Michuzi za Swaumu Shekhe,
Hii iweke maana si uchafuzi wa hali ya hewa wala si kudodosa swaumu za wadau. Ni hali halisi inayofaa kujadiliwa kwa kina.
Zamani ilikuwa ni wanaume waliokuwa wakilalamika, kwamba wake zao hawataki kuwapa chakula cha usiku kama wanavyotaka. Lakini baadae yaani siku hizi ni zamu ya wanawake kulalamika.

Katika nyumba nyingi siku hizi hasa mijini wanawake ndio wanolalamika zaidi kukosa chakula cha usiku kama wanavyotaka kutoka kwa waume zao.
Kwa nini hali hii?

Ukweli ni kwamba maisha yamebadilika sana na kila mtu anajitahidi sana kutaka kuhahakisha kwamba anafanya kazi hadi anaishiwa nguvu kabisa, akili na mwili vinachoka. Wanaume wengi wanaolalamikiwa na wake zao kuhusu kupata uhaba wa chakula cha usiku ni wale wanaofanya kazi sana .

Ningependa kuwashauri wanaume kwamba wakati wanafanya kazi zao mchana wakumbuke kwamba kuna wake zao wapendwa ambao wanawasubiri jioni kuzungumza nao na zaidi ya hapo. Wakumbuke hawajaoa kazi bali wameoa wake. Pamoja na kwamba ni muhimu kwao kufanya kazi, lakini wakumbuke kwamba kazi hazina mwisho.

Kuna jambo ambalo wanaume na hata wanawake hawalijui vizuri, hili ni lile linalohusu mazoezi. Mtu anapofanya mazoezi anawezesha damu kuzunguka na kufikia sehemu zote za mwili kwa kiwango kinachotakiwa. Kukaa ofisini kutwa na kurudi nyumbani na kukaa kwenye kochi na kuangalia TV siyo aina ya maisha inayoshauriwa tuishi. Mwili unapochangamka kwa damu kufika kila mahali kwa kiwango kinachotakiwa hamu ya kutoa chakula cha usiku na kukipokea huwa kubwa.

Lakini mbaya zaidi ni kwa wanawake wenyewe pia. Kuna wanawake ambao bado wanaishi kwa miiko ya karne moja nyuma. Hawa wanangoja wanaume zao wawachokoze, wasipofanya hivyo, basi hata mwaka watakaa wakilalamika kwamba hawapati chakula cha usiku. Tukumbuke kwamba hata wanaume nao ni binadamu pia, huhitaji wakati mwingine kushtuliwa, kwani wakishtua wao tu kila siku, kuna wakati hukinai.
Mdau wa Lanchi ya Usiku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Halo halo sasa kumekucha....kina mama tuwe mstari wa mbele kote kote yaani wanawake na maendeleo isiishie kwenye utafutaji vijisenti tu babu yaani tuendeleze libeneke la mstari wa mbele hata kwenye nanihiiiiiii jamani tuamke sasa ebo....

    ReplyDelete
  2. WEWE ULIYOANDIKA NAKAL HII NAFIKIRI SIO MZIMA WA AKILI. UPEO WAKO WA KUFIRIA NI MDOGO SANA.SIONI HATA FAIDA YA KUKUPA USHAURI NAONA ITAKUWA KAMA KUMPIGIA MBUZI GITAA.

    ReplyDelete
  3. Nimefurahi sana kuisoma mada au point ya mazoezi (chakula cha usiku) ni afya Je kwa wale ambao kwa bahati mbaya hawakubahatika kuolewa au wameachika je!! labda utasema wafanye mazoezi ya kawaida ila kutoka na miundo mbinu na uafrika wetu mimi kuvaa bukta na kuanza kukimbia barabarani ni vigumu, pia viwanja vya mazoezi hakuna katika mitaa ya uswahilini je hili linaaje????

    unashauri wafanye nini?

    ReplyDelete
  4. wewe anon wa 02:10:00 PM mi naona wewe ndiyo hazimo kabisa. Sasa ubaya wa makala hii ni kitu gani maana umekuwa so broad hata sipati picha wazimu wa huyu mwandika makala uko wapi. Hebu changia kwa point tuone concern yako iko wapi labda utatubadilisha mawazo.

