Kitendawili kilichotegwa takriban miaka mitatu iliyopita na aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa jeshi la polisi,Mkoa wa dar es salaam (ACP) Abdallah Zombe na wenzake wanane wameachiwa huru sasa hivi katika mahakama kuu ya Tanzania.
Kwa habari na picha zaidi zinakuja
Tunaheshimu maamuzi ya Mahakama kwa hatua hii, nini tunajifunza au ni kipi kinafuata baada ya kesi hii?
ReplyDeleteMama yangu!! Natamani Mwalimu Nyerere angefufuka leo. Haya ndo mambo ya sheria za bongo. Bongo mambo tambarare babake!!!!!
ReplyDeleteAiaseee hongera sana baba.......................................
ReplyDeleteWacha tuone reactions za Watanzania sasa!!!
ReplyDeletehiyo sio breaking news sababu aliachiwa ditopile mzuzuri, na sasa yuko wapi?
ReplyDeleteDuh?!!!
ReplyDeleteLeo kweli tutakuwa wengi tunajikuta tukiiiga lile tangazo la Tigo kwa jinsi hukumu hii inavyoshangaza...
nilisema, nitalia na sasa wacheni nilie. nikimaliza nifute machozi na kushukuru 'wasomi' wa sheria.
ReplyDeleteDu karibu uswazi mwanangu. akabidhiwe tena ofisi yake
ReplyDeletebongo tambarare, bado mramba na wadau wa epa. kweli wabongo kwa kutoa hukumu nje ya mahakama...sisemi
ReplyDeleteAMAAAA KWELI TANZANIA HATUNA SHERIA
ReplyDeleteMTU AMEUA,ANAACHIWA HURU, BASI HAINA HAJA YA KUWA NA SHERIA.
TUNA MLAAUMU SANA RAISI
WATANZANIA HATUJA KUBALI KABISA NA HILO SWALA
LAKINI MTU AIBE KUKU TU ATAFUGWA MIAKA KIBAO, KAMA HIVYO HAKUNA SABABU YA YULE MTOTO RAMA KUKA GEREZANI
NA YEYE AACHIWE HURU
Hii haijatulia; lazima wanategwa kama Liyumba; kaka tutafutie full transcript ya hii judgement.
ReplyDeleteHuu Mfumo wa kulindana... Mwisho wake utakuwa mbaya!!!
ReplyDeleteArobaini zikifika, kila mwenye duku duku atalitolea kwenye makoo na mali za viongozi.
Mifano ipo Ghana, Gabon, Guinea.. na nchi likuki zilizo shuhudia mapinduzi na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
ilikuwa changa la macho hilo. poleni wafiwa.
ReplyDeleteHii ndiyo serikali ya Tanzania Bwana watu wanazuga zuga tu Dereva wa Mohamed Trans hata mwezi haukuisha kafungwa ilihali ajali huyu jamaa kwa kukusudia huru hureeeeeeeeeeeeeeee na Kikwete weweeeeeeeeeeeeeee ...
ReplyDeleteThis is why our judicial system sucks. We have no hope and it is very embarrassing. Shame on us.
ReplyDeleteMMM KILA SIKU NASEMA HII NDIO TANZANIA ZAIDI UIJUAVYO HAYA SASA KIDUME KATINGA URAIANI
ReplyDeletebro michuzi naona bongo tunapoelekea pabaya kama kweli hawa wakina zombe na wenzake wameachiliwa huru na sheria imewekwa kwa watu maskini Tanzania na ndio maana majambazi yanazidi kuendelea.
ReplyDeleteDuuuuuuuuuuuuuuh,Sasa muda wote walikua wanangoja nini kuwaachiaaaa???
ReplyDeleteAaaaangh!!!
