'CUF MSIDANDIE LIFT YA BURE'
Mkuu wa nanihiiNinaomba nitoe maoni yangu kwa Umma wa Watanzania kuhusu hili sakata la Bunge na Utawala(serikali).
Nimesoma kwenye vyombo vya habari vya Kibongo kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni amemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano kujiuzulu wadhifa wake, kutokana na mwelekeo wa kisiasa Dodoma.
Mimi nafikiri ameenda mbali kidogo, Watanzania walipopiga kura 2005 hawakumpigia Malaika kura, walimpigia binadamu kama wao, kama kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, serikali imekubali kushindwa bungeni na kuomba muda wa kutekeleza maazimio ya Bunge, mimi kama Kijana wa Kitanzania ninafikiri tumeanza kuwa na Democrasia ya kweli.
Ninapenda kuwakumbusha Watanzania kwamba Rais Kikwete ndio Rais ambaye amekubali democrasia ndani ya bunge kuliko marais wengine wote waliopita. Alikuwa na uwezo wa kuwanyamazisha Wabunge wote kupitia vikao vya CCM na hakuna ambaye angefurukuta hata wapinzani. Wabunge wote hawa tunaowasifu kwa ujasiri walikuwepo hata wakati wa Mkapa, mbona hatukujua majina yao.
Wako wapi akina Masumbuko Lamwai, Mabere Marando, Abbas Mtemvu, Lyatonga Mrema na wengine wengi, wote hawa walikuwa moto wa kuotea karibu bungeni. Ila kwa sababu JK amebadilisha mwelekeo wa Dodoma na kuuweka wa Democrasia zaidi wapinzani wanafikiri kuna ugomvi kati ya Wabunge wa CCM na Serikali yao.
Hii ndio Democrasia ambayo majirani zetu wamekuwa wakinufaika nayo miaka nenda miaka rudiHii ndio Democrasia tuliyokuwa tukiililia Watanzania, uwezo wa kumpinga mkubwa wako bila kumkosea heshima, Wabunge wa CCM sasa wanaipinga serikali yao bila kuitwa watovu wa nidhamu. Hakuna vikwao vya akina Kolimba, wala Iddi Simba.
Hakuna Kikao cha dharura cha Kamati Kuu wala cha Kamati ya Secretarieti ya Maelekezo Makao Makuu kama ambavyo tuliyasikia huko nyuma. Ninaomba Wapinzani wasitake kuichonganisha Serikali na Wabunge wake halafu wakaja poteza uhuru wa kuikatalia serikali. Hii ndio mara ya kwanza katika historia ya nchi kwa kumbukumbu zangu, ambapo serikali imekubali kushindwa katika mijada ya Bunge.
Kwanza ninaomba kuipongeza Serikali ya Kikwete, kudumisha Democrasia ya kweli, na kukubali makosa pale panapooneka kuna makosa. Nafikiri tuangalie kwa macho manne haya mabadiliko hayakuja kwasababu tuna wabunge machachari bungeni, ishitoshe hawa wabunge wote walikuwepo kipindi kilichopita isipokuwa Zito na Shibuda.
Ingekuwa Kipindi cha ndugu waliotangulia sidhani hata kama kuna mtu angejiuzulu, wala uchunguzi ungeruhusiwa toka Bungeni, sasa tusijisaidie kambini kabla mazoezi hayajaisha. Sisemi kwamba serikali haina makosa, ila ninachotaka kuwakumbusha Watanzania wenzangu tusidhani tumefika hapa tulipofika kwenye Democrasia ya kweli kwa sababu haya matatizo yanayotokea leo serikalini ni mapya, la hasha, fisadi kama hizi za Richmond na pacha wake Rada ni marudio tu kwenye nchi yetu, tofauti kubwa ni kuwa, this time, Serikali imekubali isifanywe siri bali wananchi waweze kujua jinsi Serikali yao inavyofanya kazi.
Sisemi kwamba serikali haina makosa, ila ninachotaka kuwakumbusha Watanzania wenzangu tusidhani tumefika hapa tulipofika kwenye Democrasia ya kweli kwa sababu haya matatizo yanayotokea leo serikalini ni mapya, la hasha, fisadi kama hizi za Richmond na pacha wake Rada ni marudio tu kwenye nchi yetu, tofauti kubwa ni kuwa, this time, Serikali imekubali isifanywe siri bali wananchi waweze kujua jinsi Serikali yao inavyofanya kazi.
Nachukua fursa hii kumpongeza Spika, kwa kuongoza ujasiri na Democrasia ndani ya Bunge, na kuruhusu mijadala bila kupendelea upande mmoja. Nampongeza Waziri Mkuu kukubali kuwa panapokuwepo na makosa mkubwa hukubali makosa yake na kuomba muda kurekebisha. Kama hali hii itaendelea kwenye nchi yetu basi tunapiga hatua kubwa sana katika Democrasia.
Kama suala ni Hosea na Mwanyika! Mbona hata waliojiuzulu hawakujiuzulu kikamilifu, waliachia Uwaziri, wakaendelea kuwa Wabunge. Kwa mantiko hiyo ni kosa kuwa Fisadi Waziri lakini ni sawa kuwa Fisadi Mbunge! Mimi ninamwomba Rais Kikwete awateue akina Hosea na Wenzake kuwa Wabunge, halafu wajiuzulu nyadhifa zao ili wote wawe sawa! Akimaliza hilo, CUF nao waanze tution ya Democrasia kwa kufanya Uchaguzi mwingine wa viongozi wao wa Kitaifa, kama walivyo Chadema na CCM.
Huwezi kuwa Kiongozi miaka ishirini, ofisi ileile, chama kilekile, nashindwa kuelewa kwanini Professor Lipumba asitumie utaalamu wake wa Uchumi kuapply "Theory of Diminishing Return" kwenye uongozi wake.
Wadau msinimeze; nimetumia uhuru wangu wa Kikatiba, kutoa maoni yangu bila kuvunja sheria yoyote, na wewe kama una maoni yako wasiliana nami kupitia barua pepe hii hapa chini.
Mungu Ibariki Afrika.
Mungu Ibariki Tanzania
Kuja WP

