(bofya mshale kuona video hii)

WASHIRIKI WA REDDS MISS ILALA 2009 WAKIWA KAMBINI KWAO KATIKA HOTELI YA LAMADA JIJINI DAR. WANAPANDA JUKWAANI IJUMAA HII KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE HALL KUMPATA MALKIA MPYA WA UREMBO WA ILALA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Hawa ma miss sijawafurahi wakati jamaa anawatambulisha kwa Michuzi wenyewe walikuwa wanaongea issue zaidi hawaja" pay attention"

    ReplyDelete
  2. Kaaazi kweli kweli!!

    ReplyDelete
  3. Hapa table manners ni zero kabisa; jamani wafundisheni!!!!???

    ReplyDelete
  4. Akina dada jamani soda siyo nzuri, especially COKE/PEPSI....jaribuni basi angalau kunywa maji

    ReplyDelete
  5. sasa hawa walimbwende wetu hata michuzi blog pia hawaijui kuna watu kweli hapa ?

    ReplyDelete
  6. Vishambaaa

    ReplyDelete
  7. "msiguse wali wangu"?

    ReplyDelete
  8. bongo jamani kwa nini tunapenda sana soda?yaani nchi za wenzetu masoda hayo ni very rare,tuna matunda kibao lakini hatunywi juice.nina mpango wa kuja kuanzisha kiwanda cha juice fresh na kupiga campeni moja kubwa mpaka hayo maviwanda ya soda yatajuta kunifahamu.

    ReplyDelete
  9. "this year...kwa kweli....tumowmbe Mungu...." lini tutaacha kiswaenglishkihayakibantu

    ReplyDelete
  10. Hahahha, Michuzi.Maharage!!!!
    Kaazi kweli kweli...

    NB: Tujifunze kufanya mahojiano na utambulisho Jamani.

    ReplyDelete
  11. Mwe wajameni! Hawa warembo wetu inaonekana ni maamuma fulani. Wako mezani kwa chakula kila mtu anasema vyake. Wanaongea wote kwa wakati mmoja. Wengi wao ni vichwa vya panzi, yaani hata blog ya Mithupu hawaifahamu!! Kwa! Ikiyo thatha kweli tutafika thithi?

    ReplyDelete
  12. Sioni ni kwanini utambulisho huu unakuja kuletwa huku duniani unaambatana na dhihaka. Haingekuwa vema kumtambulisha michuzi bila kuwakejeli wahusika? Ilikuwa na ulazima gani kuwaambia watu wamanuna kama wamekula mbilimbi?

    ReplyDelete
  13. Wajifunze kuwa na pesonalty.

    ReplyDelete
  14. Mie KUhusu hao kuwa maimuna haisumbui sababu hata venezuela wanapeleka Mtu wa Tafsiri Lugha yetu ni kiswali. Ila Nizamu muhimu wangemsikiliza jamaa michuzi ni nani? Alafu michuzi angejitambulisha vizuri naye, Hawa Miss wengi Ushamba na Utoto unawaangusha kambi ikiregea nao wataregea wataumiaaaaaaaaa.

    Ila Ile Ya Michuzi Maharage hata mie nimecheka DUH!!!!... Naona mnawapooza na Soda. Pazi.

    Next Time jamani muwataarishe kabla hawajazalilika mbele zawatu kwengine. Pazi

    ReplyDelete
  15. aaah kudadadadadedededekiii,mikeleleeee,ukichanganya na kwaa kwaaa kwaaaa!!,,,ya kunguru wa ZANZIBAR ni balaa tupu.

