NDUGU JAMAA NA MARAFIKI, FAMILIA YA OWINO INATANGULIZA SHUKRANI TELE KWENU NYOTE MLIOTOA HUDUMA YA AWALI/HARAKA KWA KAKA YETU PETER MARA ALIPOFIKISHWA HOSPITALI YA BUGANDO KWA MATIBABU MARA BAADA YA KUVAMIWA NA MAJAMBAZI AKIWA SAFARINI KWENDA SHIRATI KUPITIA BARABARA KUU YA KATI.
KHERI PIA KWA MADAKTARI WOTE WA BUGANDO KWA TIBA NZURI NA MAKINI. SHUKRANI PIA KWA MARAFIKI NA WATANZANIA WOTE WALIOPATA FURSA KUMJULIA KHALI NA KUTUMA SALAAM ZA TIBA NJEMA NA MAOMBI YA UNAFUU WA HARAKA. MUNGU AWABARIKI.
AIDHA TUNAWASHUKURU MLIOHUZUNIKA ZAIDI NA KUTAKA KUANDAA MICHANGO YA ZIADA ILI KUSAIDIA KTK HUDUMA YA TIBA KWA PETER. NAOMBA NIWAHAKIKISHIE KUWA TUNATHAMINI ARI YA UPENDO HUO LAKINI FAMILIA IMEWEZA NA INAENDELEA KUMUDU HUDUMA ZOTE ZA TIBA VIZURI KWA SASA.
PETER AMETOKA HOSPITALI NA ANAPONA HARAKA NYUMBANI. FAMILIA HAIJAANDAA UTARATIBU WOWOTE WA MICHANGO NA TAFADHALI MASHAURI KAMA HAYA LAZIMA YAWE NA IDHINI YA FAMILIA.
KWA UPENDO NAWASHUKURU NYOTE,
MUNGU AWABARIKI.

Maina Ang'iela Owino
k.n.y
FAMILA YA OWINO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Haya dada, tumekupata vizuri. Asante, Akunyimae kunde??

    ReplyDelete
  2. My two cents

    Kuna issues mbili hapa:
    1) kuna watu ambao huwa wanafanya harambee na kukusanya michango bila kuombwa na wahusika, na wakati mwingine michango haifiki kwa wahusika.

    2) Kuna matatizo yanayohitaji msaada bila kufikiria, kama misiba etc. lakini kuna mambo mengine tuwaachie ndugu na marafiki wa karibu washughulikie. Siyo kila kitu kinahitaji misaada. Watu inabidi tujitegemee, siyo kila shughuli kuchangiana. Eti ni jadi ya watanzania!!! jadi gani. Tunakuwa tegemezi sana, mpaka watu hawaweki fedha pembeni kwa ajili ya matatizo yanayoweza kuwatokea huko mbeleni, wanajua tu kwamba watachangiwa!!! gimme a break!!

    ReplyDelete
  3. Kumbe kuna watu walishataka kufanya harambee bila idhini ya familia...duh wabongo nuksi kweli.

    ReplyDelete
  4. Mbona tuliambiwa juzi tu kuwa huyu jamaa yupo hoi bini taabani, sasa familia inakataa michango, makubwa

    ReplyDelete
  5. Wewe Maina hiyo ni kufuru ya jeuri ya tupesa ambato ni twa mpito. watu wanataka kutoa msaada na wewe unakashifu watu yaani kama wanakimbelembele cha kutaka kusaidia. kesho unapatwa na tatizo ambalo linahitaji watu wakusaidie utafanaya nini? na watu je wakingoja ruhusa yako ili upate msaada utawataarifu wangapi. Achana na huto tu tabia twa kuiga twa kizungu eti ruhusa ya familia inatakiwa ili kutoa msaada. kumbuka KUTOA NI MOYO WALA SI UTAJIRI. PLESASE STOP THAT S@@@@T.

    ReplyDelete
  6. Obama unaona deal imeota mabawa,iwapo wataitaji msahada watatangaza kama walivyo tutangazia sasa. kamakweli unamoyo wa kutoa wako wengi wanaoitaji msahada sio hapo tuu.

