na mdau diaspora writer
Hi all!
I would like to comment on this London Photo that I took and which has created alot of traffic on blog ya jamii. What the readers should know is that the first white building is a PUB and the brown one is Forestage Police station.
The road might look smaller because there is a Bus Lane. Only specified vehicles (buses, taxis i.e. Hackney Carriages, emergency services and cyclists) may enter a bus lane during operating hours.
Vehicles not in those categories will be liable for a Penalty Charge Notice if they enter a bus lane. Thus reducing congestion on Public routes .Even parking and waiting restrictions may also be in operation outside of bus lane hours.
If your vehicle is viewed in a bus lane during the restricted hours the registered keeper will receive a Penalty Charge Notice. Raising road user awareness of bus lane restrictions has resulted in clearer bus lanes and an improved and more reliable bus service. This has encouraged more people to travel by bus. That’s why you see that most of the vehicles in the picture use the two available lanes as the rest is reserved for the above mentioned public Transport.
Section 120 of the Highway Code states: Bus and tram lanes. These are shown by road markings and signs. You MUST NOT drive or stop in a tram lane or in a bus lane during its period of operation unless the signs indicate you may do so. (Road Traffic Regulations Act Sections 5 & 8), unlike home where daladalas drive even on the pavements.
Wadaus should appreciate the fact that London's bus network is one of the biggest in the world, with 8,000 buses, 700 bus routes, and over six million passenger journeys made every weekday. So it can be a logistical nightmare for a third world country to run such a fleet in your area even for a week.
This road is Romford road in forest gate -London Borough of Newham .Newham is an old small Roman town that has now grown to one of the most vibrant and multicultural boroughs in England.Ther are a total of around 32 boroughs in london
There are around a total of thirty two boroughs in London. They are:, Sutton , Enfield, Barnet , Harrow, Lewisham, Havering Barking and Dagenham, Redbridge ,Newham, Redbridge, Waltham Forest, Haringey, Bromley, Islington, Camden, Brent , City of Westminster, Kensington and Chelsea, Southwark, Tower hamlets ,Hackney, Hounslow, Bexley, Hillingdon ,Corydon, Richmond, Kingston upon Thames ,Merton, Hammersmith and Fulham, wondsworth ,Lambeth.
A lot of East Africans live in Newham .Ugandans own most of the shops and pubs around this area especially in Forest Lane. Also, please take note that the small green vehicle is a road sweeper, not a Bajaji as some one had suggested.
Regards
Diaspora Writer


unafananisha usingizi na kifo wewe. tupe utafiti wa mlinganisho kati ya bongo na UK:
ReplyDeleteJe hiyo foleni ya kwa mama
1. ilidumu muda gani,
2. inatokea mara ngapi kwa siku/wiki,
3. ilitokea maeneo gani
4. je ni nini sababu za foleni hiyo huko kwa mama
ukishafanya utafiti wa mlinganisho wa maswali haya kwa hizi nchi 2 tofauti sana ndiyo utumwagie data na mtazamo wako huo..vinginevyo unafananisha kifo na usingizi wewe
hapa mdau hajakosea kwani hapa hasa wakati rush hours ndo utalala hapo mpaka unafika ilford au kama utakata kulia kuelekea uwanja wa west ham unaweza kumaliza ndoto .
ReplyDeletemaeneo haya ni uswahilini hasa ama tunaweza kusema uhindini kwani huwezi ukagundua kama upo mtoni hata mzungu adimu . pamoja na yote ni tofauti kidogo na bongo.
Ukweli ni kwamba Black wall tunnel kukiwa na ajali basi ni mtafutano pia A2. pia muda wa saa 10 hadi 11 na wakati mwingine 12 jioni foleni kubwa kubwa.
ReplyDeletealex kama nakuona vile!!! haya mwana endelea kupata fosters baridi hizo kwani summer ndo hiyoooo karibia utaanza kuomba za moto sasa
ReplyDeleteMbona barabara ndogo hivi , watu wanaweza vipi kuendesha hapo ! Naomba kuwakilisha , Mdau Kitangali
ReplyDeleteAnon namba moja unataka kusema London hakuna foleni?? Au unamwelekeo gani na hio hoja yako.
ReplyDeleteMdau wa Mon Aug 24, 09:40:00 PM, Uingereza ni kisiwa kama zanzibar, barabara kubwa zitamaliza ardhi ya nchi... hizo ni planning mkuu, halaf kumbuka kuna watu milioni sitini kwenye kakisiwa hako kanakoingia mara zaidi ya nne kwa bongo... tehe tehe...
ReplyDeleteNB: Kama London kuna foleni ndio maana yake nini!??? So what!??
Mbona kama Bukoba vile au Tabora jamani ???au njicho zangu kengeza wadau??
ReplyDeletemtabakia hivyo hivyo kujilinganisha na London wakati wenzenu wanakula bingo na world cup.bongo lala....nchi mbovu mbovu nilikuwa huko majuzi.
ReplyDeleteYani watu wa mikoani utawajuwa tu wakisikia Ulaya wao akili yao Ulaya Magorofa Marefu tu kila sehemu Labda kila mtu anatembea kwa Gari. Usafiri wowote unafika kaka watu hawajali Gari binafsi. Toweni fikra zinazowapoteza.