Kisoda2
"Masikini haishiwi NDOTO"
MUNGU WANGU! TUMEKWISHA, YAANI MIJAMBIZI INARUDISHWA KITAANI. KAZI KWELIX2
ReplyDeleteSAFI KABISA, WALA MSIJIDANGANYE KULAUMU HII NDIO SYSTEM YA TANZANIA NI NZURI NA YA HAKI, KWA MAFISADI TUUUU hongera JK
ReplyDeleteNilijua kitu kama hicho kitatokea tu
ReplyDeleteHao waende wakajichimbie mahala, manake hapo nje ya mahakama watu tele wanawasubiri watolewe, sijui wanataka kuwatoa macho au ndio roho zao.
ReplyDeletewanajamii wa blog mie kama cjaamini vile.duu thats life.
ReplyDeletecarlos M
kaka michu ya kweli haya kaka, duh kama ndo hivi maafande watumaliza mtaani hakianani
ReplyDeleteHABARI NDO HIYO....WATANZANIA TUJUE ANGALAU SHERIA KIDOGO..KUA JUKUMU LA KUTHIBITISHA KOSA SIO LA MAHAKAMA NI UPANDE WA MSHTAKA IN THIS CASE POLISI...MAHAKAMA KAZI YAKE NI KWA KUTUMIA USHAIDI HUO (WA POLISI)KUTHIBITISHA "BILA SHAKA YEYOTE" KAMA WATUHUMIWA WALISHIRIKI..NA SIO USHAHIDI WA KIMAZINGIRA (TUME,MAGAZETI ,MA STORY ZA VIJIWENI NK...NK)..TUJIFUNZE WA TZ KUTOKANA NA HILI NA KITU HIKIHIKI TUNAKOSEA KWENYE ISHU ZA UFISADI
ReplyDeleteNAWAKILISHA MDARESELAMA
MIMI SIKUBALII WALA NINI , SIKUBALIIII BWANA MIMI SIKU SIKUBALII HATA KIDOGO, A-A-A-AA MIMI HATAAA SIKUBALII KWANINI HIVI, MMM MIMI SIKUBALI AAAH WAPI SIKUBALIII
ReplyDeleteHii nchi sasa tuwaachie wenyewe! Yaani hapo ni kiinimacho tu! So dissappointing!
ReplyDeleteHivi ni kweliii au naota jamani, naomba mtu aniamshe pls!!!!!
ReplyDeleteDuu!!!!!!!! this is tooooo much!! What a shame!!!!
ReplyDeletesorry to say " siipendi nchi yangu. thanx
ReplyDeleteMwisho wa siku Mungu mwenyewe atashuka kuja kutoa hukumu ya haki, Hakuna mamlaka yoyoduniani inayoweza kutoa hukumu kama ya Mungu, Mimi sishangazwi na hukumu hiyo, kama umeau au haujaua wewe ni nani katika nchi hii? Mungu aaangaliwe wee ni nani bali anaangalia binadamu kwa usawa ule ule bila kuweka Classes. Haya tutayaona zaidi na zaidi hap hap ndani ya bongo. Wadau wenzangu mtakubaliana nami kwamba binadamu wachache wanaoweza kutoa angalau haki kidogo hata kama ni ndogo kama punje ya ulezi. Watanzania mnaiyona hukumu hii? kila mtu atakuwa na dukuduku lake juu ya hili. Napenda mimi mwenyewe Michael J.L niwakilishe
ReplyDeletendio maana wabongo humaliza biashara mapeemaaa wanachukua sheria mkononi basi shughuli nyingine zinaendelea!!!
ReplyDeleteTanzania, Tanzania
ReplyDeleteNakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe ... Read More
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania, Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
wallah kwa niaba ya Wananchi wa Kilombero tunasema hivi HUYU ZOMBE HATUMSAMEHI NA TUTAMCHUKULIA HATUA MIKONONI MWETU LABDA AKAISHI MBINGUNI, SATU!!
ReplyDeleteKama mambo ndio hivi basi elimu ndio jawabu: (http://wachumi.blogspot.com/).
ReplyDeleteDuh..hii ilikuwa bonge ya tamthilia..And they lived happily ever after..
