bofya mshale uone video hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. hehehehe..yaani, jamaa kamvisha kanzu na kibarakashia, akamvua..akabadili mawazo; akaamua kumvisha tena. na mpambe wake akavishwa, pia.

    cafu alikuwa noma.

    ReplyDelete
  2. ...dah, ananikumbusha mambo ya Ramadhan Chombo " Redondo"

    ReplyDelete
  3. Hii kitu ukiiona hata kama unatoka kufukuzwa kazi au kutaliki utacheka tu.

    ReplyDelete
  4. Duh haya ndio yalikuwa mambo ya Ali Maumba wa Coastal Union kipindi kile, sijui jamaa yuko wapi siku hizi na anafanya nini, mdau mwenye data plzzz !!

    ReplyDelete
  5. Hapo unaambiwa huyo ni fulubeki. Hujakutana na viungo waliotokea Brazil ...Ronaldinho anayetuliza krosi kwa mgongo huku akitoka mbio, Robinho anayeurukaruka mpira mpaka beki anaanguka kwa kizunguzungu, Kaka (kunradhi wadau wa Man U, najua mnakumbuka alivyoacha mabeki wenu wanagongana wakati anaenda kumsalimia kipa wenu) anayekimbia kama anateleza uwanjani. Yaani kama Hussein Marsha vile.

    ReplyDelete
  6. Anony wa 04.26 umenikumbusha mbali sana kuhusu Ally Maumba kwani hata uchezaji wa Nwako Kanu nilikuwa naufananisha sana na wa Ally Maumba hata Team kongwe ya Simba walimtafuta sana ili ajiunge na team yao lakini ilishindikana masikini sijui hata mpira wake uliishia wapi jamani!

    Muddy

    ReplyDelete
  7. Mdau umenikumbusha mambo ya Marsha...nakumbuka alikuwa anacheza dakika tisini kwenye mvua bila kuchafuka.Kanzu alizokuwa anapiga si mchezo.....nakumbuka George weah alipigwa kanzu na marsha taifa,hakuamini...Marsha yu wapi waheshimiwa.....

    ReplyDelete
  8. Michael Paul 'lailoni'

    ReplyDelete
  9. Mdau uliyeuliza MASHA ako wapi. MASHA ako UK ila sijui anafanya nini kwa sasa.
    Mdau-UKEREWE

    ReplyDelete
  10. inaonekana mimi mmenisahau!!! hamkumbuki mambo yangu nyie vijana wa siku hizi???
    Ni mimi
    Athuman China.

    ReplyDelete
  11. Ni nylon sio "lailoni"asante

    ReplyDelete
  12. wewe china ukumbukwe umefanya nini? siku hizi unazuiwa na watoto wadoogo hufurukuti mara unarusha ngumi.

    ReplyDelete
  13. Imeshiptwa na wakati hii ina vumbi na watu tumeshafanya zaidi ya hio.

    ReplyDelete
  14. Alafu kumbe huyo aliyevalishwa kanzu mbili pamoja na mkanda kumbe ni Nedved, alafu mwaka huo huo akawa mchezaji bora Ulaya, wazungu bwana...

    mdau,
    Ashkmatit

    ReplyDelete
  15. Wadau mbona mimi Zamoyoni Mogella (golden boy) hamnikumbuki?

    ReplyDelete
  16. Huyo aliyevishwa kanzu ni Nedved kweli na huyo mshikaji wake wa pili kuvaa darizi si mwingine ni yule mu argentina ambaye Beckham hawezi msahau, Diego Simeone, game ilikuwa Roma na Lazio wakati huo..wapinzani wa jadi wa jiji la Roma ambapo kuna wajomba wengine walishangazwa na vijana wa Guardiola...

    ReplyDelete
  17. - mtaaluma huwezi hata kujua 'anapigia' mguu gani!..

    ReplyDelete
  18. Jamani Wadau, Hivi Mnamkumbuka Marehemu Hamisi Gaga Gagarino, yule jamaa alikuwa Hatari, Hakuna Kiungo kama yule aliyepata kutokea Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...