Mkuu wa Wilaya ya naniniii!!!!
Kijikaratasi hiki kimesambazwa na baadhi ya watu leo baada ya Sala ya Ijumaa Malindi. Hii ina maanisha nini?
Mdau Zenji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 48 mpaka sasa

  1. Kwangu mimi naiona kama sehemu ya demokrasia, sehemu ya kutoa kile ulicho nacho moyoni, ama kwamikutano, vipeperushi au redio nk.

    ReplyDelete
  2. Aisee kwa hiyo Tanganyika ni beberu katika hili,wazanzibar tazameni mbele na si hapo mlipo kwa sasa.Mimi mtanzania nawashauri dhambi hiyo haitakoma kamwe ni mpaka mtakapokuwa unguja nnchi na pemba nnchi....tuwe pamoja tu.Angaliene Ngazija

    ReplyDelete
  3. Chacha Marwa, MusomaAugust 21, 2009

    KAMA MAMBO YAMEFIKIA HATUA HII, BASI NI BORA TUKAWAACHA HAWA WENZETU WAZENJI WAKAONGOZA NCHI YAO KIVYAOVYAO BADALA YA KUWASHIKILIA KAMA LUBA.
    NADHANI NYOTE MNAJUA KUWA MUUNGANO ULIOPO NI MAKUBALIANO YA MDOMO TU KATI YA MWALIMU NYERERE NA MZEE KARUME NA HAKUNA MAANDISHI HATA YA KWENYE TOILET PAPER.
    KAMA WENYEWE WAMESHTUKA BASI TUWAACHE WAJITAWALE.

    ReplyDelete
  4. Kule Mbeya tunasema 'IMBOMBO NGAFU!!' kule Tanga tunasema
    'KIRUUU!!' Mwanza tunasema
    'BHOKULA UBHUJIKU!!'na Singida tunasema 'TAPI ULUGANO'-maana yake 'HII KALI'

    ReplyDelete
  5. Haimaanishi chochote, Zanzibar bado itabaki kuwa Mkoa, mkileta nyodo tunawadunda.

    Bara taifa kubwa!!! macho yenu!!!!!!

    ReplyDelete
  6. Uchochezi tu huo wa watu fulani.

    ReplyDelete
  7. Wadau wenye utaaramu ni Muungano naomba mnisaidie; hivi katika muungano huu nani anafaidika?
    Siku zote mtazamo wangu naona ndugu zangu wa Zanzibar wanafaidika zaidi kwani wanapata ajira zaidi kuliko bara, vile vile wao wanapata huduma nyingi kutoka bara mara nyingine bure.
    Je kwa kuwa wao hawataki Muungano kwanini tusiwaachie wakaondoka?
    I could be wrong ila wenye utaaramu naomba wanisaidie

    ReplyDelete
  8. Uncle Michuzi,
    Naomba niwe labda wa kwanza kuchangia hii mada iliyotolewa na mdau wa zanzibar.
    Kikubwa kwangu ni kujibu swali lake la hii ni nini?

    na nafikiri kwa mimi mtanganyika ninayeishi hapa unguja(huwezi kupinga kujiita mtanganyika wakati kuna mzanzibari) labda naweza nikawa na upeo mdogo katika kulitolea jibu swali lake.

    Naanza kwa mawazo haya:
    Umoja wa Wazalendo ni chama cha siasa ambacho hakijapata usajili bado, kina lengo la kuwaunganisha wazanzibari wenyewe ili wazijue haki zao kwanza, waujue umoja wao umeegemea wapi ili siku wakiwa katika nafasi nzuri ya kuutambua undugu wao waweze kuja na hoja kabambe kuhusu mambo yanayotia doa muungano wetu> hizi ni fikra zangu. Lakini sasa, inaonekana kuwa umoja huu unawasahau wazanzibari ambao hajaishi hapa zanzibar kwa muda mredu na hata wazanzibari ambao wanaongozwa na jaji wetu mkuu.
    Kama mtu anatoa mwamko kwa wazanzibari walio waislam ili kujilinda na gaidi tanganyika na kuwasahau watu muhimu kama wakina Augustino Ramadhani ujue hana lengo la kuwaunganisha wazanzibari bali kuwatenganisha. Ni nafasi nzuri sasa kwa wao kufikiri nini mzee kingunge alisema.
    Siasa haiwezi kutenganisha watu kwani misingi yake imejijenga katika sheria zitungwazo na watu wenye imani na fikra sawa. lakini dini ni chombo kitenganishacho watu kwani sheria zake nyingi ni za kijadi, kuzibadilisha ni vigumu na zimejengwa katika imani. kama inatokea mtu anatumia pesa nyingi na muda kutenganisha watu katika misingi ya dini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mfungo wa ramdhani, inapasa wazanzibari wenyewe wafunge kwa ajili yake ili apate kubadilika.
    Pili kama tunashindwa kujua tatizo letu limeelekea wapi basi ni rahisi zaidi kufahamu msambazaji wa taarifa hiyo si mzanzibari.
    Jamani, wazanzibari, hebu shikamaneni ili nasi watanganyika tuelewe misingi yamalalamiko yenu yameegemea wapi.
    Asante!

    ReplyDelete
  9. Inamaanisha kwamba mtu katoa fikra zake anazodhani ni muafaka. sasa kazi kwako kuchambua kama ni fikra sahihi fuata kama sio sahihi chapa lapa!!

