiumia kwenye ajali hizi au kupoteza maisha hamna anayejua kusue. watu wanajipeleka hospital wenyewe na hakuna hata anayekuja kuwapa pole...
Hawa watu wa nje hamna mchezo hapo lazima mtu asue hapo..... Sasa hivi watu wataelewa maana ya kufanya biashara za kujali usalama wa watu kwanza kuliko kukimbiza magari ili kuwahi biashara.
Ajali za bongo inasikitisha sana sijui serikali inafanya nini kuhusu hili?