bofya mshale kuona video hii

mkurugenzi wa vitambulisho vya uraia zenji akiongelea matatizo yanayotokea visiwani hususan katika swala la dftari la kudumu wapiga kura na vitambulisho vya makazi katika kongamano iliyoandaliwa na CUF karibuni kuzungumzia matataizo hayo jijini dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Jamaa hotuba yake inaonekana defensive sana, lawama zimekuwa nyiiingi, Mkumbusheni kwamba anaongea na THE MOST POPULAR POLITICIANS IN THE WORLD,
    Ndugu mkurugenzi jaribu kuwa more POSITIVE, Refrain from complaining too much, avoid repeating sentences, Dont be and dont look aggressive. Stay calm during the speech and look people in the eyes when you r talking to them.
    Just free advice.
    Milele globu ya jamii
    Milele mdau no:1

    ReplyDelete
  2. DAFTARI LA WAPIGA KURA DU
    Kweli hatuna mipango ya kujikwamua kiuchumi ni kufikiria tu kuiba na kuhofu kuibiwa kura. Si unajua mwizi hawezi kumuamini mwenziwe.
    tunapoteza muda mwingi na mambo haya hebu tufikiria ya maendeleo ya nchi si kutegana tegana na kuhofu kuibiana
    Mchambuzi

    ReplyDelete
  3. Mzanzibar 100%August 24, 2009

    Aah wallah mie nimenyimwa mke Pemba, sheha kanizuia kuowa kabisaa eti sina kitambulisho cha ukazi wa zanzibar (ZAN ID)!Sasa ikiwa mpaka kuowana tuwe na vitambulisho vya ukazi, basi huenda hata wengine tusiruhusiwe KUFA zanzibar sababu hatuna vitambulisho vya ukazi! Yaani tunaendeshwa kama nchi ya mfalme juha...!
    Haya basi nke shakosa na ftari nala magengeni, ntakwenda owa Tanga mfungo mosi inshaallah mie sharti mke atoke mwambao wa pwani,nshazoea JODARI na TASI siwawezi SANGARA na SATO wa bara!

    ReplyDelete
  4. Haki ya Mungu!! Duuh!? Huyu jamaa anataka kusema kwamba Zanzibar inaweza kuibeat Afrika ya Kusini kwa population registration system waliyoirithi toka kwa kaburu na passbook law? Au Mkenya na 'kipande yake' aliyoirithi toka kwa Muingereza?

    Halafu kabla kamera haijatembea nilifikiri anaongea na Pro Lipumba tu kumbe alikuwa anawalecture hadi kina Dr Salim, Judge Warioba, Maalim Seif na waheshimiwa wengine kadha wa kadha. Anayetulinda Mungu wallahi hawa kina Athumani wetu wote wagonjwa wazimu.

    ReplyDelete
  5. Huu ndiyo upuuzi wa watendaji wetu kukubali kuwa watumwa wa wanasiasa ili walinde masilahi yao. Huwezi hata siku moja kuongea kwenye seminar yenye watu wenye vichwa na wanaojua nini maana ya haki, kuongea kama unasuta watu na kukaripia. Huyu anachotaka kuonesha ni kuwa yeye yupo huru na anajigamba kuwa si mwanasiasa wakati analeta propaganda zile zile za kudivide and rule za kila mwaka.

    Nchi kama Zanzibar yenye wakazi wasiozidi hata robo ya Dar es Salaam, kuna na matatizo kama hayo?. Huu ni upuuzi na ukiritimba. Mkurugenzi inaonekana kuwa ni kada mzuri wa siasa za chama kilichompatia kazi hiyo. Shame on us Africa! LOL!

    ReplyDelete
  6. Jamaa anaongea na "authority" ya ajabu.Duh!Mtu kama huyu ofisini lazima atakua mtemi kwelikweli.Huwezi kutumia mabavu namna hiyo kwenye kuongea,hasa unapoongelea maswala ya msingi kama hayo.

    Mungu Ibariki Tanzania!

    mdau.

    ReplyDelete
  7. Mwanzoni, nilikuwa nashanga pia jamaa anavyoongea kwa jazba lakini mwishoni aliposema kuwa walikaa naviongozi wote wa siasa wakakubaliana utaratibu na pia walikuwa wanachekeana ccm na cuf, lakini walipoeanda kwenye majukwa yao wakapeleka ujumbe tofauti na kusababisha jazba kwa wafuasi wao mpaka kupelekea huyo sheha kumwagiwa acid, kweli hata mimi ningeongea kwa hasira hivyo hivyo! viongozi wetu inabidi wawe.responsible, na waelewa nguvu ya maneno na athari zake katika jamii!! its not a game!!

    ReplyDelete
  8. Jamaa anaongea mambo ya msingi....wana siasa waache kupotosha wananchi....ameongea kitu cha msingi sana...ELIMU...ni tatizo kubwa sana kwenye hizi nchi zetu.........

    ReplyDelete
  9. Ni kweli kwamba jamaa anaongea mambo muhimu lakini jinsi anavyo present hayo mambo muhimu is COMPLETELY WRONG.
    Guys you dont talk with high level politicians like Dr salim Ahmed Salimu,Josef Sinde warioba,Shehe Sharifu Hamad and Profesa Lipumba kwa hasira namna ile with ya hands!!! that is disrespectful,
    These r the people who can help you to find the solution of whatever the matter facing the country... this MKURUGENZI NEEDS TO LEARN "COMMUNICATION SKILLS"
    thanx.

    ReplyDelete
  10. Mzee Nanihii,

    Nimevutika sana na hii issue. Sijui kama kuna uwezekano wa kusikia na upande wa hao wanaolalamika tukaweza kujua hoja zao na wanahisi tatizo ni nini.

    ReplyDelete
  11. Tatizo la kurukia kutoa maoni bila ya kuwa na the whole picture ndio hilo la kuishia kutoa hukumu isiyo sahihi. Hasira za huyu jamaa kwanza zinatokana na waraka uliondikwa kwa pamoja na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi ambao umejaa upotoshaji, uongo na shutuma zisizo na msingi ambao ulisomwa na yeye kutakiwa kurespond. Pili alikisarishwa na jinsi Media wanavyokumbatia uongo huo bila ya hata kutaka kuthibitisha au kubalance stories zao hueneza upotofu huo kwa jamii, tatu jinsi upotoshaji huo unavyosababisha athari kubwa huko Pemba kiasi cha watu kuchomewa nyumba na kumwagiwa tindikali za macho bila ya sababu za msingi. Viongozi hao hawastahiki kuheshimiwa hata chembe. Ni vizuri huyu jamaa amewaonesha ni wapumbavu kiasi gani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...