Kama tulivyoanza wiki iliyopita,wiki hii tena tunagusa kwenye anga za siasa. Kama umekuwa ukifuatilia kwa makini yaliyojiri wiki hii, kubwa zaidi lilikuwa suala la Mheshimiwa Spika,Samuel Sitta, kukingiwa kifua na wapinzani kutokana na kile ambacho CCM(chama chake Sitta) wamekiona kama “kuwageuka” baada ya kuruhusu masuala ya mijadala ya ufisadi iendelee bungeni.
Walimtishia kumpokonya kabisa uanachama kama asiposikiliza.
Kinadharia wanachosema CCM ni kwamba ukiwa mwanachama au mbunge kupitia CCM,basi sio haki kunyooshea vidole mambo “mbofu mbofu” yanayoweza kuwa yanaendelea ndani ya CCM. Wanadai kama kuna kutofautiana,basi mambo hayo yamalizwe katika vikao vya chama na sio mahali pa wazi kama vile bungeni.
Kinadharia wanachosema CCM ni kwamba ukiwa mwanachama au mbunge kupitia CCM,basi sio haki kunyooshea vidole mambo “mbofu mbofu” yanayoweza kuwa yanaendelea ndani ya CCM. Wanadai kama kuna kutofautiana,basi mambo hayo yamalizwe katika vikao vya chama na sio mahali pa wazi kama vile bungeni.
Wao CCM wanasema ni haki yao kumhoji au kumkemea Spika kwani yeye ni mwanachama wa CCM kama walivyo wengine. Anayesema hivyo ni Katibu Mkuu wa CCM,Yusuph Makamba. Kisha anasema bunge ni mali ya chama tawala cha CCM!
Je unadhani nini kinaendelea ndani ya CCM? Spika Samuel Sitta yupo sahihi? Makamba yupo Sahihi? Samuel Sitta ndiye mwanasiasa wetu wa wiki hii.
Mjadala huu upo hapa na


jamani suala la six lipo wazi kwa kila mpenda haki na maendeleo ya nchi yetu. kuhusu makamba, chonde chonde, muacheni huyu ndg apumzike tu. sio vema sana kujadili uhalali wa kauli zake. pia si sahihi kumlinganisha six na makamba, utakuwa unamuonea mmojawapo kutokana na uwezo binafsi na nia ya ndani ya kila mmoja kwa umma wa watanzania. tuangalie namna gani tunaweza kuifanya tanzania iwe ni mahali penye neema shirikishi wa watanzania wenyewe.
ReplyDeleteHawa Jamaa(CCM) Lazima wabadilike, CCM isiwe kimbilio la waovu, kiwe chama safi kama kilivyokuwa wakati wa Mwalimu, Tunawafahamu watu safi tuu ndani ya chama, lakini wamemezwa na uwingi wa mafisadi na watu greed, hii ni hatari kwa taifa kwani CCM ndio chama tawala
ReplyDeletetopic nzuri sana. hope you'll make this a fair playground by allowing comments, feelings, ideas of different dimensions. la sivyo ukianza mtindo wako wa kubania maoni fulanifulani basi hakutakuwa na maana ya kurusha hii topic hapa
ReplyDeleteahsante
Kwa ujumla Mjadala unaoedelea kuhusu Mhe. Sitss hautupi matumaini sisi tulion nje ya “Chama”.Tunashngaa pale watu wenye sifa kama “Tambwe Hiza” na Mwanasheria wa CCM wanapo kanusha kuwa kauli zinazohusiana na kummwonya Sitta hazikutolewa kwenye kikao cha NEC. Wakati hoja hizo zinatolewa na wazito kwenye chama cha ajabu Mhe. Sitta amekuwa kimya tokea vyombo vya habari vimeripoti hoja hii ya kukandamizwa kwa mhe. huyu. Mpaka sasa Sitta ambaye ni mwanachama hai wa CCM hajapata “kukanusha wala kuthibitisha” kauli hizi nzito juu yake. Aidha, kwa upande mwingine, watu kama Mhe. Mwakyembe (Mbunge Machari), Mhe. Kingunge (Mbunge wa Upinzani ndani ya CCM), na wengine wote ambao wametajwa na vyombo vya habari kutoa matamshi aidha ya kumkandamiza/ kumtishia Sitta au kumtetea hawajadhubutu kutamka jambo lolote kukanusha au kuthibitisha tarifa zilizotolewa na vyombo vya habari. Hivi nini ilikuwa nia ya CCM kumpitisha kwa kishindo Mhe. Sitta???walitaka awatete CCM kwenye chombo makini cha wananchi kama Bunge?. Ona sasa hata ufisadi uliokuwa ukisemwa juu ya Sitta na Kingunge pale Ubungo Terminal umefunikwa na mjadala huu!. Hali inatisha kwa sasa.
