jaji mkuu wa miss tz dk. ramesh sha akitangaza kumi bora
mshiriki namba nne margareth peter azirai baada ya kukosa nafasi katika 10 bora
mabaunsa wamwondoa mrembo aliezirai jukwaani. wakati tunaenda hewani mrembo huyo alikuwa ameshazinduka na hali yake inaendelea vyema. wataalamu wanasema hiyo huenda ilikuwa ni mfadhiko.
Aidha redds miss ilala bado hajatangazwa wakati huu ambao ni saa saba na dakika kama 40 za asubuhi, na miss redds-michuziblog pia atatajwa mara tu malkia atapotangazwa




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. athumani issaAugust 08, 2009

    michuzi unatudanganya sana na wewe au una wenge nini saa saba imekuwa asubuhi sema saa saba usiku bwana.

    ReplyDelete
  2. mhhh! Huyu nayee atupishe hapa. Ina maana alijua atashinda ama? Ovyoooooo eti kaenda kujilaza hana haya au ndio akumbukwe? Wizi Mtupuuu

    ReplyDelete
  3. heheheh alizani atashinda masikini halafu duuh hata kumi boraa wamemwaga ,hahahah

    ReplyDelete
  4. masikini mfadhaiko tu, wamemuahisi atashinda kumbe ata kumi bora kakosa dahhh

    ReplyDelete
  5. pole sana dada. hayo ndio mambo ya kutaka uzuri. sisi wasichana tuna tabia ya kujinyima chakula kwa muda mrefu ili tuwe wembamba, lakini matokeo yake mara nyingi ndio hayo. pole sana dada. kula chakula hata kama ni kidogo ili upate nguvu. kula chakula, tumia vitamins na fanya mazoezi hauta nenepa.

    ReplyDelete
  6. Pole sana dada, lakini usije ukaona na njaa nayo imechangia, presha ya kukumbuka upi mguu unatangulia kutembea kushoto au kulia,kulia au kushoto, halafu baada ya vyote hivyo halafu unaambiwa humo katika kumi bora.

    Kutokuwa katika kumi bora sio inamaana wewe sio mzuri,

    Ukileta majaji wengine, unaweza ukaona wamekuweka katika tano bora.

    Mara nyingi kumbuka ya kwamba kila mtu ana mtazamo tofauti katika vitu. Mwengine anasema kitu hii safi kabisa anakipenda wakati mwengine anasema mimi hii sawa na sifuri sipendi sipendi kabisa.


    ni hayo tu.

    P.E.D

    ReplyDelete
  7. high expectation from nowhere,wewe kula unenepe matako that is african woman hutofautiani na wale waimbaji waliletwa na rose walifikiri ya kwamba marekani ndiyo mbinguni sasa yako wapi wanatangatanga ovyo

    ReplyDelete
  8. Alichezesha kete vizuri na alikua na uhakika, sasa mambo yalivyoenda ndivyo sivyo akuamini macho yake, masikini mtoto wa watu!!

    ReplyDelete
  9. WALIMU MNAOANDAA HAWA WATOTO PAMOJA
    NA MAMBO MENGINE MENGI MAZURI PIA
    MNAPASWA KUWAANDAA KI-SAIKOLOJIA ILI WAELEWE KUWA KATIKA MASHINDANO
    YA AINA YEYOTE KUNA KUSHINDA NA
    KUSHINDWA.UKISHINDA UTAPONGEZWA NA
    UKISHINDWA WAPONGEZE WASHINDI.DAIMA RESPECT WENZIO WOTE MLIOSHIRIKI
    PAMOJA REGARDLESS OF THE OUTCOMES.
    WALIMU WAPENI HAWA WATOTO MULTI-
    VITAMINS SUPPLIMENTS KWA SABABU
    WANAKULA KIDOGO KUEPUKA MATUMBO
    KUTOKEZA.WAPENI VEGIE-SALAD NA MAJI
    KAMA DINNER MAANA NIMEONA HAPO JUU
    WAKULA WALI, NYAMA NA SODA.SODA NI SUMU.WAPENI JUICE NA MATUNDA FRESH.
    TOTO TUNDU-UPPER MARLBORO.