    ReplyDelete
  7. wajaluo utawajua tu, sasa kama hataki michango si angenyamaza tu kwanini aandike, basi angeikusanya akaipeleka hata kwenye vituo vya watoto yatima basi, hebu kuweni wastaarabu sio kujifanya mna pesa wakati ni kwamba riziki inapatikana tu. huko shirati ni wana kijiji wangapi wanahitaji missaada?? excuse me!! si ungewasaidia wanakijiji wote wanaokuzunguka ndio ningejua kweli hamhitaji michango, jamani michango ni jadi yetu waafrica sio kwamba eti ukichangiwa ni kwamba wewe ni masikini, ila kwa wale malimbukeni wachache wanafikiria kuchangiwa ni kuonekana masikini. ofcourse African we are all poor, unless uwe mgombea wa thithiemu, chidumu chama cha mapindudhi.

    ReplyDelete
  8. Hey Mr Obama,

    Yaani wewe utapokea msaada hata kama mahitaji yako yanajitosheleza eti kwa sababu unaweza kuja hitaji huo msaada siku nyingine? Huo ni UTAPELI.

    Maina, tena kwa heshima kabisa amesema familia inajimudu "VIZURI KWA SASA". Maana yake ni kwamba akihitaji msaada ataomba na wale wote wenye moyo watasaidia wakati huo. Kosa lake liko wapo; nyie ndio wale mnaoendekeza tabia ya kuomba omba misaada bila sababu yoyote.

    Nani alikuambia lengo ni kupata watu wengi zaidi wa kuchangia?? Kwani umesikia ni harambee ya kujenga shule hiyo.

    Hebu elimika kidogo...

    ReplyDelete
  9. Hata hapa DAR watu wakisikia msiba au ajali inahitaji michango wako mbelembele.Wakisha changisha wanapotea na fedha.Mbona hii nyingi tu.

    We anony unajiita obama koko, UNA UDHAIFU AU BEEEEEF. Sasa mbona huyo Maina amekua Clear kwenye statement yao na ameshukuru tu sana.Wapi amekashfu au kufuru. Watanzania tubadilike.

    Siku zote kabla yao tukio halijawa Public, familia inakubali kwanza sasa hapa kosa wapi? Tabia gani ya wazungu ameiga? Amesema kwa sasa....ina maana mambo yakiwa magumu wataomba....Wengine WIVU tu.

    MAYUNGA K.A
    Mwana wa Nchi

    ReplyDelete
  10. Michudhi,
    Watu kama Obama wa mabox msiwape nafasi humu.
    Walizaliwa na hasira,wamekua na shida, wanakula kwa taabu, wanalala kwa matatizo na hata kazi ni mikosi...sasa wana hamishia kwa wengine. Statement iko brief and clear. Yeye kwa nini anato KUFURU kwa Maina. nahisi huyu ni mtu wa karibu kwake au mmoja wa waliotaka kuchangisha Pesa.

    Stan Njau

    ReplyDelete
  11. Daftari lishaanza pita kwa watu, lingine limewekezwa kwa Bongoflavour Shop Reading,hata wanandugu hawana TAARIFA.

    Pelekeni Credit Crunch taratibu WABONGO. Familia ni vema wajue na wakubali.

    Family matters jamani!!!!!Hilo sio geni.

    ReplyDelete
  12. HAKUNA HARAMBEE / MICHANGO KWA ....
    Jamani nadhani wakati mwingine busara iwe inatumika zaidi badala ya kuleta NYODO ktk maswala ya kijamii kama haya. Hivi ww Bw. mdogo ungetoa taarifa tu ya maendeleo (afya)ya mgonjwa usingeeleweka? Kwanza kichwa cha habari hapo juu hakiendani kabisa na matarajio ya wengi wetu hasa ambao unawaelezea walitoa misaada bila ya idhini ya familia!! Eti ninyi ndio mnatarajiwa kuwa viongozi wa kesho na nyodo za vijicent visivyo na uhakika, anyway poleni sana next time jifunze namna ya kutoa taarifa, NYAU WW!!!

