KAKA MICHUZI NAOMBA NIPATE MAWAZO TOKA KWENYE BLOG YA JAMII, MIMI TOKEA JUZI 21/8/09 NIMEANZA KUFUNGA SWAUM, ILA NIPO ULAYA MASHARIKI, SASA HAPA KWETU NA SAMA HII MCHANA NI MREFU SANA, YANI MPAKA SAA 3 USIKU JUA HALIJAZAMA.
IMENIBIDI NIFUNGULIE SAA 2 NA DAKIKA 20, USIKU ILA JUA HALIJAZAMA. NA NAKUMBUKA BONGO NILIKUWA NAFUTURU SAA 12 NA NUSU, SASA SIJUI KAMA NIPO SAHIHI AU LA.
NAOMBA NIPATE MSAADA JUU YA HILO.
MDAU HEMED

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Asalam aleykum, hiyo ulaya uliyopo mwewe ni ulaya ipi? ss hv waislamu wapo duniani kote, kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na waislam wenzako wa mahala unapoishi wakupatie ratiba ya mawio na macheo ya jua ambayo yanaendana pia na nyakati za sala. au watu huko kwenu huwa hawasali? maana ukishajua mda wa sala basi ushajua mda wa kufuturu na kula daku. allahu wa rasulahu ndio wanaojua zaidi ila nadhani ushanifahamu ninachokimaanisha.
    the living legend, Ukraine.

    ReplyDelete
  2. Assalam aleykum, mimi ningependa kukupa msaada hapo kidogo kwa ninavyoelewa, mimi pia nipo ughaibuni UK, sijui upo wapi, inabidi ufuate saa ya kufuturu katika nchi uliyokuwepo hata kama jua linazama sa nne ya usiku unakula saa nne ya usiku. na kuna ramadhan time table, zinapatikana misikitini na kweny mtandao hapa uhaibuni kukupa exact time unayotakiwa kula .na ratiba za swala pia.kama upo UK serch ramadhan time table utapata inategemea upo mji gani ndani ya UK .Allah warasullu aalam, Hakika Mwenyez Mungu ndiye mjuzi wa yote.wabillah tawfik.

    ReplyDelete
  3. Ingia kwenye website hii http://www.islamicity.com/PrayerTimes/ na ujaze nchi na mji unaoishi utafanikiwa kujuwa muda wa swala zote, kama hujafanikiwa basi usifungulie mpaka uhakikishe jua limezama.

    ReplyDelete
  4. Ndugu Hemed, kama walivyokwisha kueleza hao hapo juu. Lazma ufungulie na saa ya maghrib ya mji uliopo. Jitahidi kutafuta nduguzo, tafuta msikiti. Aidha nakushauri uingie kwenye tovuti hii hapa: http://www.islamicfinder.org/ Kisha uchague nchi uliyopo weye, Mungu inshaAllah akuongoze. Ramadhan Kareem kwa nyote.

    ReplyDelete
  5. Kwa elimu yangu ndogo ya Uislam, katika kufuturu unatakiwa ufuturu baada ya jua kuzama na si kwa kufuata saa za kizungu. halafu unasema "saa 3 usiku" lakini jua linakuwa halijazama, kipimo cha usiku ni jua kuzama, sasa itakuwaje usiku wakati jua halijazama!

    ReplyDelete
  6. Nadhani ndugu wewe fanya kila saa 12.39 au 12.40 futuru kama huku bongo achana na mwanga wa jua

    ReplyDelete
  7. WEWE UPO ULAYA GANI MPAKA USIJUE MUDA WA KULA FUTARI????? DUNIA YOTE IMEJAA WAISLAM NA MISIKITI SASA KWANINI USIWEZE KUPATA RATIBA YA KUFUTURU KUPITIA MSIKITI NA KAMA UPO MBALI NAWE UNAWEZA PIA KUDOWNLOAD ADHAN KUPITIA HUO MTANDAO WAKO

    NA UKAPATA KUJUWA VIPINDI VYOTE VYA SALA JUST GO GOOGLE WRITE ADHAN.COM UTAJAZA NCHI ULIPO MJI ULIPO NA ITAKUWA IKIADHINI KILA MUDA WA SALA.

    mdau uholanzi nawatakia waislam wote popote mlipo funga njema ya mwezi mtukufu wa ramadhan.

    ReplyDelete
  8. Ramadhan Kareem.

    Ndugu yangu japo upo ulaya mashariki. ninajua utakuwa na imani yako ya kiislamu japo itakuwa ni mwezi mtukufu mpaka mwezi mtukufu. Inawezekana kabisa eneo ulipo kusiwe na msikiti au usifahamiane na muislamu yoyote kulingana na mazingira ya huku ulaya.

    Ila unaweza kujiunganisha na uislamu katika eneo lako kwa kudownload "ATHAN SOFTWARE" yenye prayer times ya miji karibu 10 million. adjust katika eneo lako basi utapa muda wa sala na hivyo kujua magharibi inaanza saa ngapi za hapo ulipo.

    http://www.islamicfinder.org/athanDownload.php

    Jazakallah khair

    ReplyDelete
  9. Hassan MwalimuAugust 23, 2009

    Assalam aleykum.Ni jambo la kumshukuru Allah kwa kutuwezesha kufikia mwezi mtukufu wa Ramadhan.
    Mi nadhan ni vyema ujaribu kufanya mawasiliano na waislam wenzako waishio hapo ulipo.Siamini kama maeneo unayoishi unaweza kukosa msikiti.Kwa uchache wangu wa ufahamu, mfungaji anatakiwa kufungua ale tu jua linapozama au baada ya adhan ya swala ya mgharibi.Jitadihi kujikurubisha msikitini na kheri itapatikana inshaallah.Jitahidi ndugu yangu kwani bila kufanya hivyo utakuwa unapoteza swaum zako kwa kufungua kabla ya wakati.
    Wabillah Tawfiq