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. Tatizo la wabongo ni wivu na kuiga. Wewe unaiha wakina mashaka na shayo ambao wamepewa vipaji. Sass hapa unazungumzia nini? Bwana kwenda zako huko ukabebe boxi. Uwezo hauna matokeo yake unajilazimisha heti kikwete asijiuzulu, mara lipumba mara takataka fani. Mnafiki Mkubwa wee, kwenda zako huko nyambaf

    ReplyDelete
  2. Huyu mtu anafundisha tuition pale Alabama mshamba sana. Angalia unayoyaandika bwana mdogo hacha kuropoka ovyo, hujui chochote kuhusu Tanzania

    ReplyDelete
  3. Kiswahili hauwezi. Kiingereza ndo balaa sasa ndo vipi mtu wangu?
    Siasa yenye haujui maneno ya kutumia. Hivi ww unatafuta nn udiwani au ubalozi wa nyumba kumi?
    Kuna shuguli kweli.
    Aibu tupu

    ReplyDelete
  4. Wakuja,

    Umetoa mchambuo/mchanganuo mzuri sana hongera. Lakini naomba nitoe hoja ya kuongeza nguvu mchanganuo huu kama ifuatavyo (una uhuru wa kukataa au kukubali - "na hayo ni maendeleo - Moi"):

    Mosi, kama unakubali demokrasia, muhimu ni kuheshimu mawazo ya wengine pamoja na kwamba hukubaliani na mawazo hayo ("agree to disagree on national issues"). Kwa hilo basi, naona ingefaa ukamsifia mpinzani aliyetoa hoja ya kungatuka kwa JK kwanza kabla ya kumkandya. Mimi binafsi, nafikiri tungejenga desturi ya kusifiana kabla ya kukandyana mawazo ya wengine, tutakuwa tunaelekea kuzuri kwa mijadala yetu. Wengi wetu tunadamkia mjadala na kutoa lolote la kukandyana hata kama mjadala unahusu nji (nchi) yetu na watu wetu. Kwa mtindo huo daima hatutakwenda mbele.

    Pili, Marekani unapoishi WPkuja ni nji (nchi) iliyoendelea (wengine husema kwamba hilo ni "taifa kubwa"). Lakini pamoja na kufikia hatua hii, bado kuna visehemu nyeti sana vya mijadala vinazuzua watu. Kwa mfano, watu wanakubaliana kutokukubaliana kwenye mambo mengi. Ya hivi karibuni ni mchakato (sina uhakika kama hapa kiswahili ni sahihi) unaoendelea sasa wa afya kwa wote au sakata la kadi za kula na kununua kwa mikopo (credit cards) na cash for crunckers na kadhalika na kadhalika na kadhalika - mengine mengi ambayo kina Larry King au Lou Dobbs wanalipwa na CNN kuwahoji watu wanaoihoji serikali hadi kufikia kuwapatia viongozi - kadi ya maendeleo (report card) ya siku mia, mia mbili nk).

    Tatu, tukubaliane kwamba blog ya jamii imetupatia hii nafasi ili tuchangie hoja bila kujali imetoka kwa Mashaka au kwa Mushy au kule Kigoma. Kasumba yetu tuipinge ya kusema kwamba huyo anatoa hoja kwa sababu anatka hili au lile.

    Nne na mwisho ni kwamba bila kuamka na kuambiana kwamba hii sivyo (na kuja na data kamili za kuonyesha ukweli wa unayosema) itakuwa ndio chanzo cha kufinyana na hii ni kwa ajili ya kupata mwelekeo mzuri na maendeleo kwa nji nzima. Tukikaa bila kufinyanaya finyana hivi kwa kuambiana tutafikiri tumefika (au tutafikiri kwamba report ya JK ni 100 (au A+) na yeye atakaa bila kuhangaika atafikiria amesha"deliver" ahadi zake za kwenye ajenda za CCM tukufu!! Mimi naona kwamba hata kama wakati fulani tutafikia maendelea ya Amerika ya kaskazini, bado tutakuwa au tutahitaji haya malumbano (mimi nayaita kufinyanafinyana: kisa - kutaka kusukuma mbele maendeleo ajenda za pale ambapo tunafikiri bado tunayahitaji kusogea.

    Kwa heshima na taadhima, naomba kutoa hoja (rafiki yako WPkuja).

    ReplyDelete
  5. Kuelekea 2010 tutaona mengi sana.. Yaani wewe kweli ni kijana.. Kwani upeo wako wa kupanua uwezo wako wa kufikiri bado pia ni mdogo.. Kama kawaida historia huwa inajiandika kila baada ya muda flani usisahau hilo.. Kama ni kuitwa ktk vikao vya siri vya chama wabunge wote wa ccm waliitwa.. Ila tunachoshukuru ni kuwa wabunge wameweka maslahi ya nchi mbele zaidi na kuachwa kuburuzwa kama kondoo..
    Waligomea maadhimio ya kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa waandamizi wa serikali.
    Kijana soma alama za nyakati.. Utendaji wa JK umekuwa ukishuka kila siku ipaayo kwa mola.
    Jana kadai watanzani waache amagari ya nasa anunue matrekta mbona viongozi wote serikali wanatumia GX V8 unajua bei zake? Ameshindwa nini kuiga kwa Mwenzie Mwai Kibaki.. Usikurukupuke toa maoni kwa uwezo wa hoja.

    ReplyDelete
  6. Nimependa hoja zako. maana hujachafua hali ya hewa wala nini, bali umesema yaliyo nafsini mwako. tuko pamoja.
    mdau,
    ughaibuni

    ReplyDelete
  7. Hili sio suala la kwamba Rais angeweza kunyamazisha au la! Wakati wa Mkapa kwa taarifa yako kulikuwa hakuna makundi na ndio maana ilikuwa ni rahisi kwa wabunge wa CCM kuketishana chini! Kwangu mimi binafsi bado sikubaliani na wewe kwamba ati demokrasia ndio sasa imekua!Ila alivyosema Rais kuna kipindi ni muhimu kusoma alama za nyakani! CCM ya sasa ina mitandao mingi tofauti na ya Mkapa!

