Mtibwa wakikabidhiwa ngao yao ha hisani ya
vodacom neshno ya zamani jijini dar leo
Mdau ,
Leo Yanga africa wamegalagazwa bao 2-1 na Mtibwa Sukari, na kuwafanya mashabiki wake kuwa wanyonge sana. Redio mbao zinadadisha kwamba siku zahesabika kubaki jangwani kwa kocha wao profesa Kondic. Maana ni hatari bin balaa na bakora zinanukia huko mahali...
Hongereni Mtibwa kuchukua ngao ya hisani ya Vodacom.
Wako mdau

Edwin Mac Temba
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Pamoja na usajili wa mamilioni ya fedha ambazo viongozi hawazionei uchungu, ukichezwa mpira "halali" Tanzania matokeo yake yatashangaza watu wengi. Mechi hii ni moja ya michezo halali waliyocheza Yanga. Kwa taarifa matokeo yalikuwa 2-1.

    ReplyDelete
  2. Acha mbwembwe kaka michu, tunajua kama unatumia BlackBerry ® smartphone from Vodacom..si wamekupa ya kazi tu....wacha kujidai.....

    ReplyDelete
  3. Duuh black berry imechapia ni 2-1 sio 1-0 sijui haya matokeo umeyapata wapi? au ndio uyanga umekutawala
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  4. these results(2-1), looks so familiar,mmhhh,I wonder where else have I seen them yesterday!!!!!

    ReplyDelete
  5. Wewe mdau kijusi wa pwani, mbona unaongea ugali wa jana sana? hapo 1-0 imeandikwa sehemu gani na hiyo blackberry iliyochapia?

    ReplyDelete
  6. Hey Misupu,
    Hebu wapatie hii website wanajumuia waone NIZA Halfan mechi yake ya kwanza video www.whitecapsFC.com wajionee wenyewe kijana wetu anafanya nini hapo CAnada

    ReplyDelete
  7. Wee anon 5 wacha kusoma habari vipolo ungekuwa msomaji mzuri wa blog hii ungeona black berry ilivyo chapia hii habari imelekebishwa ilipotoka kwa mara ya kwanza iliandikwa 1-0 hivi sasa imelekebishwa na wewe ndio umesoma yote kwasababu ya internet kwa jirani.
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  8. Acha undanga wewe Kijusi, hamna habari kiporo hapo labda comment yako ndio kiporo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...