Michuzi!
Umedhihirisha pasina ubishi kuwa wewe ni mbunifu ulietukuka na hakika hii ni blogu ya jamii. yaani hapa hata kama hujabandika kitu kipya kwa muda wadau tunaburudika tu kwenye 'maoni'. hakika yanatia raha na swaumu hiii aaaaaa.. muda wenda wapita.
sasa basi baada ya lile darasa la waalimu/walimu (naona hadi sasa droo ngoma, hamna upande ulioshinda/ulioshindwa baada ya mtandao wa TUKI kupata kwikwi) naomba nije na darasa la kiinglishi baada ya nami pia kusumbuliwa na maneno fulani niliyoona bwalo la maafisa wa polisi pale oystebay. naomba kujua maneno sahihi ni yepi na kwa nini. maneno yenyewe ni:
1. POLICE OFFICER'S MESS
2. POLICE MESS
naomba kuwasilisha
Mdau Masaki
------------------------------------
Bro Michuzi!
Mambo? Nime-attempt kunyambua
Kiinglish kama ilivyoombwa. Naomba kuwakilisha!

The clarification to the Kiinglishi; ‘Police Officer’s Mess’ and ‘PoliceMess’ is as follows: First it is important to define ‘Mess’ in this context; which is:
Either;
1] a place where a group of people, especially members of the armed forces,have meals together
Or:2] a group of people, especially members of the armed forces, who have meals together
Or:3] a meal eaten together by a group of people, especially members of thearmed forces

Therefore the first kiinglishi ‘Police Officer’s Mess’ is wrong because it simply means a ‘mess’ of one Police Officer. The correct version aught to be ‘Police Officers’ Mess’ if one wants to name the place as defined in point [1], which I believe is what they/he/she intended.

The second kiinglishi ‘Police Mess’ is also correct with a slight change in that ‘Police’ here means an institution. It can therefore apply to all three definitions.
BY Lute wa Lutengano
Mdau wa Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Mhhhh hili neno lina walakini sijui kwa nini limetumika kwa hao wakubwa maana mbona pande mwingine linatoa tasfiri ya uchafu uchafu au mvurugiko wa mambo hivi! sasa..haliko friendly hili...

    ReplyDelete
  2. Mkazi wa MastabeyAugust 27, 2009

    Ndugu Mdau Masaki ni Oyster Bay na siyo Oystebay.

    Ni Police Officers Mess and Police Mess.

    ReplyDelete
  3. mdau hapo masaki ni c/o mjomba nini? ni oysterbay na sio oystebay.

    ReplyDelete
  4. Kwanza mimi mwenyewe sijawahi ona hilo tangazo, lakini kabla sijatoa maoni naomba uangalie kama univyoandika POLICE OFFICER'S MESS ni sahihi, hasa neno OFFICER'S. Mimi naona ingekuwa OFFICERS'.


    Kwanza neno mess lina maana nyingi katika lugha ya Kimombo kwa maelezo zaidi tembea Oxford English Dictionary ambao inapatikana bure kwenye mtandao.

    Kimsingi POLICE OFFICERS' MESS ni sahihi. Kwani kutokana na Oxford Dictionary neno MESS lina maana ya mahali watu wa cheo fulani haswa katika jeshi huwa wanakutana na kupata mlo.

    Hapa ni nukuu ya Oxford Dictionary
    "A company of people eating together. Each of the groups into which a military unit or ship's company is divided, the members of each group taking their meals together. Later also: the place where meals are taken by such groups; a place where personnel, esp. of similar rank, regularly eat or take recreation together (also occas. in non-military contexts)"

    Nadhani hii inasaidia.

    ReplyDelete
  5. The mess at a military base or military barracks is the building in which members of the armed forces can eat or relax.

    example: ...a party at the officers' mess...

    ReplyDelete
  6. ni "Police Officers' Mess"... Yes, dem messy too, Zombe!

