abiria watarajiwa wakiangalia ratiba ya treni ya reli ya kati leo ambapo baada ya treni la bara kuingia, la kutoka dar kwenda mwisho wa reli halikuondoka na badala yake wameahidiwa litaondoka kesho saa kumi. redio mbao zinasema hakiondoki kitu hapo hiyo kesho hadi kieleweke maana jamaa wameshagoma na wanasubiri waziri kesho aje aongee kwa herufi kubwa kwani wana madai kibao hayajatekelezwa na tajiri wao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kazi kweli BONGO kila sehemu ukigusa tu ni sio,MUNGU tusahidie.

    ReplyDelete
  2. MWEKEZAJI AMESHINDWA KUWEKA HATA LCD DISPLAY TUNATUMIA UBAO NA CHAKI, KWELI WATANZANIA TUNAHITAJI MAOMBI !!

    ReplyDelete
  3. Michuzi nakuomba kwa niaba ya wada wa blog ya jamii, tuambiwe ukweli kweli juu ya huyu muwekezaji anaonekana kama mdogo wake na richimondi, kila kukicha mgogoro, ratiba mbovu kero kila siku na serikali yetu inakwena kuongea nao ila hatuoni matunda. huyu jamaa hajaleta kitu chochote tena cha kushangaza hata mishahara ya wafanyakazi wake analipiwa na serikali. kama serikali imeweza kulipa mshahara kumbe hata kufanyia mtengenezo engine pamoja na mabehewa inaweza. wamuondoe huyo kanjibahi anaonekana kushneh.
    hivi na yule boss niliyemuona kwenye TV anawakatalia waswahili wenzake madai yao hana uhusiana na mh. JK kweli? mh hatufiki (chukua chako mapema)amen

    ReplyDelete
  4. Haya ni matunda ya serikali yetu ya kusaini mikataba ya ovyo bila kuchunguza kama hao wawekezaji wanauwezo. Ona sasa wananchi ndio wanapata taabu ya usafiri. kama hata mishahara wanashindwa kulipa, mabehewa ni machafu, kunguni, mende, panya huu ndio mwekezaji????? jamani hizo 10 percent zitatufikisha mbali. Waendezao hawafaii!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. TANZANIA KWELI NI NCHI YA KUFIKILIKA UNAMLETA MWEKEZAJI KUTOKA NCHI HII UNATEGEMEA NINI. WAFANYABIASHARA WENGI KUTOKA NCHI HII NDO WANAOWABIA WATANZANIA.MTU ANAKUJA MASKINI BAAADA YA MIAKA MITANO ANAKUWA TAJIRI ANAANZA KUWASAIDIA MASKINI HUKU ANANYONYA MARA MBILI YAKE.TUMECHOKA WACHA TUWAPE UKWELI

    ReplyDelete
  6. Hivii,wizara ya Matreni na whatever inafanya nini? BONGO NUKSI TUPU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...