BAN KI –MOON AFUNGUA KONGAMANO LA MAZINGIRA
Dunia inaweza kukabiliana na Matatizo yanayoikumba kama vile umaskini katika nchi zinazoendelea, njaa na magonjwa bila kuharibu Mazingira
Hayo yameelezwa leo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon wakati akifungua kongamano la kimataifa la mazingira Nchini Korea ya Kusini.
Bwana Moon ameeleza kuwa uharibifu wa mazingira unapelekea Upungufu wa Maji ambao unaathiri idadi kubwa ya watu na kuleta madhara ya magonjwa kama vile utapiamlo.
Pamoja na kuipongeza Korea ya Kusini kwa kuwa Mfano bora kwa utunzaji wa mazingira, ameiasa pia kuongeza jitihada zaidi katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.
Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, aliongea kwa kusema kuwa nguvu za pamoja zinahitajika kutoka katika sekta zote za jamii, ili kukabiliana na suala zima la uharibifu wa Mazingira.
“Nitaalika Viongozi wote wa Dunia ili kujadili tatizo la Mbadiliko ya Tabia Nchi.” Alisema.
Bwana Moon alisisitiza kuwa , Nchi zinazoendelea ni lazima ziwe na mipango na matendo ambayo ni lazima yapimike na kuripotiwa ili kufikia malengo ya kukabiliana na suala zima la uharibifu wa Mazingira.
Kongamano hilo la siki mbili la Mazingira litajadili pia suala la sera mchanganyiko zitakazoweza kutumika kushughulikia suala zima la matumizi ya Nishati na usimamizi wa mazingira kwa ujumla.
Kongamano hilo linahururiwa na wataalam mbali mbali wa masuala ya mazingira na Mawaziri wa Mazingira kutoka nchi mbali mbali Duniani ikiwemo Tanzania.
hongera mama kwa kuchapa kazi, nyinyi ndio wanawake tunaowahitaji katika Tanzania tulionayo, sio mafisadi wanaoiangamiza nchi.
ReplyDeletekila la kheri mama.
Wee Anonymous 05:09:00
ReplyDeleteWacha kusema mambo usiyo yajua na kumwaga misifa ispostahili- Angalikuwa ni Waziri MAKINI tena mwenye dhamana ya Mazingira asingesubiri Watanzania na mifugo yao wafe na wengine kuathirika vibaya kule kwenye Mgodi wa Barrick Northern Mara - bado mpaka leo anajikanyaga kuwachukulia hatua wachafuzi hao wa Mazingira. Look "No research No right to speak" Good Day!
tatizo lenu mwosha kinywa unasubiri hatua zichukuliwe kwa mkono, kiongozi hakurupuki tu. busara lazima, hata hivyo utunzaji wa mazingira unaanzia kwa wananchi wenyewe........kua na busara wewe.
ReplyDeleteDADA BATILDA UNANIVUTIA SANA KWA HIJAB YAKO SAFI.UNAPENDEKEZA NA INAKUPENDEZA.
ReplyDelete