Home
Unlabelled
kura hazikutosha kwa illuninata miss universe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kweli,,, kaka Michuzi bahati haikuwa yetu, lakini ni lini bahati itakuwa yetu? wausika wajalibu kuangalia ni wapi penye tatizo
ReplyDeleteMdau,, Malaysia
tatizo si internet.watanzania wangapi wanayo habari ya kupiga kura.we unafikiri mtu wa s.africa atamkumbuka mtz
ReplyDeleteKwa kweli uncle sijajua na naomba kuuliza kwa kuwa swali hili huwa linaniumiza kichwa kila siku nionapo habari za mamiss hapa kwenye blog yetu hii ya jamii, Huwa mtu akitakiwa kuwa miss ni lazima awe mwanamke na hili tunalijua kabisa na ni kweli ndivyo ilivyo sasa niombe kuuliza je anatakiwa awe wa namna gani, moja nzuri wa sura, kama ni hii basi mwaka huu kwa sura wote si wazuri, pili ni wazuri kwenye elimu?kama ni hili basi tuonao, tatu wazuri kwa urefu, umbo zuri au ni wazuri wa namna gani kwa kuwa kwa sura mwaka huu mh LUNDENGA kachemsaha hana hata mmoja
ReplyDeletetatizo ni letu watz hatuwapigii kura kuwapa support ya kutosha ila tunajua sana ku-comment
ReplyDeleteMI naona ok ni wazuri,hata kama wana elimu ya chuokikuu,upeo wao ni mdogo sana.
ReplyDeleteMimi binafsi nasoma huku Europe,kuna wakati wanakuja maprofesa kutoka afrika,kusema kweli wanakuwa disqualified huku kulingana na jinsi yao wanavyoreason.
Kwa hiyo elimu ya chuo kikuu haitoshi,ila kwa wao muhimu zaidi ni yule aliyepata elimu yake katika nchi za ulaya,Japan,America(USA) na Australia...
wanaosoma hata India,China huku hawana market,Wahindi wanakuja huku wanakaa bila kazi,sababu hakuna anayetaka kuwaajiri.
Muhimu,Elimu yetu kuibadilisha,na ifuate moja ya Elimu za Ujerumani,USA au Australia.
Kuwa na Elimu si kusoma vtu vgumu,bali ni kusoma vitu vchache vitakavyosaidia wengi,pamoja na wewe pia.Hii ni dhana waliyo nayo wanafunzi wengi wa kitanzania,na hata waliopo Mlimani,matokeo yake...less competative...na hawawezi kufanya kazi kama maexpert au hata maexperties.
SUbiri niwape mfano huu,
niliandika barua wizara ya Elimu,nilikuwa nataka kuomba mkopo,
nilipata majibu,ila hawakunijibu nilichouliza,wao waliniambia...hukufuata sheria za uhandishi wa barua,sijui tarehe haikai juu,au adress inakaa chini na n.k...this was stupid...hata kama nimekosea namna ya kuandika,ujumbe wangu mmeupata,kwa nini hamkunijibu kuhusiana na Ujumbe wangu...nyumbani wanadeal na vitu vidogo vya kipuuzi,wanaacha main issues...na hili ndilo tatizo letu...
Asilimia pia kubwa ya wageni,wanaotoka Afrika,wanafeli somo la hesabu,Statistics zinaonyesha hivyo,ingawa nyumbani walikuwa wazuri wa hesabu,kwa hiyo hapa tatizo ni kwamba nyumbani,mathematics is about calculation,wakati huku ni about thinking and then calculate.
Ni hayo tu kwa leo.
I tried to vote there.......tatizo jingine ulikuwa ni urasimu katika hio website yao.It needed some kind or registration and stuff before you can vote! sasa hilo tu mie nalo lilinikimbiza kwani am not that devoted fan of these contests and my assumption is that most of tanzanians too.Compared na nchi nyingine,haswa za latin america where beauty contests are next to religion!
ReplyDeleteni kweli kabisa, bahati yetu ikifika tutalibeba taji, usiku wa saa tisa nimeamka na kukaa karibu na tv, nilipoona hayumo katika 15 bora nilitimua zangu nikaenda kulala.
ReplyDeletenext time wabongo tupinge kura kwa nguvu.
Mungu ni mwema
nilikuwepo kwenye tukio la jana hapa Bahamas,
ReplyDeleteKwanza nilijisikia fahari Kubwa sana kuwa nchi yangu iko represented, kudos to waandaaji huko Tanzania and keep it up
Nilijaribu kutafuta watu walioongozana na Binti yetu bila mafanikio, sina hakika kama walikuwepo maana hata kwenye ushangiliaji ilikuw ani mimi na familia yangu na Kenyans niliofahamiana nao kwa muda mfupi.
