Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na JK
Dk. Asha-Rose Migiro aibuka kidedea
katika kura za maoni
Na Cecilia John wa Maelezo.
Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Dk. Asha Rose Migiro ameibuka kidedea katika kura za maoni za kumpendekeza Raisi mwanamke kati ya viongozi wanawake 9 Tanzania kwa asilimia 36.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Kampuni ya utafiti ya Synovate, zamani ikijulikana kama Steadman group, Aggrey Oriwo leo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dar es salaam wakati wa kuelezea matokeo ya kura za maoni ya wananchi kuhusu hali ya kiuchumi,kisiasa na kijamii.
Oriwo alisema kwamba Dk. Migiro alishinda kwa kiwango kikubwa dhidi ya wanawake wenzake kwa 36%, akifuatiwa na Anna Kilango Malecela 20%, Margaret Sitta 10%, Anna Tibaijuka 5%, Sophia Simba 4%, Getrude Mongela 2%,Mama Salma Kikwete 2%, na Hawa Ghasia 2%,.
Utafiti huo ulifanyika kati ya tarehe 9-17 mwezi juni mwaka huu ukihusisha wanaume ambao walikuwa 52%,na wanawake 48%, kutoka vijijini 56% ya idadi yote ya watu na mjini 44% ya idadi yote ya watu.
Aidha matokeo ya utafiti huo yametokana na maoni ya watu elfu mbili (2000) ambao walikuwa wanapatikana mikoa yote ya bara na visiwani kwa kuzingatia takwimu na idadi ya watu kama ilivyodhihirika kwenye sensa ya 2002.
Mashaka yuko nambari ngapi?
ReplyDeletewaha wee mama wa kuheshimika nampenda sana huyu mama naamini atawaamha wanawake wingi sana tanzania kufuata mfano wake na kina baba watatuheshimu nampa kura zangu bila ya kinyongo kama miujiza ilitokea amerika onyango obama kuwa rahisi na huyu mama atakuwa rahisi wa kwanza mwanamke tanzania na kura atapata bila shida
ReplyDeleteRAIS ATAKAEIBUKA KIDEDEA NI YULE ATAKAYE WAHAKIKISHIA WATANZANANIA WAZALENDO (SIO WATANZANIA WAZILAO) KUWA ATAKUWA JASIRI KAMA RAIS JOSEPH KABILA WA DRC. UAMUZI ALIOCHUJUWA RAIS KABILA HIVI KARIBUNI CHA KUWASTAAFISHA KWA MANUFAA YA UMMA MAAFISA 1,200 WA SERIKALI YAKE NDIO UNASUBIRIWA KUCHUKULIWA NA RAIS WA TANZANIA HIVI SASA. BOMB-SHELL KAMA HILO NDILO PEKEE LITAWAADABISHA MAFISADI NA WANAFIKI WANAOIFILISI NCHI YETU TANZANIA. KAMA MAMA MARIA NYERERE ALIVYO SEMA JANA MAFISADI WAMECHUKUWA NAFASI YA WAKOLONI WA ENZI HIZOOOOO.. JK KASI MPYA, NGUVU MPYA, NA ARI MPYA VIKO WAPI????! KIONGOZI AKIISHA KUTUHUMIWA KUWA NI FISADI KAMA RAIS MWENYE UCHUNGU WA WALIOKUAJIRI HUNA HAJA YA KUTAFUTA USHAIDI NA KUPELEKANA MAHAKAMANI. SUMMARY DISMISAL NA MALI ZOTE ZINATAIFISHWA BACK INTO GOVERNMENT COFFERS BASI KILA MTU AANZE MBELE KWA MBELE. HAPENDWI MTU HAPA. MH SAMWEL SITTA AKIWA KAMPALA KASEMA - AMEFANYA KAZI SERIKALINI ZAIDI YA MIAKA 30 LAKINI HAKUWEZA KUMUDU KUJILIMBIKIZIA MALI KIASI WALIVYOFANYA BAADHI YA HAWA WATUHIMIWA WA UFISADI KATIKA SERIKALI ZA AWAMU ZA HIVI KARIBUNI NA YA SASA. BAADHI UNAPOKUTANA NAO AWE SERIKALINI AU MBUNGE ANA HARUKU KALI YA UFISADI. MAANA INDICATORS HAZIJIFICHI. LAKINI KWA VILE USHAHIDI NDICH KIGEZO CHA KUTIMULIWA KAZI WANAPETA TENA WANA DHARAU ISIYO KIFANI MAPAKA UNAPOKARIBIA UCHAGUZI. DR ROSE KAMA ATAKUWA NA FEATURES HIZO KURA YANGU NA NAAMINI ZA WAZALENDO WENGI ATAZIKUMBA... KILA LA HERI SHEMEJI, MIMI NI MWITA WA TARIME
ReplyDeleteWape wape vidonge vyao mwita. wakimeza sawa, kama hawataki vidonge watumie propol!! mafisadi wametuchosha bongo..
ReplyDeleteMwita niko na wewe kabisa..... Kaka michuzi tafadhalli fikisha ujumbe.
ReplyDeleteMwita umesema kweli, uzuri wa sura ama jinsia ya mtu si chochote katika urais wa nchi. kinachotakiwa ni kuwa na rais atakaye kuwa jasili, mwenye uwezo wa kuwawajibisha wabadhilifu wa mali ya umma. wale wanaotufanya kila siku turudi nyuma kimaendeleo, wale wanaotuibia fedha zetu tulizozificha kwenye mtungi wetu BOT. wale wanaoagiza madawa feki ili sisi tuzulike ila wao wakatibiwe ulaya n.k
ReplyDeleteHuyo ndio aina ya rais tunayemhitaji katika nchi hii ambayo inaendelea kumezwa na walafi kila siku na uku mamlaka husika ikichekelea kuona kuwa walala hoi wana sulubika.