    ReplyDelete
  8. Kwenda zako kumbaf haya ndo majitu yanayojikomba. Ww unajua nini kuhusu CUF???

    ReplyDelete
  9. Ww mdengereku "theory ya diminishing return" inaingiaje hapa ? Au ndo hichobulichokariri shuleni?
    Naomba umwandikie shayo shayohill@yahoo.com au mashakajohn@yahoo.com watakupa Masada wa kitaaluma
    kuliko kuropoka. Unajua nn kuhusu cuf... Unajutakia matatizo

    ReplyDelete
  10. Bongo kweli kichwa cha mwendawazimu!

    Hivi huyu aliyeandika haya mawazo..ndo anasoma ughaibuni..harafu kesho anakuja na pipa eti "kuwatumikia wananchi"? Kwa kugombea ubunge?


    Mungu tunusuru taifa lako. Yaani kuna wengine wanatoa mawazo unajifikiria mara mbili mbili wanafikiria nini?


    Pathetic!

    ReplyDelete
  11. CUF NI CHAMA KINACHOFUATA DEMOKRASIA SANA.MWAKA HUU MWEZI WA NNE WAMEFANYA CHAGUZI ZAO ZA NDANI KWENYE NAFASI YA MWENYEKITI KULIKUWA NA WAGOMBEA WATATU-PROFESSOR LIPUMBA,PROF ABDALLAH SAFARI NA MGOMBEA MWINGINE SIMKUMBUKI.

    CCM NAO WANAFANYA SANA CHAGUZI ZAO ZA NDANI KWA WAKATI.NI CHADEMA AMBAO KISHERI WALIKUWA WAFANYE UCHAGUZI MWAKA JANA HADI SASA HAWAJAFANYA.

    LIPUMBA AMEKUWA MWENYEKITI WA CUF 1999 ANA MIAKA KUMI. MWALIMU NYERERE ALIKUWA MWENYEKITI WA CCM KWA MIAKA MINGAPI?

    SEMA LINGINE KWA HILI HUNA CHA KUSEMA.

    ReplyDelete
  12. Kuja WP nakuunga mkono kwa kiasi fulani. Uhuru wa kujieleza, kutoa hoja, habari nk ni kitu muhimu ambacho utawala huu umetuletea. Hatua inayofuata baada ya ufisadi kuwekwa wazi, wahusika wanapaswa kuchukuliwa hatua mara moja. Ikiwa ufisadi utawekwa hadaharani kwa uhuru wa habari, halafu hao hao mafisadi wakalindwa, wakaendelea kukalia nyadhifa zao, hiyo itakuwa ni dharau kwa Watanzania na Matokeo yake ni mabaya. Tunahitaji kiongozi ambaye atamfukuza kazi kazi mzembe, mla rushwa, fisadi bila huruma. Kuhusu Demokrasia ya CUF na TLP, no coment, lakini sidhani kama tuna credible upinzani katika Tanzania.

    ReplyDelete
  13. MWACHENI ASEME MAONI YAKE,ISITOSHE WALIOCHANGIA HAPA WENGI WAMEANZA FUFATILIA SIASA JUZ JUZI TU.UKWELI NI KWAMBA MIJADALA KAMA YA RICHMOND NA MENGINEYO ENZI ZA MWALIMU
    AU MKAPA SASA HIVI ZILISHAMALIZWA KWENYE VIKAO VYA CHAMA NA SI BUNGENI
    ATAKEPINGA ANASUBIRIWA NEXT UCHAGUZI ANAENGULIWA, KAMA NI WA UPINZANI WANATUMIA KILA ILA YA KUMCHOMOA.NI NANI ALIYEKUWA ANAPENDA KUFATILIA BUNGE ENZI ZILE,KILA HOJA MAKOFI(IMEPITA UPINZANI UKIPINGA INAPIGWA KURA).
    NI NANI ASIYEJUA KUWA SASA UHURU WA BUNGE NI MKUBWA KULIKO MWANZO.
    WATNZANIA TUJIFUNZE KUPIMA BADALA YA KUWA MAFISADI WA KUPAYUKA.
    KILA SERIKALI INAMAPUNGUFU YAKE,MAPUNGUFU YA SASA YANONEKANA KUTOKANA NA UHURU WA KUTOA MAONI NJE NA NDANI YA BUNGE ILA , SWALA LILOBAKI SASA NI SUALA LA UTEKELEZAJI NDO AMABLO NI AFIFU.UNGEONA VP MAPUNGUFU YA MKAPA WAKATI HATA VYOMBO VYA HABARI VILIPIGWA BITI(HALO UNAHATARISHA USALAMA WA TAIFA,UKIJIFANYA USIKII UTAHUJUMIWA HAPO). BIG UP KIKWETE SEMA REKEBISHA UTEKELEZAJI UWE WA FASTER KIDOGO

    ReplyDelete
  14. Ni jambo la kushangaza na pia la kutia wasiwasi kwamba mpaka kufika hapa tulipo leo bado pimajoto zetu hazijatambua hasa nini kiini cha kupanda kwa joto la mwili kisiasa hapa kwetu Tanzania.

    Nipo tayari sana kukosolewa lakini hakika ni kwamba matatizo yetu Tanzania si vyama vya siasa na hata wale ambao wapo kwenye madaraka ama nyadhifa za juu kabisa katika majukwaa ya siasa ndani ya vyama hivyo.

    Tutakuwa tunafanya siyo busara na siyo haki kuzidi pelekea lawama vyama vya siasa na hata uongozi wake kumbe wapiga ubuyu wengine kabisa wpao pembeni kuwaachia wenye meno watafune.

