Dear Bw. Michuzi,
Mimi ni mwanahistoria kutoka Marekani. Sasa hivi, ninaishi Bongo.Ninafuata sana blog yako!
Mimi ni mwanahistoria kutoka Marekani. Sasa hivi, ninaishi Bongo.Ninafuata sana blog yako!
Nimeamua kukutuma email ili kuomba msaada wako. Ninasoma historia ya Tanzania, na sasa, ninafanya utafiti kuhusu maisha na utamaduni wawatu walioishi mjini wakati wa miaka 1960s na 1970s.
Mwaka huu,nimewahoji wanamuziki wengi wa wakati ule, na nimesoma magazeti ya wakati ule, kama Uhuru, Mzalendo, Nchi Yetu, nk. Sasa, ningependakujua zaidi historia za naitklabu, hasa za Dar es Salaam, Morogoro naTanga.
Kwa mfano, Dar es Salaam, ilikuwa Arnautoglu, Margot,Princess, Kibarua/Amana, Gateways; Tanga ilikuwa Mwananchi Bar, Firstand Last, Tangamano; Morogoro, ilikuwa Sabena, nk. Sijui kama labda wewe, au wadau wa blog ya ya jamii watakuwa na mawazo, au mapicha, au hadithi, ili kunifundisha historia hii?
Nakushukuru sana!
Endelea na kazi yako nzuri!
Emily Callaci
Emily Callaci
Em,
ReplyDeleteKiswahili kizuri sana umeongea rafiki yangu...am proud of you.
See you soon.
Hope you manage to get answers from this blog...inajulikana sana!
Goodluck!
Emilly? mwiislamu? Unamtuliza mkeo kwa makofi? What a shame? Wewe si Mwiislamu wala Mkristo bali baradhuli tu!
ReplyDeletehapa inabidi utoe hela,watu hawatakupa historia bure wakati wewe utaenda kuifanya kama documentary na utalipwa huko marekani. weka dau watu watajitokeza kukupa hizo info unazotaka.tena haina hata haja ya kuja kwenye blog ya michuzi, onana na wazee waliokulia mijini hapo Dar,then unaenda morogoro na Tanga.hao watakupa hizo info zote. hivi hujui archeologists wanawalipa locals ili kupata info then wanasema wamezivumbua!! bongo tambarare ndugu,no money no service..michuzi naomba kuwakilisha.
ReplyDeletekuna klabu nyingine ya starehe dar ufukweni feri iliyoitwa Banda la ngozi ilikua maarufu sana miaka ya 60's,white house na safari risot,Hotel Africana kimara
ReplyDeleteMdau Tarime
hili sasa dili wanablogu changamka upesi
ReplyDeleteAnon wa Aug 29 11:46 usimtukane Emily yeye ni mwanahistoria wala hampigi mkewe. Kabla hujakomenti angalia kwanza unamkomentia nani...
ReplyDeleteMwanahistoria unafanya utafiti mzuri na ninaamini wadau wengi nikiwa mmojawapo watanufaika na taarifa zitakazowekwa na wadau. Ila nina swali, maisha na utamaduni wa watu wa mjini ni zaidi ya kuongea na wanamuziki na kumbi za starehe. Au wewe ulitaka kujua tu kuhusu kumbi za starehe zilizopo mijini na siyo "tamaduni za watu za mjini" Kila la heri katika utafiti wako
Pale magomeni mapipa kulikuwa na Chimoka Bar. Ilikuwa imeungana na gas station ya sasa iliyopo pale njia panda
ReplyDeleteMorogoro kuna DDC ndiko alikokuwa akipiga Mbaraka Mwishehe na ziko nyingine nyingi
Big up
Pale karibu na soko la samaki Feri ilipo Swimming Club miaka ya 1963 64 65 ilikuwepo Banda Beach tena nakumbuka Hevy boxer Titus Simba ndiye alikuwa bouncer pale miaka hiyo. Pale Banda Beach akina Papa Micky wa Nova success ndiyo wakipiga pachanga pale. For more info contact me at pkonkoli@yahoo.com
ReplyDeleteEmily,
ReplyDeleteMoja ya njia rahisi ya kufanya utafiti wako ni kuwatafuta vijana wa wakati huo ambao walikuwa wamiliki wa kumbi au wanamuziki au madj.