ReplyDeleteKwa anon wa saa 10;55 PM, naomba nikijulishe kuwa anon namaba moja ana maanisha kuwa linganisha mataifa yanayofanana fanana yaani embe kwa embe na chungwa kwa chungwa sasa wewe unalinganisha kunde na mchicha. Sawa foleni bongo zipo sasa wewe unalinganisha foleni za bongo na UK hivi una maana unataka kutuambia kuwa bongo tuone ni kawa tu kuwa na mafoleni kwa sababu hata UK yapo ama? Nadhani hapo ndiyo napotofautiana. Kero za foleni za bongo tofauti na majuu hivyo tusijiliwaze tufanyie kazi ili tuendelee. Wewe linganisha UK na mataifa mengine kama hayo hayo sisi bongo inabidi tufanye kazi kubwa sana. HITIMISHO; BONGO SIYO TAMBARARE KAMA UK WEWE MTU WANGU HEBU FIKIRI FIKIRI!
ReplyDeleteiwe isiwe london si bongo kama bongo hilo gari la icecream mshasema ni la bakhresa.
ReplyDeletehuyo mwenye kusema eti aliye andika anafananisha usingizi na kifo hata hana aibu. kwani foleni za magari ulaya hazipo. hapa toronto kuna foleni kubwa sana wakati wa rush hours. hata kwenye highways foleni bado zipo. barabara za london ni nyembamba sana na haziku planiwa vizuri. barabara za london ziko kama vichochoro.
ReplyDeleteDuh ndio maana hawa jamaa wa uk wakija north america huwa wanashangaa kumbe kwao badooo!
ReplyDeleteHacheni maneno maneno yasio kuwa na mpango nyieee!! Foleni ni jambo la kawaida nyakati za asubui na jioni sehemu karibia zote duniani, iwe paris,New York,London,Tokyo,Nairobi Cape Town na hata jiji la maraha Dar es salaam nyumbani. Ni vikasoro vidogo vya ustaharabu tukiweza kujifunza na kuzibiti,kama kuchomekea na kutoka nnje ya barabara basi,hatutakuwa mbali na hawa wakoloni.Mdharau kwao ni mtumwa!!! Dar hoyeee!! Ulaya ziiiiiiii!!!!
ReplyDeleteLondon poor tuu,hakuna chochote hapa wadau, majengoo ya zamaniiii tokea enzi na mama yake na bibi Queen alipokuwepo na yamechoka kichizi hata kwa utalii hayafai,wanachojitaidi ni kufagia na mazingira kuwa masafi basi lakini wadau hapana deal kabisa,mtu yeyote hasijigambe kwamba akitoka UKEREWE katoka sehem babkubwa hakuna!!! wazee hivi vijumba vyumba vyake ni kama stoo zetu bongo,tena wakati wa winter mtu akijamba ndani na hiter zikiwa on ujue balaa!!! Napamiss hom kchizi hapo jijini bongo,, mambo ya organic fud na nini. Jamani tuwe wa kweli???? Au nyinyi wezangu ni wale mliojilipua??? Mnakaa ndani kusubiri kukinga kila mwisho wa week mambo ya BENEFIT??? Ndio maana mnaponda kwenu!! haya jamani!!
ReplyDeletelondon bado katika sistem za barabara wako nyuma sana,mdau yeyote aliyetembea nje ya uk atathibitisha kuhusu hii choka mbaya.kama utanote hata hiyo picha iliyotumwa ni barabara moja ila gari zinaenda opposite direction,wanashindwa na hata morogoro road
ReplyDeletejamani huku kuna highway ambazo hakuna hata taa moja unasafiri kwa high speed ila katika ya mji mataa ni lazima mshingae sana enyi wadanganyika mnajifariji kwa mifano ya ajabu ajabu tena mshukuru bongo ni joto laiti kungekuwa na winter kama ya huku london mngepata akili haraka,ngoja nikabebe box nipate euro 2000 kwa mwezi sijui ni mshahara wa bosi gani huko bongo exchange rate 1 euro = 1800tsh
ReplyDeleteKaka hapo ndio UK/GREAT BRITAN hawa jamaa achana nao kabisa kwani wametuzidi bomgo zaidi ya miaka mia moja mbele kama ulibahatika kupata elimu ya secondary uingereza ndio nchi ya kwanza duniani kufanya MAPINDUZI YA VIWANDA (industrial revolution) yaani bidhaa zote zinazotokana na viwanda hawa jamaa ndio waliogundua kwenye karne ya 17 huko sijui wakati huo bongo tulikuwa tunaishi mapangoni au wapi yaani sipati picha kabisa,kama umewahi kusikia watu kama ISACK NEWTON,LAMBERT na ABORT wametokea hapa wewe nende uganda au kenya kapige picha halafu mjilinganishe kati ya yenu nana choka mbaya huku usipime kabisa ndio maana naona bora nibaki huku huku ughaibuni kubeba box kuliko bongo
ReplyDeletenawasilisha mdau scotland
anonymous wa 04:59:00 am unacheza sana na akili yako fupi. Inaelekea una database ya zamani sana ya mishahara ya bongo, njoo kidogo uone watu wana fanya kazi za heshima zenye hadhi za elimu zao na pesa wanatengeneza kama kawaida. Wenzio wanajenga na kuendesha magari mazuri na hata kufungua miradi mbalimbali we unakazania kusifia boksi.