    ReplyDelete
  10. kweli umaarufu hauji bure baada ya kukosa hata kwenye kumi bora akajiangusha ili akumbukwe hana lolote.

    ReplyDelete
  11. YANI KUNA WATU WENGINE WANAROPOKA TU, HATAKAMA HAJUI KITU HAWEZI KUSEMA HAJUI AKAULIZA, AAA!.. WAO KAZI YAO NI KUKOSOWA TU WATU!!

    SASA HAPO BRO MISUPU KAKOSEA NINI KUSEMA SAA SABA NA DAKIKA 40 ASUBUHI?? WEWE KWELI HUYUI KUSOMA SAA ALAFU UNAMKOSOWA MISUPU, YUPO SAHII KABISA IT WAS (1:40 AM) CMN SHIT GO BACK TO SCHOOL!!

    ReplyDelete
  12. Wizi Mtupu! Huko kudhirai kulikuwa staged. Yup Ramesh ametupa hii nyeti. Ni mambo ya Publicity Stunt.

    ReplyDelete
  13. SABA ASUBUHIAugust 08, 2009

    WEWE BWEGE WA KWANZA HAPO JUU SHULE GANI UMEENDA?NANI KAKWAMBIA SAA SABA NI USIKU?IKISHAFIKA SITA NA WATOTO WAKE INAHESABIKA NI ASUBUHI OK??NEXT TIME SIO UNAMZODOA MICHUZI KABLA YA KUFANYA UCHUNGUZI,NENDA KWANZA KATAFAKARI HIVI VITU 2 PM NA AM,AKSANTENI.

    ReplyDelete
  14. wadau wameshapuliza kidonda halafu top ten umeikosa ni lazima uzime

    ReplyDelete
  15. Jamani kuna watu na viatu na isitoshe wengine tulikimbia hesabu za saa darasa la 4 sasa mnategemea nn

    ReplyDelete
  16. TAFADHALI, NAOMBA TUNAPOKOSOANA
    TUHESHIMIANE. BWANA MICHUZI ALIKOSEA KIDOGO KUHUSU MUDA. WEWE UNAYESEMA IKISHAPITA SAA SITA USIKU NI ASUBUHI, HUO NI UTAMADUNI WA KIZUNGU (A.M). WAZUNGU HAWANA MANENO YANAYOTAFSIRI SAWASAWA NA KISWAHILI ASILIMIA 100. ASUBUHI (MORNING), LAKINI SI KWELI KUWA (A.M) YA USIKU NI ASUBUHI. KISWAHILI TUNA MANENO HAYA:-
    Asubuhi - Mchana - Adhuhuri - Alasiri - Jioni -Usiku - Usiku wa Manane - Alfajiri ......

    UNAYESEMA MICHUZI HAJAKOSEA, USITUMIE JAZBA KAKA. KAMA UNAFUNDISHA KISWAHILI KWA MTINDO HUO, UNAPOTOSHA WATU. NDIO NYIE MTAFUNDISHA KUWA "'BABA MDOGO" ANAITWA PIA MJOMBA, KISA WAZUNGU WANAMWITA "UNCLE".

    Mdau wa Kiswahili Sanifu.

    ReplyDelete
  17. Kusoma tumesoma sana. Na tunaongea vizuri Kiswahili na Kiingereza. Lakini saa 7 usiku ndiyo sahihi katika Kiswahili. Kiswahili si Kiingereza. Saa 7 haiwezi kuwa asubuhi katika Kiswahili. Ni sahihi kusema 7 usiku = 1 o'clock in the morning katika Kiingereza na lugha nyingine za Magharibi km Kifaransa. Siku hizi kuna watu wanasema: "mwisho wa siku = at the end of the day". Haya yote ni makosa ya DIRECT TRANSLATION. Usahihi wa "End of the day" = hatimaye, mwishoe..... Kwa Kiswahili "Mwisho wa siku = Jioni". Iko mifano mingi ya upotoshaji hususani katika vyombo vya habari na redio za "ma-check bob". Tusiharibu lugha yetu kwa ulimbukeni wa Kiingereza.