    ReplyDelete
  7. We mdau wa Masaki kama Lugha haipandi ni haipandi tu sasa mbona tofuti hapo iko wazi kabisa!!!!!SIYO KILA POLISI ni OFFICER ndo maana kuna POLICE MESS hii ni kwa wote yaani polisi wa kawaida na maofisa wao na POLICE OFFICER'S MESS hiyo ni MESS kwa ajili ya Maofisa tu hivyo wale polisi wadogowadogo hawaruhusiwi kujimix humo! Understand,verstanden,umeleewa????

    ReplyDelete
  8. mdau unaposema police huyo tayari ni officer. huna haja ya kuongeza neno officer. hivyo sahihi ni police mess. na sio police officer's mess.

    ReplyDelete
  9. 1.Police Officer's Mess = Bwalo la maafisa wa Polisi
    2.Police Mess = Bwalo la Police

    Maana ninayoipata ni mwamba
    1.Bwalo la Maafisa wa Polisi tu,
    2.Bwalo la mapolisi bila kujali ni maafisa ama la!

    Nawakilisha,
    MANUTD-DIE-HARD-FAN from TMK!

    ReplyDelete
  10. Nijuavyo mimi hilo ni Bwalo la MAOFISA WA POLISI kama ambavyo hao walioamua iwe hivyo walikusudia, na hilo si ajabu kwani katika Majeshi ni hali ya kawaida.

    POLICE OFFICER'S MESS;

    Hapa ile kusudi la kuwa Bwalo la MAOFISA linaondoka na kuonyesha kuwa ni la OFISA peke yake. Kiinglishi sahihi ingekuwa POLICE OFFICERS' MESS.

    POLICE MESS;

    Hili sio kosa sana, kwa sababu ukweli unabaki kuwa ni Bwalo la Polisi. Lakini ukiliacha hivyo linaondoa ile kusudio la mahali hapo. Kwamba hapo halikukusudiwa kuwa Bwalo la polisi wote bila kujali vyeo vyao, bali kusudio lilikuwa ni kwa ajili ya MAOFISA.

    Kwa hiyo kwa maoni yangu kiinglishi sahihi kingekuwa ni POLICE OFFICERS' MESS.

    Mdau USA.

    ReplyDelete
  11. Wewe mwenyewe ujatumia manemo sahihi; Hakuna neno "YEPI" bali "YAPI".

    Kuhusu maneno sahihi nafikiri yote sawa mzee

    ReplyDelete
  12. The first one clearly refers to a single police officer while the second one may imply a mess (not in the social context) caused by Police. They are both incorrect. The correct version is Police Officers' Mess.

    ReplyDelete
  13. Bro Michuzi pole kwa swaumu.
    Nilitaka kumjibu mdau hapo juu kwamba jibu sahihi ni Police officers'mess kwa maana ya kwamba ni bwalo la maafisa wa polisi na si police mess ila kwa sababu wabongo tunapenda short-cut basi watu wameamua kuita police mess ambayo inakuwa na maana nyingine kabisa kwa maana kwamba polisi ameharibu au mambo yapo au polisi yupo vululuvululu au tafrani.
    Halafu nilitaka kumwambia mdau kuwa hakuna neno pasina ila lipo neno pasipo na sio oystebay ila oysterbay,c'est tout pour le moment.

    ReplyDelete
  14. Oystebay/Oysterbay; police officer's mess/police officers' mess

    ReplyDelete
  15. Ukiwa na maana ya kusema Bwalo na Maafisa wa Polisi maneno sahihi yatakuwa Police Officers' Mess. Ukisema Police Mess itamaanisha Bwalo la Polisi.

