mdau akipiga taswira ya banda la kuuzia gesi Kigamboni lililowaka moto na kutokea milipuko mikubwa asubuhi ya leo. mtu mmoja amejeruhiwa na nyumba kama tano hivi zimeharibika kutokana na mripuko huo ulioleta fadhaa kwa wakazi wa kigamboni na katikati ya jiji ambako milio ilisikika kama mabomu ya mbagala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hii yote ni sababu serikali (sirikali) yetu ni mbovu. Kwa nini nasema hivi? Leseni zinapotolewa kwa kitu chochote, iwe biashara ya kuuza maandazi au gas kama ilivyotokea hapa, ni lazima kufanyike upekuzi (inspection) kuonyesha kwamba eneo hilo linfaa kwa biahara kama hiyo. Mimi ninadiriki kukuambia kwamba kitu kama hicho labda hakikufanyika. Wajamani mnasemaje kwenye blog ya jamii? Michu mdogo wangu naomba nitoe hoja hii.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana waathirika. Si zaidi ya mwezi mmoja nilikuwa hapo nyumbani TZ. Nilikuwa napita hapo Kituo cha mafuta bamaga,nikamwambia mdogo wangu: hivi hawa wanaofanya biashara ya gesi wana elimu ya kutosha ya usalama kweli? Mitungi ya gesi imewekwa karibu kabisa na vituo vya mafuta.Nobody seem to care. Vigogo wenyewe wanapita hapohapo na kujaza mafuta magari yao.Madhara yake ndiyo haya, gesi zinauzwa kama njugu mitaani, serikali iweke utaratibu mzuri wa mambo kama hayo,hivi vitu ni hatari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...