ReplyDeleteTANZANIA HIYO, SISHANGAI KABISA. NAKOSA HATA AMANI. HIYO NCHI BORA NIFIE HUKUHUKU NILIKO. NAMSHUKURU MUNGU KUZALIWA HAPO, LAKINI SITAREJEA NCHI ISIYO NA HAKI, IMEJAA RUSHWA, KUJUANA, WAKUBWA WANA SHERIA MKONONI NK.
ReplyDeleteMwananchi.
............imekaa vizuri hii ndio bongo bwana darisalamu. kudadadeki bonge ya chenga.........
ReplyDeleteKwishneyiii...
Kama kawaida changanya madawa.
Imekaa vipi hii
Hiyo ndio tofauti ya sheria na haki, wameachiwa kwa mujibu wa sheria!!!
ReplyDeleteKila mmoja alijua kuwa mnyonge hana haki tokea siku ya kwanza ya kesi hii. Ufisadi na rushwa vimetawala kila kona ya nchi yetu hata kwenye vyombo vya sheria ambavyo vinawasaidia mafisadi zaidi kuliko wanyonge wenye haki zao na kuishia kudhulumiwa.
ReplyDeleteHongera mahakama kwa kuidhinisha dhuluma dhidi ya wanyonge
NAAAAM!
ReplyDeleteMBINGU NA JESHI LAKE LOTE VIKAMALIZIKA NA HUKUMU PIA IKATOLEWA!
IKAWA ASUBUHI IKAWA JIONI SIKU YA HUKUMU:
ÙˆَÙ…َÙ† ÙŠَعۡÙ…َÙ„ۡ Ù…ِØ«ۡÙ‚َالَ Ø°َرَّØ©ٍ۬ Ø´َرًّ۬ا ÙŠَرَÙ‡ُ
ReplyDeleteThe way I look at it is that the real courtroom is before Him where you will be rewarded for everything you did no matter how small or big
Wakatabahu
Û¥
ndugu zangu , subirini hatima ya albino kanda ya ziwa muone ... ikifuatiwa na baba wa pacha mbili ufukweni alafu muone uwiano
ReplyDeletekang`aaa!!!!Tanzania zaidi uijuavyo !!!
Tufunge safari uchaguzi 2010 hureeeee...
Sikuamini macho yangu hii inauma sana kuachiwa wauwaji wa wazi wazi kabisa. Kwa hilo sidhani kama tutakaa salama. Tume iliyounda ya Jaji Kipenka ilionekana kwamba hao watu waliuwawa na nani sasa kama hao wameachiwa?????????Lakini MUNGU YUPO NA YEYE NDIYE ATATOA HUKUMU YA MWISHO. Poleni sana wafiwa.
ReplyDeletejamani 2010 kweli CCM wabaki? kama mambo ndo haya...katika utaratibu huu napendekeza alex masawe awe raisi,zombe makamu wa raisi waziri mkuu rostam aziz, lowassa akajenge chama imekaaje hii???
ReplyDeleteTATIZO WA TA TUMEZOEA KUWA NA HABARI ZA MAGAZETI NA VIJIWE, Tupate hiyo judgement ndo tuamue, me binafsi namkubali sana judge Masati na ni judge of court of appeal, tuone reasoning ya judge ndo tuamue kama kachemka au la.....kumbukeni pia criminal charges u have to prove beyond reasonab;e doubt.....so watanzania tuache habari za kijiweni na za magazeti, tukome kutuhumu watu wana hatia wakati hawana...shame on you all ambao mnafwatilia habari za vijiweni na hamna data zozote hasa nyie wa TZ mnaojifanya mpo nje ya nchi mnajifanya mnajua wakati hamna LOLOTE
ReplyDeleteMDAU TZ
Next to be free is Liyumba, hii ndo bongo bwana. Wenye nazo wapo juu ya sheria wakati wote
ReplyDeleteaghhhrrrr!!!!
