Warembo wanaowania taji la Miss Ilala wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kitengo cha Vodacom Foundation wakati walipotembelea makao makuu ya ofisi hiyo na kujionea jinsi ya shughuli mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo ya urembo
Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (kushoto)akiwaelezea jambo Warembo wanaowania taji la Miss Ilala jinsi kitengo hicho kinavyofanya kazi zake za kusaidia jamii.

Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza(kulia) akiwaelezea jambo Warembo wanaowania taji la Miss Ilala jinsi kitengo chake cha Masoko kinavyofanya kazi zake.
Warembo wanaowania taji la Miss Ilala wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kitengo cha masoko cha Vodacom
Mkuu wa kitengo kinachotoa huduma ya M pesa Franklin Bagalla(katikati)akiwaelekeza warembo wanaowania taji la Miss Ilala namna ya kujisajili na huduma ya M pesa walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania
Ngeleja kumshuhudia Redd’s Miss Ilala

Mwandishi wetu
WAZIRI wa Nishati na Madini William Ngeleja anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kinyanganyiro cha kumtafuta mrembo wa Redd’s Miss Ilala katika shindano litakalofanyika Ijumaa hii Agosti 7 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati ya kanda Miss Ilala, Jackson Kalikumtima alisema kuwa tayari waziri huyo amethibitisha kuhudhuria shindano hilo linalotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Akifafanua Kalikumtima alisema kuwa kwa mujibu wa mwalimu wa warembo hao Regina Mroni na matroni wao Nelly Kamwelu ni kwamba warembo hao wako tayari kwa shindano na kinachosubiriwa sasa ni siku ya mpambano huo wa fani ya ulimbwende.

“Mwalimu wao amenithibitishia kuwa warembo wako tayari kwa kila kitu, kuanzia mavazi, kutembea kwa mikogo yaani ‘catwork’ na kujibu maswali kwa ufasaha kutokana na mafunzo mbalimbali waliyoyapata wakiwa kwenye kambi yao iliyoanza Julai 14 kwenye hoteli ya Lamada & Apartements iliyopo jijini,” alisema Kalikumtima.

Mbali na hayo alisema kuwa jana ilikuwa siku ya warembo hao kufanyiwa uamuzi wa awali ‘pre judgement’ kabla ya siku ya shindano ili kufahamu uwezo na ufahamu wao kiujumla lengo likiwa ni kumpata mlimbwende mwenye sifa za kuiwakilisha kanda hiyo ya Ilala.

Vilevile warembo hao walipata fursa ya kutembelea magazeti ya kampuni ya New Habari Cooperation ambapo leo wanatarajiwa kutembelea kampuni ya The Guardian Limited kujifunza hatua mbalimbali zinazipotiwa katika uchapishaji na uandaaji magazeti.

Kabla ya hapo pia walitembelea maeneo mbalimbali mkoani Arusha, Kampuni ya utengenezaji video ya Sofia, Hifadhi ya Taifa ya ziwa Manyara, Kiwanda cha Banana Investiments Limited, Makumbusho ya elimu ya viumbe ya Arusha, TBL Arusha na maeneo mengine.

Warembo wanaowania taji hilo la Redd’s Miss Ilala kinyang’anyiro kitakachofanyika Agosti 7 kwenye viwanja vya Karimjee ni Glory Mwandwani, Pendo Lema, Nyamizi Mihayo, Irene Karubaga, Husna Omar, Neema Sylivester na Everyline Gamasa.

Wengine ni Fatma Bongi, Khadija Muhecha, Margareth Motau, Julieth Mombury, Sylivia Shally, Glads Shao, Anne Mkandawile, Doris Jimmy, Zena Mbasha na Winfrida Mmari





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MICHUZI NIMEKUONA LIVE KWENYE SKY 194 BEN TELEVISION KUMBE UNAJUA KIMOMBO KIASI HIKI? HONGERA SANA UMEKULA NUSU SAA LIVE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...