

Nimekutana na huyu mjamaa
Kioma Siyanga Timu Ngayega
Maputo Mozambique wiki iliopita ni mfanya biashara, yeye anasema baba yake alikua Mtanzania mwanafunzi huko Maputo na alimtelekeza na kurudi Dar baada ya yeye kuzaliwa na kuwa registered huko na baba yake kwa majina hayo.
Anaomba Globu ya Jamii imsaidie kutangaza ilu kumtafuta mzazi wake au familia ya karibu.
Mdau Dar
mdau wa maputo mbona umeacha mambo muhimu kyataja? ilikuwa useme jina la jamaa na la baba yake ili iwe rahisi ketu kama tunamjua kuunganisha. pia mwaka ambao baba yake alikuwa maputo ni muhimu.kutaja tu kuwa mdau wa maputo anamtafuta baba yake haitoshi. toa maelezo zaidi.
ReplyDeleteNAJISIKIA HUZUNI NYINGI NILIPOSOMA HII MESSAGE,
ReplyDeletetabia hii ya wanaume kutokuwa na utu na ubinadamu, baadhi wameuvua ubinadamu sijui niwaite nini ??????
hii imekuwa ni tabia ambayo wanaume wengine huwafanyia wanawake na watoto wao ila akiona ana future (mwelekeo wa kimaisha mzuri hasa!! FINANCIAL ) utamsikia na sii huyu tu kuna wanachuo wengi huingia mitaani na kujiita majina kama economics, surve, save, na mengine mengi, anapomaliza chuo anamwacha mama wa mtaani na mtoto anapokuja chuo basi kuuliza inakuwa kaziiiii kweliiii,
tuwasaidie wakina mama, pia jifikirie je ingekuwa wewe humjui baba au leo hii umesoma unamuuliza mama, baba yangu anaitwa nani na akakujibu economics how do you feel!!! jamani ubinadamu !! huo ni uchungu na simanzi kubwa usipomjua BABABABABA!!
mimi nina Baba na Mama ni watu wazima nami ni mtu zima but najikuta nadeka hata kama hawana pesa.
TUKEMEE TABIA HII
KAKA POLE SANA. I HOPE BABA YAKO HAKUITWA LECTURE ROOM. KARIBU BONGO
Ni vizuri ukiweka majina yake pamoja na ya mama yake. Na hata chuo alichosemea baba yake
ReplyDeletejina au majina?
ReplyDeletesasa huyu jamaa jina lake nani? na baba yake mtafutwa anaitwa nani? alisoma maputo chuo gani?? alirudi bongo mwaka gani? tupe dataz tukupe baba yake....
ReplyDeleteKama mimi ni huyo Baba...nikisoma hapa mtoto wangu amenitoa kwenye Michuzi kuwa "nilitelekeza" naweza nikajikausha kabisa...wala nisijulikane.
ReplyDeleteUjumbe wangu; hii habari imetolewa vibaya kwa kila kitu.
Kwa kufuata majita ya mdau, ni dhahiri kuwa yana asili ya Mtwara, Lindi, Msasani-DSM na Tanga ambako wenyeji wa Mtwara alihamia.
ReplyDeleteKwa vile mwaka wa kuzaliwa unaonekana wazi ktk kitambulisho, na majina yanaonekana 'Kioma Si-Yanga Taimu Ngayenga' ni sawa na ya watanzania wenzetu wa kusini, lazima kuna ndugu, jamaa na marafiki wa baba wa huyu kijana watajitokeza kumfahamisha kuwa kijana wake anamtafuta.
Kumbuka vita vya RENAMO-FRELIMO Tanzania ilipeleka askari wengi na 'wanausalama a.k.a wanafunzi' kusaidia Frelimo isiondolewe madarakani Mozambique.
Mdau
Chakumwenda Chibiriti
Mahuta-Shimoni
Mtwara.
Duh hilo jina limekaa kimpira mpira "SIYANGA TIMU" bali NI SIMBA YA MSIMBAZI.(jamani utani tu wadau msimind)
ReplyDeletelakini mbona umeweka ID yake humu. Kesho utakumta Mnigeria naye anayo hiyo license.
ReplyDeleteBack to the topic hayo tutayaona mwaka 2012 na kuendelea vijana wa OH,MD and TX. Wengi wao wakishajua child support inanukia wanahama State
unasema mwaka baba yake alikua huko si ungalie huyu anamiaka mingapi tu jamani. Leseni inasema 26/5/81 huyu baba yake alikua miaka ya 80
ReplyDeleteanafananafanana na bambo!!!
ReplyDeleteLAKINI KAMA VILE ANAFANANA NA PHILIPO MANGULA! SIJUI NYIE MNAONAJE WADAU.
ReplyDeleteNaungana na mdau hapo juu kulingana na aina ya majina ya huyu kijana inaonekana kabisa kuwa huyo baba, atakuwa, kati ya makabila ya kusini. ni mmakonde ama mmakua ama mwiyao. Ninaomba kati ya makabila haya kama kuna ukoo wa majina hayo ya kijana, basi mjiulize mara mbili ni nani alikwenda uko na mtapata jibu. mchukueni kijana wenu,kwanza anaonekana shupavu na ana kibarua chake si mnaona lesseni ya gani?
ReplyDeleteLamuhimu nikusaidiwa huyo kijana kama kuna watu wanamuelewa baba yake binafsi imeningia huzuni kwa huyo kijana kutomjuwa baba yake isitoshe wakuu hilo jina ni miongoni mwa majina ya Tanzania ?kwani kwa upande wetu huku zanzibar naweza kumwambia jamaa hatuna mtu mwenye jina kama hili na badala yake atafute upande wa wapili pia mnaweza kumsaidia kueleza ni jina la kabila gani .
ReplyDeleteKaka yake ni Kaijage wa TFF asikwambie mtu
ReplyDeleteAtakuwa ni mwanangu kwa sababu amefanana na mimi na pia nilisoma Mozambique na nilikuwa na 'vishindo' wakati niko skuli.
ReplyDeleteKama kweli baba wa huyu kijana alikuwa mwanafunzi huko Mozambique basi ubalozi wa Tanzania nchini Mozambique unaweza kuwa na kumbukumbu na kujua alitokea mji gani kabla ya kwenda huko na kama alikuwa mfanyakazi watajua alitokea ofisi gani.
ReplyDeleteNampa pole sana. Asikate tamaa hata mie baba angu alitenekeza nikiwa mchanga... aliniacha na mama na kurudi kwao Zimbabwe lakini juzi juzi kaja kunitafuta baada ya miaka 43 kupita. Iko siku Mungu atamkutanisha na baba yake