mkuu wa polisi mkoa wa dodoma kamanda Zeiloti Stephen, akizungumza na wana habari na kuonesha silaha zilizokutwa na majambazi sita waliouwawa na wanachi wakishirikianana polisi saa kumi na moja alfajiri ya leo katika barabarab ya Dodoma - Iringa wakitokea Mtera kati ya Mlima wa Fufu na Mlodaa wilaya ya Chamwino , ambapo majambazi hao waliweka mawe njiani na kuliteka basi la King Cross likitokea Iringa kuja dodoma na Gari Ndogo mbili na kuwapora vitu mbali mbali vya abiria hao na hao wenye gari ndogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Safi sana ni hatua nzuri sana kwa wananchi kusaidia kuua majambazi na sio kuwakamata. Mimi binafsi sipendi kumkamata jambazi napenda kumuua hapohapo lazima adabu iwepo. Nadhani umefika wakati muafaka wananchi kutolaumiwa kwa kujichukulia sheria mkononi hasa linapofika suala la majambazi, kisitokee chombo chochote cha serikali kulaumu wananchi kujichukulia hatua mikononi kwani tukiwapeleka polisi uchunguzi huwa unachukua miaka hata 20 wakati mtu kakamatwa live!na pengine mwishoni anatolewa.

    Wananchi shime jambazi akikamatwa ni wa kuua tu, sioni jambo jingine zaidi ya kuyaondoa maisha anayoyatumia kuumiza wengine. wakipelekwa polisi wanatoka, sasa kilichobaki ni hicho.
    Mdau HSL

    Kama inafaa Michuzi nawasilisha.

    ReplyDelete
  2. Thank you wananchi wa dodoma na polisi, This is what im talking about! Niliposti koment kwenye habari ya ndugu owino kwamba wananchi its about time tutetee maisha yetu wenyewe toka kwa haya majambazi. Nilisema kina baba ndani ya mabasi mnaposafiri bebeni visu na mapanga madogo vilevile kina mama bebeni pilipili na mchanga, hivo vitu vidogo vinaweza kuwa ndo tofauti pekee kati ya uhai na uzima wako, pia nilishauri kabla basi halijaondoka abiria watangaziwe kwa utulivu (mfano kama wanavofanya kwenye ndege) wakishakuwa wamekaa tayari kwa safari kwamba ikitokea wamefikwa na janga hilo wajitetee vipi, kwani inasikitisha kuona majambazi 6 au hata kama ni 10 wanaua na kupora basi lenye watu 60 hivi hivi bila watu kujaribu kujitetea kwa namna yoyote ile! Tujenge mentality ya amazako ama zangu, sababu tunajua hamna namna nyingine yoyote! Thats the only way to deal with these brutal killers!
    Hongereni sana tena, na Mungu awalinde kwa ujasiri wenu huo! Amen.
    Mdau,New York NY

    ReplyDelete
  3. Sasa ni kuwaponda vichwa tu. Mahakama zinawaachia km Zombe na wenzie. Tungewaponda vichwa akina Zombe mwaka 2006, leo tungekuwa tumekwisha wasahau kabisa.

    ReplyDelete
  4. ila bado vibaka wa uwanja wa Ndege wa JNIA-julius Nyerere International Airport wanaoiba kwenye mabegi ya watu nina usongo nao. na TRA wanaoweka tax ya juu na tathimini ya juu ya viwango halisi ya bidhaa na kusingizia Invoice kuwa ni feki. nina usongo nao bado hawajaingia kwenye 18 zangu ama zao au ama zangu.
    mdau asiyependa wizi.

    ReplyDelete
  5. Tukiungana hivi majambazi yatatukoma mbona!