    Sipendi kugeuza baraza hili kuwa mahala pa malumbano marefu ya kujadili neno baada ya neno baada ya msitari wa kila anayechangia hoja humu. Hivyo sinto fuata msitari huo japo kwa kunena wazi kwamba tatizo letu Tanzania ni ‘ujuaji uchwala’ ambao huzaa lafudhi mbiu kama vile ‘Fisadi’ na nyingine nyingi tuu.

    Hapa panatakiwa uzalendo wajameni, hapa panatakiwa uamsho hashwa wa hamasa ya kusema kwamba mimi ni mtanzania ni nipo hapa kuinusuru Tanzania na watanzania wote, kwamba hapo walipo watanzania wanajivuna na kusema kwamba “nchini kwetu tuna hili na lile la maendeleo igeni toka kwetu”.

    Mataifa mengi yametujua sisi kwa mambo haya ya ulaghai usiyo na utajiri, kale ka 10% kametushishia kabisa hadhi mpaka wengien wakafika kusema kwamba unakwenda Tanzania masikini baada ya muda si mrefu weye ni tajiri kushinda hata serikali yenyewe!! (Sasa hapa hili ni la wanasiasa ana vyama vyao vya siasa!!!?? ).

    Mimi niliupokea ujio wa JK kwa matumaini makubwa na mpaka leo hii ninayo matumaini hayo ikiwa tu JK atafumbua macho na kuangalia mbali kidogo nje ya baraza lake la mawaziri ambalo linahujumiwa kila siku na kuonekana kana kwamba yeye mwenyewe JK anaendekeza mambo fulani fulani ambayo yanatokana na mawaziri wake, ambayo kwa kweli siyo hata wao.

    Ninathubutu kusema kwamba JK anatakiwa sasa kuangalia watendaji. Kuanzia makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa kurugenzi zote muhimu, maana hawa KWA TAARIFA YENU ndiyo waharabifu, hawa ndiyo mafisadi haswaa… hawa ndiyo wanajua ndani nje ya kila kitu ndani ya wizara, hawa ndiyo wanataarifa zote zinazohusu maendeleo ya kila sekta ndani ya wizara zao, hawa ndiyo wanaopindisha mambo mengi kwa ajili ya anasa zao ama za kumkomoa alieye juu yake ama hata jirani yake ili yeye tu apate nafuu na familia yake, hawa ndiyo wanaowarubuni mawaziri kuingia mikataba ya giza, hawa ndiyo watayarishaji wa 10% hata kama wao watapata shillingi ya kununulia kitumbua lakini kubwa katambulika kwenye kutia sahihi ya 10%, hawa hawasemwi hata kidogo kwa woga kwamba ukiwasema watafanya hujuma kubwa zaidi maana wapo jikoni ni rahisi wao kutia sumu kwenye mchuzi, hawa ndiyo wanatupeleka hapa tulipo na baadaye tunabakia kutiana vidole sisi wengine na wao kukaa pembeni kama vile hawapo, hawa ndiyo wanatuamulia leo tule nini kama Taifa na ni shughuli gani ama mradi gani ufanikiwe, HAWA NDIYO CHIMBUKO LA MADHAMBI YOTE NCHINI KWETU!!!!

    Nimelipasua JIPU.. pwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!! (dRU)

    ReplyDelete
  15. WE MTU KAMA KIKWETE ANAFUATA DEMOKRASİ MBONA PEMBA HIVI SASA WATU WANAKATALIWA KUANDIKISWA KTK DAFTARI WAKATI HAKI NI YAO?JE KUNA DEMKRASIA GANI KUMNYIMA MTU KUCHAGUA RAISI NA MBUNGE WAKE? NA RAIS KIKWETE YUPO KIMYAAAA SI KAMA HAJUI AU AONI! MICHU USIIBANIE NDOKWANZA TUNAAMKA

    ReplyDelete
  16. Kila mwenye mawazo ana haki ya kuyawakilisha kwa jamii kistaarabu na heshima, Huyu ndugu yetu katumia heshima na ustaarabu wote kufikisha mawazo yake maswala yajadiliwe. Sasa iweje watu waanze kumlinganisha na fulani na fulani, eti anataka sifa au anashindana na kina fulani kwakuwa tu katoa maoni yake? Hili ni swala linaloonyesha ni kiasi gani watu wengi hawana upeo wa kufikiri. Inasikitisha sana kuona mtu anatumia muda wake kuandika maneno ya kumkandia mwenzake na akipewa yeye wasaa wa kuandika hawezi hata kuandika mistaru kumi akaeleweka. Ndugu mtoa hoja kawakilisha mawazo vizuri kabisa, Michuzi tunaomba heshima irudi kwa blog yetu ya jamii, wachafua hali ya hewa naona wanapenya sana siku hizi.. kitu kidogo tu anamuiga mashaka na shayo? hivi mnadhani hao kina mashaka wanafurahia kuona majina yao yakitajwa pasipostahili?? Tuwe wastaarabu jamani.
    Binafsi sijaona lolote alilokosea mtoa hoja.

    ReplyDelete
  17. Wadau mnaompondea mwandishi naomba niwarekebishe kiswahili hii ni aibu tujifunze haya mambo madogo huwa inanikera sana kuona hata kiswahili tunaandika madudu.
    Anon wa kwanza sio heti ni eti
    Anon wa pili sio hacha ni acha
    Mngejirekebisha kwanza kabla ya kuanza kumponda mwenzenu kwani hata nyie mna tatizo la kuandika

    ReplyDelete
  18. Huwezi kumkosoa mwenzio kabla hujajikosoa wewe mwenyewe. Kuhusu Kiswali watu wote tunaandika makosa. Na ili tatizo la uandishi wa Kiswahili tulishaliongelea awali. Hatuna haja ya kurudia. Unajua hapa kuna watu wanajifanya wao ndo wanajua sana Kiswahili kumbe hakuna lolote. Halafu Watanzania tunamponda sana Mr. Kuja, kila anapoandika hoja yake yake lazima watu wajaribu kumkosoa. Ni vyema ukaandika cha kwako tukakosea kuliko kuandika maoni kwa mwenzio na kuanza kumtukana bila sababu. Wanasema toa ulicho nacho moyo ukiya kitoa utapata kupumua vizuri. Sasa Mr. Kuja ili tatizo lilikuwa linamsumbua sana, sasa akaona kuwa ni vyema alitoa kwa wahusika ili wachangie maada, lakini cha kushangaza ni kwamba watu bala ya kuchangia maada wanatukana. Ningeshauri kama uwezi kuchangia jamani usitukana, kwani si lazima uchangie maada.