ReplyDeleteSETA MWENYEWE FISADI MKUBWA MNAFIKI MARA NGAPI AMEKUA AKIWAPIGA VITA WAPINGA UFISADI WA UKWELI KAMA ZITO?
ReplyDeleteHAO WENGINE WAKINA SLAA NI WANAFIKI TU VIBARAKA WA MENGI NA NDIOMAANA HAELEWANI NA ZITO NA MAREHEMU CHACHA WANGWE!!WALIKUA NA PLANI YA KUMFUKUZA KABISA CHACHAWANGWE.
PIA MKITAKA KUJUA SITA NI FISADI KUBWA LINALOTUMIA KIMVULI CHA VITA YA UFISADI KULINDA MASLAHI YAKE!!LEO UKITAKA KUMPINGA JIMBONI KWAKE AMA MAGAZETI YATAKAYO ANDIKA MACHAFU YAKE HUWA ANATUMIA NAFASI YAKE YA USPIKA KUYAKANDAMIZA MAGAZETI YANAYOFICHUA UCHAFU WAKE NA WALE WATAKAOJARIBU KUMPINGA JIMBONI KWAKE HUWAITA MAFISADI AMA WAMETUMWA NA MAFISADI KUTISHIA MASLAHI YAKE.
SASA HIYO TUNAYOITA DEMOCRASIA IKOWAPI?
INAMAANA HII LEO UKITAKA KUCHUANA NA MTU JIMBONI WEWE NI FISADI NA UMETUMWA?HAWA NDIOWANAOTAKAKUFIA MADARAKANI.
AMALEO MAGAZETI YANATAKIWA TU KUANDIKA DHAMBI ZA MTU MMOJA TU?WENGINE MIUNGU WATU?
SITA NIFISADI MKUBWA KAMA WAKINA ROSTAM WOTE SAWA WANATUDANGANYA NA SIASA ZAO CHAFU WOTE WAPO KIMASLAHI NA NDIO MAANA HATA SIKUMOJA HUTOSKIA WAMEONGEZA MSHAHARA WA MANESI BALI KILA SIKU WANASEMA MISHAHARA YAO NDIO HAIWATOSHI WAONGEZEWE.
ETILEO SITA KAPATA MPINZANI KTK CHAMA WACHUANE BUNGENI NA MAGAZETI YAMEANDIKA UCHAFU WAKE ANADAI AONGEZEWE ULINZI!!ANAMUOMBA WAZIRI MKUU AMUONGEZEE ULINZI BINAFSI HELA AMBAZO SI ZAWAZIRI MKUU NI ZA WALIPAKODI NDIO WATAKAOGHARAMIA ULINZI HUO WKT WALIPAKODI WENYEWE ROHO JUJU KUTOKANA NA UJAMBAZI NA UHALIFU MWENGINE HAWANA ULINZI
Hili swala ni tete...!
ReplyDeleteila tu kumbukeni kwamba sisiemu wana treak nyingi so mkikurupuka 2015 ni sisiemu tena, hili ni chezo la kupunguza kura upinzani.