    ReplyDelete
  10. Maswali mengi hewa! wewe umeambiwa huo ni mtihani unahitaji majibu. Anamaanisha soma hiyo karatasi sasa kama huelewe muulize mwenzio acheni kutuchosha na hadithi hizo hizo January hadi December.

    ReplyDelete
  11. Mana yake ni FATAKI wa siasa sasa wewe mwambie SIDANGANYIKI!

    ReplyDelete
  12. Mtoto akililia wembe mwache umkate.......uliimbwa na sikinde.

    ReplyDelete
  13. watu wachache kama hawa ndio wanawachafua waislam waonekane wabaya magaidi nk sasa hoja yake kama ni mambo ya muungano na tanganyika kwa nini ahusianishe na uislaam?

    ReplyDelete
  14. UNCLE NANI HII,

    KWA MUDA MREFU SASA TUMEKUWA NA MALUMBANO KUHUSU UZANZIBAR NA UTANGANYIKA,NIMEKUWA NAFUATILIA KWA MBALI NA BADO NITAFUATILIA KWA MBALI KWASABABU YANIUMA MNO KUKAA NA NDUGU YANGU NA KUANZA KULUMBANA KUHUSU UDUGU HUO. ILI NISIENDELEE KUUMIA NA KUANZA KUJIULIZA NANI ATAFAIDIKA NA NINI, MIMI NINGESHAURI KILA MOJA AKAE KWAKE, NDIO! ZANZIBAR IWE NCHI INAYOJITEGEA! HATA KWA KUFUTA MUUNGANO HUU AMBAO BILA SHAKA UNA WALAKINI! KAMA UNGEKUWA UMEWEKWA VIZURI TUSENGELUMBANA BUREE! KENYA UGANDA NI NDUGU WA KARIBU TU, NA SASA HIVI TUNAPANGA MIPANGO MIZURI YA KUWA NA FEDERATION , PAMOJA NA MIPANGO HIYO KUWA TARATIBU!NINGEPENDA KUTOGOMBANISHWA NDUGU YANGU KWA ARDHI NA MALI! AU KWA UELEWA MDOGO UZALENDO/MSHIKAMANO!
    NASIO HIVYO TU JE WABARA TUMEJIANGALIA VIPI KWA SWALA HILI?
    TUKAE TUKIJUA KWAMBA MAMBO HAYA HAYAJI HIVI HIVI TU, KUNA SABABU, PLEASE LET US WORK ON THIS, PAMOJA.

    MZEE WA MWANZA

    ReplyDelete
  15. hakuna tofauti wa waraka wa kanisa katoliki kutetea dini yao.kwa kule zenji walichofanya ni sawa ikizingatia asilimia kubwa ni waislamu na lengo kuu ni kuacha machafuko na ni dhahiri kuwa wasipokuwa makini inaweza jirudia ya miaka ya nyuma na majeshi ya bara ndio upelekwa kule, kwa tanzania mafundisho watu yanawaingia ukizingatia vifungo vya dini kuliko njia nyingine.

    MWISHO NI KUWA TUJIEPUESHE NA UDINI KANI UNAWEZA ANGAMIZA TAIFA LETU NDANI YA MUDA MFUPI. MACHAFUKO YA KIDINI NI MABAYA SANA.
    NA TUELEWE KUWA WARAKA WOWOTE UKITOLEWA NA KIKUNDI CHA DINI KUHUSU MAMBO YA SIASA,KAMA KUCHAGUA VIONGOZI LAZIMA KUNA INTEREST ZA DINI HUSIKA.AMANI ZANZIBAR, AMANI TANGANYIKA .HUDUMU MUUNGANO.VIONGOZI WA KIDINI WAACHE UBINAFSI

    ReplyDelete
  16. HII NI DALILI KUWA HUKO VISIWANI WATU WANANJAA KALI UJUWE DEBE TUPU HALIACHI KUPINGA KELELE
    AU KELELE ZA CHURA HAZIMZUII NG'OMBE KUNYWA MAJI
    KWA MAANA HIYO BASI WALE WAVISIWANI WENYE UWEZO SIRAHISI KUWA KTK MAMBO HAYA ILA MAMBO HAYA NI YA WENGI WENYE NJAA NA NJAA YAO HAIJARETWA NA BARA ILA ITAKUWA IMELETWA NA KASUMBA YAO YA UMWINYI

    ReplyDelete
  17. kwa kweli Mungu awasaidie hawa wazanzibari sijui wafanywe nini kuona wanakula na kipofu, maana wenyewe hawajiwezi kabisa nilienda huko kikazi mbona nilichoka watu wanaingia ofisini kuanzia saa nne -tano, tulivyotoka lunch nikawambia wawahi kurudi nataka kazi iliyonipeka nianze kutuma ripoti kwani asubuhi sikupata muda nao ehh wakaniambia sie mpaka kesho tukienda lunch haturudi, jamani sio kazi ya serikali ni private, niliwaambia hakuna wakuwafanyia kazi hapa mtarudi na nataka iishe walikaa mpaka saa 4 usiku. Hawataki kunisikia hata jina

    ReplyDelete
  18. Sikinde waliimba "mtoto akililia wembe............"

