Mkuu wa mkoa wa naniii.. pole kwa kazi. Kwa mara ya kwanza nami nashiriki katika kujulisha jamii kuhusu inchi yale yatendekayo nje ya nchi yetu. Naomba niwatumie watanzania wenzangu picha mbili hizo kati ya nilizozinasa katika jumba la makumbusho la Taifa hapa London. Nilifurahi sana kukuta moja ya maonyesho ya africa, nchi yetu ilikuwa imetengewa ka sehemu kwenye vitu mbalimbali na wazungu wengi kutembelea na kupiga picha. Kwa upande mwingine kulikuwa na film fupi inayoonyesha jinsi gani kina mama watumiavyo kanga, kama uonavyo huyo mama nilimnasa akiwa anapiga vigegele huku akikimbia huko na kule. Kwa kweli ilikuwa furaha na ningependa bwana Michuzi niwashirikishe na watanzania wenzangu kuwa hata sisi tupo katika mataifa. Mzee mpya wa libeneke


Ni jambo zuri sana kuwepo na makumbusho ya namna haya kwani hata unaweza kukumbukia tulipotoka lakini ningependa zaidi kuwepo na vitu mbali mbali tulivyotumia wakati huo kwa mfano hapo naona khanga mbali mbali na vitenge lakini sijaona kitenge cha mawingu ambacho ndio kilitamba sana wakati huo...mdau uholanzi
ReplyDelete