Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo imekabidhi zawadi kwa washindi watatu wa promosheni ya Tigo ijulikanayo kama KILA MMOJA ANASHINDA
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi wa Tigo Jackson Mmbando alisema Promosheni ya Kwaruza kila mmoja anashinda leo imetimiza washindi watatu na wamejishindia zawadi tofauti kila mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi wa Tigo Jackson Mmbando alisema Promosheni ya Kwaruza kila mmoja anashinda leo imetimiza washindi watatu na wamejishindia zawadi tofauti kila mmoja.
"Ijumaa iliyopita tulimkabidhi bwana Raymond Sinda toka Dar es Salaam shilingi milioni Tano, na leo tunao wengine wawili Barat Nathwani aliyejishindia milioni moja na Amran Suleiman Nassoro aliyejishindia laki tatu.
"Makabidhiano haya ni ishara tosha kuwa wateja wetu wameanza kuneemeka na promosheni hii Ambapo lengo la kuanzishwa ni kutaka kufaidisha wateja wetu walioko nchi nzima.
"Bado tunaendelea kusambaza vocha hizo za promosheni kila mahali na tunaendelea kutoa wito wateja waendelee kukwaruza na wahakikishe wanatumia zawadi zao mara baada ya kukwaruza vocha za KILA MMOJA ANASHINDA", alisema Mbando.
Amesema ikiwa mteja wa Tigo atanunulia muda wa maongezi wa 2,000, 5,000, 10,000 atapata zawadi ya muda wa maongezi 100, 250, 500 au 750 pia zipo zawadi zaa pesa taslim 300,000, 500,000 au 1, 000,000.
kila vocha ina sehemu ilioandikwa neno (ZAWADI) na kufichwa ambapo mteja anatakiwa kukwaruza na akishaijua zawadi yake vocha au pesa taslim atafuata maelekezo yafuatayo ili kujipatia zawadi yake mara moja.


Tunawashukuru sana kwa hii promosheni yenu,angalau imeshuka hadi uwezo wa kawaida, na tungefurahi zaidi kama mngeshuka hadi chini kabisa, yaani hata mtu akinunua vocha ya mia tano anaweza akapata chochote, kwasababu wengine sio lazima wanunue vocha ya 2,000/- papo hapo, anaweza kwa siku akatumia zaidi ya hiyo, lakini hununua vocha za 500/- kila akiishiwa salio.
ReplyDeleteKwangueni mshinde
i really admire your blog kwa kazi nzuri unayoifanya especially unapoi update kwa matukio ya kila siku.
ReplyDeleteplz dont stop here keep on educating us with your blog coz we learn alot of issues kuhusu life na watu pia. keep on entertaining us as well as educationg.