ReplyDeleteALIYESEMA MAJAMBAZI WAMERUDISHWA MITAANI NI KWELI KABISA. KUMBE JAMBAZI MAFIA MKUBWA ANAACHIWA KUJA KUZIDI KUFANYA UFISADI WA UUWAJI. ILA TUSIMUHUKUMU MTU HATUWEZI KUJUWA MOLA NDIO ANAJUWA. KAMA KAFANYA BASI ATALIPWA HAPAPA. PAZI.
ReplyDeleteBwana ametoa na Bwana ametwa,jina la Mungu na lishukuliwe kwa kila jambo.HUKUMU YA MWISHO MTOAJI NI MUNGU PEKE YAKE JAMANI.
ReplyDeleteduuuu jamani kweli serikali inapoelekea pabaya sana na sheria imewekwa kwa watu maskini, babu seya na wanaye wanahatia kifungo cha maisha jela,dereva wa mohamed trans anahatia miaka 30 jela na zombe na wenzake wameuwa kwa makusudi eti hawana hatia na wameachiliwa huru! ivi tunaelekea wapi jamani?ccm inajiwekea wakati mgumu huko mbeleni kwani inaoneana aibu sana na kuongoza nchi wamechoka.
ReplyDeleteZe komedi waliwahi kuigiza hii kesi ya kina Zombe ina mazingaombwe nakumbuka yule mpoki alisema "mi nina mdogo wangu hakufanya mtihani wa form 4 akaenda kwa babu ukatumwa mzinga NECTA mbona matokeo yake yametoka amefaulu kwenda form 5"
ReplyDeleteTUNAPOTEZA MUDA KUFIRI KUNA FISADI ATAONJA JELA TANZANIA,JELA KWA SISI WANYONGE TENA HUKUMU UTOLEWA KATIKA MWEZI MMOJA TU.
ReplyDeletesheria na haki vitu viwili tofauti.
ReplyDeletewewe ulitegemea afungwe yeye alitegemea atoke sasa hapo jipime uko sahihi au?
mimi najionea sawa tu kwakuwa sikuwa naye nilalamike kuwa alikosa, au tunahukumu kwa kukasirishwa na mashtaka? angalia upande A pia angalia upande B yote yawezekana tujenge nchi yetu tusifuate ya mtu mmoja kuna watu milioni 40 wanatutegemea.
WASIOPENDA HAKI WAKO HASI HATA KOMENTI.
ReplyDeleteHIVI HAIFAI ZOMBE ASHINDE?
It’s not hard to see the frustrations of my fellow countrymen/women! And no one can blame them for that because it has been too long and lots of cases have been judged under the same ‘kangaroo court’ and nobody appeared to change something. It's just business as usual!
ReplyDeleteIs it our legal system or people who implement it (or all of them) to be blamed for this? Or maybe our politicians?
This judgment, apart from other things, it clearly shows inconsistency in our legal framework which is allowing some ‘potential criminals’ to slip off the net.
Of course, they say; “you are innocent until proven guilty” but how many times we have seen 'people without power' (normal citizens) became “guilty until proven innocent”?
In my memory of following these ‘high profile cases’ (cases involve big hogs) in Tanzania, the verdict of these cases are always known even before the case started!
Tanzania of today is not the one of 40 years ago! We have lots of so called ‘intellectuals’ in different areas. Most of our today's MPs are graduates and some with the highest level of education qualification, PhD degrees but still we can’t move on in anything! WHY? What's the point of being over proud of a first class degree while you can't make any change to help your suffering people? Something’s wrong somewhere!
I think it’s time for our politicians and intellectuals to do something in our legal framework in order to save it from being perceived 'BIAS' i.e. "it’s only there to serve a ruling class", as it's for the case NOW.
______________________________
Mzee Wauyagauyaga
Huo ndio utawala bora lakini yana mwisho hayo ni damu ya mtu na kama hayana mwisho everythings goes around will comes around leo judge katoa hiyo hukumu kama ni haki hawakuua basi kheri yake na kama wametenda basi malipo kwa mungu.wafiwa sala zenu ni muhimu na mungu ndio anajibu lenu inshaallaah kama hukumu si hapa dunia hata akhera wataikuta huko hakuna wakili mjema wala mjeuri!