pia wajumbe wa chama ndio chanzo cha uozo na mizizi ya mafisadi wao ndo wanampitisha mgombea kwenye kura za maoni iwapo tu utawahonga pesa nyingi,hawaangalii huyu mtu anatufaa au ana qualification za kuwa mbunge wetu. mtashangaa kuona mafisadi wote wameshinda kwa kura za maoni 2010.HII HUWA INANIUMA SANA.. NA HATA NAFASI YA UJUMBE BILA KUJUANA AU HELA HUPATI.. DOLA LIMESHATEKWA JAMANI
Watanzania wenzangu; huu sasa ni wakati wa kukataa kuendelea kundanganywa kwamba CCM ni chama kinacho tetea hali ya wanyonge.Hiki chama sasa ni cha Majambazi/Mafisadi/Majizi/Wahujumu na Waongo wakubwa.Kinachoendelea sasa ndani ya chama na serikali ni kulinda kwa nguvu zote maovu yote tunayoyaona na yasiyoonekana yaendelee kuwa ni haki kwa CCM.Hili la Sitta na NEC ni dalili tosha kuwa CCM wanaonyesha kuwa wizi waliofanya wasisemane wao kwa wao kwani wote ni wezi.Lakini nampokeza Sitta kwa kuruhusu mjadala wa Mafisadi ujadiliwe Bungeni, wakati akijua fika nayeye ni mmoja wa Mafisadi wakubwa.Ndugu zangu Watanzania sasa tuseme inatosha CCM si baba yetu wala si mama yetu! Hivyo wabunge wa CCM walionamapenzi mema na TANZANIA waendelee na msimamo uleule wa kuwafichua Mafisadi; musiogope kufukuzwa CCM, kwani kura mtapata tuu hata kama hamkupitia CCM.Watanzania sasa tutachagua mtu safi na si jina la chama tena.
ReplyDeleteMakamba. malekela, Kingunge na wengine wachache wanatakiwa wapotee nchini TAnzania.
ReplyDeleteWanahisi Tanzania ni ya kwao na sisi wengine ni mijinga.
Wamejitaengenezea majina na wanasema na kukomandi kila watakacho
Wanajali maskahi yao na mitoto yao
Wanasiasa wote wa tanzania hamna kitu, wako motivated kuchuma pesa ya wananchi mengine yote ni cover. Mbona hamana maendeleo yeyote kwa wananchi wengi tangu uhuru. Kwao wao madaraka ni pesa ya bila kuitolea jasho. Wote ni mafisadi hamna hata mmoja mtu safi katika siasa. wezi tu.
ReplyDeleteKwa wanayotokea ndani ya NEC ya CCM SG Makamba yuko right. Yanayotokea ndani ya Bunge Sita is equally right. Ila ni kuwa makini kuwa nguo zako za ndani hufulii hadharani.
ReplyDeleteKaka Michu hii nimeipopoa kwenye mtandao
ReplyDeleteBy GAME THEORY
In the wake of new allegations against him, its obvious Tanzanian politics this weekend will defined by one gruesome paradox. Samuel John Tegeza Sitta aka Mr 6 is finished. Yet he still commands, or at any rate makes, regular appearances on the stage. There is endless, lively speculation about how much longer he will remain speaker of the parliament.
One doesn’t need to hit on jamiiforums.com (JF) or back benchers Canteen in Dodoma to understand that ever since his appointment ‘mzee Six’ has been at the apex of the culture of deceit and downright fraud which has destroyed the once luminous reputation of the our parliament.
The historic role of a Speaker is to make sure that Parliament calls ministers to account, and acts - as it has done throughout history - as the sovereign and authentic voice of Tanzanians. In otherwords Speaker is elected to defend the privileges of ‘Bunge letu tukufu’. Those privileges are free speech, free access to ministers and to information, free accessibility to government officials and complete oversight of the government.
It has been a mystery for over three years just why Speaker Sitta not only failed to defend any of these things but actively aided those who attacked them and sought to limit and control them. In the wake of latest allegations which mirrors his Louis XIV public funded life style as per media reports , among other things includes his $10,000 a month rent that in 5 years will cost tax payers close to 1 billion shillings! Now the mystery is solved.
He just didn't understand what the words "defend the privileges of the parliament" mean! I wonder how he even defends those $2,000 a week pharmacy bills which tax payers picked the tab, let alone and those alleged mysterious PYT’s (pretty young things), maybe he thinks it means defending 'perks', 'corruption' and 'the ability to squeeze the last drop of cash out of the public till'! At this stage I can say Mr Sitta has created and defended the world's first bottomless trough exclusively designed and endlessly refilled by the pigs themselves!
The Richmonds, Kiwiras, Radars, IPTL’s and this latest Sitta’s lavish accommodation just confirms that our new rulers are parasites, who enrich themselves constantly at the taxpayers' expense. Ask anyone trying to make ends meet and he/she will tell you that these new breed that rule us routinely abuse power, lie and suppress and manipulate the truth. They never admit error or failure, they always shuffle responsibility onto someone else. In daily life, unlike the old Establishment, they are graceless and self-obsessed.