    ReplyDelete
  10. Asalaam aleikum,
    NI vyema ukawasiliana na msikiti wako wa karibu watakupa ratiba.Kuna tovuti hii fanya kuitembelea itakupa time za swala na kunfunga na kufungua kwa sehemu yoyote ulipo duniani.http://www.islamicfinder.org/ kama una lamtopu wako fanya kudowload itakupa mwaka mzima time za swalat.Uko mji gani hukusema

    ReplyDelete
  11. mimi nionavyo fanya kama bongo kwani mafundisho ni yale yale mbona idd tunasherekea tofauti sisi na saudi arabia na wote ni waisilamu na tunafunga ramadhani pamoja

    ReplyDelete
  12. Assalaam alaikum ndugu HEMED.kwa kawaida na ilivyo sahihi kufuturu ni mara tuu baada ya jua kuzama au tuseme kuingia kwa sala ya magharibi. bahati nzuri nami pia nipo ulaya mashariki (saint-petersbur russia). hapa sisi tunafungua saa 3 na dakika 30 kwa leo, keshesho itakua saa 3 na dakika 27. hivyo kama hupati ratiba ya swaumu hapo ulipo naomba tueleze mji uliopo tutakusaidi insha-allah. au wasiliana nami kwa e-mail binseif74@hotmail.com. MAASSALAAM.

    ReplyDelete
  13. audhubillah minashetan lajini ndugu yangu pole sana kwani hata mimi mmission najua muda wa kufuturu upo ulaya gani? manake huku ulaya wamoroko na waturuki wakumwaga hadi huku kwetu poland wapo. muda wa futuru jana ilikuwa saa 2.59 leo ni saa 2.57 kama upo na poland.
    james phillip
    poland

    ReplyDelete
  14. MIMI NI HEMED NILIO OMBA MSAADA HUU. NASHUKURU SANA NDUGU ZANGU WAISLAM NA WASIO WAISLAM,KUNIFUNUA UPEO WANGU AMBAO KIDOGO NILIKUWA NA UTATA.NIMEFANYA YOTE MLIONIELEKEZA IKIWEMO KUANGALIA WEBSITE, NA KUTAFUTA MSIKITI.HAPA NILIPO WAISLAM NI WACHACHE SANA ILA NIMEFANIKIWA KUPATA MSIKITI NA NA PIA NIMEPATA RATIBA. NAWASHUKURU SANA NDUGU ZANGU KWA KUONESHA NI JINSI GANI TUNAJALIANA.
    MWENYEZI MUNGU ATUJAALIE MFUNGO MWEMA WA RAMADHAN.

    ReplyDelete
  15. ASSALAAM ALAIKUM!

    WALLAHI SWALI LAKO LIMETUSAIDIA WENGI SANA.

    NIMEPATA RATIBA YA SWALA YAMJI WANGU, ALHAMDULILLAH.

    WAISLAM WAPO ILA TUPO MBALI MBALI SANA, NA MISIKITI PIA IPO MBALI.

    SHUKRAN KWA ISLAMICITY.COM NA KWA BRO ALIE TUAMBIA HII SITE.

    RAMADHAN KAREEM

    ReplyDelete
  16. Nenda www.islamicfinder.org kisha download athan(azan) ukishamaliza chagua mji na nchi baada ya hapo utapata nyakati zote za swala na pia PC yako itaadhini mida ya swala ikifika kama PC itakuwa ON na ina speaker.

    ReplyDelete
  17. kaka michuzi matunda ya globu ya jamii tunayaona mungu atuongoze sote kwa jumla !

    mdau kaomba msaada tutani asaidiwe ulaya ni kubwa hasa ulaya ya mashariki inawezekana yupo mbali na waislam au hata msikiti ila ameshapata maelekezo kiasi fulani atafaidika.

    kwa kuongezea kutokana na maaelezo yake anatakiwa kuftari mida hiyo ya saa nne kibao kinazunguka time zimebadilika miaka minne iliyopita hapa uk tulikua tunakula daku kumi na mbili asubuhi na kuftari saa tisa kutokana na time ilivyokua lakini sasa tuna futari mbili na dakika ishirini kwa kuanzia ramadhani za mwanzo.

    mwisho nawatakia ramadhani kareem kwa wote .

    ReplyDelete
  18. kama watu wanasema huyu jamaa ale futari saa nne, jee anakula daku saa ngapi. futari ilianzia nchi za uarabuni ambapo jua lilikua linatua saa kumi na mbili na nusu. kuna nchi za kaskazini kwenye arctic circle ambazo ziko canada na ulaya kaskazini na wao wakati wa summer jua linatua baada ya saa nane za usiku na wakati wa winter jua linatua hata saa sita mchana. jee watu ambao wanaishi kwenye hizo sehemu na mara nyingi hakuna waislaam wanatakiwa kufturu saa ngapi.

    ReplyDelete
  19. Katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa ramadhan wengi wao wanatenda visivyo bila ya kuelewa basi mimi ningependa kuwaletea tovuti hii inayohusiana na Uislamu, maamrisho yake, dua, sala, Visa kila kitu cha maarifa ya Uislamu. Naomba watembelee

    WWW.ALHIDAAYA.COM

    humu watapata kila kitu. Vikiwemo pia wakati gani wa kufuturu na wakati gani mzuri wa Kula daku. Lugha ni ya Kiswahili.

    RAMADHAAN KAREEM.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...