ReplyDeleteUsione sifa mtanganyika wewe, kubali failure ili upambane vizuri na maisha siyo kujisifia na vibarua, wenzio wanaofanya hivyo si kwamba wanapenda ni hali ya maisha tu imefikia hapo la kama wangepata kazi mbadala za kujiajili au kuajiliwa zenye hadi nzuri na good pay wangefanya.Unasahau kuwa asilimia kubwa ya watu wa jamii yako mliharibu form four ama six home mkaenda huko kutafuta maisha, tafuta pesa ila usijisahaulishe kuwa boksi ndio suluhisho la kila kitu.
Ushauri wa bure: piga boksi uwekeze popote pale iwe nyumbani au huko na msaidie pamoja na kuwazika wazee wenu wanaofariki, kwani mnatutia aibu sana vijana wenzenu, mnajisifia mnatengeneza pesa za boksi wazee wenu wanakufa mtaani mnashindwa kuja na wanazikwa kiaibu sana.
Ni maoni yangu tu.
NI NCHI MOJA TU YA AFRIKA AMBAYO INA ZIPIGA CHINI NCHI KIBAO ZA ULAYA NAYO NI (SOUTH AFRICA)TU
ReplyDeleteWewe Anonymous wa Tarehe Tue Aug 25, 04:59:00 AM, bure kabisa, mshahara wako wa Tsh 3.6 M kwa mwezi London ni sawa na mshahara wa Tsh 450,000/= Bongo ukilinganisha gharama za maisha...huwezi kuona hili sababu kichwani ziro..ndo maana unabeba box
ReplyDeletehiyo barabara ni ya kitongoji tuu jamani kama vile kigogo au sehemu nyingine,soo mclinganishe sawa na main road za bongo,
ReplyDeleteNIMEZIPENDEZA SANA HIZI COMMENTS LKN YOTE 9 KUMI HILI LA WABEBA BOKSI KUJISIFIA NA HUKU WAZAZI WAO WAKIFA BONGO HATA NAULI YA KUJA KUZIKA HAWANA SHAME ON YOU!!KWAKWELI TUKATAE TUKUBALI LONDON IS A VERY OLD FASHION CITY"TAZAMA BARABARA HIZO WATU WANAPISHANA TU KAMA MUHEZA VILE HAMNA HATA 2WAYS BANA.HIVYO VIJUMBA VYAO SASA NI SAWASAWA UCHUKUE CHUMBA KIMOJA CHA DAR KISHA UKIGAWE CHUMBA HICHOHICHO KITCHEN,LIVING-ROOM,BED-ROOM NA TOILET.NA MTU AKITEMBEA NDANI KWAKE WEE ULIE CHINI UNAMSIKIA AKIKANYAGA MAISHA YA KINYONGE SANA WANAISHI NDUGU ZETU WA UK,TENA HALI INAZIDI KUWA MBAYA KWAVILE AJIRA HATA HIZO ZA BOKSI NA VIZEE HAMNA SIKUHIZI.MTU AKIFIKIRIA KURUDI HOME ANAJIULIZA ATAENDA KUANZIA WAPI??ANON:AUG25 ;10:09:00 AM USIJIDANGANYE SOUTH INAZIPIGA BAO NCHI ZA ULAYA SOUTH YENYEWE INAPIGWA BAO NA NCHI KIBAO ZA AFRIKA MAISHA MABOVU KULIKO YOTE HAPA DUNIANI YANAPATIKANA SOUTH AFRIKA TU KWENGINE KOTE KUNAFATIA
ReplyDeleteAnony wa kwanza hapo juu mbona umeandika kwa jazba namana hiyo!! Angalia mwenzio (anony wa pili toka juu) alivyoeleza kwa ustaarabu, anony wa kwanza yaelekea ulishabadili hata utaifa wewe, na inawezekana umeshindwa kubadili ngozi tu nawe ukaonekana mzungu! Kama umemwelewa sawasawa mtoa mada, hakutegemea kuona foleni kama hiyo kwa mama kulinaganishwa na Dar (Bongo). Tuwe wastaarabu katika kuelimishana.Hata kama ni mbeba boksi, ni njia mojawapo ya kujipatia riziki cha msingi angalia yasikulevye!!
