simba taifa kubwa
yanga imara

Kitimutimu cha mechi ya marudiano ya Simba na Yanga sasa kufanyika sept 6 kwenye uwanja uliopo 16th st na kalmia, baada ya Yanga kukataa kuchezea wanja la Taifa Meadowbrook park kwa madai ni mbovu, huku wakilia mara ya mwisho kwamba ooohhh....tumefungwa kutokana na uwanja.

Habari toka ndani ya klabu hiyo ya jangwani zinasema kocha Meya amesimamishwa kwa muda na nafasi yake kuchukuliwa na Yasin Manyoka kufuatia ilichopata toka kwa watani wa jadi Simba april 26 mwaka huu mabao 3-2.

Simba wao wanadai ushindi upo popote,nyie Yanga badilisheni uwanja mara mia lakini kipigo kipo pale pale. Khaaakhaaaa sisi tunacheza GOZI la kisasa,alisikika Bamchawi(Mkakile),akimkebehi Luka Kinyang'anyiro shabiki nambali one wa Yanga Washington Dc.

Timu zote zipo kambini kwa maandalizi ya mechi hii ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa hapa na majirani zake. Kuna habari Simba wamemtumia tikeki Saleh Londa ambae kwa sasa yupo Tanzania kwa shughuli za kifamilia. watabiri wa michezo wanasema endapo kama Simba itarudia mchezo iliocheza April 26, basi Yanga itakula kisago kingine kwa mara ya pili mwaka huu.

Yanga hawakubaliani na maneno hayo wao wanasema, wakigangamala na kudau kwamba kila siku sio jumapili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Vijana wanaotuwakilisha huko Sudan vipi leo, wametutoa kimasomaso? Sijapata chombo cha habari kilichotoa habari hiyo.

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi, nilikuwa sijui kama wewe kumbe ni shabiki damu wa Simba. Naona unaipalilia kwelikweli Simba na kuiziba kiana timu ya wakubwa "Yanga". He he he he he he!!!!!!!

    This Is Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  3. michuzi tukituma comments zetu kuhusu hawa jamaa wabeba boksi wa usa na hii mipira yao unatubania lakini jamaa wanaboa sana hawa kwavile ulishaweka game zao wanavyocheza huo mpira wenyewe utadhani ni viwete sasa sioni sababu ya kutubandikia mechi zao humu daily AU KWAVILE WAKO MAREKANI??????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...