    ReplyDelete
  5. Wakey wakey
    Kiswahili ni lugha ngumu sana
    Huyo jamaa hapo juu hazungumzi habari za chakula au FOOD
    Cant you understand
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  6. Man, I need one of these women !!!!
    Nataka mimi mke/mwanamke wa aina hiyo !!!
    Sam

    ReplyDelete
  7. Mie naona bado watu dini kwenye vichwa vyao vipo chini mkisoma dini na kuwacha mila za watu wa nje na kwenda na njia za dini basi matatizo yote yataisha haya. Kuanzia kulalamika mpaka kustahamili mungu ndio anajuwa sio nyie.

    ReplyDelete
  8. kweli wewe anon wa 02.10.00 pm wewe mwenyewe ndo hazimo,watu wanaleta hoja za maana ili tuzidiscus,na wengine tupate mawazo ya watu,na wewe unatuwekea usiku.watu wengine bana!!!

    ReplyDelete
  9. Jamani kaka Michuzi, hawa watu yaani mimi nawashanga; kwa sababu kama mama anaona bwana hampi chakula basi yeye apike chakwake. Maana wakina baba wanategemea akina mama ndo wapike sasa kama wanakuwa wakipika kutusaidia sio mbaya lakini tusiwalazimishe basi kwani wanakuwa wanachka jamani. Bye, wako mdau wa Kakete.

    ReplyDelete
  10. Huyu anon wa 02:10:00 ameponda sana huyu bwana aliyepost hii mada.Mimi sioni ubaya wa hii mada,ni mada ambayo ina mambo ya kweli kuhusu maisha.Nina wasiwasi huyu anon atakua AMEKUBWA NA HILI TATIZO,na ndo maana amemponda sana huyu mdau aliyetoa mada hii.

    Mkulima-kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  11. Kaka michu nimeipenda sana makala hii. Kweli wababa mara nyingi hufanya kazi kwa ajili ya kutoshereza familia. Pia ikumbukwe mama pia ana haki yake katika chakula cha usiku, ila wamama nao waseme na wazee wao kwa maneno matamu yatakayo mshawishi wababa wawe na hamu na chakula cha usiku. Kweli baba ameludi amechoka mama naye kauchuna tuu, kumbe moyoni anahitaji chakula kumbuka hata baba ni binadamu siyo mpaka awe na njaa yeye tuu ndiyo adai, hata wewe mama ni haki yako kudai masaa 24 madamu una njaa na hili linasaidia katika kudumisha ndoa na uaminifu. Jac

    ReplyDelete
  12. kaka michu 'ZIS MADA IZ PERFECT'nimeipenda na ushauri ni dhahiri kabisa,sasa huyo anon wa saa 6:45 ndiyo kituko kingine hajaelewa kapsaa,wadau tusome vizuri na kunyambua maana kaka michu katumia "TAFSIDA"kufikisha ujumbe kwa jamii,hamaanishi chakula as in Food,anon wa saa 6:45 upo hapo?????

    ReplyDelete
  13. Nikiangalia hizi comments baadhi nimegundua kuwa kuna baadhi ya watoto wanachangiaga mawazo katika mada. Imekuwa ngumu kwao kuelewa hiki CHAKULA CHA USIKU NI NINI kwani wao wanachukulia ni chakula kama chakula cha kula. La hasha si hivyo, na si kila neno hadi mtu aongee wazi japo mafumbo kidogo naimani wengi mmefundishwa mafumbo mashuleni.


    Hili jambo la chakula cha usiku kwa wababa kutowapa wake zao ni kuwa wanaume walio wengi wamekuwa na vimada nje hivyo unakuta huko keshatokea kwa kimada keshapewa chakula basi akifika nyumbani anakuwa hata hisia hana tena.

    Naimani mwanaume aliyekamilika lazima atakuwa na hisia hata kama akija amechoka japo akilala ile mida ya asubuhi asubuhi saa kumi kumi au kabla hajaamka ataweza hitaji chakula labda tuu kama atakuwa alipewa chakula pengine.

    Pia ni kweli wanawake wengi tunajisahau wakati mwingine. Tunakuwa nasi busy na mambo yetu watoto, kazi nk. Mapenzi tunayahamishia kwa watoto tunamsahau baba. Hili halitakiwi mwanaume pia anahitaji kushtuliwa kidogo kufanyiwa vitimbi hivi na vile yeye mwenyewe atatoa chakula.

    Jamani naimani Kitchen Party bado zipo kina mama mlioolewa mmezipata, na wale ambao hamjaolewa mnaudhuria katika kitchen party hivyo mnauzoefu nini chakufanya kwa waume wenu.