ReplyDeleteMichuzi, my experience so far, this is the post that will have fetched more comments than any other ever!! the number of comments will be record breaking, keep a close eye and observe this!!
ReplyDeletesidhani kama huwa michuzi una kawaida ya kurecord topics zinazovunja record kwa kupata responses nyingi kuliko nyingine. ni vizuri ungekuwa unafanya hivyo ni vizuri kwa historia ya blog yako pia. na pia itakuwa vema topic itakayovunja record ya kupata comments nyingi zaidi katika mwaka husika uwe unairusha mwisho wa mwaka na kuwafahamisha wadau kuwa hii ndo topic iliyovunja record kwa kupata maoni mengi zaidi ya topic yoyote katika mwaka husika. inavutia.
HAPO BADO..
ReplyDeleteNASIKIA KK ANATAKA KUMTEUA ZOMBE MKUU WA MKOA.. AU KUMPANDISHA CHEO KWENYE UPOLISI...
BONGO SYSTEM
Wamesamehwa duniani,lakini hukumu ya kweli inawangoja!
ReplyDeleteLiyumba, Chenge na wengineo nanyi mtaachiwa tu wala msiwe na presha....bongoland wanaofungwa ni wale wachovu tu...wenye pesa kutesa si kwa zamu bali ni daima. Wahenga hawakukosea waliposema PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA
ReplyDeleteOK. Marehemu walikamatwa Sinza na hilo kundi la Zombe (polisi), wakiwa mikononi mwao na pingu wamefungwa wakakutwa wameuwawa kwa risasi huko msitu wa Pande. Chini ya ulinzi wa Polisi Zombe na kundi lake, hawa ndo watu wa mwisho kuwaona marehemu wakiwa hai tena chini ya ulinzi wao, wanaachiwa huru, hawana hatia.
ReplyDeleteJaji ameamua vipi? Yaani sioni maelezo waliyotoa yanayoeleweka kukana kosa hili. Imekuwaje? Au tuseme kuwa marehemu wakiwa chini ya ulinzi wao, muujiza ukatokea, wakakutwa msituni wamepigwa risasi. Zombe na wenzake wakasema hao ni majambazi.
I mean, how come? Mtu yupo chini ya ulinzi wako, hajiwezi kwa kuwa umemfunga pingu, unapaswa kumpeleka kituoni, kesho anakutwa kauwawa msituni, jaji ana onaje kuwa Zombe na wenzake hawana hatia? Wamepigwaje risasi? I am pissed off!!!!
Hii ni kesi wala haikuhitaji kutumia miaka mitatu wala siku nne.
We Tanzanians are so fucking stupid.
Imekaa vibaya, hii bado haijatulia. Kali P upo wapi?
ReplyDeleteJaji na wazee wa baraza, hivi hawa wazee wa baraza elimu yao ikpo vipi?
ReplyDeleteNdugu zanguni hapa ndipo unapokuja ukweli wa mambo kwamba sheria zipo kwa ajiri ya kutetea na kuwalinda watawala na siyo kutetea wanyonge kama inavyonadiwa. Kiukweli hili ni suala la kisheria zaidi, according to the letter of the law watuhumiwa hawana hatia na jamhuri imeshindwa kuprove hilo over the court. But kihualisia watuhumiwa wanayakujibu, hata kama wameshindwa kujibu mbele ya mahakama, watajibu mbele ya mwenyezi mungu. Na hii inaonyesha jinsi gani serikali isiyokuwa makini, wanakurupuka kila kukicha imetumia gharama nyingi kwenye tume ya jaji Kipenka na kutoa report kwamba Zombe na wenzake wanachakujibu mbele ya mahakama. Lakini leo hii, serikali hiyohiyo kupitia mahakama inakwambia hawana hatia. It reach a point tunajiuliza umakini wa serikali yetu hatupati majibu!! Sasa umefika wakati ndugu zetu tujaribu njia nyingine ya msingi na sio serikali hii ya chi chi M.