ReplyDeleteNdugu zangu kama nilivyosema hapo awali na watu wa ukweli wananisaidia, U.K CHOKAAA TUU, Mijengo tokea enzi za bibi yake na mama yake Queen hata kwa utalii si kivutio. Si tunaona hapa watu wavyoishi jamani kwa kazi za kusubiria mpaka AGENT ampigie simu ndio mtu ana uakika wa kula siku hiyoo,bongo cheti ajira uakika na maisha poa,Tshs 10000 kariakoo sokoni wewe mtu,haya hapa hiyo ni Pound tano kasoro mtu mzima zama nayo Tesco unaweza toka unalia kisukuma wazungu wakakushangaa.je hapa ulaya wabongo wangapi wanavyeti na wanafanyakazi za maana tupe list unayejiita meya wa U.K.Hapa ubaguzi ndio nyumbani kwao ila wanaficha sana kuogopa kashfa za ulimwengu na walimwengu,JE! HUO UZURI WA MAISHA HAPA UKO WAPI WEWE MWANGA WA NYIKA.Kwa m-bongo unayeingia hapa U.K kama uendi shule na kuwa na mawazo kuwekeza kwenu bongo future hapa ziro!! Tuwe wakweli jamani!!!!!!Wakina kaka hapa wengi wamebaki ndoto zao zime baki hewani mara tu baada kuwasili hapa, waki dada hao sisemii maana ni aibuu kwa jamii yetu na Taifa letu la maadili. Bongo big-up sana watu wanafanya mambo sasaivi na ninawakubalii, watu hapa kuvaa nguo za Primark na kula vyakula vya kuzindikwa Tesco ndio wanasahau nyumabani hawa ni MALIMBUKENI hakuna haja ya kubishana nao, kubeba BOX si maisha!!! hii ni option ya mwisho kabisa katika maisha ya hapa ulaya,born anayebeba box unaweza mtafuta week husimpate, sasa hawa WANAANGA WA NYIKA si elewi wanachojisifia hapa.Misemo mingi ina akili na haizeeki na itaendelea kudumu,GO EAST,GO WEST, HOME IS BEST WAZEEE.Amani.
ReplyDeleteWewe anon, Tue Aug 25, 12:16:00 PM -
ReplyDeleteMbona unaleta ya kuja hapa?. Unaelewa kwa nini nyumba zimekuwa ndogo au kugawanywa katika saizi hizo? Huelewi kwamba wakati jua likiwa huko kwenu, huku au huko kunakuwa baridi na ili kupunguza makali ya baridi saizi hizo hazitahitaji kuunguza mafuta ili kuongeza joto kwenye chumba kikubwa kama hicho cha huko kwenu manzese?
Na kama ulikuwa hujui hii itakusaidia sana kupunguza makali ya kukosa mvua (ambazo unazitegemea kwa chakula, au kupunguza hizo elinino zinazokuja na nyie hamjajitayarisha kukabiliana nazo). Basi mdau kama ulikuwa hujui, hii au hizi ndio sababu kuu za msingi.
Sababu nyingine ni kwamba ardhi imepimwa mpaka kiwanja cha anko nanihii cha mapumziko au kuzimu milele, na pengine keshanunua tayari. Je wewe unajua hata nyumba yako ya milele itakuwa wapi!
Hapa au huko, wenzio wamefanya miundo mbinu (""town planning"") mpaka kufikia karne kumi na mbili zingine zijazo. Na si hapo kwenu (au niseme kwetu?) ambapo mipango kama hii inaangalia hapo usoni tu ("short-lived planning/myopic"). Na zaidi wewe anon, ulikuwa unajua kwamba pamoja na kwamba hivyo vijumba ni vidogo, watoto wakitaka kwenda kucheza wanapata sehemu zao za kuchezea pia? Hizo sehemu hazijaingiliwa na mafisadi, na wana mipango miji wameziachia vema tu.
Michu mdogo wangu nawasilisha hoja hii. MH (Mtoa hoja ndogo ndogo).
Tarehe Tue Aug 25, 12:16:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous (INAENDELEA KUTOKA JUU...)
ReplyDeleteMichu mdogo wangu hii inaendelea MBELE KWA MBELE.....MH....
Na si hapo tu, kukiwa na alama za barabarani, vIbajaji au mabajaji yanazijali sana hizo alama! Na hata kama watoto wangekuwa wanacheza, zingesimama. Hata kama ni raia wale wakubwa kiumri (mama au baba mzee) wangekuwa wanakatiza hiyo barabara, ni lazima wangefanya hivyo (yaani wangesimama na kuwaacha wapite). Je wewe, pamoja na kwamba sio mbeba mabox, unapata fursa hii hapo kwenu (au hapo kwetu)? Na sio hilo tu, bado mtu akipata ajali, au akiugua anaweza kwenda kutibiwa haraka, na ikiwezekana "ambulance" ikitakikana inapatikana mara moja ikiwa ni chini ya dakika mbili au tatu vile (mfano tu). Hii si ni ndoto ya kuotea mbali hapo kwenu (hapo kwetu) wewe anon. Labda ndoto hii itakakuwa kweli baada ya miongo minne au mitano hivi, kama si zaidi ya miaka mia tatu ijayo!
ReplyDeleteWewe anon, hapo kwenu wewe ambae si mbeba mabox (au hapo kwetu mimi mbeba mabox) - je ulijua kwamba ukimaliza kazi unaweza kurudi nyumbani, na ukapumzika, ukaoga na maji moto, baridi, au vuguvugu (lile joto la maji roho yako ingependa), bila kujali kwamba NUWA, DAWASO, DAWASCO au TAnesco wamechukua maji au umeme wao? Na je ulikuwa unajua kwamba hawa wadosi wakitaka kufanya hivyo itabidi wanitangazie labda miezi minne kabla au hata mwaka mzima kabla kwamba siku fulani kutakuwa na tatizo kama hilo. Na sababu itabidi wanipe - na iwe ya msingi sana? Je hawa vidampa wako watakuambia. Sana sana utaniambia kuwa huwa wanatangaza kwenye magazeti ya uwazi au udaku...wewe, hebu nikalie pembeni mdau.
