anko nanihii akiwa na mdau lusekelo lazalo mwakasege
anayeomba msaada tutani
GLOBU YA JAMII LEO IMEKUTANA NA MDAU LUSEKELO LAZARO MWAKASEGE AMBAYE ANASUMBULIWA NA ULEMAVU WA KUWA NA MIFUPA DHAIFU, AMBAPO MIGUU YAKE HUVUNJIKA KILA IPATAPO MSUKOSUKO KIDOGO. HIVI TUNAVYOONGEA LUSEKELO KESHAVUNJIKA MIGUU MARA 23 KATIKA NYAKATI TOFAUTI TOKA AZALIWE HUKO KIJIJI CHA MPUNGUTI, MWAKALELI, WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA MWAKA 1968.
MADAKTARI WAMEMSHAURI LUSEKELO ATAFUTE CHOMBO CHA USAFIRI ILI AENDELEE NA SHUGHULI ZAKE ZA FUNDI UMEME HAPA JIJINI. PIA ANAOMBA MSAADA WA HALI NA MLI ILI AWEZE KUPATA MTAJI WA KUENDELEZA MAISHA YAKE AMBAYO KWA UMRI ALIONAO NA MARADHI INAMPATA SHIDA SANA KUMUDU.
LUSEKELO ANASEMA YEYE HANA MAKUU, ANAOMBA MSAADA WA FEDHA ZA KUMWEZESHA KUPATA KIBAJAJI AMBACHO PAMOJA NA USAFIRI WAKE YEYE BINAFSI PIA ANAWEZA KUFANYIA BIASHARA. BAJAJI MOJA SIKU HIZI NI TAKRIBAN SHILINGI MILIONI 5 ZA KITANZANIA.
ANASEMA NAMBA YAKE YA SIMU YA MKONONI NI +255 713 195 974 NA NAMBA YA AKAUNTI KATIKA BENKI YA
AKIBA COMMERCIAL BANK NI
ACC NO. ACB 020803951027
unaweza pia kuandika nini unachoweza
kumsaidi kupitia email ya globu ya jamii ambayo ni
Bro Mithupu unapenda uchokozi wewe!!! yani maaaakusudi kabisa teh teh teh. haya bwana subiri comments za wadau!!! mh kwa hiyo na wewe hapo leo umeonekana hasheeeem mwenyewe. ha ha ha na wewe leo michuzi TOLU!!! nadhani memphis gizzles wamekuona mwanangu NBA draft ya mwakani usikose kutupia ka-jina kako Tolu michuzi
ReplyDeleteWewe michuzi ukiwa wa kwanza kukutana na ombi hili kabla ya kulileta kwetu, umesha-pledge chochote lakini??. Pledge mtaalam na sisi tuko nyuma yako tunafuatia, michango kidogokidogo hatimaye hiyo M5 itatimia tu inshalah, matatizo haya ni ya kila mtu na huweza kumkuta yeyote kama si wewe basi mwanao. kutoa ni moyo usambe si utajiri. ahsante kwa taarifa lets see how to go about helping this lad
ReplyDeleteMzee wa Mishupu...mpatie jamaa website hii na awasiliane na wawakilishi hapo TZ na ataweza kusaidiwa: www.kiva.org
ReplyDeleteSASA WEWE MICHUZI MBONA UNAFANYA HII ISSUE IONEKANE NGUMU SIUNAJUA MHESHIMIWA HASHEEM THABEET YUPO NYUMBANI NA WEWE UNAJUA FIKA JINSI YA KUMPATA NA KUONANA NAYE KWA NINI KAMA UNASHIDA HUYU BWANA ASAIDIWE USIONGEE NA THABEET AMPE KIASI KIDOGO? HASHEEM KALIPWA HELA NYINGI SANA HUU MSAADA WA DOLLAH 4000 KWAKE NI KAMA KUTOA SUMNI WAKATI UNASHS MILLION MOJA. TENA USIONE AIBU KUI POST HII COMMENT MWAMBIE HASHEEM AMPE FWEDHA USITUGASI SISI BWANA HATUNA HIZO MIL.5!
ReplyDeleteLABDA TWAWEZA KUBADILISHA HAYA,LAKINI EPA, RICHMOND,TWINTOWER,LOWASSA,CHENGE,LADA TUSIJIDANGANYE.
ReplyDeletemdau lusekelo pole sana kwa matatizo uliyopata ya kuvunjika miguu. pili hongera kwa uamuzi wako wa kuomba msaada kwani ni kheri wewe unae omba kuliko wale wezi waliojaa pale airport na kuibia watu.
ReplyDeletekumbe bora nikuchangie wewe ulieomba kuliko nisubili kuibiwa na vibaka wendawazimu wasio na haya pale airport. kesho nitakupigia simu nikutumie japo kidogo haba na haba----- michuzi malizia
KABWE unajua unapotoa maoni yako usiwasemee watu wengine, coment yako inaonyesha ni mtu mwenye uwezo mdogo sana wa kufikiri ambaye umezoea kutoa michango ya sherehe tu ili upate fursa ya kula na kunywa hebu tambaa zako kule, michuzi please coments za MASENENE kama haya Usizipe nafasi kwenye glob ya watu. unapokuwa hutaki kusaidia kitu usihamasishe na watu wafanye kama wewe, mimi binafsi nitamchangia huyu ndugu.
ReplyDeletemmh mifupa dhaifu kisha anataka kuendesha kibajaji? kwa madereva wa bongo wanaoendesha ovyo si watamtoa roho kabisa? nadhani labda atafuta japo corolla lkn bajaji sio muwafaka kwa uendeshaji wa bongo.
ReplyDeletepole sana mdau na inshaallah utafanikiwa
Hivi huyu bwana Lusekero ana mke na watoo? Wadau huyu mtu niwakusaidia kiukweli,hayo ya Hasheem niyakwake bwana.Tujueni wada mtu kuwa na hela nyiingi sio kuitoa au kusaidia,,kutoa ni moyo wa huruma tu.Mimi nitakurushia hata euro 200,,itakuwa imetosha kwa mimi mpiga box kila siku.
ReplyDeleteWe mtoa maoni wa kwanza unatupa dhambi wenzio kwamba Michuzi alikuwa Thabet ii jamaniii acha uchokozi
ReplyDeleteni multiplescrosis ni ugonjwa wa kuvunjika mifupa ovyo ovyo tu hata ukijikwaa tu, hauna tiba, ajifunze kuishi nao tu. ni wa kawaida sana kwa akina mama wenye umri mkubwa ambao wamemaliza umri wa kusafiri mwezini, hutokana na upungufu wa iron.
ReplyDelete