    ReplyDelete
  6. Police mnatakiwa kuwa na technic za kuwakamata wahalifu na wala siyo kuwaua kwani kufanya hivyo kwanza mnapoteza chance ya kuwakamata BIG FISH,blv me hao mnaowakamata na kuwaua ni just SMALL FISHES, YOU WILL NEVER STOP THE CRIME BY KILLING THEM.
    U need to get more training and more TACTICS ON HOW TO GET THEM A LIVE,WHO STATED TO SHOOTS?IS IT POLICE? OR THE CRIMINALS?
    OFFICERS U HAVE TO BE SMART ON DOING YA JOB, CUT THE ROOTS NOT LEAVES. U CANNOT KEEP KILLING PEOPLE, YOUR OWN PEOPLE, IS AGAINST THE HUMAN RIGHTS
    BE SMART, WORK SMART AND THINK SMART.
    UPENDO UKO WAPI?
    mungu ibariki globu ya jamii
    mpe maisha manene MDAU NO:1

    ReplyDelete
  7. Nasi sote tujiangalie vizuri katika matendo yetu ya kila siku kama kweli nasi hatustahili kuhukumiwa kama hayo majambazi ya Idodomiya!

    ReplyDelete
  8. Tukimalizana na majambazi tuanze na mafisadi....Ping ping ping

    ReplyDelete
  9. ewe mdau wa new york umenichekesha sana haki ya nani kweli una mbinu kali duh! saafi saana huko dododma akuanzaye mmalize full stop
    mdau canada

    ReplyDelete
  10. Gonga majambazi shaba za kichwa kila kona mnapoyaona alafu kwa wale ndugu zetu wa mikoani nawapa taarifa njema

    mimi na kikosi changu tumeamua kufanya safari ya kuja huko ili tupite kwenye yale maeneo ya majambazi

    wale wanaosimamisha magari na kuanza kupiga mapanga tumejiandaa kuja kupiga shaba kama kwenye cinema kwani tunataka kuwakomboa ndugu zetu wa mikoa ya mbali

    baada ya jitihada za wananchi kupambana na majambazi jambo ambalo polisi wamelishindwa na sio kulishindwa ni wakubwa wao waliojaa ufisadi wanashindwa kufatilia suala hilo


    na tukimalizia kwa majambazi tunarudi eapoti ya uwanja wa ndege tunawategea vitu fulani alafu tukiwapata hatuwafikishi mahakamani tunawagonga shaba za kichwa


    tukimaliza eapoti ya uwanja wa ndege tunahamia kwa mafisadi wakubwa tunawateka na kuwamwaga mavi kwa kuwapiga shaba za vichwa

    bila hayo ndugu wananchi serikali yetu haina uwezo wa kupambana na matukio kama hayo kwani viongozi wetu wanaogopana wenyewe kwa wenyewe

    mwananchi wacha kulala wakati wa kulala kushnehi iliyobaki ni kujitolea ili kuweka nchi yetu maisha ya amani na sio amani hiyo inayotangaziwa kila siku

    mungu ibariki nchi yangu tanzania wabariki na watu wake komesha ufisadi na uzembe wa viongozi hewa na wakifika kwako hao viongozi hema ewe mungu wahukumu vibaya sana. mdau uholanzi

    ReplyDelete
  11. Mdau Sun Aug 23, 04:46:00, nakuunga mkono.

    Kuuwa majambazi kila kukicha hakusaidii kupunguza ujambazi.

    Kumaliza ujambazi ni kupata intelligence info toka kwa majambazi kwa kujaribu kuwakamata wakiwa hai.

    Halafu Polisi itapata taarifa kuhusu miundo, wafadhili,masoko n.k ya ujambazi. hiyo itapelekea kungoa 'mzizi' wa ujambazi na itachukua muda ' ujambazi kukua ' tena eneo hilo.

    Mtindo wa kuuwa bila kutumia mbinu za kuwakamata hai majambazi umepitwa na wakati.

    Mdau
    Mossad

    ReplyDelete
  12. kusema ukweli hili jambo limenifurahisha sana wadau,coz mwezi wa 4 mwaka huu niliponea chupu chupu kwenye hiyo milima ya nangoro!walipanga mawe barabarani luck gari niliokua nayo ilikua ya 4*4 so nikasave ila gari ya kampuni ya watu wa mawasiliano huku chini iliumia sana.
    ukifika migori wakijua uko mwenyewe kwenye gari wanapigia wenzao walioko chaka!then wanakuteka...sio watu hao
    mdau london

    ReplyDelete
  13. YALEAYALE YA JAMAA WA MAHENGE?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...