In sum, they have no standards whatever except their own advancement. Yet they are indignant when anyone exposes their behaviour and turn savagely on those who call them to account. More significant still, Bunge has completely lost its historic role as the primary source of information about the activities of the executive arm of the state.
At least in the old establishment days, ministers with a statement to make used always to bring their news first to the Bunge. This convention has now been abandoned. It is now normal for important statements to be leaked first by those ‘mutants’ at Magogoni and to the JF armchair critics brigade, then only announced as an afterthought to Parliament.
Lets face it, the loss of reality is now total. Although neither Speaker Sitta nor his entourage can bring themselves to acknowledge as much, the ‘spika wa Bunge letu tukufu’ no longer counts in JK’s government, except for the admittedly noteworthy and striking reality that he can continue to call himself Speaker of the House .
Lesson we learn from ‘Mzee Six’ fiasco is simple, when you appoint ignorant, poorly educated people to positions as the Speaker of the house, your rules and regulations decline, your etiquette disappears along with manners, respect and responsibility.
...dRU
Sitta ameongezewa sifa kuliko anazostahili. Tuliona alivyoshughulikia suala la Zitto, alivyomdhibiti Bwana Mapesa juu ya suala la majitaka ya mgodi wa North Mara. Lakini sasa hivi amefanywa shujaa.
ReplyDeleteNadhani ni mbinu ya CCM kuhakikisha anapita katika kugombea ubunge.
Anachosema Makamba ni kuwa, Bunge ni la CCM hivyo endeleeni kuichagua CCM.
ReplyDelete"Ukiona Chama Cha Mapinduzi kimenza kuwakumbatia Matajiri basi huo ndio mwisho wa Chama Cha Mapinduzi" Julius Kambarage Nyerere. JK ORIGINAL SI JA KUBUMBA.
ReplyDeleteTatizo hapa si 6 wala ma-rope, bali ni sisiemu. wana macho lakini hawaoni. kwa vile wanatazama puani, leo tu, wanafikiri watatawala milele. kitu ambacho tunapaswa kupigania ni mageuzi ya katiba. haya yote tunayosikia - mara ufisadi, mara serikali inavuliwa nguo, mara ... ni kwa sababu ya kutumia katiba ya ujamaa kuendesha mambo ya demokrasia na ubepari. hii ni sawa kabisa na unavyoona tunaendelea kuendesha magari ya kibepari katika barabara za ujamaa. jamani katiba imechoka, na kama hakuna mhusika ambaye yuko tayari kuanzisha mchakato (ni lazima awe ni rais - maana maoni yakitolewa na mtu mwingine waCCM wanafikiria watu hawampendi JK, wanasahau kuwa leo ni JK, kesho atakuja mtu kama Nduli Idd Amin!!!) tutaendelea kusikia hizi hadithi za 6 na ma-rope tena kwa sana!!!!!!
ReplyDeleteHUYU MZEE MAKAMBA INAONEKANA WAZAZI WAKE WALIMTAFUTA KWA DAWA HUYU NA NDIO MAANA ATAKACHOKIONA YEYE KINA MASLAHI KWAKE ATAKUWA RADHI MUMZIKE ARDHINI MZIMA MZIMA LAKINI HATOACHA KUKITETEA KWA NGUVU ZAKE ZOTE...SASA HEBU TURUDI UPANDE WA TATU WA SARAFU MAKAMBA HUYU KAMA ANGELIKUWA ANAWATETEA WANANCHI KAMA ANAVYOUTETEA UGALI WAKE CCM TANZANIA TUNGEJIVUNIA SANA NA KUFARIJIKA NAYE LAKINI KWA MTAZAMO WNG MIMI NACHAGUA DEBE LA POMBE MARA 100 KULIKO MAKAMBA
ReplyDeletedu ama kweli watu wanakuwa na uwalakini mkubwa sana na uwezo wa ndg makamba. mchangiaji wa kwanza na wa mwisho, mmeleta kali. ni kweli, inawezekana hana tija sana maana hata wanaCCM wenyewe kwa nyakati tofauti wamekuwa wakionyesha kutoridhishwa na utendaji wake. kwa taifa hana kitu, ni vacuum tupu. basi ndio fiongosi wetu, na hapa JK anajuta kumteua maana sasa ni mzigo na sio msaada kwake tena. ni fundisho, wakati ujao kutakuwa na umakini zaidi. ila kwa sasa tuvumilie tu, maana watanzania kwa uvumilivu ndio jadi yetu!