Nilienda karibu show zote, kwani coincidentally haya mashindano yalinikuta nikiwa niko vacation huku Bahamas.
Kura nilimpigia Illuminata pamoja na dada yetu toka South Africa na Egypt
Binti yetu Illuminata alifanya vizuri katika National Costume confidence aliyoionyesha kwenye Nation costume ndiyo iliyotakiw aionyeshe na kwenye costume zingine.
Kwenye show moja ya swimming costume na Nguo ya usiku, kwenye nguo ya usiku binti yetu ilionekana hakuizoea vilivyo nguo yake kwenye kutembea japo Nguo ilikuwa NZURI SANA i.e. FANTASTIC
Maoni binafsi:
Nafikiri tunahitaji mazoezi zaidi kwa mabinti zetu ili kujiongezea confidence.
Kujichanganya na kuwa active kwenye activities mbali mbali ni muhimu sana ingawa ni big challenge depending on maandalizi.
Sikuwapenda wapiga picha, kwani hawakupost picha nzuri za binti yetu mfano picha ya swimming cost inaonyesha yuko kwenye msitu wa Sea grapes
Otherwise Binti yetu Illuminata ana quality zote za kuwa Miss Universe, Congratulations to you ILLUMINATA and for your good representation of our beloved Country TANZANIA, trust me UMEONENAKA SANA TU kwani watu wengi nilioongea nao waligusia jinsi ulivyo mrembo.
SHE IS UGLY MAN! Thant is the reason, choose someone beautiful!!!!!!!!!!!!!!!!!!please.
ReplyDeleteUnajua michuzi neno CHANGE ni muhimu sana hasa kama unataka kuendelea. Viongozi wote wa mambo ya urembo hasa wa ngazi ya juu inabidi WAJIUZURU ili kuruhusu new luck,new face,new managements and NEW SYSTEMS.
ReplyDeleteunajua makocha kama Scolari,Ranieli,Keegan na Morinyo siyo makocha wabaya lakini inapotokea kwamba mafanikio na malengo hayafikiwi ktk kazi zao wanafukuzwa au wanaamua kujing'atua
Sasa viongozi wetu wa fani ya urembo siyo kwamba ni wabaya ila tu inabidi watoe fursa kwa vipaji vingine vijaribu kutetea taifa letu.
milele globu ya jamii so as mdau no:1
thanx
Here we go again...!Kashindwa kwa sababu hamna kula.Je mmeangalia uzuri wake,figure yake,nguo alizovaa usiku huo zilimkaa kupita wengine??je anakichwa kuliko wengine.
ReplyDeleteUnafikiria miss venezuela alishinda kwa sababu nchi zima ilipiga kura?hata kidogo.
Mimi na mke wangu tuliangalia event na kabla hata hawajafikia kwenye last question,tulisha hisi miss venezuela,portorico,australia and kosovo watafika finally na ndivyo ilitokea.
Mimi na mke wangu tulimpigia kura illuninata before event.Lakini kwenye kumchagua nani shinde sisi wenyewe tulishindwa kuona kama anastahili.
Lakini kajaribu na Tanzania inabidi wachague wasichana na wajitangaze kwa kufanya mambo mbali mbali duniani,shule,style na Uzuri.Waache kuchagua mtu kwa kuwa anauwezo wa kuonga.
Comment mlizotoa ni nzuri sana, hasa kuhusu mabadiliko na nini kifanyike ili mabinti wa bongo waweze kushinda kwenye hizo contests. Kibaya ni kuwa wahusika wanasumbuliwa na ugonjwa unaitwa denial (kuto kukubali ukweli na hali halisi) hivyo mwakani msubiri mambo haya haya tu.