Je pamoja na kukutangazia kwamba kuna mgao, si bado unalipa bei ile ile ya maji kwa siku thelathini, wakati labda umepewa huo mgao kwa siku kadhaa za mwezi (sisemei wale wenye LUKU hapa). Sasa wewe uko gizani asilimia themanini ya umri wako, utaniambia nini mimi mbeba mabox, ambae ninafurahia mchana na usiku (kukiwa na mwanga wa kutosha)- hata libeneke sina wasiwasi, ninaamua muda wowote wa kusoma au kuandika kwa ndugu yangu michu. Wewe uhuru huo unao?
Utaishi miaka mia na au zaidi mia mbili, hata kama si mbeba mabox, utafurahia vipi hizo pesa (pengine si zako), wakati umefungwa mdomo hata kutoa maoni yako? Utasema siku za zama hizo. Lakini nakumabia uhuru huo huna. Huwezi kusimama kidete kwamba hutaki hili au unataka lile, bila kukaribia keko au kule ukonga (kunakoweza kuwa nyumba yako yenye giza kwa miaka kadhaa). Pamoja na kwamba mimi ni mbeba mabox, lakini uhuru huo ninao, na ninao saaana.
Na je ulikuwa unajua kwamba, mimi unayeniita mbeba mabox, ninaweza kwenda kazini, nikaacha gari yangu milango au madirisha wazi? Au nikaacha nyumba yangu wazi bila kujali vibaka? Pia, ulikuwa unajua pia kwamba ninaweza kuacha milango ya nyumba wazi, TV na Radio (sijui kama nina redio nyumbani kwangu!!)nikaenda kazini au kulala bila kujali wezi wadogo wadogo kama hapo kwako wewe mswahili (mimi pia mswahili)!!
Na zaidi ya hayo, je ulielewa kwamba, nikienda sokoni, vyakula vyote vimepimwa na kwamba ninakula vyakula vyenye protein ya kutosha, wanga wa kutosha na kabohydreti za kutosha! Na ninakuambia, kabla sijafika hapo, polisi watakusimamisha wakuombe usile zaidi kwani unaweza kuondoka wakati wowote (unajilia lia tu ovyo)... Si unajua tena kwamba wewe ukienda sokoni unajinyakulia tu ovyo, tena vyakula vingine vya miaka ya arobaini na saba? Na hata kiti moto, kimepikwa nusu nusu, na hakuna mpima afya aliyefika kukagua. Na wala hujui kama hiyo kiti kilipatika kule manzese (kwa fisi))))..
Hata nyama ya machinjioni wewe unajinyakulia tu. Mara kwa mara, unaweza ukawa unasaidiana na mainzi yaliyojichana hapo kwenye duka la mchagga au machinjioni tangia asubuhi!
Je unajua naweza kukaa nyumbani kwangu baada ya kubeba mabox na nikapiga simu ofisi ya sirikali kusema kwamba ninahitaji kitu fulani au nikatuma tu "email (barua pepe)" fupi. Ofisi hizo za sirikali zitanipatia hiyo/hayo mahitaji yangu, pengine bila hata mimi mwenyewe kuondoka nyumbani kwangu - upo hapo? Hiyo ni ndoto, ya kuotea mbali hapo kwako (kwetu).
Michu..asante kwa kuzipangia hizo dondoo.....
Na je ulikuwa unajua kwamba mimi nina uwezo wa kupiga kura yangu na ikahesabiwa (na ikawa kigezo cha kuchagua sirikali). Japokuwa hii ina kasoro zake, lakini uwezo huo ninao. Ninao pia uwezo wa kutaka kujua pesa zangu ninazolipa kama kodi zinafanya nini sirikali kuu, na sirikali za mtaani. Wewe ndoto hiyo itafikiwa utakapokuwa katika nyumba yako ya milele.
ReplyDeleteHayo niliyokupatia hapo juu ni machache tu, na wala usinichokoze tena (mimi mbeba mabox) kwani, nikiendelea kukupasha, naona utakimbilia nyumba yako ya kudumu kunako asubuhi au jioni hii. Siwezi kukuelewesha zaidi.
Michu mdogo wangu, huyu anon, ni "stereotype" - kasikia mbeba mabox, kafikiri kila mtu aliyeko hapa au huku au huko ni mbeba mabox.
