Hello MICHUZI,
HAYA NI MAPOROMOKO YA MTO LUVANYINA AMABAO HAUKAUKI MWAKA MZIMA. UPO KATA YA KIPAGALO TARAFA YA BULONGWA WILAYA YA MAKETE. YANAZALISHAUMEME MWINGI TU NA HOSPITALI YA BULONGWA IMEKUWA IKITUMIA UMEME HUU YENYEWE NA WANANCHI WA TARAFA ILE. Je Tanesco hawawezi kuona hili??
Mdau Josephat wa Makete
maji yakienda kwa kasi kwenye mtambo wa kuzalishia umeme
kwa msiofika Makete haya ndio baadhi ya mandhari yake



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. iringa iko juu inatisha kwa mandhari zake za asili/nature na hali ya hewa swaafi

    idumu

    ReplyDelete
  2. wakinga tuko juu, wenye wivu mjonyonge, na ndo nishasema sasa!

    ReplyDelete
  3. Kuna mito mingi tanzania ambayo Tanesco wangeweza kutega mtambo wa kuzalisha umeme. Nafiri sio wabunifu kabisa. Tanzania haiwezekani ikawa ikilala giza sehemu nyingine, au mgao wa umeme kila kukicha. Umeme wa uhakika ni chachu ya maendeleo. Hebu angalia kwamfano TRA inashindwa kuzibidi ukusanyaji kodi kwa sababu hawatumii tekinonogia katika kuhakiki uuzaji wa wafanyabiashara mbalimbali. Ikianzisha utumiaji wa tekinologia wakati vyombo vyenyewe vinahitaji matumizi ya umeme. Itakuwaje pale umeme ukikatika. Ni mtazamo tu.

    ReplyDelete
  4. Haya si maporomoko wala nini.Hii ni sehemu ya mto unapotiririka na hakuna dalili ya kuwepo maporomoko.Ungejaribu kupiga picha mwanzoni mwa huu mto labda tungeona hayo maporomoko unayodai.Somo la jiografia lilikupita kushoto

    ReplyDelete
  5. madhanri mazuri mpaka mbu hawatii mguu ila ule ugonjwa wa radioni unapenda sana sehemu zenye baridi

    ReplyDelete
  6. Kumbe yule mganga wa jadi pale mnazimmoja ni tapeli? Dawa zake moja kaiita LUVANYINA na nyingine KIPAGALO!!

    ReplyDelete
  7. MAKETE BI WILAYA YENYE VIVUTIO VINGI LAKINI IPO KWENYE UMASIKINI WA KUTISHA SANA,AJABU WENYEJI WAKE AMBAO NI KABILA LA WAKINGA NI WAFANYA BIASHARA WAKUBWA KATIKA MIJI KAMA MBEYA,DAR ES SALAAM NA IRINGA LAKINI KWAO HAWAENDELEZI KABISA WATAJENGA MBEYA,TUNDUMA,MAKAMBAKO,NJOMBE,SONGEA,IRINGA,MOROGORO KWAO NO,WANATAKIWA WABADILIKE MAKETE ITAENDELEA ZAIDI

    ReplyDelete
  8. Mpiga Picha angeshuka chini kidogo ya hapo picha ilipochukuliwa kuna sehemu maji yandondoka urefu wa mita 150

    ReplyDelete
  9. our country is beautiful. I love it!!!

    ReplyDelete
  10. Mbigiri hayo maporomoko kweli yapo kwenye huo mto.

    ReplyDelete
  11. Msiwapeleke huko Tanesco. Wana balaa..wakishaingia huko mto utakauka...kwani Ruvu unapotezaje maji kama si balaa la Tanesco? Ni kati ya mito mikubwa Tanzania...hatawataki Tanesco huko kabisaaaaaaa

    ReplyDelete
  12. watz bwana eti m2 anaandika i love my country halafu anajiweka anonymous sasa huo upendo uko wapi?unaogopa nini kusimama kidete kwa jina lako na kutamka I LV MY TANZANIA!!!

    ReplyDelete
  13. MNYALUKOLOAugust 25, 2009

    WAKINGA WANAIMANI ZA KISHIRIKINA NA NIWASHIRIKINA WAKO JUU SANA KIBIASHARA NA WENGI WAO WANAPATA UTAJIRI KWA KWA USHIRIKNA NA YUKO RADHI AVAE SHATI JEKUNDU JANUARY MPAKA DECEMBA BILA KUBADILISHA HUU NI MMOJAWAPO WA MFANO UKILINGANISHA NA MAKABILA MENGINE YAISHIO IRINGA WANAOGOPEWA SANA LABDA HILO PIA LINAWAFANYA WAKIMBIE KWAO WASIJENGE KWA KUOGOPANA

    ReplyDelete
  14. Tutajie megawatt zinazolishwa ndo tujue kama TANESCO wanapaswa kulaumiwa au la si sentensi iliyokaa kisiasa "yanazalisha umeme mwingi tu". Vinginevyo hujapambanua wingi wa huo umeme.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...