Timu ya Pool ya mkoa wa Ilala (pichani juu) imeonesha ubabe katika mchezo huo unaokua kwa kasi hapa nchini na kutwaa ubingwa wa taifa katika mashindano ya Taifa ya pool yaliyofikia kileleni siku ya Jumamosi katika Ukumbi wa Royal Zambezi ulioko Mwanjelwa, jijini Mbeya.
Katika mashindano hayo yanayodhaminiwa na Safari Lager, timu ya mkoa wa Ilala iliibuka mshindi baada ya kuwaadhibu mahasimu wake wakubwa, ambao ni timu ya mkoa wa Kinondoni. Wenyeji timu ya mkoa wa Mbeya ilijinyakulia nafasi ya tatu baada ya kuilaza timu ya mkoa wa Mwanza. Ilala ilijinyakulia kombe, medali na kitita cha shilingi milioni tatu, wakati Kinondoni walipata shilingi milioni mbili na Mbeya shilingi milioni moja na laki mbili
bosi wa masoko wa TBL David Minja ( wa pili kulia) na meneja wa Safari Lager Anko Bundala (kulia) wakiwapongeza washindi baada ya kuwakabidhi kitita chao


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...