    ReplyDelete
  19. Nyie wazanzibari acheni hizo chokochoko. kumbukeni kuna wapemba kibao Tanganyika. mkivunja muungano huu tafuteni ngalawa za kuwavusha ndg zenu wapemba waishio bara na mali zao zitataifishwa.

    ReplyDelete
  20. Someni historia uzuri hayo ya vipeperushi yalikuwepo tangu enzi,Muungano una wenyewe hatuwezi kuona watu uchwara wakiuchezea. Msione vyaelea vimeumbwa............

    ReplyDelete
  21. Mi naona wasituzingue hao,kama wanaona wanafanywa jimbo,basi wajue kuna mikakati ya kufanywa wilaya na baadaye labda kuwa kata,kama ilivyo kata ya 14 temeke...
    kama wanaona wananyonywa waanze mbele,kwanza hawana hata kitu,kazi kucheza bao...
    MI naona suluhisho ni Unguja na Pemba kujitenga na kuwa nchi mojamoja na rais wa pemba kuwa Hamad na wa Unguja kuwa Karume na wa Bara baba lao Kikwete.

    Mtoto akililia wembe kama ni wako,haumpi,kama si wako unampa...sasa hao si wa kwetu basi wapewe wembe,waanze kuchinjana wao kwa wao.
    Michuzi rusha oni langu hili.

    ReplyDelete
  22. Wakati dunia nzima inaangalia jinsi ya kuungana, nyie mnafikiria jinsi ya kufarakana. Duh. Michu mdogo wangu paaza sauti waambie wako dunia ya BC (kabla ya yesu kristo kuzaliwa). Michu mdogo wangu nawasilisha, MH

    ReplyDelete
  23. Haya sasa - Mambo ya "Uvumbuzi wa Mafuta".
    Mie naona hakuna muungano (Union). Kilichopo ni "Intersection".

    ReplyDelete
  24. HUU NI UCHOCHEZI, MATUMIZI HAFIFU NA TAFSIRI MBAYA YA DINI YETU YA AMANI YA KI ISLAMU, MAONO MAFUPI YATOKANAYO NA FIKRA DHAIFU ZA UTENGANO.

    2.MATAIFU YENYE UCHUMI KOMAVU YANAUNGANA KWA MITINDO NA MIUNDO MBALIMBALI ILIMRADI NGUVU MOJA NA WANATUMIA MAUNGANO YAO KWA MANUFAA BORA ZAIDI. SISI WATANZANIA NI BORA TUENZI MUUNGANO WETU AMBAO HAUKUJA KIMAKOSA. TUTAFUTE JINSI GANI JAMHURI YETU ITATUNUFAISHA KATIKA USHINDANI HUU MKALI WA UTANDAWAZI.

    3.VIONGOZI WOTE WA SIASA WANAOONA MBALI LAZIMA WAKEMEE KWA KAULI MOJA VITENDO HIVI VYA KUCHOCHEA MACHAFUKO. HUU PIA NI UGAIDI TU.

    4.TANGANYIKA ILIKWISHA ZIKWA.UTAMBUZI WA KITAIFA NA KIMATAIFA NI NCHI YA TANZANIA.MWANDAAJI, MCHAPISHAJI NA MGAWAJI WA VIPEPERUSHI HIVI LAZIMA ATAMBUE YU MWENYE MAKOSA NA TULIPOFIKA KUITAMBUA TANGANYIKA NA TENA KAMA MKOLONI NI MAKOSA YA JINAI. JAMHURI NI VEMA IMSAIDIE HARAKA.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA. UMOJA NI NGUVU.

    MAINA ANG'IELA OWINO.

    ReplyDelete
  25. Mtanganyika 100%August 21, 2009

    Unauliza mikarafuu pemba??? Hiyo inamaana wazanzibar washaamka wanataka Tanzania yao!

    ReplyDelete
  26. ndugu zetu hizo wanazoleta sizo
    nchi kubwa kama England,France and,
    Germany zinaugana na zinaona zimechelewa wapemba ndio kwanza wana
    njaa ya kujitenge kweli shule sio starehe ni...

    ReplyDelete
  27. Hivi bongo au wabara tunapata nini kutoka kwenye muungano huu? Kila kitu tunawapa hawa watu na hawashukuru, kuna vyuo vikuu vingapi huko zanzibar? Chuo kikuu tulisoma nao kibao wamejaa nyumba zote kwa pesa ya muungano. Hembu jk wape vacation ya mwaka mmoja tuone kama wataweza kusimama na mwarabu atashuka tena kuja kuwatumikisha na ndiyo wanachotaka!!!

    ReplyDelete
  28. Ndugu bila kuchagua dini siku zote historia inaonyesha watu wanapojaribu kupigania haki zao kwa kutumia mlengo wa dini wameishia kupata matatizo wenyewe.
    Mifano ni mingi kuanzia kwa ndugu zetu wa Uharabuni, Northern Ireland n.k.
    This is cheap politics where people have no concrete policies to unite the mass, instead they rely on easy targets like religion..
    Trust me..hawa watu hawawapendei mema ndugu zetu wa Zanzibar..