ReplyDeleteWANANICHEFUA TU NA KUNIONGEZEA HASIRA, WATANZANIA HATUESHIMIANI YANI TUNASUMBUANA TU KWA MAMBO YALIYO WAZI, WALA HUITAJI TOCHI KUWEZA KUYAONA HAYA. MASLAHI YAO NA NJAA ZAO NDIZO ZINAZOTUSUMBUA WATZ.
ReplyDeleteTuje kwenye hoja,
Hoja ya CCM kuwa maswala yale yamalizwe ndani ya vikao vyao hayana msingi,kwa sababu hoja zile si tu zinaihusu CCM bali pia zinamanufaa makubwa kwa Taifa, CCM ni chama tu ambacho kimantiki chama ni watu, na watu hao ni watz ambao wamekipa nguvu ya kushika dola, hivyo watu wa CCM wajue kuna mambo yanayowahusu wao moja kwa moja hayo watamaliza kwenye vikao vyao, lakini mambo yanayohusu watz na hasa yakiwa bungeni pia yamalizwe bungeni kwa uwazi na kwa manufaa ya taifa.
Pili kimsingi nakubaliana na Makamba kama anasema wao wanahaki ya kumhoji spika kwa kuwa tu ni mwanachama wao hiyo ni sahii ila hili liwe fundisho kwetu, ukiangalia kwa undani unaona mgongano wa kimaslahi kwa mh Spika, mhe Spika kama kiongozi wa bunge nafikiri hakustahili kuwa tena mjumbe wa NEC, hapa naona suala la katiba lina rudi tena. Lazima tuweke mipaka,na misingi bora kwa viongozi wetu, ingekuwa vyema kwa Spika wa bunge kubaki kama mbunge wa chama husika na sio tena mjumbe wa mkutano mkuu wa chama husika.Hili tulichukue kama funzo, wenzetu wanaendelea kwa kuwa matatizo kama haya hawayaruhusu tena kujirudia.
Kauli ya mheshimiwa Makamba ya kuwa bunge ni mali ya chama tawala, ina utata kiasi, na utata huu unakuja kwa kuwa huwezi kusema kwa haraka alikuwa anakusudia nini hasa kwa kauli hii, ila mwanasiasa yeyote makini na mwenye busara za kutosha kwa upeo wangu mdogo naamini hasingeweza kutoa kauli kama hiyo, haya mi nayaita ni mapungufu yanayoturudisha nyuma kila sika na ndio chanzo cha matatizo mengi yayotukabili watz (porojo).
Tukirudi kwenye suala la kinaendelea nini ndani ya CCM, naona ni vugu vugu tu ambalo hawakuwa wamelizoea na kama watanzania wengi tungekuwa na elimu kidogo ya kujitambua huu ungekuwa wakati muafaka wa kufanya mabadiriko, chama hiki sioni kinatupeleka wapi, imefika wakati tukaruhusu mgombea binafsi, natuombee huyo mgombea binafsi ashinde na achague mawaziri kutoka vyama mbali mbali kwa njia hiyo tu tutasonga mbele na kufikia tunakotaka.
Hasa kwa kuwa kila atakayechaguliwa atafanya kazi kwa manufaa ya nchi na akiboronga atafukuzwa pia, sio kulindana kama kunakofanyika sasa ndani ya CCM.
Mh Sita kwa kiasi kikubwa yupo sahihi, lakini kama mwanasiasa msafi alipaswa kuliona hili tangu awali na angeachia ujumbe wake wa NEC mapema.
MNAOIPINGA CCM MNA LENU JAMBO KWANI MKUTANO MKUU WA CCM HUKO DODOMA KWA KAULI MOJA ULIAMUA KUTETEA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO,KWANI MASUALA YOTE YALIYOKUWA YANAYUMBISHA NCHI MFANO MAHAKAMA YA KADHI NA WARAKA WA KANISA TAYARI CCM IMEYAWEKA WAZI,SISI WANTAZANIA TULIOKO UGHAIBUNI TUNAIUNGA MKONO KWA ASILIMIA MIA MOJA KWANI CCM NDIO CHAMA PEKEE KISICHO NA UDINI WALA UKABILA,TUTAENDELEA KUFUNGUA MATAWI ZAIDI YA CCM HUKU ULAYA NA USA,MUNGU IBARIKI TZ
ReplyDeleteMakamba, Chiligati na wengine vikaragosi wa ufisadi... watu wanawalia timing mnatuchosha. Kama hamkujirekebisha mtaishia kubaya. Wananchi wataamua kutumia haki yao kuwaweka pembeni kisiasa.