ReplyDeleteAsanteni
Anon wa Mon Aug 17, 05:27:00 PM
ReplyDeletenadhani hujui yepi yaliyojiri na kesi ya kina babu seya, ni kweli walilawiti watoto wetu na wala hawakusingiziwa. Tuache sheria ifanye kazi yake sio kuongea tu humu labda kweli kina Zombe wako innocent
Wewe unayemlilia Nyerere wacha kutaka kutuletea ujinga wako hapa.
ReplyDeleteNchi inaendeshwa kwa mujibu ya sheria na huo ndio uamuzi wa mahakama.
KUSEMA UKWELI KAMA MTU ANGEINGIA MOYONI MWANGU ANGEONA UCHUNGU NILIO NAO JUU YA NCHI YETU KWA KWELI HII SIO HAKI KABISA TENA KABISA,KILICHO BAKI SASA KUKAA HUKU HUKU UGHAIBUNI NISIJE NIKARUDI BONGO NIKAUA MTU BUREE.HIII.HAPANA SERIKALI IKO WAPI??CCM IKO WAPI KAMA CHAMA TAWALA.MAMBO YANAKO ELEKEA NI BURUNDI NA RWANDA 1994 WE SUBIRI MTAONA TU.NCI INANUKA UCHAFU.JAMANI JAMANI MWALIMU HEMBU FUFUKA HATA KWA DAKIKA MOJA UONE.
ReplyDeleteNahofia kusema kuwa hili ni pigo kubwa kwa utawala wa sheria nchini. Ni wazi kuwa hukumu hii imemaliza kabisa imani ya watanzania kwa asasi za utawala na utoaji wa haki nchini. Itachukua muda mrefua na gharama kubwa kuwafanya watanzania walio wengi haswa wale wa mjini kuamini tena kuwa mahakama zetu zipo kwa ajili ya kutoa haki kwa kila mtu na sio kwa wenye nguvu tu.
ReplyDeleteHata hivyo naamini wa kulaumiwa hapa ni upande wa upelelezi na ushahidi (polisi na waendasha mashtaka)kuliko mahakama.
Tusishangae kuona ule utamaduni tuliojijengea wa KUCHOMA tuwaitao vibaka ukawageukia tuwaitao MAFISADI...
Inasikitisha kuwa kuna wengi waliokuwa wakishangilia "ushindi" ambao ni wazi ndio cheche za mwanzo za mlipuko mkuu ambao watanzania tumekuwa bize tukiuandaa.
omarilyas
watanzania wengi hatuna utamaduniwa kujifunza, ni wavivu wa kudadisi ni waoga kupindukia,tungekua na uelewa wazaidi wa sheria tungeelewa nini kinaendelea,lakini kadri tunavyoenda elimu inazidi kuwa kubwa tutakuja kuelewa nini cha kufanya.
ReplyDeletekwa sababu wengi hatujui sheria ndio maana hatuna uhakika kama maamuzi ya hii kesi yako sawa au sio sawa.