    ReplyDelete
  29. Hongereni wadau kwa kutoa maoni.m
    Mada hii inaonekana kuwa na mvuto kwa watu wengi. Nadhani kinachotakikana ni hoja na sio jazba na gazabu. Mimi siungi mkono kuhusisha dini katika hili kama hiyo makala ilivyosema. Kinachojitokeza hapa ni kuwa Wazanzibar hawaridhiki na uendeshaji wa muungano kama ulivyo sasa. Na kama kweli Zanzibar ilikuwa ni dola huru yenye maamuzi yake wenyewe kuna mambo mengi ya kuzingatia kwa hali ya muungano ulivyo. Kwani hivi sasa hawana mamlaka ya kufanya maamuzi pasina ruhusa ya Serikali ya Muungano ambayo kwa madai yao ndio hiyo Mkoloni Tanganyika. Kama huwezi kujiamulia mambo yako basi huna uhuru na yule anaeamua ndio matawala. Sasa kama wanaotawaliwa hajarizika na mtawala, huyo mtawala anakuwa mkoloni.
    Kwa kuhofu hali kama hiyo Tanzania imekuwa makini sana katika Jumuiya ya Afrika ya mashariki ili isije ikawa kama ilivyo Zenj katika muungano. Waacheni wazanzibari yaheee!!!!!!!!! nao waseme, wanaonewa etiiii!!!!!!!!!.

    ReplyDelete
  30. Nshimimana aka DumisaneAugust 21, 2009

    inategemeana hapo!? Maybe, Maybe Not.. SIKUJUA KAMA ITAKUWA HIVI!

    "... na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao ..."

    = = =
    Buffalo (karibu na Glory Nursing Home),
    New York

    ReplyDelete
  31. WAACHE HUO MUUNGANO UISHIE KILA MMOJA AKACHUKUA CHAKE KILA MOJA AKAJUA NINI CHA KUFANYA KWA KUWA HUU MUUNGANO NAONA UNAJENGA CHUKI TU,SIONI MWISHO WAKE UTAKUWA MZURI NASIONI ZANZIBAR KWA NINI TUSIACHANE NAO SISI BARA TUNA SHIDA GANI NA ZANZIBAR???? WAVIVU,ELIMU DUNI IPO ZANZIBAR HAIPO BARA,ZANZIBAR NI SAWA NA NA WILAYA TENA YA ILALA TU KWA UKUBWA HATA BAGAMOYO NI KUBWA LAKINI UPENDELEO WANAOPATA KULIKO HATA MKOA MKUBWA WA MBEYA AU ARUSHA ,TUACHANE NAO TUONE NANI??? ATASAGA MENO

    ReplyDelete
  32. jama mbona tumengangania muungano uvunjwe...wapemba warudi kwao...na upumbavu kama huo...tuamke hapa bara serikali yetu itutengezee ajira, iboreshe miundo mbinu, iongeze chansi za kusoma na mambo ya msingi...sio viongoz kwenda beverly hills na sie kulumbana kati ya upemba na ubara...wte watu tu...nchi zilizoendelea watu hawaziliwi na pesa waungwana...tuamke jamaa sio tukae vijiwen na kuongea utumbo mara tunawasaidia wapemba mara ivi mara vile...ni wangu matazamo tu waosha vinywa msijenge chuki

    ReplyDelete
  33. Huu ni mdahalo mzuri sana nilikuwa nachelea kuingia kutoa maoni kutoka na utete wa mada yenyewe, hadi sasa kuna watoa maoni wametoa hoja za msingi na kuna wale waliashiria jazba kulingana na sehemu wanayotaka katika muungano wetu wa tanzania. Hata hivyo wengi wetu kutoka pande zote nadhani tunakubaliana kwamba kuna matatizo ya msingi katika muungano wetu, ndio maana umekuwa ukitikiswa kila kukicha kutoka pande zote mbili. Jamaa zangu wachache sana kule Zanzibar wanaelewa kuwa hata bara kuna watu wengi tu wamechoshwa na muungano, ndio maana wanafika kuita bara ni mkoloni wa Zanzibar.

    Lawama hizi zinatoka na jinsi muungano wenyewe ulivoasisiwa, kwani ushirikishwaji na ridhaa ya wananchi ilikuwa ndogo sana, hali kadhalika, msingi wa katiba nyenyewe ya muungano una mashaka kwa vile katiba ya sasa ya muungano inafanana sana na ile iliyotumika tanganyika kabla kuungana. Hili ndio chimbuko la matatizo yote haya, muungano wetu ni association of unequals ndio maana matatizo hayaishi, kwa mfano mtu wa bara akilalamika Zanzibar iko over represented bungeni atakuwa na hali ya kuhoji hilo kwa vile ni ukweli na hali kadhalika malalamiko kama hayo kutoka kwa wazanzibari.

    Tatizo ninaloliona kule Zanzibar ni kwamba watu wanalinganisha hali ya kiuchumi ya zanzibar kabla ya muungano na sasa, ndio maana malalamiko yanakuwa mengi, ni kweli kipindi cha nyuma zanzibar ilistawi zaidi kiuchumi licha ya kuwepo ubaguzi kati serikali ya kisultani. Zanzibar ni sehemu ndogo sana hivyo kuiwekea sera za uchumi sawa na bara nikuionea ndio maana inashindwa kupiga hatua mbele na badala yake kila kukicha hali ya maisha inazidi kudidimia. Licha ya matatizo ya kuichumi kuna wazanzibari, ambao naamini ni wachache sana wanaokerwa na utaifa na identity ya uzanzibar kimataifa, hawa nahisi kidogo wapo irrational, manake kama kukasirika wanapoambia Zanzibar sio nchi inatokana na ueleo mdogo, nadhan hata mtoto wangu wa miaka 4 anaweza kunielewa kwenye hili, huwezi kuunganisha nchi mbili ukapata taifa moja litwalo tanzania na bado ukawa na taifa linaitwa zanzibar nje ya tanzania.