Michu mdogo wangu nawasilisha hizo dondoo kwa huyo mdau wa Tarehe Tue Aug 25, 12:16:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
jamani acheni kujifariji kijinga na bongo hata mie nimezaliwa huko ila siyo mimi peke yangu nimekimbilia ulaya yaani ukija huku utashangaa sana kwani kila binadamu wa hii dunia anakimbilia london siyo wabongo tu kwani WAARABU,WAHINDI,WACHINA huku ndio wamejazana kuliko hata watanzania nasikitika sana karne ya 21 ndugu zetu watanzania karibu asilimia 80 bado wanajiita wakulima huku wakitumia jembe la mkono mimi nionavyo hao sio wakulima BALI NI WAKWETUA ARDHI halafu nasikitishwa na huyu mbongo anayejilinganisha na uk wakati hiyo mishahar anayosema mikubwa huku watu wananunua kikombe cha kahawa cha msingi tujitahidi kuiga maendeleo ya wenzetu ili watanzania wengi waondoke kwenye maisha ya kuishi chini ya $ 1 kwa siku hii ni changamoto sio kashfa hata mie nikikamilisha miradi yangu huku may be i can go to tz
ReplyDeletenawasilisha mdau WALES
kwani kama unaishi ughaibuni na mzazi wako kafariki bongo ukashindwa kuwahi mazishi kuna tatizo gani?je unaweza kufufua mtu aliyekufa?haya mambo ya kufa ni ya kawaida kwa binadamu ndio maana tusoma kwenye maandiko kuwa tutende yaliyo mema hapa duniani ok!
ReplyDeleteacha uongo bwana unadanganya watu mchana kweupe kabisa TANZANIA wenye mishahara mizuri ni wabunge,mabosi katika idara za serikali na wafanyabiashara wajanja wajanja wachache kwanza kima cha chini shilingi 80,000 ambazo ni $75 huku usa hiyo ni kibarua wa siku moja tu mbona wabongo kibao wanatuma $ baada ya kubeba box na hizo hizo ndio serikali inanufaika nazo ila bongo in home lazima nitarudi kwani mkataa kwao ni mtumwa
ReplyDeleteMtake msitake Africa bado hatujaendelea tuko nyuma sana,wote mnaosifia bongo muangalie vizuri kabla hamjaongea kwanza pesa za misaada zinatoka wapi,hata rais wa nchi ana jamaa zake maskini hata hospital hamuwezi kuhudumiwa,nyie mnaoshi bongo msifananishe UK na BONGO lenu fanyeni kazi kwa bidii muijEnge nchi yenu(yetu) mko nyuma sana kimaendelea achaneni kufananisha ulaya na bongo.na hao wanaosema wanalipwa mishahara mikubwa bongo wanabiashara labda MAFISADI hahaha,WATU WACHACHE SANA WALIONDELEA BONGO KWA JUHUDI ZAO BINAFSI WENGI WAO NI WEZI NA WAHUJUMU UCHUMI AU BABA zao wahujumu uchumi,watu nimesoma nao na bado kipato chao kipo kidogo sana kulinganisha na elimu zao,na wapo watu uku UK wabongo wanakula hadi 10mil kwa mwezi kwa elimu zao na juhudi,ukiangalia bongo kuanzia HEALTH CARE,EDUCATION, INFRASTRUCTURE NA KILA KITU YOU ARE WELL BEHIND UK fanyeni kazi kwa bidii acheni kufananisha UK na bongo hata chembe mnapoteza muda THINK HARD BEFORE YOU COMPARE THESE TWO NATIONS. Angalieni watu WIKIPEDIA KUHUSU NCHI HIZI MBILI NA MRESEARCH VYA KUTOSHA KABLA YA KUANDIKA UPUUZI,Na mimi niliyeandika ni mbongo ninayeipenda bongo. kuna raha yake bongo lakini msicompare BONGO na UK kwani mnapoteza muda wenu ambao mngeutumia kujenga nchi, na sio kila mtu anayeishi UK kajilipua na anapewa cha mama,kuna watu wanaishi kihalali na wanafanya kazi kihalali.na kazi ni kazi wanaosema wabeba maboksi wana jamaa zao masikini kupundikia uko bongo,uku hata kama mtu maskini lakini serekali inamjali hamuwezi kufanisha na uko,
ReplyDeleteHivi ubishi wa hapa nini ? maisha mazuri au uzuri wa majengo / uzuri wa barabara uchumi wa nchi utajiri na umasikini au kipato cha mtu wa chini kweli foleni za magari wabongo wabishi lol nimekubali mtu anabisha tu hataukimwambia kuku hakojoi atatoke mtu atabisha hapa kuna tajiri tz na kuna maskini newyork lakini huwezi kulinganisha nchi za 3rd world na 1st short& clear
ReplyDeleteNaina wote mnazungumza lakini ukweli wenyewe foleni hiyo imesababishwa na matengenezo ya barabara kuna watu wanaweka mabomba mapya ya gesi kwenye kona baada ya mc donald au kwenye njia ya kuelekea disco la fisi kwa wale uliofika,sio tu mnatoa kometi bila kuwa na uhakika, kuhusu majengo ya zamani serikali imeamua kutunza historia ya nchi, kuhusu barabara wakati zinatengenezwa London haikuwa na magri mengi kama sasa hivi, hapa kila nyumba ina wastani wa magari zaidi ya mawili,naona watu wengine wanaanza kuzungumzia kuhusu maisha ya hapa au kufananisha London na bongo mkae mkijua hivi ni vitu viwili tofauti.