mungu ndio muamuzi wa kweli na ndio maana akaweka kifo kwa wote kuonyesha usawa.na malipo ni hapahapa duniani
asanteni
asante
nchi yetu mpk kesho iko chini na itaendelea hivo kwakuwa hakuan justice..marekani au nchi nyingine yoyote yenye maendeleo(sio za africa)wanafata sana haki hata uwe MP kudadekiii hata raisi ukimess up ur down! sisi huku mtu akishakuwa na madaraka bass anaambiwa tunazuga zuga tu humu baba utatoka tu usijali! mi kwakweli &*(&£%£%£&*£&£*!!!!!!(natukana sanaaaaaa)
ReplyDeleteNIMEKASIRIKA.IM PISSED OFF.sina imani na nchi yangu! PERIOD
ReplyDeleteHaaaa,,,,, mambo gani haya jamani sasa tunaogopa kurudi nyumbani bora tutafute uraia huku tuliko make sasa Tanzania nchi ya amani sasa itakuwa nchi ya vurugu. Kweli huyu jamaa kaachiwa sasa mda wa miaka mitatu ni nini walichokuwa wakipeleleza ata mmoja wao hakuna mwenye makosa mahana wale masela walikufa kwa miujiza.. Poa tu ngoja tusubiri atima ya Tanzania
ReplyDeleteN.B Dereva kasababisha ajari ata mwezi bado kalamba 30 jela hakuna ata investgation yoyote,,,
Mda,,,, Malaysia
Nchi yako au yaMAFISADI? unajipa moyo,wenye nchi uwaoni,KAUWE WEWE MBUZI TU UONE KAMA NCHI YAKO!
ReplyDeleteNA ZE KOMEDI ORIGINAL YETU NDIO IMEISHIA HAPO...!WADANGANYIKA MPOOO....?!
ReplyDeleteSITAHAMA TANZANIA..NITAFIA HAPA HAPA..NAOMBA MUNGU NISHUHUDIE NA IKIBIDI NISHIRIKI KWENYE KUTAFUTA HAKI ZA WANYONGE...HAIJALISHI NI MBINU ZIPI..ZIWE ZA KUMWAGA DAMU AU VYOVYOTE VILE..HT YESU ALILAZIMIKA KUMWAGA DAMU ILI WENGI WAKOMBOLEWE!
ReplyDeleteSASA NI HV, ZIHARAKISHWE HT HIZI ZA KINA MRAMBA, YONA, RICHMOND NA EPA..WAFUTIENI TU MASHTAKA KWANI KWA HALI ILIVYO NDIO MWELEKEO..LOWASSA ANAKULA MATUNDA YA WAZIRI MKUU MSTAAFU JAPO ALIJIUZULU KWA TUHUMA ZA UFISADI!
LAKINI TUNAONA..HAYA YANAFANYIKA HADHARANI, KUNA HAJA YA KUANZISHA MOVEMENT ZA CHINI KWA CHINI ILI KUWEKA MAMBO SAWA KAMA WALIVYOFANYA WAMAREKANI WEUSI WAKATI WA KUDAI HAKI ZAO..
KINACHOFUATA NI kujitoa muhanga kufanya 'kitu mbaya' tena mchana kweupeeee kila mtu akiona ili tujipeleke wenyewe polisi na tuhukumiwe on the spot! Ili ndio mahakimu waonekane wanafanya kazi kiproffessional zaidi..
Ditopilie aliua kweupee mchana mbele ya umma, lakini MUUZA SURA JK alimpa pole na kumwambia ''tuko pamoja ndugu yangu katika hili'' na aliachiwa mchana kwa dhamana..
Na ndivyo ilivyo, sheria inafanya kazi kwa maskini tu na wasio na watu wa kuwasemea..na ndio wamejaa magerezani, kesi za kuku vibaka wakwapuaji na wengine wa kusingiziwa! TUFANYEJE WATANZANIA?
HAWA JAMAA WAJITAHIDI WATEMBEE FULL MITAANI TUTAKULA NAO TU NA TUTAJIPELEKA WENYEWE POLISI TUHUKUMIWE, TENA WASIUNDE TUME ZA KUPOTEZA HELA..MAKE SIYE WADOGO WADOGO, VIKARAGOSI NA MASKINI
HATUUNDIWI TUME..sasa basssi!
onyo: CCM MJIANDAE..TUTATAKA MAJIBU YA YOTE HAYA KABLA YA KWENDA KWENYE VITUO VYA KUPIGIA KURA MWAKA 2010!
Mwenyezi Mungu apewe sifa, natoa salamu zangu za rambirambi kwa familia za wafia.Pia nawapongeza mawakili wa pande zote mbili kwa kutimiza wajibu wao !!!!!! Na nawaomba watanzania wote kwa ujumla kuwa makini.
