globu ya jamii imekumbana na bango hili maeneo ya barabara ya kenyatta na kinondoni rodi. mdau mwenye data za mstakabali wa bango hili msaada tutani tafadhali...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. hiyo ni novel moja ya nguvu sana nimeisoma, yani ni nzuri sana ziko mfululizo nne, na hapa karibuni HBO wameitengenezea sinema na ikaaktiwa na mwanamuziki Jill Scott .Mwandishi Mmarekani mmoja aliishi Botswana au Namibia na hiyo novo ina setting ya huko south,ni nzuri sana, isomeni hiyo wapenzi wa vitabu mtaipenda, ila sijui kwa nini iko hapo labda hapo ni baa wataionyesha sinema yake.

    ReplyDelete
  2. Hapo ndo maudhui ya marketing yanapomfikia mlengwa walinuia ku-catch your attention. Ni kama advertisement za sasatel kama unakumbuka zilikuwa na vibwagizo kama 'more sasa na less ...'

    ReplyDelete
  3. Jill Scott haishi Botswana ila alikwenda kuact hiyo show ambayo inabase on one novel. Niliiangalia yote na inachekesha sana nadhani inaitwa Number one detective ...inahusu mwanamke alikua amerithi hela ya baba yake akafungua No.1 Ladies Detective Agency na inaelezea mambo mengi yanayoendelea huko nchini kwao kama yale yanayotokea africa yetu kila siku rushwa, kunyanyasa wanawake, etc etc...its a funny....Naona wameona imependwa hivyo wanandelea na second season....

    ReplyDelete
  4. Kuongezea maelezo hapo juu, movie yake inaonyeshwa sana Mnet....inahusu mwanasheria wa kwanza wa kike Botswana, huyo kwenye bango ndio mwanasheria mwenyewe.
    Ila kiukweli kabisa sielewi mantiki ya kuweka hiyo kwenye bango. Sijui wanatangaza watu waiangalie hiyo movie Mnet ama wakasome kitabu..ama sijuii...inatatiza

    ReplyDelete
  5. nadhani maelezo yalioelezwa na wadaukuhusu hiyo film/ novel yanaeleweka! kama sijakosea nia ilikuwa ni kujua sbb ya hilo bango kuwa hapo, muhusika/ama mwenye kujua aeleze sbb ya kuwa hapo!! inaonyesha kiasi gani film hiyo imepata umaarufu mpk TZ ipo, nasi waTZ tujitahidi kujitangaza kwa wenzetu

    ReplyDelete
  6. aah asikudanganye mtu,hiyo ni kampuni ya kipepelezi ya akina mama wameianzisha,nia na madhumuni ni kuwasaidia akina mama wenye waume zao wakware waweze kukamatwa,naskia wana vitendea kazi ka vya wale watu wa CHEATERS kule states.

    ReplyDelete
  7. Hiyo series naifuatilia sana... lakini ata mimi niliona hiyo bango hapo... (na haliko moja) nilishangaa kuliona kwasababu akuna ishara yoyote yakuonesha kuwa inatangaza nini? nikimaanisha kuwa akuna kuonesha kuwa labda dstv ndo wanaonesha hiyo series kwahiyo watu wafuatilie au kuwa ni channel ya nyumbani.... kwahiyo ikanifanya nijiulize maswali shungu mzima..... au labda au waweka mabango ndo wanaitangaza.... sijaelewa... maana liko peke yake...

    ReplyDelete
  8. ni tamthilia ambayo kuna wakati ilikuwa ikionyeshwa na bbc kila jumapili jioni.

    ReplyDelete
  9. We anony wa Sun Aug 23,08:57:00 am,take time to read and understand things[DumbAss],AMESEMA MWANDISHI WA KIMAREKANI ALIEWAHI KUISHI hizo nchi mbili za Sauzi,sio kwamba Jill Scott anaishi huko.Jill Scott is the one who potrayed the main character,sio tu unabwatuka eti Jill Scott haishi huko,hata mdogo wangu wa Manelumango High anajua hicho.don't rush to respond to things before you understand ze point,ni hayo tu.

    ReplyDelete
  10. Hiyo ni movie,imetoka hivi karibuni tu ya jill scot ameiact akiwa botswana inaitwa samething is DICTACTIVE..wala sio novel.jaribuni kitafuta na kuinagalia kwa uzuri ni nzuri sana

    ReplyDelete
  11. HIYO NI SERIES INAYOITWA NUMBER ONE LADIES DETECTIVE AGENCY INATOKANA NA SERIES NOVEL ZINAZOHUSU BOTSWANA NA HUYO MPELELEZI MWANAMKE ZILIZOANDIKWA NA A. McCALL SMITH (ONE OF HIS BESTSELLERS). KWA SASA INAONYESHWA KWENYE DSTV CHANNEL 103 JUMAPILI SAA1 12 MPAKA SAA 2 JIONI NA KURUDIWA TUESDAY.... SO THE BANGO NI DSTV MARKETING YA HIYO SERIES ILI MUWEZE KUWASHA LUNINGA ZENU HALAU WAWAWEKEE MATANGAZO MENGINE YA PEPSI, SALAMA CONDOM NA KADHALIKA...YOU ATTRACT THE VIEWERS.

    WACHEZA MOVIE BONGO MNAWEZA KUANGALIA NA KUIGA ILI VITABU KAMA VYA KINA ELVIS MUSIBA NA NDUNGURU VIFANYIWE SERIES NA KURUSHWA DUNIANI.

    ReplyDelete
  12. Hapo nahisi pamefunguliwa salon ya kike ya kutengeneza nywele kama za huyu hapo bangoni..

    ReplyDelete
  13. kama mdau alivyo andika hapo juu, hiyo ni series ambayo inaoneshwa DStv kila jumatatu saa mbili usiku, iko bomba sana. ila communication iliyotumika hapo ipo katika mfumo wa sequence, kama utapita eneo lilipo bango hilo, kuna mabango mengine mawili ambayo inabidi yaendane ili ujumbe uupate vizuri, kwa kifupi bango lakwanza linasema "sometimes the best man for the job is a woman" lapili ndo hilo linasema "No 1 ladies dtective agency" na latatu linasema "mondays at 20h30 only on M-net, exclusive to DStv". kwahiyo ukiyaona yote matatu in a sequencey utapata maana kamili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...