
Ifuatayo ni ratiba ya shughuli za kumuaga baba yetu mpendwa Mzee David Elias Mgwassa aliyetutoka siku ya Jumanne Agosti 25, 2009 na ambaye anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi Agosti 29, 2009 huko nyumbani Manda, kandokando ya Ziwa Nyasa.
Shughuli hii itakuwa palepale nyumbani kwa marehemu, Kijitonyama (nyuma ya showroom ya magari ya Samoyaz, usoni pa geti la Kijitonyama maghorofani.
*Saa 6 - Chakula
*Saa 7 - Sala kumuombea marehemu
Saa 8 - Heshima za Mwisho
*Saa 10 - Safari kuelekea Manda kwa Mazishi Kuanza
Familia inatoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani kwa kutufariji katika wakati huu mgumu wa maombolezo.
Bwana alileta,
na Bwana ametwaa.
Jina lake Lihimidiwe
Amina
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...