    ReplyDelete
  19. Mtambo Wa Kurekebisha TabiaAugust 04, 2009

    NYIE MNAOMSAKAMA MWENZENU MARA KACHEMSHA MARA ANAWAIGA KINA MASHAKA SIJUI MLITAKAJE. MLITAKA AANDIKE KAMA NYIE MNAVYOFIKIRIA. SASA HAYO YANGEKUWA MAWAZO YAKE AU YENU?

    KWA NINI NA NYINYI MSITOE MAWAZO YENU?

    HUU UGONJWA WA WATANZANIA WA KULAUMU KILA KITU SIJUI UTAPONA LINI. JIREKEBISHENI.

    ReplyDelete
  20. Ndugu KujaWP nakubaliana na wewe mia kwa mia. Watu wanasahau historia haraka. Ukweli Rais JK ni kiongozi ambaye ni tolerant na mzalendo haswa. Hivi ingekuwa awamu ya Tatu hawa akina Seleli na wenziwe akina Ole Sendeka mnafikiri wangeendelea kuikemea serikali? Hata kidogo. Kwanza wangekumbushwa kuwa majina yao yakija mwakani kuingia kwenye kugombea ubunge yatakatwa. Not under the able leadership of JK. No. Hivi mnafikiri JK angeruhusu Net Group Solution ya makaburu ichukue nafasi ya mameneja wazalendo wa TANESCO ili kumtengenezea deal na ulaji wife na shemeji yake? Au angeruhusu NBC iuzwe kwa ABSA kwa bei ya kutupa au ATC ichukuliwe na makaburu ikamuliwe halafu turudishiwe? Jamani mbona mnasahau? Hivi hamuoni uchafu wa Richmond JK hakuulea? Au makashfa ya EPA hakuyalea wala kuyavumulia? Mbona hamuoni na macho mnayo jamani.Hivi kama JK angekuwa Rais wa awamu iliyopita mnafikiri angeifukuza menejimenti ya kizalendo ya TANESCO na kuwaweka Net Group Solutions ili kuwapa ulaji wife na shemeji yake? Au NBC angeiuza kwa ABSA kwa bei ya kutupa?

    Ingekuwa Richmond iko awamu ya tatu mnafikiri ingesababisha Sumaye aachie ngazi?

    Mheshimiwa JK tuko na wewe usiiogope. Mola ambaye tunamuomba kila siku akupe baraka na akulinde hatakuacha uangamie mheshimiwa.

    ReplyDelete
  21. Ni demokrasia gani hiyo imekuwa?kuna ndugu zangu wa kipemba ambao wamezaliwa hapo wengine kwa bahati mbaya hata pale unguja au dar es salaam hawapajui,lakini hivi sasa hawandikishwi ktk daftari la wapiga kura sababu wanaambiwa si wazanzibar wakaazi wakati wan mpaka vyeti vya kuzaliwa sasa sijui ni demokrasia gani hiyo inakua wakati huyo anayesifiwa kuwa kaleta demokrasia analijua hilo na kanyamaza kimya?sasa wewe uliyeandika waraka huo usiangali kumoja tu angalia kila kona ndiyo uweze kutoa hayo maoni yako.kweli demokrasia mtu kukataliwa haki yake ya kuchagua,kama munaona pemba si kwao basi watfutieni ambako ni kwao wakapate haki yao ya kuchagua kiongozi wanaemtaka.

    ReplyDelete
  22. mimi binafsi nakubaliana hoja za watu wengi baadhi ya za waliopinga na kwa upande mmoja nakubaliana na wp kuja.
    waliopinga nimekubali neno moja ambalo ni" kujifunza kusoma nyakati". kwa maana kwamba wakati huu ni wakati muafaka kwa kinacho anza kufanyika ktk siasa yetu.
    nakubali kwa waliosema tuiangalie historia kwa misingi kwamba JK aliwahi kubanwa kipindi kile cha 1995 kwamba bado hajaiva, na matokeo yake kipenzi chetu mwalimu kwa kumuamini kipenzi chake ben akampigia debe hadi akashika madaraka. ben kafanya mazuri machache ikiwemo kurudisha heshima ya elimu na kazi,lakini kafanya uvundo mwingi sana hasa baada ya mwalimu kutangulia mbele ya haki.
    JK ameingia madarakani akaikuta beaurocratic system ambayo ni gigantic system iliyokuwa(INAYO)ENDESHWA NA WATU WADOGO(small people).kwahivyo vita anayopigana nayo sio vita rahisi kama unavyoweza kudhania. nayeye kama mjeshi nadhani hilo analijua maana adui wake haonekaniki kirahisi,anaweza kuwa yuko karibu sana anakula naye,hivyo basi ni vita ya akili ya hali ya juu(ASOMAYE NA AFAHAMU).
    binafsi ninazipongeza juhudi zake,japo pia ninashauri asilegeze kamba, kwa maana ni bora kufa kishujaa historia itasimama kama ilivyowazi kwetu sote kuwa kuna mapungufu mengi yaliyojitokeza nyakati za mwalimu,lakini mwalimu alipenda haki na usawa kwa wote!angeza kujitajirisha maana wasomi walikuwa sio wengi,lakini hakuwa na tamaa hiyo,na historia imesimama kumtetea.
    JK mimi binafsi ninakupongeza,maana tactic zako zinaonyesha matumaini kwa miaka ijayo kama hauta waogopa wanaokusudia kuwa kikwazo.
    mwisho nimependa hoja ya mchangiaji aliyegusia watendaji wa serikali MAKATIBU WAKUU,WAKURUGENZI. hapa kweli ndipo ulipo lala mzizi wa uchafu,maana wengi wa hawa ni professionals ambao siasa huwa haiwagusi,na ndio haswa wanapaswa kuanziwa kuwekwa kitimoto ili waeleze kilichofanyika kwa kuwashirikisha mawaziri wao husika.

    mdau-ugaibuni masomoni.