ReplyDeleteJingine ni suala la kusema haikuwa bahati yetu or sijui Mungu hakupenda a.k.a majaaliwa. Hii mambo ya kumtegemea mungu apende au sijui majaliwa ndo inawalostisha wabongo sana tu. Watu wanaacha kufight na kutimiza wajibu wao wa kujifua kwa juhudi na maarifa, kujielimisha, kufanya mazoezi ya kufa mtu, kupanga mikakati ya maana na kutambua makosa yaliyofanyika jana yarekebishwe leo na kesho kuwe na mabadiliko wanamtegemea Mungu awafanyie. Hivi mnadhani huyo Mungu anawahudumia ninyi tu? Je wengine nao hawamuombi? Sasa amsaidie nani ashinde na taji lipo moja? Acheni uvichaa wenu. Timizeni wajibu wenu kwa kuhakikisha kuwa mnawaandaa wawakilishi wenu vya kutosha katika kila idara, kuonge kiingereza cha manzese haitoshi, ni bora kwenda kuongea kiswahili na mkalimani ili hali mwakilishi wenu anauelewa na uwezo wa kuchanganua mambo. Kujieleza ni suala gumu mno hasa kwetu sisi wabongo, inaitwa communication skills, hizi watu hujifunza mashuleni tangu wakiwa wadogo sana mpaka vyuo vikuu, sisi hatufanyi hayo. Yaani Miss wa kibongo anasimama kujadili issue mtu unaficha uso, kudadeki.
Hii si kwa mamiss pekee, hata wanasoka wetu na wawakilishi mbalimbali wa sanaa na michezo hata wasomi katika taaluma wanazolingia. Kama jamaa hapo juu alivyoeleza, wasomi wenyewe wa chuo vikuu vyetu, uchambuaji wao wa mambo ni wa kipuuzi mno, unaweza ulie. Mfano halisi, Kikwete alipokuwa akijibu maswali ya watanzania waishio USA kuhusu suala la duo citizenship, akasema, wasomi tena wasomi hasa hapa bongo wamemshauri alitupilie mbali suala hilo kwa kuwa watu "watakula huku na huku". Hii ni hoja ya kijinga na ya kishenzi kupindukia kutoka kwa msomi na raisi kuichukua kama ilivyo kuueleza ulimwengu kuwa, Tanzania hatutakuwa na duo citizenship kwa kuwa watu watakula huku na huku.
Mimi binafsi nimeshakaa sana na wabongo wasomi wa mlimani na vyuo vingine, yaani wengi wao, walifaulu mitihani tu, elimu hawakupata (huu ndo msingi hasa wa elimu ya bongo). Hoja zao ni afadhali za mkulima ambaye hakuona darasa kabisa, wabishi wa kufa mtu, tena hukimbilia tu hoja bila hata kuielewa inaanzia wapi. Hawana tools kabisa za uchambuzi wa mambo, hata kama walizisoma huko shule, lakini inapokuja wakati zinahitajika kutumika kwenye hoja, mijadala au kutatua tatizo, hutupwa pembeni kabisa, wakafuata elimu zao za mitaani.
Hivi niambie msomi gani huyo, afuatwe na rais wa nchi kuombwa ushauri juu ya hoja ya duo citizenship akasema haifai kwa kuwa watu watafaidi kwa kula huku na huku? Maana yake ni kuwa, hawa wasomi wenyewe hawakuzisikia kabisa au kuzisoma hoja zilizotolewa na watu juu ya faida ya kuwa na hiyo kitu na itumikaje, itamsaidia nani na kadhalika. wao waka kurupuka tu na jibu hilo la kipumbavu. Bahati mbaya rais wetu naye ndo hivyo tena.
Hivyo basi kwa upande wangu sioni kama kutakuwa na mabadiliko yeyote katika uendeshaji na uchaguzi wa warembo wanaotuwakilisha kwenye mataji mbalimbali hapa duniani. Wahusika watakuambieni tu, mtatuambia nini, sisi tunafanya hivi kila siku?
BONGO BWANA!!!
lazima tukubaliane na ukweli msichana wetu alihitaji kufanya zoezi kukaza mwili, alihitaji kupata stylist amfundishe mambo mengi haswa katika uvaaji nguo tofauti na alitakiwa awe na confidence kubwa sana ambayo alishindwa kuionyesha iwake pale. Lakini yote 9 kumi bwana wale wanawake ni walikuwa wa nguvu sana kiasi kwamba ilikuwa si rahisi kumchagua iluminata. Labda mwakani mjaribu kuwashauri mabinti wetu wafanye zoezi sana kabla ya kuchaguliwa huko. nafikiri pia hata yeye mwenyewe iluminata alijua kuwa hatachaguliwa lakini heri kaenda vekesheni. na mwisho kabisa ka michuzi mpeleke kwa yule mganga wa jadi uliemtoa juzi kusudi amwoshe nyota yake, waswahili wamemchafua bure :) ngoja niishie hapa swaumu ni kali.
ReplyDeletemi ningeomba miss tz awe tofauti kama alivyokuwa yule dogo aliyeingine 10 bora, upara ulimpa chat men..
ReplyDelete