    Kwa mtanzamo wangu Zanzibar, inahitaji irudishiwe mamlaka ya kujiamulia maswala ya kiuchumi na kibiashara mradi hayakiuki katiba ya jamhuri, kwa kweli hata bara nahisi mikoa yetu inahitaji kupewa mamlaka fulani ya kujiamulia maswala kama viwango vya kodi na mambo ya kibiashara, ili iweze kunufaika zaidi kutokana bidhaa wanazozalisha au kuweza kusaidia wananchi wa mkoa kuhisika, kwa vile hali ya kuichumi haifanani tanzania nzima. Kwa mfano madini yanaiyochimbwa mirerani yanapaswa kunufaisha zaidi huko hali kadhalika vitu kama korosho kwa kusini au kule mtera wanakotumia maji kuzalisha umeme na sio kusiphon utajiri wote huo kuupeleka dari salama ukaliwa na wajanja.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  34. NI WAKTI WA WAISLAMU SASA KULILIA HAKI ZAO ZAMSINGI NIWAZI KILA PALIPONA JAMII YA KIISLAMU PANA MAKANDAMIZO,KUNYIMWA KWA HAKIZAO,MM NASAPORT JAMBO HILO KWA MKONO MMOJA COZ WATAFANYA NINI NA HAWANA VYOMBO VYENYE SAUTI KWA NIABA YAO NATAJIRI WA KIISLAM HAWATAKI KUJITOLEA KATK HARAKATI WAO NI MPIRA NA WAO SIASA NA KUOGOPA WATAGONGEWA HODI NA TRA WAKISAPORT HARAKATI ZA KIISLAM FANYENI SIRI BASI ACHENI UPUUZI KIFO KIPO ADHABU ZA KABURI ZIPO NA MOTO UPO,KUZIBANA KWENU PESA ZENU KUNAATHIRI MENGI KTK KIZAZI CHA KIISLAMU JUENI HILO.MDAU GREECE

    ReplyDelete
  35. wotw huu ni umaskini tu, france na monaco, uk na scotland, china na hongkong, wote hawa wanaendelea vizuri tu

    ReplyDelete
  36. Naupongeza huo witu uliotolewa hapo wa kuhamasisha umoja wa wazanzibar ila naomba nitofautiane na hizo propaganda zilizotumika hapo, kwa mfano kutafuta mchawi wa ubaguzi wetu na kuitupia lawama bara moja kwa moja ni kuionea! Tumeanza kubaguana toka enzi za ukoloni, sijui huyo mpemba, yule muunguja, mimi mwarabu sijui wale wavuka maji, au wengine kujiona wanamapinduzi na kadhalika.

    Lazima tukubali wazanzibar wengi tuna sumu ya ubaguzi inatiririka katika damu zetu kwa hiyo tusitafute mchawi. Kwa mfano tunavyolalamikia wabara waliohamia karibuni kuona hawana haki ya kuishi zanzibar, hebu tujiulize kama tumewakaribisha waarabu waliotoka miles chungunzima nao wakajiita wazanzibari hatuoni haya kuwabugudhi jamaa zetu wa karibu kutoka bara kuanza kuwaita wavuka maji sijui vichogo na majina mengine ya kukashifu kama hayo?

    Ubaguzi tuna uentertain wenyewe, kwa mfano swala la serikali na utawala, hebu niambie hii hali ya sasa ya siasa ya zanzibar ambapo uwakilishwaji wa wapemba katika serikali ya mapinduzi ni mdogo sana licha ya kuwepo wanachama wa CCM na wananchi wengine kutoka pemba wanaomuunga mkono Karume na wenye uwezo wa kujaza nafasi hizo, kweli hapo bado tunaclaim wa bara ndio wabaya wetu? wakati kwenye serikali ya muungano kuna viongozi kutoka pemba zaidi ya waliomo katika serikali ya Karume? ubaguzi kama huu rais Karume anausimamia bila woga wakati hata mwenyewe akichosha watu huandamwa hadi na wanaCCM eti baba yake ni mhamiaji tu Zanzibar hana asili ya Mwera, mara sijui kwao Malawi. Tuache hizi chuki hazijengi, hata kama wananchi wa pemba wangekuwa hawakumpigia kura hata moja its unfair. Bara kuna utaratibu mzuri ambapo karibu kila mkoa umechangia viongozi katika serikali even though hakuna ulazima huo kikatiba.

