BWENI LA WANAFUNZI WASICHANA LA SHULE YA SEKONDARI YA IDODI MKOANI IRINGA LIMETEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO NA KUSABABISHA VIFO VYA WANAFUNZI 12 PAPO HAPO NA WENGINE 15 KUJERUHIWA VIBAYA NA KUKIMBIZWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA IRINGA, KWA MUJIBU WA HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI SASA.
KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA IRINGA AMETHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILO ILA CHANZO CHA MOTO HUO BADO HAKIJAFAHAMIKA MPAKA SASA.
BLOGU YA JAMII INAFUATILIA KWA KARIBU TUKIO HILO NA ITAWALETEA TAARIFA KAMILI BAADAE KIDOGO. HIVYO TUVUTE SUBIRA.


Inasikitisha sana kupoteza watoto wetu katika mazingira ya namna hiyo. Sina cha kulaumu zaidi ya kusikitika na kusema kazi ya Mungu. Ila nadhani ifike wakati sasa tubadili namna tunavyojega majengo ambayo ni public hasa kwenye mashule, Hospitali, nk
ReplyDeleteUjengaji wetu wa majengo umekuwa ukizingatia "aspect" ya ulinzi "against" wezi na sio usalama kwa ujumla wake.
Ninavyoelewa usalama ni pamoja na uwezekano wa kukimbia iwapo ajali itatokea ndani ya nyumba. Mabweni ya wanafunzi wa hiyo shule iliyopata ajali nimefika mara kadhaa hayana uwezo huo.Na sio shule hiyo tu shule nyingi sana za bweni pale Iringa ziko hivyo. Zimejengwa kwa "assumption" ya "accident-free dormitory" Hii si sawa kabisa.
Mara nyingine mabweni yamejengwa kinamna ili kuzuia wanafunzi wasitoroke, ni kweli lakini ndo bweni la wanafunzi 400 liwe na mlango mmoja jamani. Hapana!Kwa namna hii watakufa wanafunzi wengi sana kwa ajali kama hizi.
Wadau tuna uwezo wa kushawishi ujengaji wa Mabweni uweje ili kuweza kukabili changamoto hizi, tena structure ya bweni la wasichana iwe tofauti na wavulana kwa sababu urefu wa dirisha pengine kwa mvulana ni rahisi kurukia kuliko msichana. Hii pia inaweza kufikiriwa kwa mahospitali na sehemu ambazo watu wengi wanaishi, hata majumbani kwetu pia, tuweke ulinzi lakini tuweke uwezekano wa kukimbia toka ndani.
Brother Michuzi Kama inafaa Nawasilisha. Mdau HSL -Netherlands.
Poleni wafiwa na majeruhi.
ReplyDeleteIla wizara ya elimu itoe muongozo wa jinsi wa kujiepusha na ajali za moto, tetemeko la ardhi n.k
Moja wa wazo langu ni kuwa Mabweni yawe na milango na madirisha kadhaa ambayo yatatumiwa katika dharura ya ajali yoyote. Hivyo milango na madirisha ya mabweni yasiimarishwe kupita kiasi. Pia kuwepo filimbi kadhaa kila bweni.
Ili kuongeza usalama, eneo la wazi linalozunguka mabweni liwe kubwa la kutosha, kutoa nafasi ya kujisalimisha . Na shule nzima iwekewe ukuta na ulinzi kwa ajili ya nidhamu na usalama wa wanafunzi.
Pia walimu wa shule husika wawe wanaendesha 'drill' yaani zoezi la kuwakumbusha wanafunzi nini cha kufanya ikiwa ajali ya moto na tetemeko likitokea, angalau mara moja kila mwezi.
Hayo maoni yakizingatiwa na wizara ya elimu, basi kutawezesha kupunguza madhara yatokanayo na ajali za moto, tetemeko la ardhi n.k
Mdau
Chakumwenda
Mdau wa HSL -Netherlands,
ReplyDeleteMawazo mazuri sana hayo, fikra hizi ndizo zitasaidia kupunguza na hata kumaliza majanga kama haya.
Poleni sana familia waliopatwa na janga hili.
Naombeni sana tusije kusema ni kazi ya Mungu. Mungu anapenda watu wake wawe na afya njema na sio kuthurika kwa mambo ambayo alitupa mbinu za kujikinga nayo.
Utafiti ufanywe na makosa yarekebishwa kama mdau wa HSL na wataalamu wengine watakavyopendekeza.
Mdau,
Reading, UK.
Kumradhi wadau lakini wakati mwingine tunamlaumu Mungu kwa mambo tuliyojisababishia.
ReplyDelete1. Hivi nchi yetu ina standards za ujenzi wa mabweni zinazozingatia usalama wa wanafunzi?
2. Nani anazisimamia na kwa nini mabweni mapya yanapofunguliwa haufanyiki ukaguzi kuhakikisha kwamba yamejengwa kwa kuzingatia viwango?
3. Kwa nini watoto wanasoma kwa mwanga wa vibatari mpaka karne ya 21 ya sayansi na teknolojia?
Taifa halijawa makini na kupunguza vifo kwa ajali zinazozuilika. Mabweni hayana fire extinguishers, hayana alarm, hayana taa za emergency, hakuna fire drills.
Mungu awapumzishe pema marehemu, amen. Mungu awape nguvu ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu katika kipindi hiki kigumu, amina.
Hivi serikali mpo wapi? tokea moto wa shauritanga mpaka leo ni wanafunzi wangapi waliopoteza maisha? si zaidi ya elfu moja sasa!! bado amjaamka! ipo wapi miundo mbinu bora kwemye ujenzi wa mabweni yetu? kwa kweli inauma sana kusikia ajali za moto kila mara zikiua mamia ya watoto wetu.
ReplyDeleteNawapa pole sana wafiwa na hasa wazazi wa wanafunzi hawa waliopoteza maisha katika ajali hii.
Naomba serikali ichue mawazo mazuri waliotoa wadau hapo juu ili kuhakikisha ajali za namna hii zinakomeshwa.