    ReplyDelete
  13. Turudishieni basi mshiko wetu

    ReplyDelete
  14. Mama wee, mie nimeshatuma mchango wangu itakuwaje??

    ReplyDelete
  15. Obama JR

    HILO NDILO TANGAZO LILILOLETA MTAFARUKU???? AMA!!!! NANI ALILIPELEKA HUKO KWA HAKI NGOWI BLOGSPOT KAMA SIO WANANDUGU WENYEWE!!! SOMA TANGAZO HILI

    HARAMBEE YA KUMSAIDIA MWENZETU
    PETER OWINO : haki Tarehe: Friday, August 14, 2009 | kiungo mahususi
    ------
    Reading uingereza tunapenda kutoa Taharifa kwamba, Daftarin la kumchangia Peter Owino Aliyevamiwa na majambazi mwanza juzi tarehe,11/07/09 limefunguliwa Bongo Flavour Reading.

    Yeye mwenyewe Bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa ya bugando (mwanza) na mipango ya kunsafirisha kwenda Hospitali ya taifa muhimbili inafanyika.
    Yeyote anakaribiswa kutoa chochote kwa kwenda bongo falaour au kulipia kwa njia ya benki.
    Kwa taharifa zaidi Piga simu
    01189585878
    07900040288
    07760200372
    07806792348
    Kutoa ni moyo,usambe ni utajiri

    ReplyDelete
  16. Mimi shida yangu ni kujua hatima ya hiyo mijambazi walio mshambulia Owino.
    Je wamaisha kamatwa?
    Je upelelezi umefikia wapi?

    ReplyDelete
  17. Na hii inayoitisha harambee wakati haijatumwa kufanya hivyo haina tofauti na Mijambazi iliyopora!Eti bila aibu na namba za akaunti wametundika mweee!

    ReplyDelete
  18. OBama JR is ana enterprenuer, he sees the opportunity and strike but this time kaingia choo cha kike, kweli hakuna aliyetumwa ujanja wa watu tu mbona hawajaandika Jina la acount zaidi ya namba na benk.

    ReplyDelete
  19. ObAMA jR

    KIAFRIKA HATUNA KASUMBA ZA KUTOFAUTISHA CHOO/VYOO, CHOO ANACHOINGIA BABA YAKO NDICHO HICHO HICHO ANACHOINGIA MAMA YAKO, KASUMBA HII MMEIJULIA ULAYA BAADA YA KUFUTWA MATONGOTONGO, SINA SHAKA HATA HUKO VIJIJINI KWENU VYOO HAKUNA. Quote! ".......mbona hawajaandika Jina la Account zaidi ya namba na benk" ......INA MAANA UNAWAJUWA HAO WALIOANDIKA, WAKATI NI NYINYI WENYEWE WALENGWA, KWELI HUU NI UBABAISHAJI MTUPU

    ReplyDelete
  20. Big Upthe Owinoz, ningeshngaa kama mgeomba michango wakato mko thawathawa,kuuguza mgojwa wa majeraha si kazi sana, lakini nawapa pole mimi pita namjua sana nimesoma naye Dublin mwa 1996/97,jamaa mshua sana hana time na perepete nyingi akiahidi kitu la=zima atatenda,naomba kama mna contact zake tafdhali.

    Mbogo.

    ReplyDelete
  21. haya majambazi dawa yao ni kuunda kikosi maalum cha kuprol kwenye barabara zote kuu hasa nyati za usiku, kwani hata yakiuwawa hayakomi. Poleni sana Owino na familia Mungu ndo mtoaji na atawapa afya njema na malizilizopotea zitawarudia, kumbukeni sala za kila wiki.
    Nyarenda

    ReplyDelete
  22. Maina, tunaomba utujulishe hali ya Peter inaendeleaje kwani tunahaja ya kujua kama amesharudi U.K ama lah, na kama amepona na anendeleaje tafadhali tu-update kupitia michuzi.com

    Mdau - Leeds england

    ReplyDelete
  23. tunasikia Peter amesharudi england na anendelea ok.kama kuna mwenye simu namba yake tafadhali atusaidie angalau kumpa pole ya mdomo.


    anes

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...