Abdallah Zombe akiongea na wakili wake Mh. Jerome Msemwa


Hukumu ya kesi ya mauaji iliyohusisha askari wa Jeshi la Polisi 9 pamoja na aliyekuwa mkuu wa upelelezi Dar Abdallah Zombe imeshaanza kusomwa Mahakama Kuu na hivi tunavyoongea Jaji Salum Masati yuko kwenye kusoma muhstasari wa hatua ya kesi hiyo ambapo sasa yupo kipengele cha shahidi wa 34.

Katika kesi hiyo ilipoanza rasmi kusikilizwa Mei 28, 2008, Zombe na wenzake wanatuhumiwa kuwaua kwa kukusudia Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi na Mathias Lunkombe ambao walikuwa wafanyabiashara wa Mahenge, pamoja na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es salaam, Juma Ndugu.

Inadaiwa kuwa watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye msitu wa Pande ulioko Mbezi Luisi wilayani Kinondoni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.


Watu hao walikamatwa na polisi kwa madai ya kuhusika kwenye tukio la ujambazi jijini Dar es salaam, ikaja kushukiwa kuwa waliouawa hawakuwa majambazi taarifa ambayo JK aliunda tume chini ya Jaji Kipenka Mussa ambayo uchunguzi wake ulisababisha kutiwa hatiani kwa watu hao na kufunguliwa kesi.

Globu ya Jamii ipo eneo la tukio. Kaa chonjo kwa taswira na habari zaidi...


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. poa Michu, tupe data....

    ReplyDelete
  2. poa Michu, tupe data....

    ReplyDelete
  3. sasa michu si ungetuambia sangapi, ina maana tusitoke hapa. si tunaenda kupiga box bwana...

    ReplyDelete
  4. Ngoja tusubili watakavyo achiwa,,,,

    ReplyDelete
  5. zombe anaachiwa huru leo

    ReplyDelete
  6. Hakika MIMI simjui ABDALLAH ZOMBE
    sijawahi kumwona sijawahi kumsikia sina habari naye lakini nimwonavyo katika picha anaonekana mtu wa mungu mashaallah anag`ara sijda inatoa nuru inaonyesha analindwa na aliyemuumba mungu awe pamoja nawe amin

    ReplyDelete
  7. ..Mimi nasubiri kuona reasoning ya jaji kwenye "chain of command"

    Yote tutajua leo

    ReplyDelete
  8. nitalia...

    ReplyDelete
  9. It should be fair..................................KAFANABO

    ReplyDelete
  10. mbona kimya, au ngoma mpaka usiku

    ReplyDelete
  11. TUNATAKA TUONE NA TUJUE VYOMBO VYA DOLA KM VITATENDA HAKI KWANI PROPAGANDA NI NYINGI WAKATI USHAHIDI UPO WAZI, ZOMBI NI MUUAJI ALIUA WENGI SI WAMAHENGE TU, AMEUA KINA MINE NA LEMA KWAKUWASHIRIKISHA NA MATUKIO YA UJAMBAZI YETU MACHO NA MASIKIO IWAPO SHERIA HAITATENDA HAKI BASI...HUKUMU YAKE NI MUNGU KM ILIVYOKUWA KWA MR. DITOPILE, WANYONGE TUKILIA NA MUNGU ANASIKIA ZOMBE SIO MTU NI JINI...

    ReplyDelete
  12. AAHHAAHAHHAH AHAHAHAHA AHAHAHAHHA ZOMBE KAACHIWA HAHAHHHA

    ReplyDelete
  13. AAHHAAHAHHAH AHAHAHAHA AHAHAHAHHA ZOMBE KAACHIWA HAHAHHHA

    ReplyDelete
  14. wote wameachiwa huru lol

    ReplyDelete
  15. duniani hakuna haki hata kidogo. Bora watu waendelee kuchukua sheria mkononi kama mahakama zinaachia watu kama hawa. Kibaya ni kwamba hukumu hii haitawaponza wengine zaidi ya CCM ikizingatiwa kwamba imetolewa katika kipindi karibu na uchaguzi. JK akae chonjo, ana kazi kweli kweli Mahenge kutokana na hii hukumu. Kweli majaji wetu wamesomea sheria za Pilato?

    ReplyDelete
  16. sidhani kama kuna haki tena nchini, wacha wafu wabebane

    ReplyDelete
  17. KAMA HII SERIKALI YA MUUZA SURA IMEAMUA KUMUACHIA BASI SISI TUTAMUUA WENYEWE KWAN HATA SISI TUNA ROHO MAYA KAMA YAKE UKIZINGATIA AMEUA NDUGU ZETU WA DAMU NA HAO CCM MWISHO WAO UMEFIKA MWAKA KESHO AFADHALI TUWAPE CHADEMA WANA UCHUNGU NA SISI MWASIKINI KWENYE NCHI YETU WAMETUNYANGANYA MALI ASILI SASA WANACHUKUA HATA HAKI ZETU ZA MSINGI

    UBIRINI HII TIME BOM MNAYOISET

    ReplyDelete
  18. MIMI SIMJUI HUYO ZOMBE LAKINI NINAONA HIVI NDIO UHURU WA MAHAKAMA. WATU WENGI WANAPENDA KUSEMA MTU NI GUILTY HATA KAMA HAWAIELEWI KESI NA SI SHAHIDI. KOTI HAITAKIWI KUTOA HUKUMU KWASABABU WATU WANAPIGA KELELE.

    ReplyDelete
  19. kama nihivyo kikwete unda tume ipeleleze kesi ya babuseya au nguza viking na watoto wake mbona mnawasweka ndani bila ya tume au tume ya uchunguzi ni kwa kuwasaidia vigogo kudadadeki zenu walahi,manikiz,greece

    ReplyDelete
  20. Tatizo letu waswahili tunahukumu kesi kabla nje ya mahakama. Waliofanya upelelezi wameshindwa kuthibitisha kwamba kina Zombe wana hatia, nyie mliokuwa mnasoma magazeti tu ndiyo mnaushahidi wa kuwahukumu hao watu. Kama hao jamaa imewachukua miaka 3 kufanya hayo waliyoyanya mnataka jaji apindishe sheria?

    ReplyDelete
  21. SASA AKAKUSANYE MSHIKO WAKE WA MIAKA YOTE NJE YA KAZI NA AFUNGUWE KESI YA MADAI ALIPWE FIDIA YAKE, WAMEMPE UTAJIRI, ANYWAY SIJUWI HUKO BONGO INAKAKAJE HUKU KWA WENZETU WANGEKWA MAMILIONI YA FIDIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...