    Hadi hivi leo hiyo kauli ya haki sawa kwa wote mimi naipinga japo ni mwanamke kwa kuwa tunakuwa tunamkosea Muumba kwani hakuweka haki sawa kwa mwanaume na mwanamke. Alimpa Mwanaume haki zake tofauti na mwanamke haki zake . Wanawake sisi sio tujipe kifua mbele saana tusome maandiko ya Mwenyezi Mungu alivyoamrisha.

    Tukumbuke yadunia wakati mwingine yanapotosha wanadamu.

    ReplyDelete
  14. We uliosema Uswahilini hakuna viwanja vya kufanya mazoezi na unaona aibu kuvaa bukta.

    Mazoezi si lazima utokea nje ya nyumba yako. Kama una uwa nyumbani fanyia mazoezi uwani kama hauna uwa una hata sitting room au chumbani. Tafuta kamba fanya mazoezi ya kuruka kamba, pushup, nk. Mbona mazoezi yanawezekana tuu.

    Acha kisingizio wewe anon tatizo mmeshazoea kujilegeza sana.

    ReplyDelete
  15. Watu wengi mmetoa maoni ama kusifu mada ama kulaumu mada na wapo wanaowalaumu wanaokosoa mada, lakini hakuna aliyechangia kiuhakika kabisa. wengi wanaona aibu kuchangia labda ni kwa sababu tatizo hili ni kubwa.
    Naungana na mdau aliyeleta hii mada mbele yetu. tatizo la chakula cha usiku kutokuliwa ama kuliwa nusunusu bila kushiba ni tatizo kubwa sana na si tanzania tu bali kalibia katika nchi zote.
    Kuna mambo mengi yanayosababisha jambo hili. mojawapo limeshatajwa na mdau mwenyewe! lakini tatizo lingine ni aina ya vyakula vinavyoliwa sasa.

    kijana wa kiume unakuta chakula chake kila siku ni chips kuku na chocolate, asklim na vitafunwa vingine kwa kweli kwa hari ya kawaida kijana kama huyu, baada ya muda uwezo wake wa kushiliki chakula cha usiku unakuwa mdogo sana.
    Mafuta yanayotumika katika mapishi ni sababu tosha ya kumaliza hamu ya chakula cha usiku.ukiwa wewe ni dk, ama uko kalibu sana na masuala ya tiba haya ninayoandika utakuwa unayaelewa sana. akina baba wengi wamekuwa wakisumbuka na matatizo haya mahosipitalini.
    Chukua mfano, mtu anakwenda kazini kwa garihata ikiwa ni daladala, anafika ofisini ama sehemu ya kazi anapata chai kwa vitafunwa vilivyojaa mafuta kupita kiasi. mchana. baada ya masaa matatu anakwenda kupata chakula, chips kuku ama mshikaki, mafuta hayo, jioni ana kalibia bar anapata safari mbili tatu na kiti!! hivi unafikili kwa ratiba hii ya mlo anaweza kula vizuri chakula cha usiku? matokeo mtu anaishi na mwenzie kwa wiki 2 wakiangaliana tu. tatizo hili pia lipo kwa baadhi ya wanawake ambao kutokana na mfumo mbaya wa ulaji na cream wanazojipaka nk. wanakosa nguvu ya kuimili misukosuko ya chakula cha usiku hivyo kujikuta wakiwa wachovu kupita kiasi na kukichukia kabisa chakula iki.muda autoshi kueleza kila kitu ila tujue kuwa ni tatizo kubwa sana na kwa kweli ndio wakati mwingine unamkuta bint mbichi kamnga'ng'nia mzee wa siku nyingi, kwa kuwa wazee wetu awajazulika sana na hari ya hewa ya sasa. wao walibahatika kukulia katika mazingira safi na salama ndio maana hata katika umri wao bado wanaweza kula chakula iki kwa umalidadi zaidi.pia ndio sababu ya ongezeko kubwa la waganga wa jadi kila mahari wakijitangaza kutibu tatizo hili. wao wameshagundua udhaifu uliopo na wanatumia nafasi hiyo japo wengi wao si wa kweli.ushauri wangu wa mwisho ni kuwa tuepukane na vyakula vya mafuta mengi na tufanye mazoezi ya mara kwa mara na mazoezi hapa sio lazima kukimbia ama kucheza mpira. hata kutembea kwa dk20 ama 30 ni mazoezi tosha.pia tujitaidi kula vyakula vya asili kama, ugali wa dona, ugali wa mtama, maharage, kunde na mbogamboga zingine.