Pale palipojengwa kituo cha treni ya TAZARA palikuwa na ukumbi maarufu sana ulikuwa unamilikiwa na Mzee Batenga. Watafute familia ya Batenga wataweza kukupa habari za ukumbi ule pengine pamoja na picha zilizowahi kupigwa na watu mbali mbali wakati huo.
Katikati ya jiji la Dar kuna ukumbi uliokuwa unaitwa New Palace Hotel baadaye ukaitwa Mbowe Hotel na sasa uniatwa Billicanas. Watafute kina Max, Freeman na Henry Mbowe na Pascal Onema wataweza kukupa data.
Royal Court pale Sea View ilikuwa inaitwa Sea View Hotel ukienda ulizia historia ya hotel ile utapata habari nyingi sana.
Safari Resort, Kimara. Kwetu Bar, Kinondoni. Zena Garden, Regent Estate. Hunters, Ubungo. Jambos, Ubungo. Princess Bar, Mchafukoge/Mnazi Mmoja.
Lusaka By Night, Keko na Hunters, Ubungo kwa habari za kumbi hizi watafute Mzee Makassi na Remmy Ongala wataweza kukupa data na clue ya kuwapata wamiliki wake.
Savannah Inn baadaye ikaitwa White House, Ubungo. Watafute Mzee Mwema Mukadjanga au Vumbi watakupa data.
Pia wapo watu mashuhuri/living legends waliokuwa active wakati wa miaka ya 60 na 70 kama kina David Mussa, Kingui Brothers especially Adam Kingui mara ya mwisho walikuwa Upanga, Dar es Salaam. George, Mark na Paul Mhuto. Mabruk na Mohamed wa The Kilimanjaro Band. Hassan Mbitta na Dick Unga wa Afro 70 Band. Wanamuziki wa The Tanzanite Band John, George, Abraham, Yona, John, Amato. King Kiki. Muhidin Gurumo na Said Mabera wa Msondo Ngoma Jazz band.
Unaweza kucheki na Tanzania Tourist Corporation wataweza kukupa data za mahoteli ya wakati huo na mameneja wake. Ukipata majina ya mameneja wa mahoteli wa wakati huo wataweza kukupa data za hoteli zao na rivary bars zilizokuwa private owned and the regural customers wao.
Good luck.
PS/Una contact address yoyote?
Vilevile kulikua na Top Life Bar Kinondoni mwanamuziki Papa Micky alitumbuiza enzi hizo
ReplyDeleteZena Garden, Mohamedi Kiluvia pale Regent Estates anaweza kukupatia data. YMCA vile vile unaweza kupata data.
ReplyDeleteBatenga familia karibu wote wametutoka dunia. Ukiangalia hizi sehemu zote zilichangia sana "social health problem" Tanzania kwa sasa na hizi sehemu karibu watu wote waliofanya kazi au kutembelea wamepata madhala fulani ya ugonjwa. Sehemu zingine kama "Magotti" pale opposite na Ex-Telecom hii ilikuwa mahali pa watu kufanya maovu na serikali ilikuwa ajali kabisa na sasa tunalipa..
wasiliana na sisi vijana wa siku hizo ili kufahamu mwanzao wa bendi za Afro 70 na vile vile Safari Trippers na ushindani wao sehemu za Chang'ombe na Temeke mis=aka ya 69 na 70.
ReplyDeletemdau
lawrence@mac.co.tz
Usisahau na UWANJA WA FISI pia pana historia kubwa sana pale!
ReplyDeleteTafuta jinsi uonane na Mr. Kitenge wa Ch.5 wa kipindi cha Mtaa Juke Box atakufahamisha vizuri ni mtaalamu wa mambo hayo.
ReplyDelete