    ReplyDelete
  18. Darasa zuri sana la kiswahili nimelipata hapa.Ahsanteni sana kwa kumkosoa huyo mtu hapo juu aliefanya direct translation.Kiswahili ni kiswahili na kingereza ni kingereza,acha kufanya direct translation.

    ReplyDelete
  19. Watu wamekula shobo na kukuhakikishia kuwa utashinda, halafu top 10 hata haupo. Lazima Uzirai!!LOL

    ReplyDelete
  20. ALIPOANGUKA TU IKASEMEKANA NI KWA SABABU YA KUKOSA KWENYE KUMI BORA, JE ALIPATA NAFASI YA KUMWAMBIA NANI? TUPUNGUZE UZUSHI JAMANI! hUYO NI UCHOVU (TENSION) LABDA NA NJAA!
    GJK

    ReplyDelete
  21. Next time guys think kabla ya kutema pumba! Much-know. Im out!!!!

    ReplyDelete
  22. Haya mambo naona yanahitaji tuyajadili, tujue tunaenda wapi. Sijui wadau wanasemaje, lakini wiki iliyopita, niliandika kijimakala hiki hapa.

    ReplyDelete
  23. Wizi mtupu Michuzi web site yaku atukuweza ku vote kwaio we all know Silvia was not suppose to win Miss photogenic.....we so are disappointed

    ReplyDelete
  24. @@@@@@@@@@@@ KUNATAKIWA KUWE NA WAHUDUMU WA JINSIA YA KIKE KWENYE TUKIO LA GHAFLA KAMA HILI ANATAKIWA AWEPO MWANAMKE WA KUSAIDIA/KUMHIFADHI HUYO DADA @@@@@@@@@@@@@@@@.

    ReplyDelete
  25. athumani issaAugust 08, 2009

    ahsanteni sana wadau kwa kunisaidia kwa hilo maana kuna watu wengine kujua kiingereza tu imekuwa taabu kwani michuzi hawezi kukosea? anapokosea tunamkosoa au mnasemaje wadau?sio watu mnajaribu kuupindisha ukweli lini umesikia saa saba usiku ikaitwa asubuhi jamani? michuzi we usihofu ulighafilika tu ninaamini hivyo tatizo ni hao wanaojifanya wanajua sana kiingereza. nawashukuruni sana mungu awabariki.

    ReplyDelete
  26. Watu bwanaaa!!! mnajifanya mnajuuuuaa! kawaida kiswahili kizuli mithupu amekosea.hiyo ilikua ni sa saba usiku,,,sa saba usiku,,,nimeandika mala mbili sio mdanganye ulimwengu eti ni asubuhi.Mliona wapi sa saba au sanane usiku unaongea eti asubuhi ???Sio mkalie kukosoaaaana tu.Najua wengi wanaosema hayo ya sa saba asubuhi niwale walio pinda kwenye mabox,,sio mkalie box tuuuu mpaka kiswahili mnakigeuze kiduchi au kichina.allah!!!

    ReplyDelete
  27. Go people.Its about time kuwapasha watu wanaojifanya wanjua kidhungu na kufundisha wasiojua kidhungu kisichoeleweka.

    Kiswahili ni kiswahili na kidhungu ni kidhungu.

    ReplyDelete
  28. Alifadhaika dada yetu

    Wakati mwingine warembo wanajiaminisha mmno kiasi mambo yakienda kombo anashindwa kujizuiaaaaaaaaaaaaaa POLE DADA

    ReplyDelete
  29. Dayati za matufaa na matango kwikwikwikwi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...