Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Anthony Mayala, anatarajiwa kuzikwa leo jimboni humo, wakati waumini wa Kanisa Katoliki jimboni humo na wenzao kote Tanzania wanaendelea kuomboleza kifo cha Askofu huyo aliyeaga dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza, kwa ugonjwa wa moyo.
Katibu Mtendaji wa Idara ya Habari ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Revocatus Makonge, alisema kuwa kikao cha kupanga mazishi hayo kilifanyika jimboni humo na kwamba kikao hicho kiliwashirikisha mapadri na maaskofu kadhaa akiwamo Rais wa TEC, Askofu Yuda-Thadeus Ruwaichi, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, na Askofu wa Jimbo la Tabora, Paul Ruzoka.
Padri Makonge alisema ibada ya misa ya maziko hayo itafanyika katika viwanja vya Kanisa la Kawekamo na kisha katika Kanisa Kuu la Epifania Bugando. Alisema, misa hiyo inatarajiwa kuongozwa na Kardinali Pengo kwa kushirikiana na maaskofu wengine kutoka majimbo ya Kanisa hilo nchini.
Kwa kawaida ya Kanisa hilo, maaskofu huzikwa ndani ya Kanisa Kuu la Jimbo, hivyo Askofu Mayala atazikwa ndani ya Kanisa la Epifania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mwenyezi Mungu alaze roho yake pema peponi, Apumzike kwa amani.Amen

    ReplyDelete
  2. Brother Mithupu, naomba nikuweke sawa kidogo kwa faida yako na wanablog. Kanisa Kuu la Epifania Bugando haliko katika viwanja vya Kawekamo. Katika viwanja hivyo kuna kanisa liitwalo Kawekamo pia. Nafikiri hapa umechanganya mambo. Ilivyo ni kwamba, misa/ibada ya mazishi itafanyika katika kanisa la Kawekamo na mazishi yenyewe yatafanyika katika Kanisa Kuu la Epifania Bugando. Yaani baada ya misa ya mazishi mwili wa marehemu utapelekwa kuzikwa ndani ya kanisa la Bugando. Kitu kingine hatusemi au kuandika Epfania ila Epifania.

    Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi-Amina.

    ReplyDelete
  3. jamani nawapa pole wanakatoliki wote na watanzania kwa ujumla.mungu aiweke roho ya marehemu pema peponi.amina

    ReplyDelete
  4. RAHA YA MILELE UUMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI, AMINA. ROHO ZA WAUMINI MAREHEMU WOTE WAPATE REHEMA KWA MUNGU WAPUMZIKE KWA AMANI AMINA. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

    Muumini - Beijing.

    ReplyDelete
  5. R.I.P Askofu Mayala,nakumbuka ulinipa kipaimara pale Nyegezi Parish mwaka 1993 ukiwa pamoja na balozi wa Vatican Augustiono M. Mungu akupumzishe kwa amani Amen.

    ReplyDelete
  6. Askofu Mayala kweli alikuwa mtu mwema sana. Aliwapenda watu wote. Daima hakujikweza. Alikuwa mfano halisi wa kuishi injili. Ka-sigara alipenda pia kukapuliza. Mungu akupokee kwake.

    ReplyDelete
  7. MwanaMaombiAugust 26, 2009

    We Misupu kwa Wakristu ni waAmini na sio waUmini.

    WaUmini ni waislamu.

    ReplyDelete
  8. Mwanamaombi, inawezekana wewe si mkatoliki. Wakatoliki tunatumia WAUMINI na si WAAMINI. Mayalla alikuwa mkatoliki, hivyo bro Mithupu yuko sawa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...