    Kwa mtazamo wangu nahisi muda umefika zanzibar inahitaji kutibu vidonda vya historia yake mwenyewe, kasumba kama mapinduzi daima, sujui yule alikuwa hizbu na kadhalika ishapitwa na wakati na ndio chanzo cha kuendelea kubreed chuki, husda na ubaguzi hadi huu unaoendelea sasa wa vyama vya siasa, kabla hatujadai huo utaifa wetu kuna haja ya kushuhulikia hilo, idea ya kuwa na serikali inayojiita ya mapinduzi haiashiri umoja wala misingi bora ya utawala na demokrasia zaidi ni ubabe tu, ukizingatia kuna wananchi mababu zao waliuliwa au wengine kufanyiwa uonevu kutoka na mapinduzi, nadhani kwa kuanzia tunahitaji serikali ya Zanzibar bila hicho kibwagizo cha mapinduzi. Najua hii nimeandika hapa ni dhambi kubwa sana kule kwetu na wangine watanichukulia mhaini nataka kurudisha usultani, ila huu ndio mtazamo wangu na wala hauhusiani na asili yangu ila kwa refference tu ngoja nijieleze, mimi Mtanzania kutoka Zanzibar, mzaliwa wa pemba, nina miaka 27, kiasili ni mweusi sina uanachama wa chama chochote na sijawahi kujumuika kuchagua kiongozi yeyote bara au Zanzibar. By the way, hakuna babu yangu hata mmoja aliuliwa kutokana na mapinduzi ila naamini wapo waliofanyiwa madhila kama hayo.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  37. Jamani, Napata uchungu kuona haka kakoloni ketu kanaanza kuchoropoka. Kwa nini tuliwaruhusu kupata kaelimu kidogo? Ilibidi waachwe wakipiga kaswida siku zote, nasi tungeendelea kukandamiza. Lakini poa tu, inji yetu kubwa. Mbona angola kuna mafuta, inatudhruru nini cc? Mbona Libya, Sudan, Dubai na nchi nyingine pia zina mafuta? Kama tulishindwa kulamba bingo wakati kazanzibar kakiwa kakoloni ketu tuwaachie kanchi kao tutatafuta namna engine ya kuzapata. Kwa uzoefu wangu, tukiwapa uhuru bado watabaki kuwa tegemezi kwa cc tuliokuwa wakoloni wao. iyo iko dunia nzima

    ReplyDelete
  38. Sasa wakiungana wazanzibari ndio itakuwa nchi yenye nguvu? Naona hayo mafuta yanawachanganya akili... hawajui kuwa miaka 10 ijayo gas/petrol stations nyingi zitatoweka nchi za magharibi? Biashara ya mafuta itadoda muda sio mrefu kwenye soko dunia ya kwanza... Kalagabahoi ndugu zangu wa-Zanzibar.
    Mdogo wangu Michuzi usinibanie..

    Mdau wa Liwale

    ReplyDelete
  39. Dini inakuwa na nguvu kuliko chochote kile.
    muungano wetu utakuwa na shida milele.
    nchi zote zilizoungana kama hizo za ulaya huwa zinafanana kimazingira.mfano nchi zote hizo zina dini na utamaduni unaofanana.
    Huu muungano wetu ni wa watu tofauti kabisa
    sijawahi kuona kuwa nchi moja ya walio waisilamu wote wakaungana na nchi nyengine ya wakatoliki.hapa patakuwa na vurugu tu.
    Tanganyika ni nchi ya wakiristo( HATA KAMA WAPO WAISILAMU BASI HAWANA NGUVU YEYOTE ILE KATIKA MAAMUZI YA NCHI)Tanganyika inaongozwa na kanisa.
    Zanzibar ni nchi ya waisilamu watupu.asilimia mia huko ni waisilamu.mkiristo huko zenj ni mgeni tu.
    sasa hapa haitowezekana kwa nchi mbili zenye culture tofauti,dini tofauti zikaungana na kuwa kitu kimoja kaka.
    mwisho wa muungano huu ni lawama tu.
    natowa mfano hapa huku kuna waraka wa kanisa ambao unatowa muongozo wa kuchagua kiongozi safi. na huko zenji kuna waraka huo hapo juu wa kiisilamu.mambo haya yatakwenda vipi.?

    ReplyDelete
  40. assalam aleykum
    Nawatakia Nyote Ramadhan Karem.

    1) Wajemeni kwanza tunasahau kuwa Zanzibar ilikuwa ni nchi kamili yenye kiti chake mpaka umoja wa mataifa (UN)

    2)zanzibar kumekuwa na taa za barabarani kuliko nchi nyingi za Ulaza seuze Africa.

    3) Kinachopiganiwa, ni haki ya zanzibar kwenye Muungano, Watanzania wengi wanachanganya madawa, kati ya idadiya watu na ukubwa wa eneo na taswira ya kinchi. Napenda nikumbushe kuwa Zanzibar na Tanganyika ziliungana kama nchi mbili (zilizo sawa) regardless ya idadi ya watu na land

    4) Kinachopiganiwa ni wazanzibari ni kuondoa ukoloni wa Tanganyika ndani ya nchi yao. It is very unfortunate kuwa Mzee Karume alizidiwa nguvu na maarifa na mwalimu Nyerere.

    5) Wajemeni munajua kuwa mpaka nembo ya Tanzania ni ya jamuhuri ya Tanganyika haijabadilishwa mpaka leo

    6)Wajemeni munajua kilichofanyika ni kugeuza Serikali ya Tanganyika kuwa Serikali ya Tanzania

    7)Nduguzanguni, munakubaliana nami kuwa misaada inayokuja Tanzania yote inabaki Tanganyika, na eti zanzibar wanapewa 4.5%, hii haki iko wapi?.

    8)Mutakubaliana nami kuwa Zanzibar imepoteza utaifa wakati Tanganyika wamejigeuza jina kujiita Tanzania.