    ReplyDelete
  16. Mess mdau kasema ina maana nyingi kimombo
    Ikiwa ni POLICE OFFICERS' MESS inaleta maana ya mahala ua ukumbi maofficers wa police wapata mlo, vinyaji ua malazi ni kwa manufaa ya maofficers kwa ujumla
    Ikiwa ni POLICE OFFICER'S MESS maaana inakuwa nyingine kabisa kwa sababu huwezi kupata mahali ambapo police officer mmoja tu anapopata chakula na vinyaji, hapo basi ile MESS inakuwa na maana ya fujo, choo au uchafu.
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  17. Si unaona mzee wa nanihii, kiinglishi watu wananukuu tu online na kutupatia majibu hapahapa kutoka Oxyford dictionary. Kiswahili bwana!!! TUKI hakuna kitu, hovyo. Mjadala wa walimu Vs waalimu umeshindwa kuamuliwa kwa kuwa hakuna chanzo cha kuaminika mtandaoni kinachoweza kutupa ufumbuzi. Wacha wabongo wawe wabishi. Hii mambo ya kulazimisha watu wasome kwa kutumia kiswahili ni upuuzi mtupu, watu wanatafuta umaarufu kwa nguvu na wakati hata kazi yenyewe ya kukitangaza hawawezi, watuache tu tuongee cha mtaani

    ReplyDelete
  18. Police officer's mess: Eneo linalotumika kwa mlo linalomilikiwa na afisa wa polisi.

    Police officers' mess: Eneo linalotumika kwa mlo linalomilikiwa na maafisa wa polisi.

    Police officers mess: Eneo linalotumiwa na maafisa wa polisi kupata mlo

    Police mess: Vurugu zote tunazokumbana nazo tunapohitaji msaada wa polisi mfano polisi kutokuja kwenye matukio ya ujambazi mpaka yasikie jambazi limeuawa nk

    ReplyDelete
  19. Police Officer's Mess = Bwalo kwa Polisi mmoja tu

    Police Officers' Mess = Bwalo la Maofisa wa Mapolisi

    Police Mess = Bwalo la Mapolisi (bila ya kujali vyeo vyao).

    ReplyDelete
  20. nashukuru kwa ufafanuzi alioutoa lutengano.
    napenda pia kuongezea hili koktokana ka kusoma maoni ya wadau wengi na kugundua kuna kosa moja wanalo lifanya baadhi ambalo ni maana ya neno POLICE.
    Kwa kiingereza neno police maranyingi hutumiwa likimaanaisha idara inayo simamia utekelezaji wa sheria za nchi(institution)na sio askari mmojs. ns ksms unstsks kumaanisha askari basi neno sahihi ni POLICE OFFICER bila kujalisha kuwa ana cheo au hana. kama unataka kusema askari polisi mwenye cheo, basi utalazimika kutaja cheo cha/vyeo vya muhusika.
    na sio kama wengi nilivyo ona wakidai kwamba police officer ni mwenye cheo,na police ni askari wa kawaida tu.
    asili ya neno police ni kigiriki cha zamani likimaanisha city, kisha ktk likatini "politia=civil administration" ndipo kupitia kifaransa policier likatamkwa kiingereza police. ambalo kwa uzima wake laweza kuwa police force,police service n.k

    mdau*******

    ReplyDelete
  21. In Lute wa Lutenagano's submission 'aught' ought to be 'ought' and not 'aught'.

    ReplyDelete
  22. Nakubaliana na anony wa 11:40 hapo juu,askari police yeyote ni afisa,ila kuna NCO = Non Commissioned Officers ambao ni wenye cheo cha Koplo na chini yake na CO = Commissioned Officers ambao ni kuanzia Sajenti kwenda juu. Hivyo hilo bwalo(Police Officers Mess) ni la maafisa wa polisi wote kwa tafsiri sahihi na halina ubaguzi.Ila kwa mazoea ni kwa ajili ya maafisa wa polisi wa vyeo vya juu.

    ReplyDelete
  23. JAMAN KSWAHILI NACHO KIGUMU KWA KWELI!
    NAOMBA TUANZISHE PROGRAM ZA KOZI ZA KISWAHILI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...