Wanafunzi wa shule ya Msingi kilimani iliyopo kitunda wilaya ya Ilala wakiwa wamekaa chini darasani na mwalimu wao akiwafundisha hii ni kutokana na uhaba wa madawati mashuleni.Vodacom Foundation imewapatia msaada wa madawati 70 ikiwa ni kampeni yake ya kutoa msaada wa madawati 400 katika shule za msingi mkoa wa dares salaam wenye thamani ya zaidi ya milioni 32.
Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba(kulia)akimkabidhi Diwani wa kata ya kitunda Osango Kaseno moja ya madawati kati ya 70 ikiwa ni kampeni ya mfuko huo wa kutoa msaada wa madawati 400 katika shule za msingi mkoa wa Dares Salaam wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 32,katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Josephine Matiku.

Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akimwambia jambo mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi kilimani iliyopo kitunda wilaya ya Ilala alipotembelea shule hiyo na kutoa msaada wa madawati 70 ikiwa ni kampeni ya mfuko huo wa kutoa msaada wa madawati 400 katika shule za msingi mkoa wa Dares Salaam wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 32.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. mwamvita kaolewa?

    ReplyDelete
  2. Aibu hii mpaka lini karne hii ya sayansi na teknolojia, hapo ni Dar je kule kijijini kwetu Gonja na Ndungu hali ikoje?? Mungu awape uzima walalahoi, na mkono wake uwaguse watawala wetu na mafisadi wao !!!

    ReplyDelete
  3. Michu mdogo wangu, umeweka kapuni comment zangu za hii habari...kumbe wewe sio ndugu yangu yangu unapendelea mahala fulani sio? Naelewa kwa nini umeffanya hivyo na siwezi kumwaga dagaa hapa

    ReplyDelete
  4. 1984 ulikuwa mwaka wa kwanza kwa wanafunzi shule ya msingi mazengo Dodoma kukaa chini, nilikuwa darasa la pili, mama wee, paka leo tatizo hili halijaisha Tanzania tunakazi kubwa

    ReplyDelete
  5. hivi kodi wanazokatwa wafanyakazi kwenye mishara yao zinaenda wapi???karne hii watu wanakaa chini!!na hapo ni dar,halafu hao wabunge mishahara yao minene na kazi kulala bungeni,mungu awape uzima wadaganyika,PIGA ,UA,GALAGAZA,TIFUA hujanito ughaibuni,hiyo hali inatisha WAKE UP PIPO!!

    ReplyDelete
  6. Wadogoza zangu poleni, hata sisi tulipitia hukohuko tena tulipewa form za kutembeza mchango wa madawati miaka ya 80 Tuliambiwa form irudi na Tsh.1500 asikuambie mtu mimi nilipataTsh200. nikaambulia fimbo3, darasa letu lilikuwa na madawati matatu tu kwa wale waliosoma Ubungo NHC na Karume primary chini ya mwl Mkuu mama Machano na waziri wetu Hayati Mayagila, Mliokuwepo mwalitambua hilo

    ReplyDelete
  7. mimi nilisoma ashira pr school dawati moja wanafunzi watatu, nikahamia dar nikajikuta nakaribishwa pale Karume kwenye darasa lenye vumbi tele nikaka chini kwa upole masomo yakaendelea

    ReplyDelete
  8. Michuzi unaminya sana bwana mpaka nimekasirika,watu tunamaliza wino bure.

    ReplyDelete
  9. yale ma X5 ya nini ikulu kama watoto wanakaa chin shuleni,mh!nchi yetu kweli kichwa cha mwendawazimu usibanie hii nasema ukweli kaka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...