    ReplyDelete
  23. Uzuri wa blogu ya michuzi ni kwamba kila anayepisti hapa akiwa na cha maana kina mashaka na shayo lazima watarudi lakini ukiwa pumba kaa huyu kuna na mokes gama hawaeudi Tena. Wanatolewa mkuku
    bwana kuja ikiwa unataka kujikita kwenye siasa basi itabidi unoe kichwa kwa sababu wewe shida yako kubwa ni kuropoka mno. Unajifanya mjuaji sana wakati ujui kwamba wataalamu wapo tu chemba wanakusubiria. Ila kiingereza hauwezi ile ya wakina shayo Kiswahili chenyewe ndo hicho Tena.haya bwana haya maji ni marefu na una mwendo kweli lakin usikifabye Jambi letu kuwa sehemu yako ya kuropokea.wewe unajua nn kuhusu chama cha CUF unajikomba siyo baada ya kusuindwa kubeba boxi marekani sijui wapi? Unajua znz kuna matatizo gani? Kama siyo ufisadi wa Jk na kundi lake tungekuwa navhaya matatizo? Nyambaf hacha zako koma vinginevyo utapata aibu kubwa saba hapa

    CUF

    ReplyDelete
  24. Mbona umeishambulia CUF bila sababu za msingi au unakinyongo na CUF? Maana tuseme wazi, japo kwa kufuata demokrasia nchi yetu inajifunza kutambaa ie haijajua kutambaa vizuri, huku kutembea na kukimbia vikitungoja lakini walau tunamshukuru Mungu kwani kama sio yeye kutujalia moyo wa uvumilivu na karama ya usahaulifu,hakika hata uwapo wa Kambi za jeshi karibu kila mkoa kama si wilaya isingefaa kitu mbele ya hasira za wananchi wengi ambao wamekua wakinyanganya haki zao za kidemokrasia(Mfano Pemba,Busanda,Bihalamulo nk ambako demokrasia kwa uwezo wa dola ilipindisha ili kukipendelea chama fulani)
    Hoja aliyoisema huyu mdau akifatisha taarifa za vyombo vya habari kuhusu kujiuzulu kwa Rais ni kwamba ile hoja haijaletwa na CUF,isipokua imeletwa na matokeo ya Richmond, ambao walaka wa serikali uliokuwa utoe majibu ya kamati ya kina Mwakyembe waliyoiagiza serikali kutekeleza mapendekeo waaliyowapa kuhusu Richmond, alihali serikali wakishindwa na kukiri kushindwa kutoa maamuzi, hali iliyopelekea Bunge kuukata walaka wao. Jamaa yangu akumbuke kwamba Mh. W. Slaa alisema kwamba kufuatia hali hii anaipa muda serikali hadi November kutoa majibu fasaha au la atapeleka hoja binafsi yakutokua na imani na serikali, akisisitiza kwamba ingekua ni serikali za nchi nyingine basi mwezi november kungekua na uchaguzi mwingine kufuatia kujiuzulu kwa serikali.
    Pia mdau kumbuka kwamba serikali ilikiri kufanya makosa katika kufanya utekelezaji wa maagizo ya Bunge, kukiri huko kwa serikali kwa nchi ya kidemokasia hakuishii tu kuomba radhi au kutoa ahadi bali ni kujiweka kando kwa serikali, kwani ukumbuke mdau kwamba Rais wa nchi pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri,kushindwa kwa serikali ni kushindwa kwa baraza la mawaziri ambalo mwenyekiti wake ndiye rais wa nchi
    Hivyo mdau,Mh.Hamad Rashid anawakilisha Wabunge wa upinzani bungeni na kama ameisema kauli ile akiwa katika kofia hiyo basi ni wazi hiyo si kauli ya CUF bali ni ya vyama vya upinzani Bungeni hivyo basi kauli yake inawakilisha msimamo ama pendekezo la Wabunge wote wa upinzani Bungeni.
    ....But Umenifurahisha na theory yako ya Diminishing Marginal Utility hivi unaweza kuitumia nyumbani kwako na mkeo? Maana sidhani ulipoiweka ni mahala pake!

    ReplyDelete
  25. hivi huyu kuja ankunywaga pombe gani?
    mm naona anapambana na wakina shayo, mkuu utaweza?
    kiatu chako namba mbili wale wanavaa namba kumi, wapi na wapi
    katulize boli weye
    au unataka ukapewe utarishi TRA na wewe, thubutu mtu kama wewe wa kujikomba ni wa kuogopwa

    ReplyDelete
  26. DON’T GET ME WRONG PUNDITS

    To all Bloggers,
    As I place my fore head across my study table, looking intently at my laptop’s 13.3 Sonny made screen, reading between the lines, I see great ideas from great people. I have great respect for my natives, who has always made me proud of my country, a poor nation rich of great inspirations.

    One simple summit bloggers, I am purely made of democratic blood. I shall never be scared of your foul-smelling comments, rather, lifted and tentatively transformed. To those who disagree and agree with dignity, our destiny is unchanged. We suffer the same, while industrializing our thoughts, regrouping our arsenals ready to lift our country into a green-pasteurized planet. We cannot revolutionize whatever a thing from these standard-seven comments.

    Don’t get me wrong left-wingers, in 1995, I was below 18, but because of great philosophy and economic policies that Professor Lipumba’s CUF campaigned, I decided to vote before my legal voting age just to demonstrate my support to the Man I thought was born to rescue the country from deepen economic adversities. Frankly speaking, with all things remain constant, days remains seven in a week, and 12 month in a year, nothing changes at Buguruni’s CUF headquarters, the illegal vote I gave them in 1995 could be the last in history. I don’t say this because I hate CUF, rather, give them a reflective mirror to amend where is broken for better tomorrow.

