baadhi ya watangazaji waliohudhuria mnuso wa send off ya Flora Nducha jana usiku. Kutoka kushoto Abdallah Majura wa BBC, Zuhura Yunusi wa BBC,Maulid Kitenge wa ITV na Radio One na Salim Kikeke wa BBC.
Da' Flora Nducha, mtangazaji mashuhuri wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, na mpambe wake wakiwakawaka usiku huu kwenye mnuso wa nguvu wa send-off yake ilofanyika ukumbi wa Msasani Beach Club jijini Dar

Da' Flora Nducha na mpambe wake wanaondoka ukumbini
Mzaa chema Mzee Nducha akiagana na Bw. Harusi Mtarajiwa na alioongozana nao kwenye mnuso huo ambao ulifana sana

Deo Mwanambilimbi akiwa na kikosi kizima cha Kalunde band, walikuwepo kutumnbuiza kwenye mnuso wa send-off ya Da' Flora





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Hongera sana Flora Nducha. Mkuu wa wilaya ya naniii usitunyime picha ya harusi. Waosha vinywa jibu hilo...

    ReplyDelete
  2. Frola ongera sana, umenikumbusha sana enzi za UD, nimefurahi sana kuona hatua uliyofikia, nakutakia kila la kheri katika maisha mapya.

    ReplyDelete
  3. Da Flora Nducha ndiyo yupi? na mpambe wake ndiyo yupi? wengine hatumfahamu tufafanulie kwenye picha kama ni wa shot au kulia tumjue.

    ReplyDelete
  4. Jamani hii nafasi ya kwenda kuishi UK na Flora niliitafuta kweli lkn wapi. Hiyo njemba ndo imepata makaratasi kirahiiiiiiiiiiiisi. Hongera njemba. Umenipiga bao la kisigino.

    ReplyDelete
  5. hongera wajina hakika unameremeta mdau uliyeuliza flora ndo yupi ni huyo mwenye nguo nyeupe jamani hata bila kuuliza inajipa tuu

    ReplyDelete
  6. hongeara flora sana,ila ulivyyo na miguu mizuri unavaa magauni marefu ya nini ungvaa gauni hadi kwenye magoti tu inatosha. we vipi, ila hongera sana

    ReplyDelete
  7. Jana kumbe ilikuwa tar 12/11/2008? Mbona sikumbuki hivyo?

    ReplyDelete
  8. Yaani wewe umeona miguu iliyofunikwa lkn kifua ambacho kiko wazi hukukiona! Mimi nasifia kifua basi.

    ReplyDelete
  9. Hapo Maulid wa Kitenge anapewa hamu ya kuoa mke wa 3

    ReplyDelete
  10. Hongera sana dada Nducha,have a nice life.ebanaa eeeh Deo Mwanambilimbi duh ndugu yangu upo? za tangu Oysterbay primary class of 87'[7b],big up boy.

    ReplyDelete
  11. michuzi hiyo mikameraX2 mnanunua mbona inawapiga chenga???
    wewe wasema 'jana' nyenzo(kamera)ktk picha inasema '12/11/2008' angalieni mtajauziwa hata na 'time Bombs'kwenye hizo vekisheni zenu mkalipua 'watu' bure!!!
    - anyway jokes aside michuzi,hii shughuli ni ya lini???

    ReplyDelete
  12. Angalia Wewe Anon; 23/08 04:25 sio kila kitu uonacho uamini in shot hayo ni mazingaombwe ya digitali kamera.Jaribu kupata moja uitumie na utajifunza mengi kwa hakika.

    ReplyDelete
  13. Watu comment zenu huwa zinanichekesha sana. eti "Hapo Maulid Kitenge amepata hamu ya kuoa mke wa 3" dah hii kali ya mwaka

    ReplyDelete
  14. nakuunga mkono ma mwili wote wewe uliyesema maulidi atapata hamu ya kuoa mke wa pili ni kweli kabisa sasa hivi ataoa njoo unioe mimi safari hii uone nitakacho kufanya ndo utakuwa mwisho wako wa kuoaoa

    ReplyDelete
  15. mi ndo mke wa 3 wa maulidi
    mwaka huu ndo nampikia futari labda mseme apate hamu ya kuoa mke wa nne..
    hongera Flora nducha

    ReplyDelete
  16. Hongera kwa ndoa. Lakini picha ni za 2008 kulikoni? Au hiyo ndiyo embargo katika uandishi? Au Mpiga picha alikosea tarehe akaweka tarehe ndiyo-siyo? Tunaomba majibu.

    ReplyDelete
  17. Docta Zuu tunakumiss huku Barking lini unarudi ?(You know who pale magorofani tukasahau pram chini) hehehe

    Hongera Da Flora Nducha umependeza Mashallah,

    ReplyDelete
  18. Jamani muacheni Maulid aoe mke wa tatu tena mbichi kabisa safari hii mdogo mwenzie!Afute dosari la mke wa kwanza na wa pili!

    ReplyDelete
  19. jamani kuuliza si ujinga kwani flora nducha ana makaratasi???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...