    ReplyDelete
  16. Aaaagh!! au wote wako katika lile jua linaoangazaga usiku??? mbona wanachemka hivyo?? aaagh bwanaeee, michuzi haya matoto mbona hayajatulia haya, yani utuluvu ziro kabsaaa, ha'fu heshima na yenyewe ziro!! ka'vipi mwanangumwenyewe michuzi kale ka ufadhili ulikoahidi kuwapa ka-withdraw utuchezeshee sisi wadau wako bahati nasibu hata ya kutambua sura ya kikwete kati ya sura mbili ya kikwete na malecela aaahg. yani mbona wameshindwa hata kukuheshimu wewe mmoja wa wafadhili wao???. au ni uswahili umezidi Ilala?? wangekuwa mamiss kinondoni we mwenyewe ungeona Ustaarabu A lakini hawa ustaarabu F!!! aaaagh wameniudhi sana, yani wanakuita MICHUZI MAHARAGE!!!! duh!!
    Kwanza mi nimebadili mawazo niliwapigia kura watatu kuwa miss fotojeniki lakini kwa ushankupe huu waliouonyesha nimebadili mawazo sasa nasema woooote wana sura mbayaaaaa, hamna hata miss fotojeniki hapo, miss fotojeniki yupo kinondoni. halafu michuzi wewe ulivyo superstaa bongo wanakujua sana hawa sema wanaleta zile tu, au mwanangu gari lako hawajaliona nini?? hebu ukitaka kuondoka hapo piga less la nguvu na honi za fujo ili wageuke waone gari lako lilivo kali!!!
    vyote vibayaaaaa!!!
    ni hayo tu.

    ReplyDelete
  17. Huyo muongeaji, anaongea na wahuni au na ladies? anaongea nao utafikiri anaongea na wahuni tu. Mijanaume ya kibongo bwana!, eti, "mlinuna kama mmekula mbilimbi" respect ladies nyie!

    ReplyDelete
  18. kaazi kweli kweli. huyo jamaa na mamiss wake wote adabu hamna!! eti mmenuna kama mmekula mbilimbi?? miss naye anaongezea michuzi.maharage?? hivi tutafika kweli wajameni? wote wanafanya mzaha wakati ni utambulisho muhimu. hii clip imenisikitisha sana na kwa mtaji huu, TZ kutoa miss world ni ndoto..halafu mamiss wanakula mlo mzito haswa na kushushia kwa soda!!! kweli bongo tambarareee.

    kaka michuzi pole kwa kufanyiwa dhihaka.siku nyingine inabidi uzipige panga clip zisizokuwa na heshima.

    ReplyDelete
  19. Mamiss Ilala wengi wanatokea uswahilini kama tunavojua kwa hiyo wakipata chance kama hizo za kutoa msosi uliokwenda shule hawataki kuzichezea..!! Nyie mnaosema English yao ngumu, hicho kiswahili chao chenyewe tu shida sehemu za L wanaweka R..!! Ndio maana kila siku Miss Tanzania wanatokea Kinondoni ambako watoto wa wilaya yetu hii wamezoea.

    Anonymous wa 04:58PM unayesema hata watu wa Venezuela wanapeleka mtu wa kutafsiri hiyo ni tofauti na Tanzania sababu Venezuela lugha yao ya taifa ni MOJA tu Spanish tofauti na Tanzania ambako kwetu lugha ya Taifa ni Kiswahili pamoja na Kiingereza.

    Mdau wa Meeda,SInza.

    ReplyDelete
  20. Mamiss hawaonyeshi kuwa hata na adabu. Mdhamini anatambulishwa wao wanakejeli kejeli tu. Au wanafikiri ukionyesha maringoringo ndio umiss? Uzuri ni pamoja na nidhamu. Ukija kwa huyo aliekuwa anatambulisha na kuongea kuhusu picha kwakweli lugha aliokuwa alikuwa anaongea si nzuri. Sasa anawafundisha nini hao mabinti hapo kambini? Wataelewa au watakuwa wanaona ni mzaha tu?

    ReplyDelete
  21. Hawa wasichana hawana adabu kabisa,jamaa alikuwa anawatambulisha,wenyewe walikuwa busy kupiga makelele yasiyo na maana.Mi nachojua mtu akikutambulisha unaitikia nimefurahi kukufahamu simple ,lakini wenyewe wala akili kwenye msosi tu.

    ReplyDelete
  22. michuzi ni kijana wa kariakoo na hao ni watoto wa ilala wana kasheshe!!!! sasa weewe unategemea nini?? hapo sawa namajani ya boga yamezaa boga its mule mule.

    mdau canada!

    ReplyDelete
  23. tena hawana adabu kweli cheki kwanza wote wako ugly duckly

    ReplyDelete
  24. Mmmhh sina la kusema. Wanakula wali ma-missi poleni hiyo shibe yake hapo majaji watakimbia...mmmh hatari na hizo soda zilivyo jaa hapo mezani hatari tupu. No personality what so ever! Naona kila mtu ameifanya hiyo ni profession....Tanzania jamani tunaelekea wapi??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...