    While we continue blogging comrades, I would like to remind the WVs (Waosha Vinywa), to watch-out their typing and word choices. This is not the place to dispose their ignorance and toilet-papered comments. With decree, this blog shall remain a place where dignified individuals table matters of high national importance to the board for debate and not caricatured attitudes.
    Thanks

    Kuja WP

    ReplyDelete
  27. Hoja kama hii haiwezi kutiwa kapuni hata siku moja, lakini hoja kinyume chake mmmh, ikitoka ina makengeza.
    Mtoa hoja anajikanyaga, kwani unapozungumzia demokrasia una maana gani, unaangalia mtu au unaangalia utaratibu. Kwasababu chuki yako kwa Lipumba haisaidii kama wanachama wake wamempigia kura, na kama unataka hiyo nafasi kwanini usiende ukaigombea ukiipata ni haki yako.
    Tatizo kubwa linaloikabili kambi ya upinzani ni uwezo wa kujiendesha kimapato, na hili ni kosawakati tunaanzisha vyama vingi. Ilitakiwa mali yote ya TANU na ASP vitaifishwe na serikali, halafu vyama vianze venyewe kujiendesha, hapo ungeona kipi chama chenye uwezo. Hivi sasa vijiji vingine havijui kabisa nini maana ya upinzani,kila siku wanadanganywa kuwaupinzani ni vita, vujo nk.
    Kila siku natoa mfano kwenye makampuni mbalimbali kama simu, kwasababu yapo mengi na yanashindana uboreshaji wake ni mkubwa, na hii ingekuwepo kwenye vyama nafikiri leo tungeongea mengine. Sasa tufikie hatua vyama vyote vipewe nguvu sawa kiuchumi, na wananchi waelimishwe kisiasa, nafikiri tutafikia hatua nzuri
    Mungu tusaidie tuelewe nini maana ya demokrasia ya kweli
    M3

    ReplyDelete
  28. MHESHIMIWA KUJA WEWE UKO MAJUU HEBU TUELEZE HIVI VITUKO VYA UFISADI VINAVYOFANYWA NA WANACCM KUANZIA NGAZI YA URAISI MPAKA CHINI HUKO ULIKO VINAVUMILIKA? YAANI RAISI ANAWEZA AKAVUTA KITU KIDOGO NA AKAACHWA HIVIHIVI KUENDELEA KUWA RAISI? HIVI CHAGUZI ZA HUKO HUWA ZINASIMAMIWA NA FFU NA SILAHA NZITO? ONA SASA CCM NA POLISI HUKO PEMBA WAMEANZA VITUKO ETI WANADAI WAMEGUNDUA BOMU CHINI YA DARAJA USIKU WAKATI WAKIFANYA DORIA! HUU NI UONGO WAKITOTO, YAANI UNAPITA JUU YA DARAJA KISHA UNAHISI CHINI YAKE KUMETEGWA BOMU! SASA HIVI NI VITUKO WAKATI WA UANDIKISHAJI, JE, UPIGAJI KURA UTAKUWAJE? TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA, ILA CCM HAIUTAKI WARAKA WA KATOLIKI UNAOWAELIMISHA WANANCHI JINSI YA KUMCHAGUA KIONGOZI MZURI BILA YA KUJALI CHAMA CHAKE, DINI YAKE AU KABILA LAKE BALI UWEZO WAKE.

    ReplyDelete
  29. Kuhusu wabunge kufungwa mdomo siku za nyuma ni swala la ukweli. Mimi mwenyewe nimeshuudia mara kadhaa wabunge wakiitwa ofisini kwa waziri mkuu pindi wanapotoa shillingi ktk bajeti ya wizara. mida ya usiku mpaka usiku wa manane baada ya hapo utakuta yule mbunge amerudisha shillingi.Kipindi hicho bunge linafanyika karijee. Hivyo serikali ya Kikwete ndio inayoendesha nchi kidemokrasia. Wadau wengi humu hawajui kitu chochote ila kwa kuosha vinywa wamejaaaliwa. Tusilete mabishano ya chama hapa. Nina mengi nayajua lkn sitopenda kuingia ndani. Kumbukeni kuna mambo ya ndani na ya nje. Haya wanayayajua wadau ni ya nje ambayo yanalipotiwa na magazeti,ya ndani hawayajui.

    Mdau SuGu

    ReplyDelete
  30. kuja wp" ungeandika kwa kiswaahili, kiingereza haukijui. sasa sony 13:3 ndo nini, kama unayo je? hebbu rudia comment yako, wabongo bwana aliadnika kiswahili kachwambwa akadhania atuelewi kiinglishi yaani kiinlishi ndo kabisa kakoroga kweli kweli, utakoma kwa kuropoka kwako.

    ReplyDelete
  31. Kuja
    Upeo wako wa kuelewa mambo ya siasa ni mkubwa. Nimekee hapa natafakari kwa dhati hii article ndo nagundua hilo. Nime kuwa nikikusikia BBC kwa muda sasa, nikafikiri unajua tu siasa za huko US kumbe hata siasa za Tanzania unaijua vizuri sana
    Tatizo kubwa ni kuwa audience wanaotoa cooment wanatoa kwa kufuata jana na leo lakini wahakaichini wakafikiri kwa makini.
    Hongera sana Kijana

    Mdu Chuo Kikuu Dar

    ReplyDelete
  32. Huwezi kupenga makamasi na kufuta machozi at the same time inagwaje yote yanaweza kutoka kwa wakati mmoja. Kuhusu Hoja ya serikali kushindwa kufanya hili na lile, nafikiri tuwape muda, ili waweze kufanya yalioyabaki miaka mitano ijayo, wamepenga makamasi sasa tuwape nafasi watufe machozi
    Kuja unaongea na wachache sana kwenye blog, kwa sababu watu husau Historia mapema.
    Lakini uko sahihi kabisa

    Idd N. UK

    ReplyDelete
  33. Mdau Kuja,
    Kiingereza chako ni hafifu na kinahitaji kufanyiwa kazi, na kwa vile una kakompyuta cha Sony nakushauri upige msasa lugha yako ya 'kiingereza' kwa kutembelea webupeji hizi:

    -www.plainenglish.co.uk
    -www.primaryresources.co.uk
    *www.bbc.co.uk/worldservice/learningenlish(grammar and vocabulary)

    Mdau
    Mackenzie

    ReplyDelete
  34. Wadau
    Kiingereza cha huyo jamaa nimekisoma zaidi ya mara sita, sitajona vocabulary iliyokosewa, nafikiri Wivu unachukua nafasi kubwa sana katika comment kuliko reality. Wabongo tukiacha wivu tutaendelea sana. Jamaa amechambua kile hali halisi na ninafikiri hata future yake imetulia.
    Wabongo tuache wivu. Tuache wanaoweza kutoa maoni watoe.

