VIJANA WA DODOMA WAKIJIFUNZA MPIRA WA KIKAPU WAKATI WA KLINIKI YA MAMBO PROJECT UWANJA WA JAMHURI, DODOMA
KOCHA BAHATI MOSES MGUNDA (KULIA) AKITOA MPIRA KWA MWAKILISHI WA TIMU YA SPURS
KOCHA BAHATI MOSES MGUNDA (SHOTO) AKITOA MIPIRA KWA MWAKILISHI WA SHULE YA MSINGI YA AMANI
KOCHA BAHATI MGUNDA AKITOA MAFUNZI KWA VIJANA ZAIDI YA 100
PICHA YA PAMOJA BAADA YA KLINIKI HIYO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA MAMBO BASKETBALL CLUB CHINI YA MAKOCHA BAHATI MGUNDA NA EVARIST MAPUNDA NA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU DODOMA WALIFANYA KLINIKI YA VIJANA WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MJINI DODOMA.

KLINIKI HIYOYA SIKU TANO ILIKUWA YA MAFANIKIO MAKUBWA AMBAPO VIJANA 128 WA UMRI CHINI YA MIAKA 14 NA WAKUBWA WAPATAO 38 WALIPATA MAFUNZO YA MCHEZO HUO
SHUKRANI ZA DHATI ZIENDE KWA WAFADHILI KADHAA WALIOFANIKISHA ZOEZI HILO IKIWA NI PAMOJA NA RAINBOW REST HOUSE ILIYOWAPA MALAZI WAKUFUNZI, SHABIBY BUS SERVICE KWA KUTOA TIKETI ZA DAR-DOM-DAR PAMOJA NA UBALOZI WA MAREKANI UIOTOA MIPIRA MITANO WAKATI WA KLINIKI YA BLUE BAND MAMBO.
TULIGAWA MIPIRA MIWILI KATI YA HIYO KWA SHULE YA MSINGI YA AMANI, MIPIRA MIWILI TULIGAWA KWA SHULE YA SKONDARI YA MAZENGO NA MPIRA MMOJA TULITOA KWA KLABU YA SPURS
TUNATOA OMBI LA KUPATIWA MIPIRA ZAIDI KWA AJILI YA MASHULE KWANI TUMEFARIJIKA KUONA WATOTO ZAIDI YA 100 WAKIJITOKEZA KUCHEZA MPIRA WA KIKAPU, WENGINE WAKIWA HAWANA HATA VIATU NA JEZI ZA KUCHEZEA
BAHATI MOSES MGUNDA
KOCHA - Mambo Project

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Good work on this one guys! nakuona mkuu yassin,thats the way to go!

    ReplyDelete
  2. Michuzi,kichwa cha habari kinasema ni mpira wa WAVU(Volleyball) japo Picha zinaonyesha ni Kliniki ya mpira wa Kikapu..Kijiwe changu hicho cha uwanja wa Jamhuri,Dodoma.Hongereni sana.

    ReplyDelete
  3. HAWA JAMAA WANAFANYA KITU KIZURI SANA TENA KWA MANUFAA YA TAIFA HAPO BAADAE. KUWAFUNZA VIJANA NI NJIA NZURI YA KUPATA WACHEZAJI BORA HAPO BAADAE. ILA NINA TATIZO MOJA TUU NA HII KLINIKI YAO, MIPIRA WANAYOTUMIA NI MIKUBWA KWA HAO WATOTO.. HAIKO PROPORTIONAL NA MIILI YAO. YAANI MPIRA ANAOTUMIA KOBE BRYANT NDIO AUTUMIE SIZE HIYO HIYO MTOTO WA DARASA LA TATU!! tuache utani jamani..
    -MZOZAJI

    ReplyDelete
  4. we mzozaji, si bora wao wametumia hiyo mipira mikubwa? mimi na wewe tumekalia longolongo tu kwa michuzi.

    ReplyDelete
  5. Thanks Bahati kwa juhudi zako za kuendeleza mpira wa kikapu usikate tamaa, pili naomba kutoa shukurani nyingi kwa kocha liyekuwa kijana kuliko wote enzi hizo Bahati alikuwa mchezaji hapo VIJANA(ZANAKI) ambaye anaitwa DELPHINUS PENESSIS juhudi zako zimezaa matunda naona vijana wako sasa hivi ndio wanondesha game lako ukiangalia akina MANASE, EVARIST na wengineo, naombo kama mtu anajua DELPHINUS YUKO WAPI nataka contact zake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...