ReplyDeleteGAZETI LA HABARILEO MBONA MNAMWANDIKA SITA VIBAYA HIVYO. JE KAWAKOSEA NINI? NIONAVYO MIMI WAANDISHI WA GAZETI HILI WAPEPEWA RUSHWA KWANI NIKIANGALIA WANAVYOMWANDIKA SPIKA SITA INAONEKANA WAZI NA WAO WAMEANZA VITA YA KUMWANGAMIZA. PLEASE HABARI LEO NI GAZETI LA SERIKALI NA SIYO LA CHAMA CHA KISIASA. ANDIKENI HABARI ZA UKWELI NA SIO CHOKOCHOKO.
ReplyDeleteJamani hawa CCM wanatushangaza wengi mwaka 2005 hawahawa wakina MAKAMBA na kampuni yao ya kupiga domo walikuwa wakijinadi kutuletea spika bora mwenye kiwango tena wakimkandia kisawasawa the then speaker mzee wetu PIUS MSEKWA. Sasa leo kafanya kweli nakusimamia kazi yake kwa mujibu wa katiba na sheria za bunge, anaonekana mbaya. Mimi nafikiri huu ndiyo mwisho wa CCM. Mzee wangu MAKAMBA amekosa staha mbele ya jamii ya watanzania inayoanza kuamka kwa kasi zaidi. Hivi majuzi nimeshangaa wapiga kura tunafuatwa majumbani kwetu na kuhaidiwa nauli pamoja na pesa kidogo ili tukachague wagombea wa CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Hivi ndiyo vitu amabavyo makamba anatakiwa aviseme mbele ya watanzania na sio kumkandamiza sita. they should know that speaker ana act as a referee anayesimamia chombo ambacho kina supervisor role over the goverment. So kama serekali yenyewe ni legelege afanye nini sasa? Amejaribu sana kuwabeba mpaka akamfungia Mheshimiwa ZITO lakin kiuhalisia CCM now hawabebeki. Chama kinahitaji kijisacrifice kwa kuwaondoa mafisadi wa aina ya kina Makamba na wenziwe wanaokumbatia matajiri na mafisadi.
ReplyDeleteWEWE UNAESEMA ULAYA MNAIFAGILIA CCM UKOME KAMA ULIVYOKOMA KWENYE ZIWA LA MAMAAKO ULAYA TULIO WENGI TUNAICHUKIA CCM
ReplyDeleteSpika Sitta yupo sahihi kabisa kwani kama mtoto wako ni mwizi ni sharti umkanye la sivyo kuna siku atachomwa moto.
ReplyDeleteNawashauri watu wote safi ndani ya CCM kama akina Sitta,Mwakiyembe Anna Malecela na wengine kukihama chama hicho na kuunda chama kipya cha siasa cha upinzani kilicho na nguvu nina uhakika mkifanya hivyo CCM itaanguka.
Makamba na Kingunge wote hao ni MAFISADI kwani umeona pale Ubungo bus terminal na makamba na issue ya viwanja vya Tanganyika Parkers vyote hivi ni dalili ya ufisadi sasa unategemea wawe against mafisadi?
MHN SITTA NI MBUNGE WA IRAMBO NA PIA NI SPEAKER WA BUNGE!!!:::??? MKE WAKE NI WAZIRI ; no wonders P.
ReplyDeleteKwani Sitta ni spika wa bunge la Tanzania au la CCM? Kama la Tanzania basi hakukosea. Labda hilo swali tungemuuliza makamba na wenzie tujue kama kaapisha kama spika la bunge la Tanzania au la CCM.
ReplyDeleteMimi nafikiri hawa wote akina Sitta, Makamba na akina Tambwe wote wana matatizo. Sitta alifanya vile bungen ili kulinda maslahi yake binafsi ili serikali imuogope. Makamba naye anaona chama kinaelekea kubaya yeye akiwa Mtendaji mkuu kwa hiyo anajaribu kukinusuru kwa njia yeyote.Siasa itatuua jamani.