    9) Jameni tuwe waadilifu, tuamini kuwa Mungu yuko kwa dini yeyote tunayofuata, dhulma haikubaliki in any case. Tufikeni wakati tukubali mambo mawili
    a) Tutendeni haki, Kama ni Muungano basi tufanyeni 50%

    b) Kama hilo ni gumu ambalo naamini watani wetu (watanganyika) hawakubali basi ni bora tugawane, kila mtu aanze kivyake.

    NB: Kuna watu wanajidanganya kuwa Zanzibar ikiachiwa itagombana au watakufa kwa njaa. Hizi ni akili potofu ambazo hazizingatii historia. We have plenty of resources including seas, possible petroleum resources, na kikubwa chao no HUMAN RESOURCES, ukichukulia ratio ya population, Zanzibar ina PhD holders wengi kuliko Tanganyika, wengi wako tayari kurudi nyumabni hata kesho kama Ukoloni wa Tanganyika wakitupatia uhuru wetu

    Kila la kheri na naomba msamaha kama nitaudhi wadau, huu ni mwezi mtukufu, tunatakiwa tuambizane ukweli bila maudhi.

    ReplyDelete
  41. Rais ni MUISLAMU,Makamu wake ni MMUISLAMU,Jaji Mkuu ni Muislamu,Waziri wa Ulinzi ni Muislamu,Mawaziri katika Ofisi Ya Rais Utumishi,Utawala Bora,Mazingira ni WAISLAMU,Waziri wa Fedha niMUISLAMU,IGP ni MUISLAMu,Kova ni MUISLAMU,Wizara Nyeti zimeshikwa na WAISLAMU,sasa Anaepinga huo Uislamu ni nani?Mbona siwaelewi?Mbona Waislamu mnapenda sana Malumbano na ugomvi?Ingekuwa ni wakristo watupu walioshika hizo nyadhfa hapo juu mngekaa kimya kama ambavyo sisi tupo kimya?Mbona sisi tunaunga mkono juhudi za maendeleo bila kulalamika,au nasisi tuanze kuomba MAHAKAMA YETU?au na sisi tuanze kuomba kujiunga na jumuia za KIKRISTO?sote tukijiamulia kuendesha nchi kidini tutafika kweli?ANYWAYZ-siku hizi samaki 1 akioza wutupi wote,unamchomoa na kuendelea na mauzo ya wazima,so mi nadhani ifike wakati tufumbe macho,hata Dunia ikisema TZ imeshindwa muungano,tuwaache wao waendelee na dini yao ili sisi tanganyika tuendeleze taifa lisilo na udini,au huyu samaki alieoza atawaambukiza na wengine!Pia yawezekana wanoung'ang'ania Muungano ni MACHOTARA wasiojua hatma yao baada ya kuuvunja!MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  42. Mojawapo kati ya haya linatakiwa lifanyike, vinginevyo huu wimbo wa Tanganyika na Zanzibar utaimbwa mpaka siku ya qiyama. Aidha MATATIZO ya muungano yaliyopo yatatuliwe au muungano UVUNJWE na kila upande uwe ni nchi inayojitegemea, vinginevyo hizi kelele hazitakuwa na mwisho!

    ReplyDelete
  43. ALIYEKWAMBIA TZ KUNA UDINI NI NANI?NI VIONGOZI WACHACHE TU WA KIDINI WANAONZA UBINAFSI,KAMA HUU WARAKA WA KANISA KANISA KATOLIKI WA NINI KWENYE NCHI YA DINI NYINGI ,KILA MTU AKITOA WARAKA WAKE TUTAANZA KUPATA WAWAKILISHI WA DINI BUNGENI. NDIO MANA CHAMA TAWALA KITAENDELEA KUTAWALA MILELE.MWAKA 2005 KANISA LILIUNGA MKONO CHAMA TAWALA, SASA HIVI LINAUNGA MKONO CHADEMA.WAISLAMU WANAUNGA MKONO CUF NA CCM.ANYWAY UDINI UNAOZUNGUMZIWA UPO KWENYE NET TU, MTAANI WATU WANAJICHANGANYA KAMA FAMILIA MOJA VILE BONGO TAMBALALE.

    ReplyDelete
  44. Kwa ndugu zangu Wazanzibar hebu tuambizane ukiangalia idadi ya wawakilishi wenu bungeni kwa kulinganisha na wawakilishi wa majimbo ya uchaguzi ya bara, mnaanzia wapi kusema mnakosa sauti kwenye mambo ya muungano? Tatizo sio muungano, tatizo ni wawakilishi mlio nao hawaendi kuwakilisha maoni yenu kwa hoja nzito bungeni. Wanaenda wanaishia kulialia tu bila data kiasi kwamba wabunge wenzao wa bara hawaoni cha kuunga mkono. Kuna wadau humu wametoa hoja ambazo walau unazisikia na kuona kwa nini watu wanalalamika. Wabunge wenu sasa wanatakiwa kujenga hoja kwa mtindo huo. Mambo ya kusema tu basi muungano hatuutaki, bila kutambua tatizo hayasaidii mtu.