ReplyDeleteMIMI NINAISHI CANADA. NINA KAZI NZURI NA NIMEMALIZA KUILIPIA NYUMBA YANGU LAKINI SIWEZI KULINGANISHA QUALITY YA MAISHA HAPA NA ILE YA NYUMBANI. NYUMBANI KAMA UNA PESA MAISHA NI MAZURI SANA. NILIPOKUA LONDON NILIONA WATU WENGINE WANAISHI MAISHA YA CHINI HATA KULIKO YA WATU MASIKINI NYUMBANI. HAO WATU WANAISHI KWENYE MAJUMBA YALIO JENGWA 1500 NA NYUMBA ZENYEWE ZIMEOZA, WAKATI WA WINTER BADO WANATUMIA HEATER ZA BOX AMBAZO HAZINA JOTO LA KUTOSHA. NYUMBA NYINGINE ZINA MENDE NA PANYA. KWANINI MTU AFANYE KAZI ZA OVYO NA KUISHI KWENYE NYUMBA MBAYA KAMA HIZO ILI MRADI AISHI ULAYA. UMASIKINI NI UMASIKINI AIJALISHI UNAISHI WAPI. AFADHALI NIISHI MAISHA YA CHINI NYUMBANI KULIKO ULAYA AT LEAST NYUMBANI UNA NDUGU.
ReplyDeleteNyie wapuuzi wa kibongo acheni kufananisha kifo na usingizi, UK mpaka hewa tunayovuta imepimwa, nyinyi walalahoi lini mtashtuka na kuacha kusifia ujinga, ndio maana mafisadi wanawamaliza na hamjui nini la kufanya mmbwa mwitu nyie, njaa zimewashika mpaka mnakulana wenyewe kwa wenyewe, na Zombe ameachiwa ngoja awamalize kunguni nyie hata haki zenu hamzijui, Zombe anawaua na kuwachukulia mali zenu bado mnamshangilia, huwezi kukuta upuuzi kama huo hapa UK.
ReplyDeleteMDAU BONGO TZ(10:01)TZ KUNA MISHAHARA NAKO? JANA NIMEONA MISHAHARA YA WAKUU WA NCHI KWENYE VYOMBO VYA HABARI:SPIKA NA JAJI MKUU WANAPATA 4M NA HIYO NI BAADA YA KUPANDISHIWA AWALI WALIKUWA WANAPATA 2M. MIMI BOKSI LANGU NAPATA $$4,500 KWA MWEZI exchange 1300 DO THE MATH,THAT MEAN MIMI NAPATA MSHAHARA MKUBWA KULIKO JAJI MKUU WA TZ SASA NIKURUDI HUKO BONGO MTANIPA KAZI GANI???????? LABDA URAIS. NDO MAANA KILA MTU MWIZI TZ NA MIRUSHWA INATIA KICHEFUCHEFU.ACHA KULINGANISHA KICHUGUU NA MLIMA
ReplyDeleteKwa harakaharaka ningependa kuwasaidia walalahoi na kuwaonyesha tofauti za Uk na Bongo, kwanza kabisa hiyo sehemu ni uswahilini yani kama bongo ni maeneo ya Tandale, pili pamoja na kwamba ni uswahilini lakini utaona jinsi drivers walivyo wastaabu, tatu kama mtaangalia vizuri kwenye hiyo picha upande wakulia una rangi nyekundu hiyo ni bus lane ni kwa ajili ya mabasi na tax tu, chombo chochote kingine hakiruhusiwi kutumia hiyo lane, na hakuna polisi wa kukuzuia au trafic huku mambo yote ni cctv cameras hivyo ukileta mambo ya kibongo na kuamua kutumia hiyo bus lane baada ya wiki mbili utakuta faini ya £80 imetumwa pale unapoishi, huku vyombo vyote vya moto vimesajiliwa kwenye anuani unayoishi,hivyo huezi kukimbia na upande wa kushoto unaona kuna ufito una rangi ya kijani, hiyo ni kwa ajili ya wanyonga baiskeli including zile za vilema,hivyo nisiwachoshe kwa maelezo mengi ila nawauliza walalahoi ni barabara ngapi za posta zina hizo facilities, na bear in mind hapo ni uswahilini ambapo wanapa-regard kama zone 3,
ReplyDeleteAnon wa Aug 25, 05.54 Unaisifia hivyo London??? Inashangaza sana kuona mtu anatoa sifa kama hizo.
ReplyDeleteAnon wa 08.29 nakuunga mkono kabisa yaani London nyumba zingine ni za zamani sana zimechakaa, na kodi bado iko juu sana pamoja na ubaya huo. Lakini utakuta watu hapa wanasifia kupita kiasi. Ukweli ni kitu muhimu sana. Ingawa kweli zipo zilizokarabatiwa vizuri lakini ni wachache wanaiweza hio kodi yake. Nyumba za miaka ya 1600's...