ReplyDeletendio huku ulaya kila nchi tumefungua matawi ya ccm na RAIS KIKWETE analifahamu hili vizuri ingawa mnatupakazia eti sisi ni watoto wa mafisadi acheni hizo bwana wabongo ndio maana hatuendelei hata kidogo WATANZANIA TUNATAKA CHAMA KINACHOTETEA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BILA KUBAGUANA EBO hivyo vyama vingine mnavyosema vya upinzani sio kweli kabisa kimoja ni cha KIDINI NA KINGINE NI CHA KIKABILA kidumu chama cha mapinduzi na kiendelee kutawala hadi wabongo wapate akili nzuri
ReplyDeleteCCM IKO SAHIHI KABISA KAMA CHAMA TAWALA HATUWEZI KUACHA NCHI KILA MBUNGE ANAJIONGELEA ANAVYOTAKA HIYO ITAKUWA SIO NCHI TENA BALI NI VURUGU TUPU TUIGE MFANO WA CHINA MKUTANO MKUU WA CHAMA UKIAMUA KITU BASI KINAFUATA NI UTEKELEZAJI TU SIO LONGO LONGO KAMA AMBAZO ZINAZUKA SASA HAPO TZ YAANI MBUNGE ANATOKA NA MANENO YA MTAANI AU KWINGINEKO HALAFU ANAENDA KUULIZA BUNGENI TUNATAKA NCHI YA NIDHAMU,HONGERA JAKAYA KIKWETE KWA MSIMAMO WAKO ULIOUNYESHA KWENYE NEC SISI TUPO NYUMA YAKO,GOD BLESS TANZANIA TUENDELEE KUISHI KWA AMANI NA UTULIVU
ReplyDeleteMheshimiwa Sitta kama ana nia nzuri ya nchi na wananchi wake ajitoe ajiunge na vyama vingine ama anzishe chama chake kwa maslahi ya umma.
ReplyDeleteKama ni mitamaa ya madaraka na ubinafsi atang'ang'nia. Chama kizima kuanzia A mpaka Z ni mafisadi na wabinafsi si Sitta tu.
Kuna mtu anaitwa Said Yakubu. Watu wajihadhari nae ana chemchem za ufisadi na kinafiki.
Haka ni kamchezo tu, safari yetu bado ni ndefu, leo litaonekana la Sitta, ndiyo jambo, kesho litaonekana lingine. Na CCM itaendelea kudumu. Watanzania tuamue moja, tuanzishe chama chenye upinzani wa kweli. Upinzani uliopo hivi sasa ni wa kibabaishaji sana, kila mtu anaangalia maslahi yake. Kwa hiyo kusema CCM haifai, bado haisaidii kama hatujapata akili ya kuwa na chama cha upinzani cha kweli. Kilichobaki tujipange, ili tujitawale wenyewe. Uhuru wa Tanzania bado haujapatikana, ndiyo kwanza watanzania tumeanza harakati za kutafuta uhuru wetu. Tulipata uhuru kutoka kwa mkoloni, na sasa tunahitaji uhuru kutoka kwenye tabaka la watawala kwenda kwa wananchi, watanzania. Na hapa ipo kazi, kunahitajika busara na umakini mkubwa sana. Safari ya kufikia huko inaweza kuchukua muda, kama watanzania wengi hawatakubali kubadilika au wataendelea kukubali kudanganywa na vijisenti ambavyo yumkini vimepokonywa kutoka mifukoni mwao
ReplyDeletemimi nasikitishwa sana na watanzania wanaoipinga sana ccm hasa katika suala la spika wa bunge samuel sitta mbona mimi sioni kosa la ccm,je ccm wamefanya kosa gani yaani kumkemea sita ni kosa?halafu kuna watanzania mnaishi nje ya nchi ninyi baadhi yenu hamuitaki kabisa ccm je mmesahau kuwa huko mliko ccm ndio iliyowalea?na wengi wengi mlikwenda huko kusoma kisha mkazamia huko,ila nashukuru kuwa hampigi kura tunaopiga kura siye tuliopo huku bongo na ndio tunaipenda ccm,sita tumemuonya tu asiache bunge kuwa kama club ok
ReplyDelete