    DC

    ReplyDelete
  35. Mdau Mackenzie
    Hizi website ulizopewa wakati ukijiandaa na GED unatuletea hapa.
    Hebu tuambie ni vocabulary gani jamaa kakosea, na wewe irekebishe. Ungetoa huu utumbo wa websites ulizopewa ulipofika hapa US na mifano kutoka kwenye vocabularies zake alizokosea ningekuona hata la saba umemaliza. Sasa website arekebishe nini!!
    Chukua Dictionary yako uangalie word after word halafu tuambie ni vocabulary gani haikustahili halafu suggest ya kwako.
    Unge muuliza mkeo kabla ya kutoa hizi comment usinge aibika
    Kuja ametoa maoni yake.wewe yako yako wapi!

    Nyambaf!!

    ReplyDelete
  36. mm nilishafikiri toka zamani upinzani hamna kitu bongo ccm itaendelea kutawala milele kwa kuwa wapinzani hawana sera 'BORA MWENDAWAZIMU ULIEMZOEA KULIKO MWENDAWAZIMU MGENI'

    ReplyDelete
  37. Mdau kuja unasakamwa kutokana na ujinga wako wa kujifanya kujua. Mbona wengine wasisakamwe heti Sony, Sony my behind. Ukiwa mjinga lazima umu ndani utaipata. Alafu hao BBC walichemka sana kumuweka mtu Kama wewe kutoa mchango wa kisiasa. Wee beba boxi ukisyaafu uridine tazanzania. Michuzi lawama ni yako na Yule fisadi John mashaka na shayo kwa maana ni wao ndo walioanzisha mambo ya kuandika kwenye hi forum Leo hii tunaona hadi famous wanna be kuja wanaleta hoja zisizokuwa na maana yaani za kujikomba tu m

    ReplyDelete
  38. Kuja:
    Hebu soma upupu wako hapo chini, wee mtu, unafahamu ile hospitali ya Mirembe, ni huko ndo unaelekea kwa maana umecopy na ku-paste kila kitu ambayo mengine haujui maana zake. Yaani matumizi yako ya lugha mwenzangu ni kimeo kikali kweli, piga brush yaani brush kubwa hicho kidhungu chako, inatia aibu kweli najisikia kutapika.

    DON’T GET ME WRONG PUNDITS

    To all Bloggers,
    As I place my fore head across my study table, looking intently at my laptop’s 13.3 Sonny made screen, reading between the lines, I see great ideas from great people. I have great respect for my natives, who has always made me proud of my country, a poor nation rich of great inspirations.

    One simple summit bloggers, I am purely made of democratic blood. I shall never be scared of your foul-smelling comments, rather, lifted and tentatively transformed. To those who disagree and agree with dignity, our destiny is unchanged. We suffer the same, while industrializing our thoughts, regrouping our arsenals ready to lift our country into a green-pasteurized planet. We cannot revolutionize whatever a thing from these standard-seven comments.

    Don’t get me wrong left-wingers, in 1995, I was below 18, but because of great philosophy and economic policies that Professor Lipumba’s CUF campaigned, I decided to vote before my legal voting age just to demonstrate my support to the Man I thought was born to rescue the country from deepen economic adversities. Frankly speaking, with all things remain constant, days remains seven in a week, and 12 month in a year, nothing changes at Buguruni’s CUF headquarters, the illegal vote I gave them in 1995 could be the last in history. I don’t say this because I hate CUF, rather, give them a reflective mirror to amend where is broken for better tomorrow.

    While we continue blogging comrades, I would like to remind the WVs (Waosha Vinywa), to watch-out their typing and word choices. This is not the place to dispose their ignorance and toilet-papered comments. With decree, this blog shall remain a place where dignified individuals table matters of high national importance to the board for debate and not caricatured attitudes.
    Thanks

    Kuja WP

    ReplyDelete
  39. Watanzania kweli tuna wivu wa kutisha. Hivi hapa ni kitu gani amekosea Mr. Kuja. Unajua tukiacha tabia ya wivu, najua tutaendelea sana. Na kitu kingine kila mtu ana uwezo wa kuandika kitu anachotaka. Sasa na wewe kama una cha kwako basi kiandike hapa, lakini sio kumkashifu mwenzio. Huyo mtu aliyetoa hizo WEB kwa ajili ya COURSE za Kiingereza, hizi course mara nyingi naziona kwa wale watu ambao wanajianda kusoma GED, kufanya PLACEMENT TEST.

    ReplyDelete
  40. kweli namuunga mkono mdau aliyemsaidia Mdau KujaWP atembelee www.plainenglish.co.uk

    Mfano wa matatizo ya Mdau KujaWP nayanukuu:
    -industralizing our thoughts?!!!
    -one simple summmit bloggers?!!!
    -to lift our country into a green pasteurized planet?!!
    -we cannot revolutionize whatever a thing from these standard seven-seven comments!!!

    Kwa hiyo ni muhimu kutumia kiingereza cha kawaida kinachotambulika ulimwenguni kote, kuliko kutumia 'bombastics' ambazo hazisaidii kufikisha ujumbe sahihi, hivyo nenda www.plainenglish.co.uk ujizatiti ktk lugha ya kiingereza.

    Mdau
    Kiparamoto
    Mbagala DSM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...