ReplyDeleteNIMEGUNDUA WENGI WANAO BISHA HAPA NI WATOTO,, AMBAO KULE BONGO MTU HAJAWAI KUKAMATA DEAL YA 100,000 KWA UJANJA WAKE MWENYEWE.NDIO MAANA WANAISHIA KUSIFIA ULAYA ULAYA TUU,,PAMBANUENI AKILI ZENU NYINYI NA KUPIGA MAHESABU YA MBALI NDIPO MTAPATA JIBU.HIZI KAZI ZA KUUA MIGONGO HAPA KWA KUBEBA BOX NA WAZEE NDIOO MNAJISIFIA SANAA.BORA UWE UNAPATA KIPATO KIDOGO LAKINI HESHIMA LUKUKI UNAKUA NAYO KWA JAMII YAKO ILIYOKUZUNGUKA.HAPA U.K WAZUNGU WAASTAARABU NI MALKIA NA WATU WAKE (ROYAL FAMILY) BAAASI, WENGINE HAWA NI VICHAA TUU.NDUGU ZETU WA VISIWANI WALIOLETA FAMILIA ZAO HAPA KUOMBA HIFADHI YA UKIMBIZI WANALIA SANA MAANA MAADILI YA WATOTO WAO YAMETEKETEA,,MTOTO AGOMBEZWI HAPA HATA KAMA ANAFANYA UTUMBO,,JARIBU UONE KAMA UJASIKIA MWELA WANAKUGONGEA MLANGONI,,WAKINA MAMA NAO NDIO BALAA NNCHI YAO HII WANAUME WA VISIWANI IMEBIDI WAWE WAPOLE TUU,,MAANA HAPA WAO NDIO WAMEOLEWA SIO KUOA TENA KIBAO KIMEGEUKA,,,HAKUNA HANAYEBISHA KUUSU ILO,,MAKAFIRI SHERIA ZAO ZANARUDI KINYUMENYUME HATA WENYEWE ZINAWACHANGANYA,, NA KURUDI KWA BIBI KUZIBADILISHA WAKATI KESHA TIA SAINI YAKE MSALA.TUWE MAKINI,,,NAJUA INAUMA LAKINI VUMILIA,,,HATA ALIYETOKA KIJIJINI AKIFIKA DAR KWA MARA YA KWANZA LAZIMA MABOMU YAKE AYAELEKEZE KIJIJINI,,,OOHH! HAKUNA UMEME NI VIBATARI TUU WATU CHOKA SIJUI NINI,,KUMBE HIVYO VIBATARI NDIO VIMEMFANYA AFIKE UDSM,,HACHA KUWA FINYU WA FIKRA WEWEEE!!
ReplyDeleteJamani London mmfika? Je mmeishi? au ama mmefika tu? Na sehemu gani nyinyi mliyofikizia, kama mmefika?
ReplyDeleteHicho kibarabara ni sehemu tu ya Romford road in east London. Romford road yenyewe imegawanyika zaidi ya sehemu 8.
Picha yenyewe iliyopigwa imechukuliwa kwenye mfinyo tu wa romford road. Urefu wa romford road yenyewe ni zaidi ya mile 4.
Romford road sio main road nikabarabara 2, kama vile utoke American chips kinondoni mpaka salender.
Mdau jaribu kupiga picha sehemu nyingine za main road uingereza kama vile A406, A13 ukiwa watoka central london na kadhalika.
Kumbuka population yamagari yaliyopo east london 2, ni sawasawa na magari ya Tanzania nzima..
Usilite league nenda ukagoogle utapata jawabu.
Mdau London
Kweli bongo tambarare, Zombe alikuwa ndani watu wakashangilia, ameachiwa wanashangilia. Umeme ukikatika wanashangilia, ukiwaka wanashangilia tena. Home sweet home, Akili ku-mkichwa.....
ReplyDeleteMpiga boksiz mwandamizi.
Kinachotia hasira ni maisha ya Tanzania ni magumu,mwenye pesa maisha mazuri na asiye nacho ni sawa na Jehannam. na asilimia kubwa ya watanzania ni masikini. Rushwa imekithiri kila kona,Mafisadi nao wanazidi kujinyakulia,Na hali ya maisha inazidi kuwa ngumu.Kwa kweli nyumbani ni nyumbani lakini nchi yetu inatia hasira.
ReplyDeleteKweli kazi ipo kama tunaongelea ili swala la foleni, wakati tunajua kuwa foleni za magari ni kila mahali. Kutembea kwa miguu na kupanda basi ndo kabisa usiseme. Haya ni maisha ya kawaida. Iwe ajali isiwe ajali foleni ni kama kazi. Mtaumiza vichwa vyenu bure. Mara bongo, Arusha, Bukoba, Makete, Mbinga foleni ni kila mahali duniani kote. Majengo mabovu na vyoo vya shimo ni dunia nzima.
ReplyDeleteMtaumiza vichwa vyenu bure.
Mdau USA
McZobizobi, hapo kwenye swala la South Africa mbona unaandika alafu unajipinga!? taratibu unakuja kasi..
ReplyDeleteAnyway, tukirudi kwenye mada kuna 3rd world (dunia ya tatu) kwenye kila Nchi. hapa Marekani kuna maeneo yamekaa vibaya vile vile au picha hazipatikani.
hapo juu Wabongo mnakuja kasi hapo, kwanini msipande pipa mkaone wenyewe, mnasubiri photoshop fotooz.
..SIKUJUA KAMA ITAKUWA HIVI!?
= = =
Buffalo, (karibia na mahali pako kama Ilala)
New York
foleni inaweza kusababishwa na mambo mengi mfano AJALI AU CONSTRUCTION
ReplyDelete