    ReplyDelete
  16. Aisee anon wa Tues Aug 25, 09:34:00 AM yaani nakufagilia ulivyo nyumbua nyumbua mada. Watu siyo kuhangaika hangaika tu mara nimelogwa mara vile kumbe ni mifumo mibovu ya style ya maisha. Kweli umenigusa yaani wewe ningependekeza wakutunukie ualimu wa sayansi ya jamii kabisa....

    ReplyDelete
  17. nashukuru kwa mliojaribu kuzungumzia baadhi ya vyanzo vya ktopewa hilo hitaji la kimwili. napenda nitoe sababu zinazoweza kumfanya mtu asipende kushiriki ktk tendo hilo.lakini sitaeleza kwa kina sana,nitagusa tu kwa muhtasari.
    1.baadhi ya magonjwa yanayo athiri mfumo wa mzunguko wa damu,kama vile kisukari,ugonjwa wa moyo n.k
    2.uzito mkubwa wa mwili,ambao unaweza kusababishwa na aina ya lishe,au unaweza kuwa sababu au matokeo ya magonjwa niliyo ya taja hapo juu.
    3. kupungua uzalishaji wa baadhi ya vichocheo(hormones)kama testosterone,au kuongezeka kwa uzalishaji wa baadhi ya hormones za kike kwa mwanaume-oestrogen. sitazungumzia sababu zake zaidi.
    4.msongo wa mawazo kutokana na sababu tofauti za kimaisha.
    hizo hapo juu ni baadhi ya sababu za kimsingi ambazo zinaweza kumuathiri mwanamume asihitaji kula chakula cha usiku.
    pia zipo sasa sababu ambazo ndizo wengi huzitumia kulaumu kunyimwa tendo hilo,ambazo sio za msingi maana zinaweza kutatulika kirahisi tu kama wahusika wana nia ya dhati:-
    1. mwanamume kuchoropoka mapema na kula gengeni(kwa bi chau) japo mimi naweza kula hata magenge manne tofauti kwa siku na nikalipa pesa bila kuacha deni!hahaha! maana afya inaruhusu lakini sifanyi hivyo maana sio busara na sio sifa!!!!
    2.kutokuweka mazingira safi na yenye mvuto wa kutaka kula msosi huo,ikiwa ni baadhi ya vyakula vinavyoweza punguza nguvu kwa mwanamume au vinavyoweza ongeza hamu ya tendo hilo(kama havitatumiwa)hivi ni tofauti kwa wababa na wamama,sitavieleza hapa;uwanja wa kuchezea mechi,baadhi ya manukato yanaweza kata au chochea hamu kwa muhusika,kukosa kubadili mtindo wa kucheza mechi au viwanja, maneno yanayo tangulia mechi yanaweza kuathiri matokeo,kwa mfano badala ya kucheza kwanza ndipo ueleze matatizo,unaanza kueleza matatizo kwanza kisha unatarajia matokeo ya mechi yawe ya kuridhisha!!?
    3.mazoea mabaya ya kutaka kuwa meche inachezwa usiku tu,hili linahusiana na hilo hapo juu pia la viwanja na style.
    4.ukosefu wa mazoezi,na kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu.
    5.matuizi ya baadhi ya madawa na pombe kupita kiasi.
    HII HAIHUSIKI ILA NAWATAHADHARISHA
    kwa wale wakaangaji wa vyakula kwa kutumbukiza ndani ya mafuta,yaani kama chips,maandazi,samaki n.k msipikie mafuta zaidi ya mara mbili,maana yanakuwa cancerogenic(yanaweza kusababisha saratani=kansa)kama mtu anauwezekano huo wa kupata saratani na angeweza kuepuka kuipata kama hatatumia. sasa walaji wa chips angalieni kama mnapo zinunua hawabanii mafuta na kurudiarudia kuyatumia.
    this was just a piece of advice!!

    mdau-**********

    ReplyDelete
  18. Duh! ukijumuisha hawa Tues 25, 11:05:00 AM na 07:38:00 PM mwanawane kama unataka BEHAVIOUR CHANGE hapa lazima ufanikiwe...yaani hawa jamaa ni wataalamu kweli kweli nawafagilia, hasa huyu wa PM yaani kamwaga hospitali nzima, hapa kazi kwetu wadau mwenye sikio na asikie...

    ReplyDelete
  19. Michuzi bump hii topic iende juu tena ni muhimu sana.

    Wengine humu sijui ni pg 13 hawajaelewa lakini kwa walioelewa we really need to discuss this in depth.

    Aliyeileta nampongeza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...