ReplyDeleteSasa watanzania wenzangu tujifunze kwa vitendo, leo tumeone hiyo kesi ilivyo endeshwa na matokeo yake tumeyaona,. Swali langu ni je tumulaumu nani ? kama siyo sisi wenyewe,. Uongozi umekuwa wa kujuana tokea siku nyingi, kulindana ndo usiseme, hususani ukiangalia upande wa vyombo vya usalama au walinda amani kama wanavyoitwa, mara ngapi wametumia nguvu kupita kipimo au wanawapiga raia wasio na hatia au kosa lolote lile (kumbuka ile ishu ya Arusha- watu wakishushwa kwenye daladala na kupewa kibano-) hapo ndo tunaweza jiuliza haki za binadamu nini maan yake na masingi wake upo wapi kwenye sheria au kwenye ubinadamu ? na jibu nani atoe kama siyo sisi wenyewe –watanzani waipendao nchi yao.
TUSEME HAPANA KWA WAUAJI- kwa kuondoa viongozi wazembe katika taasisi zote. Hiyo ni kazi yetu vijana wazee haooooo wanaelekea kustaafu, tuanze kazi ili watoto wetu siku moja wahukumiwe kwa haki bila kuangalia uwezo wao kiuchumi, madaraka yao au uhusiano wao ni vigogo, bali wahukumiwe kulingana na makosa yao na kwa mjibu wa sheria za nchi.
Kesi ya Nyani, kapewa nyani.
ReplyDeleteHivi kweli watanzania na akili zenu finyu mnadhani kuna muendesha mashtaka (Polisi) gani hapo Bongo anaweza kupeleka ushahidi mahakamani wa kumtia hatiani bosi wake (Zombe). Hawa jamaa wote wameweka mtandao wa kulindana, kuanzia IGP mpaka mshika kirungu kule chini. Huwawezi kutosana kwa kuwa wote wachafu na wanasaidiana kuficha siri zao. Washenzi watupu mbwa hawa.
Hu si uamuzi wa mahakama, bali ni uamuzi wa jaji alieendesha hiyo kesi. Sheria wala haki havijafuatwa hapa bali pesa na kujuana kama si kuogopana.
Tatizo la Bongo, Jaji, wazee wa baraza, muendesha mashtaka, wakili wa utetezi, watuhumiwa na serikali yao ukiangalia kwa umakini utaona kuwa wote wana uhusiano wa karibu kabisa au by reference.
Naungana na anony hapo juu anayesema, hawa walikuwa ndo watu wa mwisho kuwaona marehemu na zaidi wakiwa chini ya ulinzi wao, motive ilikuwako ambayo ni money, muder weapons were there, the bodies were there. Inakuwaje waachwe huru? Halafu huyo jamaa wanayesema alitoroka polisi hata hawawezi sumbuka kumtafuta kwa sababu hawatakuwa na kisingizio tena, wanajua alipo.
Hivi mali za marehemu, madini na fedha zipo wapi sasa? Au nazo ndo zimedhulumiwa kama walivyodhulumiwa haki yao?
Uhakika ni kuwa Bongo mapinduzi hayawezi kutokea hata siku moja, wananchi wamegawanyika makundi makundi. Wengi ni waoga sana, wengine hawajui kesho wataionaje, hivyo wamekuwa tegemezi mno kwa hao wanaowakandamiza (Kumbuka mtu akikandamizwa sana, humtetea mkandamizaji daima), wengine ndo ma mbumbumbu hawajui A wala B, wengine wajuaji mno (hujifanya) lakini yote tisa kumi ni kuwa waTZ wengi ni wabishi mno tena hubisha bila kuwa na data zozote.
Hivyo, watawala wenu wataendelea kuwakandamiza daima na hakuna lolote mtafanya kuondokana na hali hiyo, mbuzi ninyi.