    ReplyDelete
  45. Ndugu zanguni Wanzanzibari, jifunzeni kutoka kwa majirani zenu, mkiachiwa mjitawale tu hukuna ka nchi katakachoitwa Zanzibar,hilo halipingiki hata kidogo, kwanza mnanini kinachowapa jeuri????mafuta mnayohisi hayapo HAKUNA MAFUTA YA KUCHIMBWA KIBIASHARA, karibia kila kitu kinatoka bara, nwaaaseni ipo siku na haipo mbali hata kidogo tutawatumua hukubara sijui mtaenea huko kwenu??hilo hamlioni hata kidogo karibia kila kitu kinatoka huku bara sio chakula nk, jaribuni kusoma alama za nyakati Rwanda na udogowake wanapigania muungano wa africa mashariki nchi zaulaya zinaungana najiuliza kinachowapa jeuri NI NINI??????????????????????????????????

    ReplyDelete
  46. Suluhisho ni kufanya "Referendum",
    Ndugu wetu wetu wa Zanzibar wapige kura ya kuchagua kuendelea na Muungano au sio. na hii kura iwe ya sauti ya ukweli, isiwe na kuingiliwa na serikali au wapingaji.
    Maoni ya kina binafsi, naona kama matusi Tanzania bara kuitwa mkoloni, naweza kukosea,lakini, naona kuwa ndungu wetu wa visiwani wamefaidika zaidi kuwa kwenye muungano kuliko Bara. Vile vile, kitu na mfano mkubwa, ni tulionyesha amani na kuanganisha nchi mbili kwenye bara letu hili la Afrika ambalo limejaa uchoyo, uhasama na vita. Of course, bado tuna matatizo ya uzembe, uvivu na rushwa.

    ReplyDelete
  47. mzee wa bunjuAugust 24, 2009

    KUHUSU MUUNGANO MIMI NAONA BORA TUUAGALIE UPYA MAANA SIO SIRI INAONEKANA WAZAZIBAR WANAHISI WANABURUZWA TU HASA WAZANZIBAR WA SASA, UNAJUA UNUHIMU WA MUUNGANO HAUKO CLEAR KWA WATU WOTE, WENGI UKIWAULIZA WATAKWAMBIA NI MUUNGANO WA KIDUGU MAANA KUNA WA PEMBA WENGI HUKU SIJUI KUNA WASUKUMA WENGI UNGUJA, SAWA YOTE HAYA NI SAHIHI LAKINI HAYA NDIO YANAWEZA JU JSIFY MUUNGANO WA HIVI?? NADHANI KUNA MENGI YA MUHIMU AMBAYO VIONGOZI WETU WANAYAJUA ILA HAWAJAPAT WASAA WA KUYAWEKA BAYANA KWA WANANCHI WA KAWAIDA. KWA MZANZIBAR WA KAWAIDA YEYE ANALINGANISHA TU HALI YA MAISHA YA ZAMANI NA SASA BASI HANA HAYA YA DETAILS NYINGI KWAKWE YEYE ANATAKA SIMLE MATHEMATIC 1+1 = 2 BASI. NAKUMBUKA ZAMANI SHOPPING WATU WALIFANYIA ZANZIBAR ZANZIBAR ILIKUA KAMA DUBAI VILE LEO VIPI??? SASA MAMBO KAMA HAYA KWA MTU WA KAWAIDA INAKUA NI NGUMU KUELELEWA, CHAMSING HAPA NIKUPITIA TATIZO BAADA YA TATIZO ILIKUWEKA MAMBO SAWA WALA SI KUTUMIA VITISHO VYA BILA MUUNGANO ZANZIBAR HAKUNA, MBONA VINGINE VIPO?? MMOJA WA WANANDOA ANAPOONA NDOA IMEINGIA LUBA NA AKAWA HONI FAIDA YA KUOLEWA, DAWA SIO KUMZODOA NA KUSEMA HANA FADHILA MAANA UKIZIDI KUMBURUZA IKO SIKU UTAKUTA ALISHA TIMUA KWAO AU KAMA NI MKME ALISHA KUTWANGA TALAKA. ( MUNGU ATUNUSURU)

    KUHUSU TANGANYIKA KUA KOLONI, WENGI WA WAZANZIBAR WASEMA HIVYO HATA KAMA NI KWA SIRI SANA, MAANA NILISHA WAHI KUKUTANA NA MZUNGU MMOJA NJE YA NCHI AKANIULIZA KAMA KWELI SISI NI KOLONI LA ZANZIBAR MIMI NIKAMKATALIA YEYE AKASEMA MBONA WAZANZIBAR HUKU ULAYA WANSEMA HIVYO? KWA KWELI SI NILISHANGAA SANA, NAMUOMBA RAISI AINGALIE UPYA WIZARA YA MUUNGANO MIMI NAONA KAMA HAIKO KIAINA!!! MAANA MAMBO YANAPAMBA MOTO WAO KULI!! NA WAKITOKA WANATOKA NA SOLUTION ZA JAZBA TU,

    YA ALLAH IBARIKI NCHI YETU TANZANIA

    ReplyDelete
  48. anayetetea muungano anatatizo asiyetetea muungano anatatizo vilevile... bora uwe kati mwaka huu muungano mwaka kesho hakuna muungano.. halafu mi najuta huyu aliyeanzisha udini haki ya nani hata mimi nafika mahali natamani kuwa kati yaani mwaka huu muislam mwaka kesho mkristo...
    hii kitu nina jazba nayo inaniuuma mpaka moyonii bora tuishi nchi zisizo na waumini wanajijua wenyewe ni waislam au wakristo lakini hawajui msikiti wala kanisa liko wapi...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...